Beki Nadir Haroub akikabana na Mallick wa Senegal juzi. Uzuri wa Nadir Haroub yeye huwaga hana mechi rahisi wala ngumu. Yaani yeye mechi zote kwake ni sawa na akaza vile vile. Big up Nadir Haroub, tunakutegemea katika defence leo usiku na Ivory Coast. Kuna jamaa wa Ivory Coast anapiga vibaiskeli kama vya Ronaldo, huyu wa kumchunga sana.

Na Florian Kaijage, Abidjan
Taifa Stars inashuka tena Jumatano katika uwanja wa Felix Hophet Boigny jijini hapa kupambana na wenyeji Ivory Cost katika mchezo ambao lazima iepuke kufungwa ili kubakia na matumaini ya kufuzu kwa nusu fainali.

Mazingira ya Stars kuhitaji kuepuka kupoteza mchezo dhidi ya Ivory Cost yanatokana na kufungwa bao 0-1 na Sengal katika mchezo wa kwanza uliofanyika Jumapili iliyopita.

Kwa upande wa wenyeji hali yao ni mbaya zaidi kufuatia kipigo kikali cha mabao 0-3 walichokipata kutoka kwa majirani wa Stars, Zambia na kuibua hofu kubwa miongoni mwa mashabiki wa Ivory Cost kuwa inawezakana timu yao ikafurushwa mashindanoni ikingali mapema.

Na kuna uwezekano mkubwa mazingira ya mchezo wa Taifa Stars na Tembo (Elephants) wa Ivory Cost utakaoanza saa 4 kamili usiku za Afrika Mashariki, yakawa ya mashaka zaidi kwa timu zote mbili kwa vile timu zilizoshinda michezo ya kwanza ya kundi A, Zambia na Senegal zitakuwa tayari zimecheza katika mchezo wa mapema saa moja usiku.

Kocha wa Stars Marcio Maximo ameeleza kufahamu na kuzingatia kikamilifu mazingira yanayouzunguka mchezo wa timu yake dhidi ya wenyeji.

‘Tunafahamu watatushambulia tangu mwanzo na kutuweka katika hali ngumu ya kimchezo hasa ukizingatia kuwa watakuwa na mashabiki wao wakiwahamasisha kwa nguvu lakini hilo haliwatishi vijana wangu kwani hali hiyo itakuwa inatia zaidi shinikizo kwa wenyeji kuliko sisi’ alieleza Maximo.

Hata hivyo Maximo alikiri kuwa ili kupata matokeo yanayohitajika dhidi ya wenyeji ni lazima wachezaji wa Stars wajitolee zaidi kikmchezo kuliko walivyofanya katika mchezo dhidi ya Senegal.

‘Dakika kama 30 za mwisho tulihatarisha maisha ya wasenegali kwa kuwa tuliwashambulia huku tukionesha nia thabiti ya kusawazisha goli, malengo yetu hayakufanikiwa, sasa tuanhitaji kujifunza kutoka yale ambaye hatukuyafanya kwa ufanisi na kuyarekebisha ili jitihada zetu ziweze kuzaa matunda ambayo watanzania wanayataka’ alifafanua mtaalamu huyo raia wa Brazil.

Alibainisha hata hivyo kuwa kutokana na tembo wa Ivory Cost kuwa na maumbo makubwa kimwili amesisitiza wachezaji wa Stars kutilia mkazo mchezo wa kugongeana kwa kuwa wapinzani wana nguvu zaidi hivyo katika hali ya kunyang’anyana mipira Ivory Cost watafaidika zaidi.

‘Ili kuwamuda watu wa aina hiyo lazima tugongeane sana tena kwa kasi kwani kisayansi mtu mwenye umbo kubwa hawezi kukimbia kwa kasi.
Kuhusu kikosi chake Maximo anatarajiwa kufaya marekebisho kadhaa ili kupata matokeo mazuri.

Sehemu ya kiungo ukabaji(namba sita) inatarajiwa kuchezwa na Nurdin Bakari akichukua nafasi ya Geofrey Bony aliyeumia katika mchezo wa Sengal huku kiungo Kigi Makasi ambaye hakushiriki mchezo wa kwanza kutokana kuwa na kadi mbili za njano alizooneshwa katika michezo ya kufuzu, anatarajiwa kuwemo katika kikosi cha kwanza ili kuimarisha mashambulizi ya kutokea pembeni kushoto na kutumia vema mipira ya adhabu ndogo na kona.

