Habari za leo kaka Michizu,
Mimi ni Mdau na Miongoni mwa wampenzi Wakubwa Sana wa hii blog,
Kwa sasa nipo huku Vienna Austria, katika harakati za kujitahidi kujipanua kielimu.
Elimu yangu ya awali,kuanzia Chekechea mpaka sekondari yaani Kidato cha nne na sita niliipata hapo Tanzania.Bila kuwachosha wadau na hotuba ndefu ningependa kuwasilisha haya mawazo yangu ambayo yananiumiza sana roho.
Siku chache zilizopita nilikuja Tanzania kwa rikizo yangu ili kupumzika kidogo na kuzungumza kiswahili.Kuna mabadiliko mengi sana niliyoyaona, lakini kuna mambo ambayo yaliniumiza sana ROHO.Yako mengi sana lakini leo ningependa kuongelea lugha ya kiswahili tu.
Imefikia wakati sasa Kiswahili kinaonekana kama ni ushamba , ama ujinga au ni ukosefu wa elimu na ni aibu kwa baadhi ya wazungumzaji; kusema kweli nilikereka sana na niliumia sana . Watanzania wachache wanaona aibu kuizungumza lugha yao. Hapa Vienna kuna Watu wa Mataifa mbali mbali, Waserbia , Waturuki ,Wajerumani ,Waingereza na kadharika pamoja na kua na Lugha moja inayotuunganisha ``kijerumani`` lakini wote wanajivunia kuongea lugha zao za kuzaliwa . Hata siku moja huwezi kumsikia Muaustria au Mjerumani anachanganya lugha yake na lugha nyingine au anaona aibu kuiongea .
SASA LEO HII Kijana wa Kitanzania anaona aibu kuongea lugha yake yakiswahili,Watu wachache wanaojifanya wako sawa na maendeleo ``Updated`` kumbe niwashamba watupu ususani kwenye vyombo vya habari ´´Media´´,Maofisini na sehemu wanazoziita za kishua, na kuna Wapumbavu wachache kwenye vyombo vya habari wanaowakatisha tamaa``discourage`` watu au wanamuziki wachache wasiofahamu kingereza.
TUMEFIKIA WAPI WATANZANIA ?
Mambo kama kama Wimbo wa Taifa mashuleni ;Kupandisha Bendera, Mchakamchaka,Nyimbo za kuisifia Nchi yetu pamoja na Mashujaa Wetu n.k. sasa hakuna tena!
Kaka michuzi, nitafurahi sana kama utanipa hii nafasi ya kuwajulisha hayo Watanzania wenzangu.
Naipenda Tanzania ,
Naipenda lugha yangu ya Kiswahili,
mdau,
Chuo Kikuu Vienna
Austria.
ok mdau bado sija jua unaongea nini kama kiswahili mbona kina zungumzwa sana ndani na nje ya nchi,nadhani una jitangazia uko nje kwa hilo tume kufahamu! kaza uzi mdau kuwania nondo yako.
ReplyDelete"sema baba waambie hao hawasikiii"!mzee wa dawa naona unamwaga usia!ha ha ha haa!
ReplyDeletenakuunga mkono mdau,lakini kitu kimoja tu unachotakiwa kuelewa,ambacho mimi nimekielewa juzi tu,ni kwamba,nchi hii sasa haina mwenyewe, uzalendo na ufia nchi tanzania ni upuuzi. enzi za nyerere na maisha ya urafiki,sasa imebaki ni unafiki,na imefikia kusema naichikia tanzania, kwa sababu hutafanya jambo zuri tanzania,uonekane shujaa, bali mtu fulani unayetafuta umaarufu kwa ajiri ya siasa. kwa sasa nchi imejaa WABEUZI, POLE.
ReplyDeleteNi LIKIZO, na sio RIKIZO!!!!!!!!!!!!
