mashabiki wa taifa stars wakiwa wamenywea baada ya zambia kusawzisha bao dakika ya 93 katia ya tano za ziada zilizoongezwa wakati Taifa Stars ikiwa inaongoza kwa bao la dakika 88 la tutazzz.
baada ya ivory coast kutoka suluhu ya 0-0 na senegal ndiyo kusema taifa stars wanapanda ndege ya kwanza kurejea bongo baada ya kukosa kuingia nusu fainali kiduuuchu.
nawashangaa wadau wengine wanaoniuliza matokeo ya ligi kuu ukerewe wakata mie macho na masikio vyote vilikuwa ivory coast. isitoshe niko kwenye mnuso wa harusi na blackberry yangu betri imeisha na hii ni post ya mwisho kwa sasa hadi baaaadayeeeeeeeeeeeeeeeeee.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Kwa kuanzio co mbaya,ila vyombo vya habari vikiongozwa na kina michuzi,tafadhalini wapeni support wachezaji kwa jitihada zao mpaka hapo na co kuwakatisha tamaa kama kawaida yenu kwa vichwa vya habari kama KICHWA CHA MWENDAWAZIMU chanyolewa tena na maneno ya kejeli kwa ujumla.
    Kifupi hata mwanao akifeli na kumdharau kwa lugha za ajabu kamwe hawezi kufanya vizuri na atakuwa na donda daima,lakini akichemsha ukamrekebisha alipokosea na kumtia moyo hakika next time atafanya vizuri,otherwise soka linakufa kutokana na vyombo vya habari pia,kama ENGLAND vile.

    LiverFool yetu tumeng'oa Rick Parry,point 3 tumekosa,kifuatacho.............
    ubingwa tuna....................

    ReplyDelete
  2. Chelsea mmeponea tundu la sindano.
    Arsenal ndugu zangu droo zinakera jamani ooh,ukijiona hufungwi ndo usishinde??
    LiverFool mmmmmh droo 10 kama Arsenal,ila kufungwa kutawaamsha ipasavyo but whatch out Red Devil they r on song,kwa mchezo huu mtalabwa hata zaidi ya Chelsea alivyofanywa maana jamaa wako kwa kasi ya kustaajabisha,wako kikazi zaidi ya timu nyingine,yeyote anayepangwa anafanya mambo,ila be zahar na wenzio wanashindwa kutumia chance wanazopata za kucheza,maajabu baadae atalalamika hapangwi,asaidiwaje??

    ReplyDelete
  3. Michuzi,

    1. Sikiliza, watu wanaofuatilia ligi za Ulaya na kusahau mechi zinazohusu taifa letu ni wagonjwa wa akili.

    2. Namuonea huruma Maximo, anaharibu CV yake, sisi ni mabwege kama nilivyosema awali wakati michuano inaanza. Wachezaji wetu hawana juhudi na uzalendo wa kutosha inabidi mpaka Maximo awaweke nje na kupanga ambao hawajakomaa na matokeo yake ndiyo haya. Tuna tatizo la kitaifa la kutokuwa makini na mambo muhimu. Sisi ni mabwege ndio maana tuna kila kitu duniani lakini ni maskini kuliko hata Rwanda ambayo ina milima tu.

    3. Hatuwezi kufika kokote kama uswahili na ushikaji utaendelea. Lazima tubadili kabisa maana ya mpira, mathalani, kuna sababu gani ya vibabu vya mitaani na waswahili-swahili kushika uongozi wa timu zetu? Haya ni mambo ya kufanywa na watu wenye upeo, elimu na wasio na njaa. Ndiyo maana wizi kwenye vilabu hauishi na makomandoo hawaishi. Sisi mabwege.

    Kwa herini, hatufiki kokote mpaka tubadili mtazamo wetu kwenye kila jambo. Vinginevyo tutabakia kuwa mabwege. Baada ya miaka mitatu ya juhudi za kufa na kupoka, tuko pale pale. Hatuwezi hata kuzifunga Kenya na Uganda!!! Hovyoooo!

    Mdau.

    ReplyDelete
  4. Pole sana Kaka, team yako ya taifa imefungasha virago kurudi nyumbani na Liverpool ndiyo hivyo tena!! Hii week-end ni mbaya sana kwako.

    ReplyDelete
  5. Tumesikitika na kujaa huzuni...hongera mababe ya taifa...'despite early exit you have made us proud'!!!

