I am fired-up for the life time Debate!
Kaka Michuzi na Wadu wote Kokote mliko,

Naomba kwa heshima nitumie lugha ya Kiswahili . Ikibidi nitakuwa ninatoa msisitizo juu kwa juu. Nafikiri wadau wamepaza sauti zao (loud and clear) sana kwenye Blog, ni lazima sauti hizo zisikilizwe ili watu tuendelee kufanya mijada yenye tija. Ninachotaka kumaanisha hapa ni kuwa kama kuna haja ya kufanya mdahalo (debate) wa ana kwa ana, nafikiri tuufanye. hakuna kitakacho haribika. If this mysterious US-blogger is a living soul, then hatuna upenyo wa kukwepa hii debate.

Mwanzoni nilishindwa kuelewa audience wa blog ya jamii ni watu wa aina gani, kwasababu ya mashambulizi yaliyokuwa yakilenga katika katika kuuwa character (character assassination) kuliko kujadili maswala ya msingi yanayolenga jamii zetu. Lakini baada ya kuwa na mijadala ya kina na upeo wa kimataifa, nimekuja kugundua kuwa blog ya jamii inafanya kazi nzuri sana kutuunganisha Watanzania, Waafrika, wakubwa kwa wadogo wasomi wenye Ma-PhDs na associates wakijadiliana pamoja. Haya ni maendeleo. Maendeleo sio mpaka tujengewe barabara ya Lami toka Chanika kwenda Mwanarumango peke yake, hata kula Ugali kwa kijiko yanaweka kuwa maendeleo inategemea na eneo unalotoka


John Mashaka sio John McCain, hawezi kutishia kutohudhuria mdahalo. I am first Tanzanian then African kwahiyo swala linalohusu nchi yangu nitaliipa umuhimu wa kwanza halafu yafuate maswala ya mataifa mengine. Sina wasiwasi na Mr John’s patriotism or love for his country, ila wasiwasi wangu ni kuwa anafikiri kutakuwepo na kushushiana heshima kwenye debate. Kwahiyo mdahalo kuhusu maendeleo ya Tanzania kati ya John Mashaka na US blogger (is long over due) imesubiriwa kwa muda mrefu sana.

Ili kuendelea kuwapa wadau kile wanacho hitaji, ninajitolea kwa mara nyingine kuwa moderator wa huo Mdahalo. Kama inawezekana tunaweza kuwasiliana na wadau wa blog ya jamii toka Bongo, mdahalo ukatangazwa live kwenye radio zetu nyumbani Tanzania. Kama wadau mnakumbuka, nilipotoa waraka mfupi kuhusiana na mvutano huu mimi nilisema na nina nukuu “…..the motion tabled by our own Mashaka John is very crucial and fair game for debate……the response dispatched by the US-based Blogger is painstakingly careful and intellectual……” mwisho wa kunukuu.

Ninatoa hoja binafsi, Debate Ifanyike Chuo Kikuu Cha Alabama- (Tuscaloosa) Mwezi wa May ( Memorial Weekend) ambako tunaweza kutumia resources za chuo ikiwa ni pamoja radio na television za serikali ya Wanafunzi kurusha matangazo hayo moja kwa moja (live) hata kwenye internet kama itahitajika inawezekana. Mimi niko tayari kushughulikia swala hili ninasubiri majibu ya hawa mabwana wawili ukubali wao ili tuweze kuleta debate.

Kaka Michuzi nikipata Majibu ya hawa jama kama wako tayari kushiriki, countdown kuelekea kwenye debate itakuwa inawekwa hapa kila wiki. Whether in Alabam au Harvard, nafikiri swala la debate halikwepeki. Nafikiri tatizo sio mahali pa debate bali nani wa ku-debate.

Mungu awabariki, Mungu Ibariki Tanzania

Wasiliana na mimi

Kuja WP
US
Email:

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. kwa kuwa mashaka pia hana shaka na mdahalo huo, ingekuwa vizuri huyo US BLOGER AJITAJE NAYE BASI.HUWEZI KUJIBIZANA NA KIVULI. ASEME YEYE NI NANI,YUPO WAPI MAREKANI,ANAFANYA NINI, ANATOKEA WAPI HAPA TZ NA NATAMANI TZ IWEJE.
    ZAIDI, sioni kwa nini kuongea au kujibizana na mtu asiyefahamika.
    kitu nyingine,wewew pia ni nani,wafanya nini huko,na unajitolea kwa masilahi gani ya taifa, kwani naamini hilo sio jina lako.