Kadhalika huenda kijana mpya Mwinyi Kazimoto akapewa nafasi ya kucheza sehemu ya mchezo huo japo si kuanza.

Safu yote ya ulinzi ikiongozwa na nahodha Shadrack Nsajigwa akisaidiana na mchezaji mzoefu kuliko wote Salum Swed na mchezaji anayepigiwa mfano kwa kujituma, Nadir Haroub Cannavaro na Juma Jabu.

Henry Joseph, Mrisho Ngasa, Nizar Khalfan, Jerson Tegete, Haruna Moshi na Mlinda lango Shaaban Dihile bila shaka wataendelea kuaminiwa na kupewa nafasi ya kulitetea taifa, japo kwa kiasi fulani Haruna ambaye alitolewa mapema kipindi cha kwanza na nafasi yake kuchukuliwa na Mussa Hassan Mgosi alionekana kuwa na siku mbaya na kumfanya asitekeleze ipasavyo majukumu yake uwanjani aliyopewa na mwalimu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Mambo ya kijinga haya, hatuwezi kuwafunga Ivory Coast. Mimi naweka dau na mtu hapa. Sisi ni mabwege duniani nimeshasema mara nyingi ila watu hamuelewi, sisi mabwege jamani.

    ReplyDelete
  2. Kaka Michu na wadau wengine, tusaidiane toviti zitakazokuwa zinaonyesha game hili ili tulio nje ya Bongo tuweze kuendeleza uzalendo wetu huku tulipo. toviti mojawapo ambayo nahizi wataonyesha ni www.sunutv.com (ya Senegal), walionyesha game yetu na Teranga (kwa lunga ya Kifaransa). Vilevile kuna RTS1 , but huwa na matatizo ya sreaming. Nawakilisha. KaKa YeNu

    ReplyDelete
  3. Mdau wa kwanza anayeweka dau anavyosema "sisi mabwege" anajisemea yeye na nani? Maximo alivyofika alisema baada ya kuibuka kidedea dhidi ya Burkina Faso kwamba timu ilikuwa inashindwa kabla hata ya kuingia uwanjani kucheza. Ndio hayo mawazo ya kusema hatuwezi kuifunga Ivory Coast. Wao wanacheza 11 na sisi tutakuwa na wawakilishi 11. Lolote linawezekana. Tusubiri dakika tisini na kuiunga mkono timu. Tusipowafunga leo tutawafunga siku nyingine lakini sio kusema hatuwezi, hatuwezi, hatuwezi. Hizi fikra za hatuwezi ndio zinatufanya tuwe watu wa kutegemea misaada.

    ReplyDelete
  4. Wachezaji wa stars kama mnaingia kwenye hii blog.Sisi tunawaona kwenye screeen za TV na computer.Mnacheza vizuri sana kusema kweli lakini mnashindwa kubadilika na mchezo unavyokwenda.Nina uhakika mna formation nyingi.Dakika 20 za kwanza lazima mtakuwa mmeshajua mtu hatari ni nani(Lakini timu zote pinzani mmeshaziona),wanaweza kubadilika,msiingie kwa kukariri!Msichoke,halafu mnategeana.Nawakia game nzuri.Kipa DIHILE zungumza na mabeki,unakaa kimya sana afande Dihile.

    ReplyDelete
  5. Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya nanihii, (cjui ni Wilaya mpya ama ni vp) naomba kwanza unifikishie huu ujumbe kwa uongozi wa Channel Ten (African Media Group) haka ka-tabia ka kuwadanganya wapenda soka hapa nchini kuwa wanatuonyesha mpira live bila zengwe kaishe mara moja, inakera na naona kama vp waachane na issue za kuonyesha mpira maana wameshindwa na wanafikia kutudanganya hata kwa kipindi hiki cha utandawazi. Tunafahamu ni kiasi gani watanzania walio wengi wanapenda kuangalia mpira na hasa kipindi hiki ambacho Champions League imefikia hatua ya 16 bora. Kitendo cha wao kukaa na kujadili mechi iliyokwisha chezwa na kuturekodia si uungwana hata kidogo. Tangu mwanzo wa mwezi huu wanatangaza kuwa wataonyesha mechi za Champions League 16 tena na kauli mbiu yao ya Live bila zengwe, ni upumbavu mtupu wanaooufanya. Mfano mzuri ni jana mechi zimeanza saa 10:45 usiku kwa saa za kwetu (East Africa Time) wao wameanza kurusha saa 11:15 hii ikiamanisha kwamba ni recorded, hivi wanafikiri tu wajinga kiasi hicho?. Mimi ningeshauri tu kama vp wauchune tu wasilazimishe fani ambazo hawaziwezi. Hivi hawana watu wa kuwaandalia program kiutaalam mpaka wanadandia vitu wasivyoweza!! Pata picha cku ni fainali halafu mchezo ndio huu. Waache kutufanya sie wapumbavu wanapenda kujikwaza kwa vitu ambavyo hawaviwezi. Cha mwisho ushauri kwa Maximo ni kuwa soka la Bongo awaachie wabongo wenyewe alipofika panatosha. I hope msg ime-delivery fasta kuliko hewa inavyosafiri.

