wikiendi hii mie,  beda msimbe a.k.a  mzee wa lukwangule.blogspot.com (kulia)  na mtaalamu wa teknolojia phares magesa ambaye ni bosi wa www.nsitz.com tulipata heshima ya kualikwa na mdau ephraim kibonde katika kipindi chake cha 'mlango wa dharura' ambapo kwa masaa matatu tuliongelea mambo ya libeneke la globu lilivyo.

kwa ufupi mada iliyotawala ni jinsi ambavyo wabongo tunavyonyata katika kuikumbatia teknolojia ya habari na mawasiliano, wakati wenzetu wakikimbilia kwenye njia kuu ya teknohama, tena huku tukitambua kwamba baada ya mkonga wa mawasiliano (fibre optic) utapoanza kazi mwezi juni mwaka huu mambo yatakuwa mswano.

tuliongelea pia umuhimu wa fani ya globu katika jamii na kutoa rai kwamba wadau wakaze buti na kuanzisha libeneke la globu kwa wingi kwani uwanda ni mpana sana. tatizo kwa sasa kila mdau anaanzisha libeneke ambalo halina tofauti na mengine yaliyo hewani, yaani ya habari na matukio ya siku. ikatolewa rai kwamba kuna haja kwa wadau kuanza kuangalia nyanja zingine ambzo hazina huduma ya libeneke hivyo kuendelea kudumaa kwa kukosa wapasha habari.

libeneke la globu mbalimbali pia liliongelewa ikiwa ni pamoja na zile za mlengo wa kushoto, mlengo wa kati na mlengo wa kulia. mlengo wa kushoto ni zile zinazosadikika kuchafua hali ya hewa, za mlengo wa kati ni zile zisizochafua hali ya hewa na kutoegemea upande wowote wakati za mlengo wa kulia ni zile zilizojikita kwenye nyanja moja tu, kama vile siasa, uchumi n.k.

wasikilizaji wengi walipiga simu kutoa maoni na wengine kuuliza maswali, mengi yakiwa juu ya udhibiti wa libeneke la globu kwa kile kinachoonekana 'kupitiliza' kwa baadhi ya globu, hususan za mlengo wa kushoto. rai ikatolewa kwa wahusika wa udhibiti wa uhuru wa habari kuliangalia swala hili kwa herufi kubwa na kuona namna ya kufanya mambo yawe mswano bila kunyima haki ya msingi ya kupata ama kupsha habari - bila kujali mlengo gani.

kwa niaba ya phares na mzee lukwangule, natoa shukrani za dhati kwa redio ya watu ya clouds 88.4fm kutupa nafasi hiyo adhimu na adimu, pia mtangazaji ephraim kibonde kwa kutukaribisha studio. vile vile tulifurahi kusikia kwamba clouds fm wanalifanyia kazi ombi letu la kupitia na kusoma habari zilizomo katika globu kama wafanyavyo kwa magazeti.

tunaiombea clouds 88.4fm maisha marefu yenye tija tele, hasa katika kipindi hiki ambapo wako njia moja kuhamia katika jengo lao huko sehemu za mikocheni ambako mitambo ya kisasa ya redio na tv imefungwa, tayari kufungua awamu mpya ya redio ya watu. 

Tunashukuru sana
-Michuzi




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. TATIZO NI BEI YA VITU, KAMA COMPUTER, SUBSCRIPTION YA INTERNET, ELIMU YA COMPUTER, SIMU NI GHARMA KUBWA SAN WATU HAWEZI KUMUDU, SERIKALI IFANYE MAKUSUDI MAZIMA YA KUTOA BURE ELIMU YA MSINGI YA COMPUTER, BEI ZA COMPUTER ZIPUNGUZWE NA KODI YAKE IFUTWE ASILIMIA 100, SIMU LANDLINE PIA IPUNGUZWE NA KUWE NA KAMPENI YA KITIFA YA COMPUTER NA INTERNET. IKIWEZEKANA SERIKALI ILIPIA MASOMO YA COMPUTER HASA KWA WATOTO NA WAZEE.

    ReplyDelete
  2. Nafurahi kuona fani ya Blog na upashanaji wa habari nchini Tanzania inazidi kutambulika kila kukicha. Ipo siku tutafika kule wenzetu walipo sasa. Mimi kwa mtazamo wangu libeneke la mlengo wa kushoto siliungi mkono kwani madhara yake kwa jamii kila mtu anayatambua. Fani hii iwe ya kujenga na si kubomoa.

    ReplyDelete
  3. Mr. Michuzi! naomba kukuuliza wewe binafsi na wengineo.
    Mara zote umekuwa ukitumia neno GLOBU badala ya BLOG, hufanya hivi kwa makusudi ama ni kimakosa!!

    ReplyDelete
  4. Mzee Naona FULANAA inang'ara iyo nyingine nini?