    ReplyDelete
  2. hiyo ni nzuri. naomba kama mambo yatakuwa sawa, uweke nafasi ya kuuliza maswali mainly kwa internet au hata simu.

    ReplyDelete
  3. ..wote mnataka publicity tuu,hakuna lolote la maana litakalosaidia maendeleo ya wananchi,kama kweli mnataka hii discussion iwe ya maana kwa nini usiwaalike watanzania na wadau wote wenye mawazo yao wachangie kuliko kutuletea ligi za mbuzi za kina mashaka na US blogger ambao nia yao ni kusikika tuu na ubishi wa copy & paste

    ReplyDelete
  4. we anon wa 4:23 mbona hujaweka jina lako na wala hujatueleza kwa wewe ni nani. mbona tunajadiliana hata kama hatukujui.

    nadhani hakuna haja ya kuweka ugumu (complications). cha msingi ni hoja na wala sio mtu. nadhani hiyo ni tabia na hulka ya kumsifia au kumdharau mtu hata kama hajasema kitu. utasikia wewe kaa chini huna lolote.

    naona kinachotafutwa hapa ni kumjua huyo mtu ili uone kama una ubavu wa kupambana. cha msingi kama uko tayari kwa masilahi ya nchi huna haja ya kujua sifa. kwanza mdahalo ni open, wote watakuwepo.

    mie nimemwona us blogger kama mtu mzuri tu kwani hatafuti sifa kwa watu kwa kujitangaza. anatoa hoja ili mradi sio matusi na kashfa. hatafuti uraisi au ubunge. anataka maendeleo ya taifa letu

    mdau wa arusha

    ReplyDelete
  5. Mbona huna heshima? umesema unatumia kiswahili.. lakini hapo kunaoenekana lugha mbili

    ReplyDelete
  6. Hi
    WASOMAJI WA HII BLOG YA MICHUZI
    NINAPENDA KUWAAMBIENI KUWA NITASHIRIKI KWA HALI NA MALI HUU MDAHALO. KUNA MAMBO MENGI YA KUJIFUNZA NA KUONGELEA.YENYE KUTAKA KULETA MWAMKO MPYA KWA MAENDELEO YA TANZANIA

    IKIFIKA SIKU YA SIKU TUPEANE TAARIFA NITAWAPA SIMU NUMBER YA KUWEZESHA MAWASILIANO.

    HATA KAMA MTATAKA VIDEO CONFERENCING, THEN, FROM LONDON, NITASHIRIKI

    WATANZANIA WENYE NIA NJEMA NA TAIFA LA KESHO LA TANZANIA, MSIOGOPE KUJITOKEZA KUTOA MAONI YENU KUHUSU NI WAPI TUNAKOSEA NA NI WAPI TUNATAKA KWENDA.

    WAKATI NI HUU.

    NAWAKILISHA

    ReplyDelete
  7. Hivi kama huyo US Blogger ni mtaalam wa debate, ni kweli kwamba midahalo yote ambayo inatangaza kuhusu Tanzania (ndani na nje ya nchi)huwa haioni au kuisikia? mbona hatujawahi (au walau mimi sijawahi) kumsikia akishiriki? Ningemshauri akaanzie kwenye midahalo ya namna hiyo, maana nafikiri hiyo ndiyo yenye maslahi zaidi kwa taifa kuliko hii midahalo ya jazba na ushabiki ambayo anaishupalia hapa. Huko ndiko tutakakoweza kuona na kupima uwezo wa mtu na uchungu wake kwa Taifa letu. Sio tu kutaka kupata sifa hapa kwa Michuzi (sifa ambazo hazikusaidii chochote), tunataka kitu ambacho hata mataifa mengine ya jirani wakisikia wapate kitu cha kujifunza na sio kutubeza. Kwanza hatukujui wewe ni nani na una nia gani na nchi yetu. Walau Mashaka tunamjua kwa jina na hata kwa sura pia. Inawezekana huyo ni miongoni mwa wale wanaotaka makao makuu ya EA yaondolewe Arusha. Mtu akishasema hataki ni bora kumwacha ili akili yake iweze kuwa huru na aendelee na mambo mengine. Hiyo debate hatuitaki (period)