ReplyDeleteNAUGNANA NA MDAU WA KWANZA. HUYU JAMAA ANAONEKANA LIMBUKENI NA SIDHANI KAMA ANAFAHAMU KISWAHILI VIZURI. KWENYE "LI" ANATUMIA "Ri" HAKAFU ANAJIFANYA ANAJUA KISWAHILI. INABIDI AKAJIFUNZE VIZURI LUGHA NA LAZIMA AONGEE FASAHA KABLA YA KUPONDA WATU. MTU KISHAJUA KISWAHILI ANA HAKI YA KUJUA LUGHA NYINGINE. NA HAWEZI KUJUA BILA KUZUNGUMZA HASA NA WALE WANAOZUNGUMZA LUGHA NYINGINE...
ReplyDeleteTULIA KIJANA.
Sijaona wazo wala kero yako kwani unaongelea kuumizwa na matumizi finyu ya Kiswahili wakati wewe mwenyewe hukijui hicho Kiswahili.
ReplyDelete1.NI "LIKIZO" SIYO "RIKIZO"
2.NI "PAMOJA NA KUWA" SIYO "PAMOJA NA KUA"
Hayo ni baadhi ya makosa machache tu ya kisarufi katika maandishi yako (sina uhakika kuhusu matamshi yako)
Naungana na mwandishi aliyesema pengine madhumuniyo ni kutaka kusema uko VIENNA na si vinginevyo.
Eti unasema " ulienda RIKIZO kupumzika na pia KUZUNGUMZA KISWAHILI!!! Shame on you.
kwanza jirekebishe wewe mwenyewe kwa kuandika na kutamka kiswahili sawa sawa, mfano wa haraka tu hakuna neno rekizo ila kuna neno LIkizo.
ReplyDeleteMr Fish
mbona huyu jamaa aloleta hii topic anajichanganya? anawakandia wanaochanganya kiswahili na engilishi halafu na yeye mwenyewe pia anachanganya, sasa tumeleweje? pia ningelimshauri nae ainue kiwango chake cha kiswahili kwani kuna maneno mengi ameandika kisivyo mfano ni kama rikizo, ususani na kadharika hakuna maneno hayo katika kiswhaili sanifu kuna likizo, hususan na kadhalika.
ReplyDeleteInaweza kuwa ni kweli .ninachojua wakenya ndio wanamchezo huo. Halafu kiswahili kama kiarabu vile kwa maana ukiwa hasa huku usa inabidi uwe carefull na wajomba .maana kunamji mmoja huko kwa waarabu unaitwa daresalam .
ReplyDeleteJamani huyo mtu ana point sasa kwanini mnamshambulia kwa vile hajaandika sahihi likizo?Its called typing error im sure ya'll in here probably struggle in your writtings yet you busy correcting someone else get a life people
ReplyDeleteMDAU MZALENDO MWENZANGU USIPATE TABU SANA NA HAWA WAKUJA,USHAMBA,UTUMWA WAO WA KIFIKRA NA UELEWO WAO NDIO NDIO UNAO WAFANYA WAKUSHAMBULIE NA KUKISHAMBULIA KISWAHILI.
ReplyDeleteJAMANI TUJARIBU KUELAWA LOGIC YA MTU IPO WAPI KWA JINSI NILIVYOMWELEWA MDAU NI KWAMBA ANAJARIBU KUWATIA MOYO WATANZANIA TUACHE USHAMBA NA TUJIVUNIE KISWAHILI CHETU TUACHANE NA FIKRA ZA KITUMWA TUSIONE AIBU KUKITUMIA KISWAHILI MBELE ZA WATU WENGINE TUJIVUNIE KAMA WAO WANAVYOJIVUNIA LUGHA ZAO.
UNAJUA TANZANIA UKIONA MTU ANAUPONDA KISWAHILI NA USWAHILI KWA UJUMLA,MCHUNGUZE HUYO MTU VIZURI HISTORIA YAKE UTAGUNDUA NI WAKUJA AMA AMETOKEA KTK MAENEO YA TABU NA PORINI KIASI KWAMBA SIO MSTAARABU(NOT CIVILISED)HANA (MAINGILIANO)CONTACT AMA COMMUNICATION NA JAMII NYENGINE KIASI KWAMBA AKIINGIA MJINI ATATAKA KUONESHA KWAMBA NA YEYE HAYUPO NYUMA NA YUPO JUU ZAIDI YA WALE WALIO MPOKEA,KINACHOFUATIA NI KUTUKANA UTAIFA WAKE.