    ReplyDelete
  5. blog not globu(globe) two different stuff naona watu wengi wanamix hii kitu like i used to hear people saying nitakudip badala ya nita kubeep naona balozi na wewe unaendeleza kimtindo

    ReplyDelete
  6. HONGERA BALOZI KWA UJUMBE

    Nakubaliana nawe ktk kipengele cha kuonesha umakini wa blog...ni vyema watu wanapoanzisha blog wawe makini, kuweka blog ambayo itasimama kwa muda mrefu...sio kuweka ktk mazingira yaleyale ambayo libeneke limeshazoeleka, hivyo unajikuta unakata tamaa.Mfano, mtu ukitaka habari za tulipotoeka vijijini kwetu, unajua kabisa MJENGWA ndio muhusika, Ukija masuala ya Picha, kuna fotabaraza, bongopichaz nk, ukija libeneke kwa ujumla ndio hapa ktk blog yetu ya jamii, ukitaka mambo ya masuala ya utetezi wa haki za alibo, ipo ya Viki wa BBC, mambo ya Scholarships kuna MAKULILO Jr, na NUKTA77 blogs, nk.Inasaidia kiasi fulani kuelimisha jamii na kuisadia ktk angle mbalimbali huku libeneke likisonga.Sasa kila mmoja akitaka awe Michuzi kwa kuweka kile kile itakuaje, huwezi kuendelea kwa haraka kwani hutokua na jipya, watu wanataka upya wako, utoke wewe kama solo.

    Naungana na mdau wa juu kwanza kabisa kwa hoja ya gharama za internet Tanzania.Hilo ni tatizo lingine kubwa lifanyalo watu wanaanzisha blog kwa nia njema ila badaye inakua ngumu kuiendeleza.Gharama ya internet imekuwa kubwa mno bila msigni wowote kwani ukiangalia mfano TTCL walipoanza ilikua bomba, ni kulipa kwa mwezi elf 30 unatumia utakavyo...muda wakabadilia unalipa kutokana utumiavyo lakini 1MB ni sh 55, hatujakaa sawa wakabadili kwa kuongeza gharama 1MB imekwenda sh 260 ongezeko la zaidi ya asimilia 200 na hukan kipya ndani yake zaidi ya wizi tu.

    MAKULILO Jr,
    www.makulilo.blogspot.com

    ReplyDelete
  7. Eti mzee wa Blog, hapo mmesimama au mmekaa?? Sioni vizuri hapo???

    ReplyDelete
  8. BLOG OR GLOBU

    Kuna mdau ambaye ni wa tatu kutoa maoni umeuliza hivi ni BLOG au GLOBU, na kwa maoni yako umesema hiyo ni GLOBU na mbona Michuzi umekua unaandika neno BLOG, ni kimakosa au inakuaje?

    Swahili limeshawahi kuuliza ktk comments flani wiki chache zilizopita, sijui kama mdau wewe au ni mwingine, ni vyema nami nikatoa tips inakuaje ktk swali lako.

    Nijuavyo hii inatwa BLOG na sio GLOBU. Na mtu anayekuwa na BLOG anaitwa BLOGGER, Kwa hiyo mdau Michuzi ni Blogger wa Blog ya jamii.Na ndio maana unapoandika title ya blog ktk address ili kufungua, mfano hii ya Michuzi unaandika WWW.ISSAMICHUZI.BLOGSPOT.COM Si unaona baada ya title ya Blog yenyewe kinachofuata ni BLOGSPOT na sio GLOBUSPOT.

    Kwa maelezo zaidi ya BLOG fungua hapa http://en.wikipedia.org/wiki/Blog

    Naamini wadau ambao ni wataalam wa mambo haya watatoa maelezo ya kiufundi zaidi kuweza kuliweka sawa hili.Mimi huo ndio muono wangu ktk swali lako la je ni BLOG au GLOBU.

    MAKULILO Jr,
    www.makulilo.blogspot.com

    ReplyDelete
  9. Ni kweli nyingi zinafanana, wakati mwingine ni kwa sababu ni rahisi kupiga/kukopi picha na kuandikia maelezo na kupost kuliko kuwa na blog inayohitaji masuala magumu kama ukianzisha ya intavyuu ina maana unalazimika kuhangaika kupata watu, kuwahoji na kutype mahojiano yote, huenda vitu vigumu vinakimbiwa ila ndivyo vizuri...wengi wanafungua za picha.
    Gharama ni sehemu nyingine, kweli tuusubiri hiyo teknolojia ya fibre huenda mambo yatakwenda sawa.
    ClousFM sina shaka nao, jamaa ni sehemu ya jamii! Big Up E.Kibonde

    ReplyDelete
  10. Mi nauliza ulikua unakula lol pop? au nini hicho mdomoni ....aaaaa kaka yangu....wee vipi sasa usiniangushe bwana...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...