Mtangazaji mahiri wa michezo wa TBC Baruani Muhuza akitangaza live mechi ya Stars na Ivory Coast. Maulidi Baraka wa Kitenge wa ITV na Radio One yuko pembeni akifuatilia mchezo
Katibu Mkuu wa Tff Fredrick Mwakalebela wakiwa na furaha na watanzania walioko Abidjan kuishangili stars baada ya gemu usiku huu
mashabiki wakishangilia taifa stars mara tu baada ya kipyenga cha mwisho kulia dakika chache zilizopita huko abidjan katika wanja la felix houphet boigny. kwa niaba ya wadau wote globu ya jamii inatoa shukrani za dhati kwa mdau huyu anayetuletea vitu laivu toka huko. mdau ubarikiwe kwani umeweza kutuweka karibu na huko mliko!

NA MPIRA UMEKWISHAAAAAAAAAA!!!!!!!

TAIFA STARS INATOKA KIFUA MBELE KWA KUIDUNGUA IVORY COAST BAO 1-0 NA KUFUFUA MATUMAINI YA KUENDELEA MBELE KATIKA MICHUANO HII YA CHAN.

STARS INAONDOKA NA POINTI 3 NA JUMAMOSI ITAPAMBANA NA ZAMBIA MJINI BWAKELI KATIKA KIPUTE KINGINE AMBACHO IKISHINDA ITAKUWA NA POINTI 6 NA IKITOKA SARE ITAKUWA NA POINTI NNE NA KUENDELEA KUWA KIONGOZI WA KUNDI HILI KWANI ZAMBIA WALITOKA TASA YA 0-0 NA WANA POINTI 4 (SAMAHANI SIO MOJA KAMA NILIVYOBOFYA AWALI). NDIO KUSEMA LAZIMA TUWAPIGE ZAMBIA (SIO SARE) KUWA NA UHAKIKA WA KUSONGA MBELE.

WADAU SAMAHANI HIYO LINK YA AWALI ILONESHA GEMU KWA MUDA KISHA IKAKATA.

ILA KULIKUWA NA HII
NIMEIPATA MAPEMA ILA SEMA MTANDAO ULIPATA KWIKWI MARA TU BAADA YA HAFTAIMU. ILA SI VIBAYA UKIITUNZA LINKI HIYO KWA AJILI YA GEMU ZIJAZO KWANI LIBENEKE NDIYO KWANZAAAAAA LINAANZA....
SAMAHANI SANA WADAU
MATOKEO YOTE NA RATIBA ZOTE





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 46 mpaka sasa

  1. hahaha ndio mie nilitaka kushangaa leo nimetizama game half time nimetoka narudisha katika hiyo web uliyoweka mara sioni tena Hongera Taifa stars umeona sasa winger zikicheza ndio striker zina tesa, Waambie Taifa stars wasiogope kushambulia kuzani watafungwa, Zambia njoeni sasa Zambia 1 Taifa Stars 4. Ngasa kichwa kama Duwa bin Said manake watu wasije kusema kama Drogba au Torres Au Berbatov hapana kama Kizota au dua bin said. from Haji Tumbo.

    ReplyDelete
  2. kaka michuzi...habari yako mkuu

    tumezipokea taarifa hizi kwa furaha sana kutoka huku bwawa la maini....

    amakweli taifa stars ni mziki mnene....tukiamua kufanya kweli tunafnaya

    Mungu zidi kuibariki Taifa Stars
    Mdau Bwawa la maini

    ReplyDelete
  3. Ho Ho Ho Ho Hoooo! Yebaaaaa!
    Kuna mdau alisema Watanzania mabwege hatuwezi kuifunga Ivory Coast akatishia nyau eti angeweka dau kwenye globu ya jamii. Angeliwa!
    Shughuli ndio imeanza lakini. Ivory Coast hawana ubavu wa kuifunga Senegal kwa hiyo tunalazimika kuwafunga ndugu zetu Wazambia ili tusonge mbele. Yote yanawezekana ila mechi itakuwa ngumu kuliko mechi zote duniani. Maximo ana historia ya kuwatemesha wenzie vibarua-Burkina Faso, Msumbiji. Uwezekano wa safari ya jamaa wa Ivory Coast kuwa imeiva ni mkubwa.