HATA KAMA SIJUI KISWAHILI SIACHI KUJIVUNIA KISWAHILI NA USWAHILI WANGU.
KWAHIYO MSIMSHAMBULIE MDAU KWA UPEO WENU MDOGO HAYO MAKOSA NI MAKOSA YA KAWAIDA KABISA KUYAFANYA KINACHOITAJIKA TUIELEWA NINI ANACHOMAANISHA.
HONGERA WAELIMISHE WATUMWA WA KIFIKRA KAKA,SIUMEONA WALIVYOKUA NA FIKRA ZA KITWANA KISA UMEANDIKA UPO AUSTRALIA WASHAINGIZA INFERIORITE COMPLEX ZAO WALIZO NAZO NA NDIO MAANA WANASHINDWA KUJIVUNIA KISWAHILI CHAO NA USWAHILIO WAO.
HATA KAMA SIJUI KISWAHILI NAUNGANA NAWE KUKITETEA KISWAHILI TUKUFU KILICHOTUUNGANISHA NA KUWATOA WATU USHENZI WAO.
Kaka Michuzi napenda niwape wazi wadau wengine katika kutoa mawazo. kila mtu yuko huru kutoa mawazo aliyonayo. unachotakiwa ni kumuunga mkono au kumpinga. mimi nashangaa wadau wengine wanajaribu kumkosoa jamaa kwa kukosea kuandika kiswahili, kwamba penye "l" kaweka "R badala ya kuchangia alichosema. Napenda kumuonya mchangiaji wa tano, ambaye amejaribu kumfunza mdau kiswahili wakati yeye mwenyewe alichokiandika ni kiswahili kibovu kuliko mdau aliyeomba mawazo yetu. Pia ajue kwamba mdau anawezekana alikosea katika kubonyeza, kiswahili alichoandika huyo "mwalimu" wa kiswahili ni kibovu na siyo atakuwa amekosea kubonyeza. Wadau angalieni hata ninyi.
ReplyDeleteNAONA WADAU WENGI WANA HASIRA NAWE NDUGU. BADALA YA KUCHANGIA MAWAZO WANAKIMBILIA KUSEMA UNAJIDAI N.K AU UMEKOSEA KISWAHILI. NIMEJARIBU KUPITIA MAONI YOTE NAONA WANAOKUKOSOA KISWAHILI NDIO WANAOONGOZA KWA KUCHAFUA KISWAHILI, IKIWA WAPO NDANI YA BONGO. UNA HAKI MDAU WA KULALAMIKA KATIKA SUALA LA KISWAHILI UKWELI NI KWAMBA MATAIFA MENGI YANAJIVUNIA MATUMIZI YA LUGHA YAO NA WANAPOKUTANA UGHAIBUNI WANAKUWA NA FURAHA SANA KUONGEA LUGHA YAO. HIYO MIMI NIMEIONA NA HATA MIMI IMENIKUTA. HIVYO WADAU MSIANGALIE JAMAA KWA VILE YUKO VIENA BASI ANAJIDAI, CHANGIENI MAWAZO.
ReplyDeleteMdau wa Austria kwa vile umesema una kipenda Kiswahili, sahihisha makosa katika unandikaji wako. Nitaonyesha neno lisilo sahihi na kufuatiwa na neno sahihi:
ReplyDeleterikizo = likizo
niliyoyaona = niliyo yaona
kadharika = kadhalika
kua = kuwa
inayotuunganisha= inayo tuunganisha
anachanganya= ana changanya
anaona = ana ona
yakiswahili = ya Kiswahili
ususani = hususan
wanaowakatisha= wana wakatisha
Ila dukuduku lako nimelipata.
