jioni hii nimetembelea fukwe ya bahari ya hindi sehemu za oysterbay na kukuta wadau kibao wakiwa wanajidai hapo na magari yao kama ilivyokuwa enzi zileeeee kabla wazee wa jiji hawajatia pini kupaki karibu na bahari. nadhani hii ni baada ya JK kuingilia kati na kuwataka wazee wa jiji waache wananchi watanue kwenye sehemu hizo na wasiwabughudhi kwani ni haki yao ya msingi. tena akawataka waziendeleze hizi sehemu kwa njia za kisasa.
Leo, yapata miezi miwili toka JK atoe agizo hilo, hakuna kilichofanyika na wala hakuna dalili kwamba wazee wa jiji wana mpango huo. redio mbao zinasema wazee wa jiji wanasubiri JK atoe mwongozo mwingine kabla hawajaanza kutekeleza agizo lake....


Ni vizuri na haki wananchi na wageni wawe huru kutembelea na kujiburudisha ufukweni. Sasa ningependekeza wakati Rais JK alitoa mwongozo mwingine jinsi ya kufanya fukwe ziwe mahala panapowafaa wanaotaka kuburudika, sehemu maalum ya maegesho ya magari iwekwe katika mpango. Magari kuegeshwa kila mahali haifai kabisa na ni mara kumi wazee wa jiji wapige marufuku kutumika kwa fukwe kama hawana ubunifu wo wote wa kuzuia magari yasiegeshwe ufukweni!!!
ReplyDeleteYaani hawa wazee wa jiji kweli sasa inabidi wapewe vijana, maana ving'ang'anizi vyao katika madaraka wakati uwezo wao kufikiri umefikia kikomo ndiyo matokeo yake haya. wanashindwa kuwa wabunifu mpaka JK awaambie nini cha kufanya?.
ReplyDeleteMfano kama wangeamua hapo kuweka walinzi wa jiji kwa usalama wa wenye magari, wajenge parking nzuri, na kila mwenye gari anatoa Shs 500 tu kwa parking pamoja na ulinzi wangewapa ajira vijana wengi tu na jiji kupata kiasi. Ila wao mpaka kila kitu kitoke juu ndiyo wanajua wafanye nini. Wawaachie vijana sasa watengeneze nchi, siyo kung'ang'ania posho tu bila kufikiri aaaaaahgggh inauzi sana
Kaka Michu,
ReplyDeleteAsante kwa picha hii, maanake imenikumbusha mbali sana!!
Mimi ninajiuliza...hivi hawa wazee wa jiji, wana elimu au uzoefu wa Town Planning? Kwa kweli inasikitisha sana jinsi hii sehemu bado haijaendelezwa mpaka leo. Miji yote niliopita duniani, fukwe kama za oysterbay zimeendelezwa ile mbaya!! Hakuna ya kwenda mbali, wangepanda tu ndege wakaenda Maputo wakacheki mambo. Tatizo la hamlmashauri watu wanapeana vyeo tu, hakuna mjuzi kule. Upuuzi mtupu. Mimi jamaa yangu narudi bongo wataona shughuli yangu!!!
Kaka Michuzi,
ReplyDeleteI was browsing "Bongo Pix" and I found very interesting clip.Switch to Bongo Pix and keep on scrolling further down till you find the clipp headed "WAWEZA KISIA NINI KILITOKEA USIKU WA JANA YAKE?",try to put it here as well so that we can have other contributors views on the scenario(it's a request brother!!).Kwa kweli nimecheka sana.Ha ha ha ha haha ha ha.
Mkulima-Kijijini Gezaulole.
jamani mbona bughudhi dhidi ya wahindi?sasa kuanza huo moto kutumia kibiriti cha blogu hiyo katika enzi hii ni elimu au ujinga...?
ReplyDeletetushazoea miyeyusho...
ReplyDeleteSasa JK atoe mwongozo kwa wao wenye kazi hii kwa nini tena? Ndo maana nasemaga kuna watu wanalipwa mishahara ya bure tu huko Tanzania,hawana la kubuni mpaka Rais wao aseme wafanye hivi na vile ndo wanafanya,sasa kuna haja ya kuwa na hawa watu kweli! Ukiangalia hata mikutano ya Rais na Wizara zake, anafanya hicho hicho, mpaka watendaji waambiwe fanyeni hivi na hivi, ndo wanazinduka...lini tutakuwa na wachapakazi, wa kujua kazi zao especially huko mawizarani lakini!Khaa!