    ReplyDelete
  4. STARS JUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUU
    ASANTE MKUU WA WILAYA KWA UZALENDO.KWANI NAFIKIRI UMEWEKA BWAWA LA MAINI PEMBENI NA KUANGALIA MPIRA WALIOCHEZA VIJANA.WALIOPONDA JUZI, UTASIKIA WANASIFIA. MPIRA HAUJENGWI SIKU MOJA. ASANTE MICHUZI, TUKUOMBEE FURAHA MARA MBILI NA B/MAINI WAFUNGE. SAFI SANA.

    ReplyDelete
  5. MICHUZI ACHA KWIKWI ZA KUTAIPU... ZAMBIA HAINA POINT MOJA WABONGO WSIBWETEKE NGOMA BADO NZITO TUNAWEZA KUHITAJI MIUJIZA

    ReplyDelete
  6. ama kweli wadau mtu si mbwa!

    ReplyDelete
  7. Rekebisha hapo, Zambia wana point nne na si moja, tukiifunga zambia halafu Ivory Coast waifunge au kutoa sare na Senegal sisi tunakuwa vinara wa kundi. Ila je Zambia watakubali???,

    ReplyDelete
  8. MICHUZI ACHA KWIKWI ZAKO ZA KUTAIPU....ZAMBIA HAWANA POINTI MOJA KAMA ULIVYOTAIPU JITAHIDI KUWA MAKINI WAKATI UNATOA HABARI...WABONGO WASIBWETEKE NA USHINDI WA MECHI MOJA PENGINE TUTAHITAJI MIUJIZA KUSHINDA NA KUENDELEA MBELE????????

    ReplyDelete
  9. chenga tumewala na kufunga tumefunga-said bargash uk

    ReplyDelete
  10. Michuzi nadhani umeteleza kidogo kuhusu twakimu za mwelekeo wa timu yetu, Zambia tayari wana pointi 4.

    Walishinda goli 3 dhidi ya Ivory Coast, wametoka sare ya 0-0 na Senegal.

    Mathematically speaking, Zambia na Senegal ndiyo zina nafasi kubwa zaidi [zote zina pointi 4 ingawa Zambia ina idadi kubwa zaidi ya magoli ya kufunga]- japo Ivory Coast na Senegal itakuwa mechi ngumu kama itakavyokuwa kwa Zambia na Tanzania.

    Zambia na Senegal zitahitaji sare, wakati Tanzania inatakiwa kushinda na pointi tatu - full stop.

    ReplyDelete
  11. kama Staz ikitoka sare na Zambia haitaongoza kundi. Sare itaipa Staz point 4 wakati Chipolopolo watakuwa na point 5 maana walishinda mechi ya 1 na wakadraw mechi ya 2.

    Hongera kwa ushindi watanzania wote; kijana wangu Ngasa katutoa kimasomaso. Kinachotakiwa sasa ni kushinda mechi ya mwisho

    ReplyDelete
  12. Neno..
    Cheupe!!

    ReplyDelete
  13. bonge moja la kichwa ngassa kafunga alafu awali nilimponda kwa ufupi wake, na tz kucheza mipira ya juu sana! lakini bado mi nadhani mipira ya juu tusicheze sana. hongera stars !!!!
    baraka

    ReplyDelete
  14. Du damu nzito kuliko maji nimefurahi kiasi cha kusahau matatizo yangu nilionayo mungu yupo unapojitahidi satrz wamefanya miujiza kuzifunga timu za west home kwao ni ndoto kwetu na am sure ivory coast itamtoa mavi senegal na sie tutashinda zambia hongera kwa mtandao wa mkuu wa wilaya itabidi upande cheo uwe wa mkoa manake hapa nipo na wa ivory coast kibao na wapopo wamenyamaza kimyaaa walikuwa wananibeza wanasema sie hatuna socer tunajua mademu tu hahah wamekoma sasa Mdau RSA marine patrol on the way to tz coast to coast

    ReplyDelete
  15. Hongera sana Taifa Stars.