Mdau wa March 27, 2009 1:00 AM umetoa maoni mazuri japo umenichanganya katika baadhi ya masahihisho uliyompa mchokoza mada. Kwa mfano unasema badala ya kuandika 'anaona' ilipaswa aandike 'ana ona'. Ukisema 'ana' na kuacha nafasi unaonyesha umiliki. Kwa mfano ukisema 'ana kaa' tungo inatoa ujumbe kwamba kuna mtu ambaye katika wakati uliopo hali ya kuendelea anafanya tendo la kumiliki ngadu. Kwa upande mwingine ukisema 'anakaa' unatoa ujumbe kwamba kuna mtu ambaye katika wakati uliopo hali ya kuendelea anatenda kitendo cha kuketi. Mada hii imenihamasisha nikarejee vitabu vya lugha yetu, ikiwa ni pamoja na Kamusi ya Kiswahili Sanifu toleo la pili ili nipate uhakika kama inabidi nifanye marekebisho katika uandishi wangu maana nami naipenda lugha yetu. Shukrani mdau kwa kuchokoza mada hii. Kuipenda lugha sio mpaka uwe nguli katika matumizi yake. Si unaona Watanzania wanavyopenda soka lakini hatuna makombe ya maana ya kujivunia. Kadhalika watu wanaoongea lugha za kigeni hapo nyumbani tusiwalaumu sana maana hata tunapoenda vijijini kuna wazee wetu tunawakwaza tunapoongea Kiswahili badala ya Kidigo (huu ni mfano tu, Wadigo naomba msinishambulie).
ReplyDeletehujakosea baba ake, ata kwenye blog hii wapo wengi wanaotuandikia kiengereza na cc wengine hatuelewi, nashindwa kufahamu kwann hawatumii kiswahili!
ReplyDeleteMdau ulitoa mada ya kiswahili mie nakuunga mkono. Hao wanaokuponda ndio wale wanaojifanya kuona aibu kuongea lugha yao.ILa kweli inakera, utakuta muda mwingine wote mliokuwepo mnafahamu lugha ya kiswahili, lakini cha ajabu utakuta mtu anaanza kuongea english. Sasa huu si ulimbukeni, kwa nn utumie english na wakati mliopo hapo wote mnajua kiswahili. Muda mwingine utakuta mpo kwenye chat ya kiswahili na wote mliopo pale mnajua kiswahili, cha ajabu utakuta baadhi ya watu kwa ulimbukeni wao wanaanza kuchat kwa english. JAMANI WATANZANIA TUPENDE LUGHA YETU. Watu wa mataifa mengine wakikutana ni lugha yao tu ndio wanayoongea.Ukiongea kiswahili haimaanishi kwamba hujasoma au english haipandi. Sehemu ya kuongea english ongea english na sehemu ya kiswahili ongea kiswahili. Sio sehemu unaona kabisa ni ya kiswahili na mliopo hapo wote mnajua kiswahili ya nn kuongeas english.
ReplyDeleteMDAU
jamani kuna viswahili vingi, kama kingereza cha marekani au uingereza. marekani tuu inategemea umetokea jimbo gani, rikizo ama likizo vyote vinaeleweka
ReplyDeleteFREEDOM OF SPEECH... WACHA WATU WAONGEA, MAANA NI HAKI YAO YA MSINGI KUOENGEA WANACHOTAKA.
ReplyDeleteNashangaa kuona mtu ametoa hoja ya maana ambayo ingetakiwa iungwe mkono lakini wadau wengi wanamkandia. Ni ajabu kabisa kuona mtu anajikataa, anajipinga hata utamaduni wake mwenyewe. Kiswahili ni utamaduni wetu, hii ni lugha ya taifa. Leo hii mtu unaikandia, unajikataa usiitwe `mswahili' tukuite nani sasa, tukuite `wakuja' au `muulaya' hata sijui tukuite jina gani.
ReplyDeleteHoja ya msingi ya mwenzetu huyu ni kutupa msukumo, ili tuzidi kuiendeleza, kuitukuza na kuiongea bila wasiwasi lugha yetu,ili siku ya siku iwe moja ya lugha kubwa za kimataifa. Itajulikanaje kama `nyie mliobahatika' kuwa huko nje hamuiongei!