    ReplyDelete
  8. We uliyeleta mada acha kimbelembele. Unajua maana ya debate au? Hii unayotafuta wewe ni ligi sio debate. Naona we ndio mwenye shida ya ligi. Mwenye mchango aweke hapa kwenye blog ya jamii wote wasome, wajadili. "Oh! Mi ntaandaa hiki na kile..." Huna shughuli ya kufanya?

    ReplyDelete
  9. Nadhani debate itakuwa ngumu kujua mshindi ni nani. Mimi napendekeza Masumbwi. Jamani kama kuna promota afadhili pambano hilo ili tujue nani mbabe. Hamna issue nyingine hapa zaidi ya nani zaidi. Masumbwi yatatoa jibu kamili, bila bias!!

    ReplyDelete
  10. Jamani tuwe makini, mdahalo utafanyikaje Alabama?

    Halafu wote hawa US blogger na Mashaka, wasituchefue. Hawajawahi kuhudhuria kitu chochote cha maana duniani wala kupata tuzo ya kitu chochote maishani. Nawshauri waendelee na blogu ya jamii kusema lolote linalowasumbua vichwani.

    Msitupotezee muda jamani. Wanaume wametulia tu. Kuna Mtanzania alialikwa kwenye Mkutano wa Uchumi wa Dunia, hakusema kitu, huu wa London kuna Watanzania watatu wana mialiko, hawajasema kitu, kule Davo Wabongo wawili walitinga hawakusema kitu, na kuna Mkutano mwingine utafanyika South Africa na mbongo mmoja anakwenda, unahusu uchumi. Hata wa Dar es Salaam tu akina Mashala na US blogger hawakualikwa.

    Haya ni mambo ya kitoto fulani hivi.

    Ehe, endeleeni.

    ReplyDelete
  11. WEWE MDAU UNAYEHITAJI MJADALA, UNA TABIA YA UMBEA NA KURUSHA VIJINENO N A NDIYO MAANA SHAYO AKAWAITA WASWAHILI...MNATEMBEA NA MISWAKI YA MITI KILA KUKICHA KAZI KUJICHOKONOA MENO MKIDAI ETI HUO NI MDAA.

    KWA TAARIFA...HII BLOG NI KAMA BARAZA LA KAHAWA PALE KIEMBE SAMAKI, MWEMBENI, MALINDI, KIVUJA KIKWAPA, SAMAKI MASHAVU NA KWA MZEE KIDAGALA NKIA.

    UTAKACHOKIONA HUMU NDANI, UTAKALOSOMA HUMU NDANI, UTAKALOTUKANWA HUMU NDANI, UTAKALOFUNDISHA HUMU NDANI, UTAKAFUNDWA HUMU NDANI, BASI ULIACHE HUMU HUMU NDANI.

    UKITOKA TU (UKIBONYEZA X NYEKUNDU UPANDE WA JUU KULIA KWENYE KOMPYUTA YAKO), HUMU NDANI, JIFANYE KAMA VILE ULIKUWA CHOONI UNAJISAIDIA HAJA KUBWA. KUTOKA NJE UMEKUTANA NA ALIYEKUZALIA MKEO... KIMYA KAMA UNAAGULIWA VILE. TEHETEHEE...MDAHALO WAUJUA WEYE