    ReplyDelete
  6. Jamani wabongo kwa nini hamtaki kukubali ukweli? TZ hakuna mpira hata kidogo. Yaani hiyo mechi yenyewe ilikuwa hovyo kichizi. Kwanza hakukuwa na formation yeyote, yaani ni sawa tu na kumtizama Michuzi akicheza pale Leaders club siku ya jumapili huku akishika chupa ya Mirinda/bia. Bongo mpira ziro kabisaaaaaa. Mungu hawezi kukupa vyote, sie ni nchi ya kitalii na hiyo ndiyo baraka yetu lakini boli....zirooooooooo!

    ReplyDelete
  7. tusimlauumu kocha wala wachezaji wadau!!! japokuwa sikubahatika kuiona hiyo game!!!
    Vijana walijituma sana na wameonyesha matumaini katika soka ndani ya Tanzania,isipokuwa bahati aikuwa yao na mambo ya Experiance katika mashindano makubwa kama haya yanayoendelea, kikubwa ni kutoa maoni ya kuijenga stars yetu, ni kweli wengi tumeumia sana lakini tusife moyo kwani nina imani kubwa sana tutakuwa mabingwa msimu hujao ila timu isibadilike sana, tujipe moyo tutafika tu, kwani safari ndefu na ngumu ndio yenye mafanikio!!!!!

    Mdau canada!

    ReplyDelete
  8. aisee nyie kamavile makocha wa zamani msijifanye kukosoa wenzenu wakati hata nyinyi pia huwa mnakosolewa sio fresh sio acheni kuilalia mlango wazi bahati ya mwenzeni amta fika kokote unafiki tuu kocha wa timu ya taifa ndio huyo huyo na strs itawika tuuaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
    Matambalale!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  9. Miaka mitatu ni muda mfupi sana kisoka kuweza kufikia tulipofika. Mara ya mwisho tulipocheza fainali za mashindano ya Afrika ni 1980. Timu ya 1980 iliundwa na wachezaji walioanza kupikwa miaka ya mwanzoni mwa 1970...miaka zaidi ya mitano hadi kumi ndio matunda yakaonekana.
    Huwezi kushinda kila siku na kila mechi. Tumecheza mechi tatu, tumefungwa mechi ya kwanza tuliyocheza tukiwa bado washamba wa michuano hiyo. Hiyo ni dalili nzuri. Tujipange kuondoa mapungufu tuliyoona tunayo huko badala ya kukata tamaa kwamba hatuwezi. Mbona inadaiwa Afrika hatujui kucheza mpira wa kikapu lakini kuna mcheza kikapu wa kibongo anatesa kikapu kwenye vyuo vikuu vya Marekani?

    ReplyDelete
  10. Kocha Maximo, wachezaji wote wa taifa stars, viongozi wa TFF, wadhamini pamoja na wapenzi wote wa timu yetu ya taifa ninawapongeza kwa kuifanya tanzania nayo ionekane kisoka. Tusikate tamaa kwa matokeo tuliyoyapata kwani huu ndiyo mwanzo wa kujipanga vizuri ili tufanye vizuri zaidi hapo baadae. cha msingi ni kuwa na muono wa mbali ili tukianza kutoka basi isiwe tunabahatisha.
    Nawaomba wabongo tuache kuikandia timu yetu ina mchango mkubwa sana katika kuitambulisha nchi yetu kimataifa kuliko hata balozi zetu. Pia kumbukeni maendeleo hayaji siku moja tu, ni mchakato unaohitaji muda, rasilimali na pia ujasiri wa kukabiliana na vikwazo vinavyokatisha tamaa ili tusifikie malengo tuliojiwekea. HONGERENI SANA mashujaa wetu wa TAIFA.
    MUNGU IBARIKI TANZANIA
    MUNGU IBARIKI AFRIKA

    ReplyDelete
  11. Jamani kwa mtazamo wangu timu yetu ya Taifa imejitahidi sana,sasa tujitahidi iwepo kwenye mashindano hayo tena na tena, nadhani tuwe na malengo kuwa ndani ya miaka mitatu tuwe na wachezaji wetu 20 watakaocheza soka la kulipwa Ulaya,hawa watatia chachandu katika timu yetu.
    2.Iwe sheria kuwa kila club inayoshiriki ligi kuu na daraja la kwanza iwe na academy moja.Na club kubwa kama za Simba na watani wangu Yanga wawe na academy mbilimbili. Pia kila wila iwe na academy moja ya kukuza soka.
    Tukifanya hivyo tutasonga mbele sana ndani ya miaka kumi.

    Watanzania wenzangu,pia tujitahidi sana kwenye nyanja zote,kule kwetu Kilimanjaro tuna msemo unasema nayezie nyuma irevusha teri*yaani hata ile ngombe ya mwisho inapotembea utaona vumbi linatoka.Maanayake,tusiache kutembea na kujitahidi na kuanza kusimama,hatutafiki,twende mbele tutaweza.
    Tujipe moyo,tutafika.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...