    ReplyDelete
  16. Yani leo imenikumbusha yalee!! @##@##%%^^@@ zao wanazima taa! Wadau mpo hapo?? Jamaa baada ya kuona kimeota wakazima mitandao!! Dah! Nadhani sasa watanzania mmeona jinsi Wawest wasivyo watu! Sie wakija kwetu aah mtawapamba tunawaramba hadi miguu lakini si mmeona leo!! Yani kwa ufupi hawataki wachzaji wetu waonekane huko majuu lakini leo ndio leo punda wale!! Piga bao nyumbani kwao mmms@@@@@h!!
    Kijana Ngassa safi sana sasa safari ya PSV inanukia, watake wasitake dogo anaondoka, ila ukirudi home angalia mamiss wakibongo si unajua wote watataka waonekane katika luninga mzee ukiwa PSV. hahhahhha yani umenipa raha sana kijana. Hongereni wachezaji wote na benchi zima la ufundi. TAIFA STARS OYEEEH!! SASA BADO CHIPOLOPOLO LAZIMA TUTAWAFANYA VIPOLO!!

    ReplyDelete
  17. Jamanii eeh naomba wote tuingia katika website ya WAZAMBIA nao wanatoa comments ili tuwatie kiwewe. Nimekuwa nawapiga jambajamba wiki nzima sasa inaonekana wanaogopa. Please ingia www.zambianfootball.net

    ReplyDelete
  18. BONGO OYEEEEEEEE!! STARS OYEEEEEEEEE!! MUNGU IBARI STAR'S HAPO TUTAKAPOKUTANA NA MZAMBIA TUMTANDIKE KAMA ILO NA KUWEZA KUSONGA MBELE WADAU WOTE HAPA UGIRIKI TUNAFURAHAA SANAAAAA!!TUNAO UWEZO NA INNSHALLAH MUNGU ATATUSAIDI ILA SAFU YA MBELE JITAHIDI VIJANA KWA .....MASHUTI YA NGUVU NA YA MBALI!!!! TUPATE USHINDI

    ReplyDelete
  19. Benayoun..wenye kombe lao wameanza kazi..man u mnasindikiza subirini makombe yenu ya kuku....!! bwawa la maini nawaaminia...ndani ya santiago bernebeu...acha kabisa...man u mpooo...na mpira wenu mbovu baina yenu na inter....liver inapiga ndani na nje...!! LIVERPOOL...ULL NEVER WALK ALONE..ALONE..EHHHH..ALONE..! Taifa stars oyeee!!

    ReplyDelete
  20. SASA TUNAPOELEKEA NI PAZURI KISOKA VIJANA MNASTAHILI PONGEZI ZA NGUVU!! STAR'S OYEEEEEEEEEEE BY CHAPAKA -GREECE

    ReplyDelete
  21. Safi sana stars kaza kiatu kwa zambia ili tuzidi kusonga mbele.
    Nilibahatika kuiona mechi ya kwanza na hii ya pili kwa kweli uwezo tunao, nia, pamoja na sababu.
    Way to go stars!!!!!!!!!!!!!

    Mdau canada!

    ReplyDelete
  22. Jamani mpira nimeutizama Ule na Senegal tumecheza vizuri kushinda Huu tulioshinda inaonesha mwanzo na senegal ilikuwa hatujawajuwa bado kutokana na game wote washacheza tumesomana sasa Zambia tuwapige 3-0 ndio kilichobakia wachezaji watowe woga wakushambulia. Cross ziwe za chini chini winger lazima kuzitumia sana. Ngassa Kichwa Benayoun alitizama kichwa cha ngassa kajifunzia kwa mtanzania Michuzi leo furaha tu. Kimoja tuuuuuuu. From Pazi.

    ReplyDelete
  23. baab kubwa stars kaza buti tena kwa mzambia ! by chapaka ugiriki

    ReplyDelete
  24. stars hongereni na ongezeni bidii, ila sisi wa bongo tunahitataji kupepewa stars ikishinda iakuwa yetu wote kama alivyosema KP ikifungwa ianakuwa ya Maxmo nimesoma comment hakuna hata moja inamtaja maxmo ila ikifungwa tu kila mtu maxmo leo hakuna anayemtaja. tuache usenene kama wa chelsea

    ReplyDelete
  25. KWA WABONGO WOTE TULIOKUWA HAPA UMANGANI LEO NI FURAHA TUPU YAAN ISIYO NAMFANO TEAM YETU IPO SWAFI SANA ILA MBELE TU Mashambulizi yanaitajika katika 18 ukifika baab kubwa star's by MZEE PAZI WA HAPA UMANAGANI

    ReplyDelete
  26. Yote tisa....