    ReplyDelete
  6. Taifa Stars! I wish you the best during today's game. This would be a decisive game, if you lose the game against Ivory Coast today, surely, you will be coming back home with shame! Our State President has indeed done much kwahiyo msimwangushe rais wetu. Leo mcheze kufa na kupona, tusiwe kichwa cha mwendawazimu, yatosha sasa:
    Alex Mawazo
    Barrick Tulawaka Gold Mine, Kagera.

    ReplyDelete
  7. Jamani zile website za online zimwageni tena basi hahahaah tuone timu yetu Wengine tunafanya kazi usiku Ula kazi ya security computer ipo leo wacha wezi waibe teh teh teh. natizama Taifa Nyotaz. Taifa Stars 2 ivory 0 leo tunataka kuona winger zote zinatumia hasa ya kulia iwache kuanguka anguka.

    ReplyDelete
  8. Much as I would like Taifa Stars to win,surely,they will be facing A Wounded Buffalo which makes the game even more difficult to predict the outcome!I cant see how Ivory Coast will consent to yet another Humiliating Defeat at their own Home Ground and them being the Hosts of this year's tournament!Jamani sisi bado!Mpira tunauweza,lakini The Winning Tricks of the Game hatuzijui;Hatuna A Winning Strategy!Katika Timu ya Soka ya Kimataifa lazima uwe na set mbili za wachezaji.Maumbile ya Wachezaji lazima yawe ya Kiriadha (Masculine Physique);Wafungaji kule mbele lazima wawe wenye Mbio kama za 100meters marathon!;MiddleField lazima iwe na watu wenye Kifua cha WAOGELEAJI NA WAPIGA MBIZI!;golikipa lazima awe mtundu kama Nyani;Formation ya timu lazima ibadilike kama Kinyonga kadri kasi ya mchezo utakavyo kwenda;Lazima pawepo na Special Substitutes wa dakika za majeruhi zile za dakika 15 za mwisho wenye uchu wa kufunga kama Simba;Ball possession na accurate short passes ni muhimu kwa timu inayotafuta ushindi nk.Hebu sasa nieleze timu yetu imesimamia wapi kati ya sifa hizo nilizo zitaja?Lazima tuwe tayari kuwauza baadhi ya wachezaji wetu hata ikibidi kwa bei ya karibu na bure mradi tu wapate timu Ulaya katika hata likiwa daraja la nne ili waibe ujuzi wa kule na kupata uzoefu zaidi ili wakija huku wao wawe waalimu wa wenzao wawapo uwanjani!Wachezaji wakisha ingia uwanjani,Kocha hana ujanja tena,hawezi kuwafundisha zaidi ya kile alichofundisha.Lazima wachezaji wenyewe wawe na uwezo wa kubadilisha kasi ya mchezo,kubadili formation kila itakapobidi ili kuwadhibiti wapinzani wao!Kapteni wa Timu lazima awe mchezaji aliyekamilika katika idara zote!Wapinzani wakiwa warefu na miili mikubwa basi pasi ziwe fupifupi,za kasi na uhakika!Midfield lazima iende mbele na kurudi nyuma,3-5-2,itafaa zaidi;mengine ni kutoka kwa kila mchezaji kujituma.----kocha wa zamani,tonnie------.Tunaomba kila la heri Taifa Stars ishinde,lakini wenyeji hawatokubali kupoteza mechi nyingine tena nyumbani na wao wakiwa ndio wenyeji wa mashindano.Tukiwazidi ufundi,wao watatumia hata nguvu ya ziada ya washika bendera ili watufunge!Ukweli ndio huo.

    ReplyDelete
  9. http://www.tv-direct.fr/live_lc2.php


    wadau kaaaaaaaaaaaazi kwenu online game hiyo Ivory Coast 0 Tanzania 3 Inshaallah.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...