Hayeni bakieni kuiga, lakini hata muige vipi, muongee kama wao, na zaidi yao bado wewe ni `mswahili tu' na mbora katika maendeleo ya kitu chochote ni `kubuni' chako'. Kiswahili ni chetu, Kiingereza, Kifaransa, kina wenyewe, sisi tunajifunza `chao' na kuiga utamadini wao.
M3
napenda kuwaunga mkono wadau SHIRIMA na SHAYO waliochangia hapo juu..nadhani dhumuni la mdau ni kuwa kiswahili hakipewei uzito unaostahili..kwamba amewasilisha wazo lake kwa kiswahili kibovu ama kizuri (sijui ni kipi) haikuwa pointi..nadhani wadau mtulize akili kwanza kabla hamjakurupuka na kuanza kubwabwaja kwani ukishaenda hewani kila mtu anaona ..nani hawaoni watu maarufu (wanasiasa, wanamuziki , wakurugenzi n.k ) wanavyochanganya kiswahili na kiingereza wanapohojiwa?imefikia hata hatua ya kuwa kuna maneno ya kiswahili eti kwa madai yao ama hawayajui ama wanapata tabu kuyatamka..du sio mchezo..
ReplyDeleteJamani uyo jamaa ametaka tu kujionesha mimi pia ninaishi nje nanilipo kila siku tunaongea kiswahili ingawa kwasasa tunaijuwa zaidi lugha ya kigeni khs Tanzania tunahiari yetu kuzungumza kiswahili au kieengreza hasa ukizingatia moja ni lugha yetu ya pili, nadhani umeumia roho kuona sisi tupo tanzania lkn tunazughumza lugha uloifata huko.sasa utsemje wanaoacha kiswahili na kuongea lugha za makabila
ReplyDeleteKILA MTU ANA UHURU WA KUTOA MAONI KWELI LAKINI KUNA MAONI MWNGINE WATU HUTOA TU BILA KUFIKIRI. NI USHAMBA HUO.ALIYETOA MADA AMEKOSEA TU KUANDIKA LAKINI WALE AMBAO IMEWAGUSA WAMEISHIA KUKOSOA,JAPO PIA KUKOSOA NA KUKOSOLEWA NI NJIA YA KUJIFUNZA AU KUFUNZA LUGHA.
ReplyDeleteWATANZIA TUJIVUNIE LUGHA YETU TUACHE KUJIDAI NA TAMADUNI ZA WENZETU MBONA WAO WANAKUJA KUJIFUNZA WASIONE KISWAHILI NI USHAMBA?[NJOO UDSM UONE].
UNAWEZA KUMSIKIA MTU AKISEMA "HUYU ANA MAMBO YA KISWAHILI.AU HUYU ANAISHI USWAHILINI SANA" KWANI NINYI WAZUNGU,USWAHILINI NI WAPI? MI NINAVYOELEWA USWAHILINI NI TANZANIA YOTE. KWANI NI NCHI YA WASWAHILI NA INABIDI TUJIVUNIE HILO LA KUWA WASWAHILI TUACHE ULIMBUKENI WA KUSHABIKIA MAMBO KICHWAKICHWA,KIINGEREZA SIO AKILI NDUGU ZANGU.
MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WASWAHILI WOTE.
Msamiati na Istilahi
ReplyDeleteManeno haya ni ya kitaaluma zaidi na ni muhimu waandishi wafahamu tofauti zake. Msamiati ni jumla ya maneno yaliyo katika lugha fulani. Kwa lugha ya kigeni yanaitwa “vocabulary”. Haya ni maneno ya kawaida yanayotumiwa na watu wa eneo fulani.
Lakini istilahi au kwa lugha ya kigeni huitwa "technical terms"ni maneno mahsusi ya kitaaluma yanayotumika katika elimu. Zipo istilahi za fizikia, kemia, bayolojia, ufundi, tiba, uongozi na uendeshaji na teknolojia.
Istilahi hizi hutumika katika taaluma maalumu katika elimu. Hupatikana kutokana na warsha maalumu zinazoandaliwa na kuwakilisha wanataaluma wa fani mahsusi pamoja wa wenyeji wa lugha ya Kiswahili ili maneno yanayoweza kutumika katika uandishi wa makala na pia vitabu vya shule.