    Hiyo bendera ya picha ya mwisho imekaaje wadau? Nadhani inabidi kuanzisha somo la bendera ya nchi yetu kwamba kijani inakaa juu na buluu inakuwa chini siku zote!

    ReplyDelete
  27. HONGERA STARS.
    1:TUNAOGOPA KUSHAMBULIA
    2:TUNANYANG'ANYWA MIPIRA MIPIRA KIZEMBE.
    3:PASS NYINGI HAZINA MACHO
    4:KIPA HANA MAAMUZI MAZURI,MWOGA,HAZUNGUMZI NA MABEKI WAKE
    5:KUZUIA KROSI ZA JUU GOLINI INATUSUMBUA(KURUKA VICHWA KUHAMISHA CROSS HATARI)
    6:VIUNGO WENGI WANASHINDWA KUMILIKI NA KUINGIA NA MIPIRA KWENYE 18,KAMA WENZETU WALIVYOKUWA KUWA WANATUPELEKESHA.
    8:BEKI ZETU GENERALLY,NAWAPA 90% YA MARKING.
    HII MICHUANO IMETUPA PICHA KUONA HASA NANI NI WACHEZAJI WAZURI,MANAKE WENGI WA WACHEZAJI WETU WANAONEKANA HAPA BONGO WAKITESA TIMU NDOGO ZA ASHANTI,POLISI,N.K

    ReplyDelete
  28. mh
    wakifungwa mikelel weee matusi lukuki adi maximo,wakifunga kila mtu heee ooooo sijui zagazaga gani!
    watu mnanchekesha kweli,,,

    ongera vijana ndo ivo taratibu tutafika

    ReplyDelete
  29. ugonjwa wangu ni wanaume wacheza mpira,,,,

    awa ndo wanaumeeeee,,mmentia raha nyie!!!

    Mungu ibariki Tanzania
    Mungu ibariki watu wake

    taratibu ndo mwendo

    ReplyDelete
  30. NGASA NJOO NIKUPE "ZAWADI YA USHINDI" KABISAAA FOR YU EXCLUSIVELY

    BAADA YA KAZI ZURI ULOONYESHA WAITAJI POZO,,freeeeshiiii mie tu nnalo

    njoo kiboy changu

    ReplyDelete
  31. ha, ha, ha Watanzania bwana tukishinda ndio utaona kila mtu anapiga picha na kujishau. Tulipofungwa hakuna hata mmoja aliyejishebedua ila haina tabu ndio tabia yetu ya Unafki wala sishangai.

    Kuhusu vijana wetu TZ STARS jana walifanya kazi nzuri sana na dua zetu zitazidi kuwatangulia kwa kila dakika watakayokuwa huko mpk kurudi kwao. KUSHINDA, KUTOA SULUHU AU KUSHINDWA NI MPANGILIO WA MATOKEO NA MAJAALIWA. TUSIONE AIBU TUNAPOSHINDWA MAANA BADO INABAKIA KUWA NI TIMU YETU TENA YA TAIFA

    ReplyDelete
  32. Quotes
    Georges Kouadio (Coach, Cote D’Ivoire)
    “I am very disappointed we lost again. We had never anticipated for such fortune during the competition.
    “We attacked throughout the game, but the Tanzania defence was up to task. They were tactically better and deserved the victory.”

    Marcio Maximo (Coach, Tanzania)
    “My players were tactically disciplined and the result showed. My team is a young team with an average age of 22.
    “The experience is very good for my team, and we will build on that in subsequent matches.”

    BRAVO MAXIMO, WAOSHA VINYWA KINA MZIRAY AIBUUUU...

    ReplyDelete
  33. Maximo led Tanzania to a memorable victory......CHAN joy 4 Tanzania
    http://news.bbc.co.uk/sport2/hi/football/africa/7780386.stm

    ReplyDelete
  34. KWELI MPIRA UNAWEZA KUIUNGANISHA JAMII IKAWA KITU KIMOJA. YAANI NI AJABU WATU WOTE LEO KATKA HII BLOG YA JAMII WAMEKUWA KITU KIMOJA.HAKUNA MATUSI HAKUNA KUPONDANA.NADHANI MUNGU ALIZILETA CHANGAMOTO DUNIANI ILI TUPIMANE UPEO,UWEZO NA MAWAZO.HEBU FIKRIA KAMA SISI NDO TUNGEKUWA WA IVORYCOAST.
    JE TUMEJIFUNZA NINI?
    ZK