ReplyDeleteMdauz JP
Samahani kwa kutoka nnje ya mada, Sasa wadau hii imekaaje??? just sad, sad,sad
ReplyDeletecheck it out!!!
http://www.newsoftheworld.co.uk/news/232205/Jades-emotional-video-interview-and-other-Jade-Goody-videos.html
God bless n keep tight fo ever!!!
michuzi tatizo lako unashabikia vitu ambavyo hamuwezi kuvitunza,hata hizo bichi zitengenezwe vipi tatizo wabongo hamjastaraabika sasa kama hapo kwenye picha magari yanasababisha uharibifu wa ardhi wewe unashabikia tu!usishangae hapo watu wanaenda haja kubwa na utashabikia tu,dawa ni kuzifanyia matengenezo na kuwatoza hela watu na walinzi juu,mambo ya bure bure yamepitwa na wakati kaka!!!!!!!!!
ReplyDeleteDu kweli bongo PAKO levo(TAMBALALE)
ReplyDeleteNilivichanga vi dollar vyangu vya overtime nilifikili nitatesa, Kufika Tanzania nikakuta nduguzangu wanatumia shilling kama vile wanapokea mishahara kila siku, BONGO kiboko yao.
ReplyDeleteThe problem with Dar is that all the beach plots have been given away to private citizens. Hili ni kosa kubwa sana kwani inawanyima haki ya msingi wanachi wa Dar kuweza kufaidi bahati ya kuishi kwenye mji uliopakana na bahari. Ni almost kama Dar ni Mji Kasoro Bahari in a certain way.
ReplyDeleteMiji mingine huwa wanajenga barabara i run parralel na beach ili asitokee mbabe yeyote wa kujinyakulia beach plot.
Hata sehemu ambazo watu wangeweza kuchungulia bahari zinafungwa - k.m pale opposite na St, Joseph... kulikuwa hamna haja ya kuruhusu makampuni ya maboti kujenga vibanda vyao pale na kuzuia mwonekano wa bahari. Pale lingebaki lile jengo moja tu lililojengwa vizuri na vibanda vyote vivunjwe.
Mahala hapa panatakiwa ulinzi kwa namba yoyote ile inayofaa. Ama pawepo diffender ama askari kanzu ili kulinda watu na mali zao. Pia vifaa vya kuokolea viwepo. Kuna mtoto amekufa kama mwezi mmoja uliopita kwa kuchelewa kuokolewa baada ya kuzama baharini
ReplyDelete..........and no one is thinking about erosion of the coast line along the beach caused by that heavy traffic!!! This was the original reason of not allowing vehicles on the beach. Lakini kama kawaida yetu tunakurupuka tu bila kutafakari au kuelewa na wala hatujisumbui kufanya hivyo!!!
ReplyDeleteSasa huu ni uchafu na uchafusi wa mazingira. Ni sawa wananchi wote wana haki ya kutumia ufukwe. Ila kungekuwa na mipangilio. Maana hapa naona ni usumbufu wa macho (vurugu mechi)!!!!
ReplyDeleteNinavyoelewa watu huenda ufukweni kwa ajili ya kuogelea, kupunga upepo, ku jog nk. Hivyo haya magari yawawazuia watu kufanya shughulu hizo. Kungatakiwa kuwe na parking somewhere else, benchies nk. ili watu wote hata wasio na magari waweze kufaidi matunda ya nchi yao siyo wenye magari tu.
kwakweli inasikitisha sijuwi tuangalie upya sifa za viongozi kabla ya kuwachaguwa na kuachana na rushwa wakati wa kuchaguwa hao madiwani maana hawako creative kabisa jamani nenda hapo Durban utafurahi na kuhuzunika kwanini Tanzania wameshindwa maana basi hata mwekezaji anaweza kupewa na mkataba wa maana ukaingiwa nasi lazima awe kutoka nje hata wabongo wanaweza jamani hee
ReplyDelete