Istilahi za Kiswahili hupatikana kutokana na Kiswahili chenyewe na lahaja zake, pia lugha za makablia yetu na mwishowe kutohoa kutoka katika lugha za kigeni kama vile Kiingereza, Kiarabu na kadhalika.
Kukodi na Kukodisha
Kukodi ni kuchukua au kutumia kitu cha mtu mwingine kwa muda maalumu na baadaye kumrejeshea. Unaweza kukodi gari, nyumba au hata nguo za harusi.
Kukodisha ni kitendo cha kuruhusu kitu cha mtu kitumiwe na mtu mwingine. Mwenye kile kitu anakodisha wakati yule mhitaji anakodi. Maneno yanayofanana na hayo hapo juu ni kupanga na kupangisha. Mtu anapanga chumba wakati mwenye nyumba ndiye anayepangisha.
Katika kuendeleza mjadala huu unaohusu matumizi fasaha ya Kiswahili nitagusia juu ya maneno yanayoandikwa kwa kutenganisha badala ya kuunganishwa. Ieleweke kuwa neno moja huwakilisha dhana moja.
Kwa hiyo utaratibu wa kuunganisha au kutenganisha neno hutegamea dhana inayowakilishwa. Kwa mfano, yako maneno mawili yanayowakilisha dhana moja. Maneno haya yanatakiwa yaunganishwe. Maneno kama sawa sawa, vile vile, wazi wazi, mbali mbali, moja moja na mengine kama hayo huwakilisha dhana moja.
Kwa hiyo yanatakiwa yaunganishwe. Tunatakiwa kuandika mbalimbali, sawasawa, mojamoja, vilivile na waziwazi kama neno moja bila kuyatenganisha.
Source: www.mwananchi.co.tz makala ya Kiswahili na Stephen Maina.
NANUKUU :"SASA LEO HII Kijana wa Kitanzania anaona aibu kuongea lugha yake yakiswahili,Watu wachache wanaojifanya wako sawa na maendeleo ``Updated`` kumbe niwashamba watupu ususani kwenye vyombo vya habari ´´Media´´,Maofisini na sehemu wanazoziita za kishua, na kuna Wapumbavu wachache kwenye vyombo vya habari wanaowakatisha tamaa``discourage." MWISHO WA KUNUKUU.
ReplyDeletesikitiko sana kwa vijana wetu hasa kizazi kipya sijui watawafundisha lugha gani watoto wao,ukizingatia tuko mijini lugha za kina babu na bibi labda wanazisikia baada ya miaka wanapokwenda kusalimia huko wiki kadhaa, hasa watoto wetu walokisoma shule za english tupu ni shida huwa nawasikiliza wanangu wanakosa maneno ya kiswahili (misamiati) kwenye sentensi zao, endapo mnapokuwa mnazungumza na akiona neno la kuweka hapo limentatiza anakuwekea kiinglish kidogo. Na zaidi ni kiswahili cha kileo ndo usiseme baadhi ya watoto/vijana wamesahau kabisa kwamba kuna maneno ya kumsalimu au kuongea na mkubwa wako, au mtu unaeheshimiana. Inatishaa zaidi utakuta babamdogo /Ami au shangazi naongea na katoto ka kakake ka miaka mitatu au ka dadake MAMBO VIPI na katoto kanajibu POA hee, lugha za mtaani ndo zilizokithiri, sikatai kiswahili kimepanuka ila nafikiri itafika mahali tutakuwa tumepotoka kabisa na kufahau kiswahili fasaha.
Naishi nje ya nchi, naongea kiswahili na kukifundisha pia. Vilevile siku zote najifakharisha kuitwa Mswahili.Siku zote nawashajiisha wanangu kukiongea Kiswahili kwa talafudhi safi na herufi sawia.Lugha ya Kiswahili inasifiwa kuwa ni tamu ikilinganishwa na lugha nyingine za Kiafrika.
ReplyDeleteNaipenda Tanzania, najivunia kuwa Mswahili na nakipenda Kiswahili.
Mdau Uajemi.