    ReplyDelete
  35. jamani kama milikosa mechi za chan...angalia kupitia www.myafricanfootball.com

    siyo lazima ulipe, we register tu na unaweza kuona mechi zote za stars. utatumiwa password kwenye email account yako amboyo ndiyo utakuwa unatumia kwenye hiyo website kucheki mechi

    quality nzuri kama unachecki kwenye t'v vile!!! Mchuzi labda u post hi msg kwenye blog kabisa siyo kwenye comments tu

    ahsante

    ReplyDelete
  36. Ndugu wananchi,
    Watanzania wenzangu,
    Kwa pamoja ,tunasema, TAIFA STARS IKISHINDA, INAKUWA YETU SOTE, LAKINI IKIFUNGWA INAKUWA YA MAXIMO PEKE YAKE>
    Ndugu wananchi,
    Ningependa kusisitiza kuwa ili Taifa Stars Iendelebe kuwakamua zaidi lazima tumpe support Maximo, Wachezaji na Benchi zima la ufundi,
    Ndugu wananchi , bila shaka mmeona wenyewe kandanda la vijana linavyoendelea kupasua anga na kuleta Heshima ya Tanzania nzima Africa na Ulaya.
    Mungu ibariki Tanzania
    Mungu ibariki Taifa Stars
    Mdau
    Nelspruit
    RSA

    ReplyDelete
  37. Mhh, naona kocha alipumua, manake tungefungwa,mmmh,sijui
    M3

    ReplyDelete
  38. Michuzi usibanie hii kila mtu asome jinsi wabongo tulivyo wanafiki tukifungwa..
    Maximo adaiwa hana uwezo zaidi ya hatua aliyoifikisha Taifa Stars
    Na Mwandishi Wetu

    MCHAMBUZI wa masuala ya michezo, Hussein Sappi amesema tukubali ukomo wa kocha wa Taifa Stars, Marcio Maximo na staili ya soka anayofundisha timu haiwezi kufika mbali.


    Akizungumza katika kipindi cha Kumepambuzuka cha Radio One jana, Sapi alisema makocha wa Brazil wengi hawana rekodi katika ulimwengu wa soka zaidi ya nchi yao.


    Alisema Brazil wazuri kwa wao wenyewe lakini hawana rekodi nzuri duniani.


    “Mimi nadhani wakati umefika sasa tubadilike, tuangalie Ulaya Mashariki, kule tunaweza kupata makocha wazuri na hata soka yao inajulikana.


    “Tunakubali kuwa Brazil wana makocha wazuri lakini kwa faida yao, wapi kuna mafanikio kwa kocha wa Brazil? Tunaona Afrika Kusini inavyoyumba.


    “Kulikuwa na Felipe Scolari, alikuwa Ureno, hakuna kitu, kaondoka akaenda Afrika Kusini, akatoka akaja Chelsea, na sasa hayupo, kuna nini pale. Angalia makocha wa Hispania, Ufaransa, Uholanzi, Russia, Jamhuri ya Czech wapo na naamini tunawamudu...,” alisema.


    Akizungumza huku akionyesha kukerwa, alisema: “Isije kufika wakati tukapigana mawe Uwanja wa Taifa pale, mimi hili nalisema kama Mtanzania mwenye haki ya kuzungumza langu na sidhani kama Maximo anatufaa tena,” alisema.

    ReplyDelete
  39. Na huu mwingine ni unafiki ulienda shule


    Kocha Mziray adai mfumo wa Maximo unakwaza wachezaji
    Na Dorice Malyaga

    ALIYEKUWA kocha wa Taifa Stars, Syllersaid Mziray, amesema mfumo anaotumia kocha Mbrazil Marcio Maximo ni mgumu kutokana na uzoefu mdogo wa timu yetu ya Taifa.


    Akizungumza jijini jana Mziray alisema timu ya taifa mpaka sasa ina uwezo mkubwa wa kufanya vizuri kwenye mashindano yoyote mpaka sasa cha msingi ni kubadilisha mfumo unaotumika sasa na kuhakikisha wachezaji kushirikiana katika kuzuia na kushambulia kwa pamoja.