    ReplyDelete
  12. MSIWE NA USHABIKI WA KIJINGA,WATU WAWILI AMBAO WOTE WANA MAWAZO SAWA YA KUTAKA NCHI YAO IENDELEE MMEENDA KUWAFANYA WAONEKANE KAMA MAADUI BILA SABABU KWA VILE MMOJA ANATAKA HAONEKANE ZAIDI.NDIO NAMUUNGA HAPO MASHAKA JE HUYU MMOJA AKIONEKANA ZAIDI ITAWASAIDIA NINI WATANZANIA AU NCHI YA TANZANIA? KWANINI HUYO US BLOGGER AIUNGANE NA WENZAKE DR.SHAYO NA MASHAKA HILI WAFANYE MAMBO YA KUSAIDIA NCHI IENDELEE? WENZAKE WASHAJIUNGA KWANINI YEYE BADO ANATAKA KUWA INVISIBLE? ANA AJENDA GANI YA SIRI AMBAYO ANAJIONA YEYE NI BORA NA HAWEZI KUUNGANA NA WENZAKE? NCHI CHANGA AMBAYO IMEKUMBWA NA UMASKINI WA HALI YA JUU NA UBADHILIFU MKUBWA HATUITAJI MGAWANYIKO TUNAITAJI MUUNGANO HILI TUJIKOMBOE.
    mdau cha "mtu mavi"

    ReplyDelete
  13. This leaves to question on tanzanians mashaka has become a sensation. Mashaka ur increadible

    ReplyDelete
  14. huyu mdudu aliyekuwa fired up, kwani yy ni nani, tunataka kumjua kwa maana yeye ndiye yule mzoga US-blogger, wote hawa wanatafuta umaarufu kupitia mgongo wa mashaka. mashaka jihadhari na hawa watu hawana lolote

    ReplyDelete
  15. Mimi namuuliza huyu muandaaji ? Unajuaje huyo US-based blogger yupo kweli USA? na kama yupo umejuaje ni mwanaume? Na je kama anataka bado kuremain anonymous itakuaje kwako. na kama hana muda wa kutravel kuja huko AL itakuaje? Think about that

    ReplyDelete
  16. Hivi wewe muuandaaji, una akili timamu mweli? Mbona una tabia za kimbea kimbea?

    Nani kakuomba usimamie mjadala? au ndo uchizi huo, je kama US-Blogger hana muda itakuwaje? Bwana kula kona wewe kishambenga fulani wewe

    ReplyDelete
  17. (US Blogger)

    Kuja WP.

    Thank you for taking the initiate to facilitate this proposed debate and for your willingness to moderate.

    I also want to thank Dr. Shayo for supporting the idea + those who have taken similar position in the past like Bongo Radio.

    I am ready to come to Alabama.I am requesting a confirmation by April 10th so that all participants can plan accordingly.

    I look forward to meeting with you in Alabama unless Mr. Mashaka turns down the offer.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  18. Wadau
    Tuijenga jamii yenye uwezo wa kujadiliana kwa kuheshimu mawazo ya wengine. Vyombo vikubwa na vinavyoheshimika duniani ni vya Mijadala, Bunge Senate mbalimbali duniani kote . Mdahalo ni njia mojawapo unaoweza kuchochea ufanisi na ushiriki (enthusiasm). Umaarufu sio shida, shida ni nani atakuwa tayari kuchukua urithi wa uongozi wa nchi yetu wakati viongozi wa sasa 15 years from now watakuwa senior citzens. Ni jukumu letu sisi Vijana Kujengana sisi kwa sisi, tukisubiri kupelekwa Dodoma kwanza ndo tujifunze kujadiliana ndo matokeo yake tunamtukana Spika, au kutolewa nje ya ukumbi kwa kutoa kauli chafu. Hivi Karibuni Prof: Lipumba alimuomba Rais aitishe mjadala wa Kitaifa kuhusu matatizo ya Wananchi. Au Lipumba naye anataka umaarufu! Swala la Debate binafsi sioni ubaya wake.
    Dr Shayo, thumbs up! Bado ninasubiria Majibu ya hawa vijana wawili kama wanaweza kushiriki otherwise tutakuja na alternative. Lakini swala la Debate liko palepale. I respect Mashaka more than you guys could think, sice I knew him before his name was mentioned anywhere in the media.
    Tuendelee kujadiliana wadau!
    I am not the US Bolgger, but the prospective Moderator!

    ReplyDelete
  19. we jamaa (hakuna cha mdau hapa) wa 5;16pm unayesema mashaka anajulikana kwneye vyombo vya habari kwani ni JOE THE PLUMBER HUYO.
    Hebu tupunguzieni mashuzi humu.

    ReplyDelete
  20. Mkasome kitabu kinaitwa "Animal Farm" ili muondokane na huu upuuzi mnaoleta kwa michuzi kila siku

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...