Heshima kwako Mkuu wa wilaya ya nanii,
Hongera kwa libeneke lako! Naomba unitundikie hiyo mandahari ya hapa Durban Beach kama mfano wa kuigwa na wazee wa jiji  hapo Dar ili kumuunga mkono JK katika juhudi za kuwaamsha wazee hao wapendezeshe miji yao !!
Ahsante
Mdau Mhandisi,
Sauzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. This is wooow,nilivyoanza kusoma nilidhani Tanzania nilitaka niseme narudi kesho toka huku niliko kumbe South Africa,jamani kuzuri.Kama sio Africa!

    ReplyDelete
  2. Hivi ndio Tanzania wanatakak ufanya nyie hamjui mshaanza kumshambulia sasa hivi karibu na bahari hakutoruhusiwan yumba kujengwa itakuwa kama eneo la Oysterbay Hotel na Nyumba zinatakiwa ziwe mbali na Bahari.

    ReplyDelete
  3. Bravo Mdau Mhandisi SAUZI. I have been impressed by your photograph from South Africa, particularly Durban Beach. Had it been our political leaders and all stake holders concerned, were creative enough and innovative, capable of learning from others and implement what they have learnt from outside, I am sure Dar es Salaam City would not be in the shape and the condition it is for now. But allas, No one cares about the development and environmental sustainability of our cities. This is high time now our leaders who get the opportunities to visit different countries to bring real changes instead of practicing corruption and other unethical issues for thei own benefit.

    ReplyDelete
  4. Kuigiza ni vizuri, viongozi wanayo lawama ya kiasi -Fikiria uwezo wetu na kotofautisha na South Africa. Rasilimali zao ni bora kuliko zetu, halafu huo msingi na infrastructure iliwanzishwa na makaburu. Na kweli baada ya miaka zaidi ya 40 ya kujitawala wenyewe, tulikuwa tuwe mbali kuliko tulipo leo. Rushwa na uchoyo wa kibinafsi ni tatizo la Bara letu lote la Afrika, angalia viongozi kama Mugabe, anafanya maparty, nunua nyumba nchi za nje wakati wana-inchi wanateseka kwa njaa na magonjwa na wapinzani wanakabwa na kulainishwa wafuate amri zake !!! Pia ndugu mkumbuke kuwa miji mingi ya nje tunayoiona ni mizuri, inajengwa na kodi za makampuni, binafsi, sales tax, kodi za kutumia barabara, kodi za mali ya binafsi. Kwa mfano Marikani kuna kodi kibao: kuna Federal Income Tax-Kodi ya Taifa) State Income Tax- (Kodi ya Mkoa), County Taxes -kodi ya Wilaya, Car Taxes, Property taxes, Sales Tax kwa cho chote kile unachonunua kama ile VAT ya Uingereza, Dividends Tax, Airports, Fishing and Hunting Licences Fees, Toll/Highway charges, na vigumu sana kuzikwepa, wala hakuna mtu anaekufuata akulazimishe ulipe, ile system yenyewe ndio inakusanya kodi hizo na kupelekwa zinakohusu.
    Usisikie harafu nazuri ya chakula kwa jirani wako na umwambie mke wako akupikie na wewe wakati hujui gharama yake na jinsi walivyopatikana!
    Sammy -

    ReplyDelete
  5. Dar Es Salaam walishaharibu tangu wagawe beach plots kwa watu binafsi. Hivi leo tunabaki kulilia access to Coco Beach na Ocean Road beach tulizoachiwa na wakoloni, wakati tungeweza kuwa na beach Mbezi, Tegeta, Boko, Bunju, Kihalaka....

    Hata kama ni kujenga hiyo Durban, utaijenga wapi leo hii? Labda juu ya kichwa chako kama itaenea.

    TUNAHITAJI PROPER CITY PLANNING NA KUFUATA MASHARTI YA MIPANGO MIJI - DAR SIYO KIJIJI KIKUBWA

    ReplyDelete
  6. MKIONA NCHI INAPENDEZA MJUE KUWA WANANCHI WAKE WAMEPATA ELIMU YA URAIA HIVYO WANATABIA WA USAFI NA KUHESHIMU MALI YA UMMA.

    ReplyDelete
  7. Mdau Manispaa ya Moshi ipo hivyo aisee njoo uone

    ReplyDelete
  8. Roma haikujengwa siku moja...

    ReplyDelete
  9. nashukuru kwa mdau wewe kutuletea picha hiyo. Huo ni mfano tuu ambao wafanya maamuzi wa Dar wanaweza wakaona wengine wanafanyanini. Ni kweli Durbani hoteli ziko ngámbo ya barabara ya beach na ule upande wa beach unajengwa vizuri sana hata sehemu ya michezo ya watoto inapatikana hapo kuliko beach zetu za ajabu ajabu mfano pale posta wanaweza kupageuza pakawa pazuri tuu na wakanufaika napo kuliko hivi sasa palivyo sio suala eti hakuna eneo la kufanya hivyo eti labda kichwani kwake mhh!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...