    Alisema mpaka sasa kwenye michuano ya CHAN anaipa namba moja timu ya Zambia kutokana na staili wanayoitumia wakishirikiana katika kuzuia na kushambulia kwa ujumla huku wakitumia pande zote mbili na pasi za uhakika.


    Mziray alisema endapo timu ya Tanzania ingefanya mashambulizi kama ya Zambia ilikuwa na uhakika wa kushinda mechi yao dhidi ya Senegal iliyopigwa bao 1-0. Stars jana ilikuwa ikicheza na wenyeji Ivory Coast.


    “Kitu kingine ni kuingiza wachezaji wazuri, katika dakika za mwishoni ili kufanya mashambulizi hii pia inachangia kutopata magoli kwa haraka... Wasenegal walitushambulia kipindi cha kwanza na wakafanikiwa kupata goli lakini kipindi cha pili walicheza kwa kujihami na ndiyo maana hatukuweza kupata nafasi ya kufunga,”


    “Stars itafanya vizuri endapo itabadili mfumo unaotumiwa sasa mtindo huu wa kucheza 3,5,2 unapoteza mipira mingi kutokana na viungo kuwa wengi hali ambayo inasababisha safu ya ushambuliaji kufa'' alisema Mziray.


    Akiuzungumzia ubora wa Maximo alisema ni kocha mzuri mwenye kila namna ya kuigwa na makocha wote kwa kuisaidia timu yetu kufikia hatua iliyofikia sasa kwa kuonekana katika ulimwengu wa soka na anapongeza wadhamini na taifa kwa ujumla kwa kuinga mkono Taifa Stars.


    Hata hivyo, Syllersaid, aliwataka Watanzania kutokuwa vigeugeu na kusahau kwa kipindi kifupi matokeo na mwenendo wa timu ya taifa.


    Mziray alisema kuna haja ya kuwa na mipango ya muda mrefu katika kuitengeneza soka ya Tanzania lakini si kuwa na mipango ya kukurupuka, kuwa unalala ukiamka unataka ushindi.

    ReplyDelete
  40. Wadau kweli hawa wanajiita "wachambuzi wa kandanda la TZ" na makocha wanaojivunia uzalenda ambao haunufaishi Taifa Letu la Kijani,Bluu, Nyeusi na Njano wakati wa kuwasikiliza na kukubali yote wanayosema umepitwa.

    Ni kama sayansi ilivyopitwa na Teknolojia, Huyo anayejiita Sappi kweli ana Uhuru wa Kujadili lakini "Kwa nini hataki ku-appreciate uwezi na mcha wa Huyu Mbrazil Maximo kwenye soka la TZ?" Mwalimu Mziray yeye ndio hata asiseme, anyamaze kwani Mwalimu Mziray ni miongoni mwa wasomi wa hali ya juu kwenye taaluma ya Michezo hasa soka, Tatizo taaluma yao hawaitumii on Field of (he/they dont practice), matokeo yake ndio hivyo kiwango cha soka kinadondoka mpaka kwenye matope, Laiti kama Kina-Mziray wangetumia uwezo na nafasi zao positively, wala tusingekuwa hapa tulipo kisoka, so Plz,Plz Watanzania wenzangu, tuwatazame vema hawa wanaojiita "Watu wa Mpira"
    Nwakilisha.
    Mungu ibariki Tanzania
    Mungu ibariki Taifa Stars
    Mdau
    Nelspruit
    RSA

    ReplyDelete
  41. Mdau wa mpumalanga umesema kweli kabisa

    ReplyDelete
  42. Michuzi, Anonymous wa 26.02.09- amemzungumzia Felipe Scolari, kama kocha aliyewahi kufundisha Afrika kusini.Hapana hajawahi kabisa kufundisha katika nchi hiyo. nadhani alikuwa na maana ya ALBERTO PEREIRA.
    Hapa chini ni historia ya maisha ya ukocha ua Scolari:

    Coaching Career:

    1982 CSA
    1982–1983 Juventude
    1983 Brasil de Pelotas
    1984–1985 Al-Shabab
    1986 Brasil de Pelotas
    1986–1987 Juventude
    1987 Grêmio
    1988 Goiás
    1988–1990 Al Qadisiya
    1990 Kuwait
    1991 Criciúma
    1991 Al-Ahli
    1992 Al Qadisiya
    1993–1996 Grêmio
    1997 Júbilo Iwata
    1997–2000 Palmeiras
    2000–2001 Cruzeiro
    2001–2002 Brazil
    2003–2008 Portugal
    2008 - 2009 Chelsea .

    ReplyDelete
  43. Jamani tusibishe, hii timu ikishinda ni yetu wote lakini ikifungwa ni ya Maximo, mimi sioni tatizo hapo.

    ReplyDelete
  44. Sikubaliani na mapendekezo ya Kocha Mziray kwamba eti mfumo wa 3-5-2 anaoutimia Kocha Maximo haufai na umekuwa ukiifanya safu ya ushambuliaji ya Taifa Stars kuwa Butu!Siyo sahihi kwa maoni yangu.Kutokana na maumbile madogo na ufupi wa wachezaji wetu wengi wa Taifa Stars mfumo wa 3-5-2 ndiyo mfumo mzuri zaidi ambao utaifanya midfield kupanda mbele na kurudi nyuma kila wakati kwa kadri kasi ya mchezo utakavyo kuwa ukienda.Hapa Mziray hana jipya anachojaribu ni kuzuga tu ili na yeye bado Kocha Mahiri!Mfumo wa 4-4-2 ni mzuri iwapo tu wachezaji wengi watakuwa na vimo virefu na nguvu ya misuli na kasi ya kujenga mashambulizi.Mfumo wa 4-5-1 nao ni mzuri iwapo tu Mshambuliaji atakuwa na misuli ,mrefu,mwepesi,na mfungaji mahiri!Lakini ukiachilia mbali Defence ambayo lazima iwe Imara na shupavu,kitu muhimu zaidi ni uwezo wa midfield kupanda na kushuka muda wote bila kuchoka,kujenga mashambulizi,na kumdhibiti mpinzani (ball control & ball possession).Otherwise,kwa hatua tuliofikia,Kocha Maximo anastahili Pongezi nyingi sana kwa uvumilivu na ustahimilivu wake katika kuwasoma wachezaji na kuyajua mapungufu ya kila mmoja wao!Nafikiri watu kama Mziray ni heri wakakaa kimya badala ya kutoa kauli ambazo hazitaijenga wala kuiongezea uwezo Taifa Stars!Maajabu yanaweza kutokea baina ya Taifa Stars na Zambia.Kujituma,Kujiamini na Kuwa na Malengo ya Ushindi ni nyenzo muhimu sana katika mechi hiyo muhimu.All the Best Taifa Stars!

    ReplyDelete
  45. Hawa wanaojiita wadau wa soka ni bora wakakaa kimya, kwa sababu kila wanavyozidi kutoa maoni yao ndivyo wanavyozidi kujishushia thamani mbele ya watanzania walio wengi.

    Mdau Sapi anasema sasa ni muda wa kuwa na makocha kutoka ulaya...simba walifungwa magoli 7-1 na enyimba katika mechi mbili walizocheza nao..ina maana Cirkovic ni mdengereko?, au ni mmatumbi?, wabongo tujitahidi sana tuachane na kasumba zilizopitwa na wakati.

    Maximo anatumia mfumo ambao anaona unafaa kwa aina ya wachezaji aliowakuta hapa Tanzania, wachezaji ambao hawakulelewa katika maadili ya michezo, wamejilea wenyewe kwenye timu za kihuni za mitaani.

    Inawezekana wengine wanamtukana Maximo kwa kufuata mkumbo tu, bila kujua wanaongea nini....kwa aina ya wachezaji tulionao miaka hii ya karibuni, itakuwa ni jambo la hatari sana tuijidanganya eti tunaweza kucheza aina ya soka tulinaloliona kwenye ligi za England na Spain..sisi bado sana ndio maana wachezaji wetu kwa sababu ya uchanga wao wanalazimika kukaba sana na kucheza kwa ushirikiano mkubwa.

    Tumpe heshima yake Maximo kwa sababu alichokifanya , amekifanya kutokana na aina ya maakuzi ya wachezaji wetu...halafu Brazil wana nidhamu kubwa ya mchezo tangu wachezaji wakiwa wadogo sana..sisi ndio tunaanza..na hatuna ubora wa kuchagua kocha , eti ni lazima atoke ulaya mashariki au magharibi..Bezinski aliyekuwa simba ni mhaya? au labda ni msukuma?...mbona simba walimtimua na yeye aliwaambia simba ukweli kwamba inahitajika miaka mingi ili timu iweze kucheza mchezo wa kisasa.

    Kina Sapi na Mziray wanaiombea mabaya timu ya taifa lao lakini wameumbuka baada ya timu yetu kuifunga Ivory Coast..tuikwepe kadri tunavyowezana aina hii ya wanafiki kwa sababu ndio inayochangia kuzifanya simba na yanga zisiwe na maendeleo.

    ReplyDelete
  46. Maximo bonge la kocha hata tukifungwa aongezewe muda anaoutaka yeye wenye kuchonga na wazidi kuchonga....someni hii

    Maximo awatangazia vita wachezaji wasiojituma Taifa Stars
    Na Saleh Ally, Abidjan

    KOCHA wa Taifa Stars ametoa kauli ya tahadhari kwa wachezaji wote ambao hawana msaada kwenye kikosi chake, wasiotaka ushirikiano na kujituma uwanjani atawaengua kwenye timu hiyo baada ya mashindano.


    Maximo alitoa kauli muda mfupi baada Stars kupambana hadi dakika ya mwisho na kuwashinda wenyeji Ivory Coast huku wachezaji kadhaa nyota wa kikosi hicho, Haruna Moshi 'Boban' na Athuman Idd ëChujií wakiwa jukwaani bila ya maelezo.


    Akizungumza katika hoteli ya Golf jijini hapa, Maximo alisema atachukua uamuzi mkubwa wa kufanya mabadiliko katika kikosi chake baada ya mashindano haya na wachezaji watakaopata nafasi ni vijana na Watanzania wasahau tena zile tabia za majina kwa kuwa si yanayocheza.


    ìUmeona timu ya leo, wachezaji wameonyesha kutekeleza majukumu yao na upendo kwa taifa. Wamecheza kwa kujitolea, wamejituma kwa nguvu na kwa kuwa nyumbani wameshuhudia mchezo huo watakuwa wameona hilo.


    Watu wa namna hiyo ndio wenye nafasi kwenye timu yangu.


    ìHakuna nafasi ya majina, hakuna mchezaji nyota kwenye kikosi changu ambaye hana msaada basi tu anachaguliwa kwa kuwa jina lake linajulikana. Kwenye kikosi hiki hakuna, safari ijayo nafasi kubwa ni kwa vijana na si vijana wa umri tu, nataka wawe na mawazo na malengo mapya pia kwa ajili ya faida ya Tanzania,î alisema Maximo.


    ìUnajua kuna lawama nyingi ambazo kama utazisikiliza hauwezi kufanya kazi, unajua kama ilivyo ada ya wengi kama timu ikifanya vizuri sifa zinaenda kwa wengine na ikifanya vibaya basi ni lawama za kocha. Bora iwe hivyo lakini nataka timu ifanye vizuri.


    ìHuu ni wakati mwafaka wa kujenga kikosi kipya cha Tanzania chenye wachezaji wenye nidhamu na uwezo wa kujitolea kwa ajili ya taifa lao. Na si wenye majina makubwa yanayojulikana kwa watu wa taifa lao, lakini hawana msaada wowote kwa watu wa taifa lao,î alisisitiza.


    Alipoulizwa sababu ya kutowachezaji Haruna Moshi na Athuman Idd walikuwa katika kiwango kizuri, Maximo alijibu kwa ufupi tu. ìHii ni timu, si mtu mmoja mmoja na tunaangalia nani yuko tayari kwa ajili ya mechi.î


    Akizungumzia mchezo huo dhidi ya Ivory Coast, Maximo aliwapongeza wachezaji wake kwamba walicheza kwa kujitolea. ìMsimlaumu mtu, mfano Henry aliumia muda mrefu.


    Alitaka kutoka nikamwambia ajitahidi hata dakika 20 kwanza. Alifanya hivyo akiwa na maumivu lakini lengo lilikuwa ni kulisaidia taifa lake. Angalia wengine kama Kingi, kacheza kwa nguvu zote. Nawapongeza sana.î


    Stars inahitaji kushinda mechi ya kesho dhidi ya Zambia kwa idaidi yoyote ili ipate nafasi ya kusonga hadi hatua ya nusu fainali huku Chipolopolo ikiwa inahitaji sare tu kupata nafasi ya kusonga mbele.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...