Brother michuzi,
naomba uweke hii kuwashituwa wadau wenzagu waishio uk.
Nimesoma katika gazeti jana na kuona katika tv leo hii asubuhi kuwa tangu kuonyeshwa wale macelebrity waliopanda mlima kilimanjaro kwa ajili ya comic relief kumekuwepo na wimbi kubwa la watu kuulizia holiday za tanzania.
Pia kumekuwepo na ongezeko kubwa la watu kutaka kuchukuwa likizo ya kupanda mlima kilimanjaro. hii ni habari nzuri kwa wizara ya utalii na serikali kwa ujumla, lakini kwa wale ambao wana desturi ya kwenda nyumbani june to august au wale wanaokusudia kwenda mwaka huu katika kipindi hicho ni vizuri waanze kununua tiketi toka sasa, kwani definetely zitapaa mwaka huu
mdau UK

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Mdau asante kwa taarifa, lakini ungetueleza ni gazeti gani(link) na channel gani za TV huko Uingereza zimepata hamu ya kuijua Tz ili tusome habari hizo kwa kina.

    ReplyDelete
  2. Habari nzuri, ila ungetupatia source hizo na webusaiti zao ili tuwa fanyie info 'bomberdment' za uhakika kuhusu webusaiti za Ngorongoro, village-cottage, mafia, Kitulo plateau(waka-ski ktk barafu)n.k

    Maana sije watani zetu wa jadi wakasema hayo uliyoyasoma ktk magazeti na kuona ktk TV, yote yako kwa watani wa jadi.

    ReplyDelete
  3. alosema mdau ni kweli hata mimi nimeona hii leo asubuhi saa moja ya huku katika BBC walikuwa wanajadili issue yote ya red nose day. na kweli wamesema kumekuwepo na ongezeko la watu wanaoulizia likizo za tanzania pamoja na trek za kilimanjaro. kusema kweli kama alivyosema mdau hata mimi nilifikiri hivyo hivyo kuwa mwaka huu tutakoma na bei za ndege kwenda nyumbani!!! ahhhhhhhhhh!!!!!!

    ReplyDelete
  4. chonde chonde maaofisa wetu wa ubalozini, msije mkalaemaa wageni wakachukuliwa na makampuni ya wenzetu japo kuwa juzi nchi zote zilikuwa hapa kuwashawishi wawekezaji waende EA

    ndiyo mlima wamepanda ila nilikuwa nasubiri credit ziende kwa jitihada za ubalozi wetu kumbe zilikuwa za nchi jirani!

    ReplyDelete
  5. Gazeti ambalo lilikava habari za wale macelebrity ni the sun na ukiende kwenye google na kusearch website ya gazeti hilo The sun utapata maelezo hayo lakini kuhusu Tvkwa kusema ukwli mimi mdau wa Uk sijaona kucover sana kwenye TV ila clip zao zote wameziweka kwenye the sun website mpaka wala jamaa waliokuwa wanasindikiza walikuwa wanaimba wazungu wetu...............Narudu kuwatafutia link ya the sun


    Kenge

    ReplyDelete
  6. link ni hii hapa http://www.thesun.co.uk
    Angaliani tarehe 16 lakini kama nilivyowaambia hapo hawali sifahamu link ya TV na sijui mdau amabye ameandika amepata wapi link hiyo pia ni kweli makampuuni mengi ya travel agency yanatangaza parkage za kutembelea tanzania na kupanda mount Kilimanjo

    Kenge

    ReplyDelete
  7. sikieni hii nyengine, nikiwa kazini kuna jamaa kashikilia kuwa sio tu mlima kilimanjaro uko kenya bali ni mlima uko nchini kenya katika mji unaoitwa tanzania! nilitaka kuzimia!

    ReplyDelete
  8. hio ni kweli,kwani hata mimi nimeona ktk CNN europer wakionyesha mara kwa mara habari za Bongo,na kesho tuesday ktk Inside Africa wataonyesha tena Bongo,kwahio tunaomba mukze kamba huko mpaka kieleweka,toeni habari kwa wingi kuwapa hao waandishi wa bbc/cnn/n.k, hao ndio ambao wanangárisha huku juu jina la Bongo, thanks

    ReplyDelete
  9. Hili ni somo linajirudiarudia lakini hatufundishiki. Mlima Kilimanjaro ni wetu, tuutumie. Sio mlima wetu lakini Wakenya wanakula robo tatu ya mapato ya watalii kutokana na mlima huo. Ubalozi wa Uingereza, Wizara ya Utalii, makampuni binafsi ya tours mpo? Wimbi hilo, pandeni msafiri nalo.

    ReplyDelete
  10. Tatizo ni kuwa Ubalozi wetu hapa London si wabunifu...Jambo lilikuwa rahisi kutoa vipeperushi na kuajili vijana wa kuvigawa kwa wenye hela(central London)Pia wangefanya mikakati ya
    mahusiano kwa kutembelea bankers hata kwenye vyuo na kuhamasisha waje kutembelea.Ajabu matangazo yamewekwa vituo vya treni vya pembeni ya mji na kwenye mabasi tu na gharama iliyotumika sijui hata kama imeleta matunda.....Tuwe wabunifu jamani Watanzania.Mi naona bora kutoa matangazo kwenye magazeti ya bure kila siku kwa mwezi mmoja ina manufaa kuliko kuweka matangazo kwenye mabasi wengi hawtayaona kama mimi tu,yaani inaniuma kweli.......Michuzi tafadhari nakuomba usibane maoni yangu

    ReplyDelete
  11. miniliona hiyo programme kwenye discovery channels,walionyesha trip nzima mpk juu kileleni na baadhi ya hsp za jirani na jins hiyo hela itakapokwenda wanapotaka kuipeleka.

    ReplyDelete
  12. kuonyeshwa kwenye tv ni moja na waliokwenda wakirudi na feedbacks zao ni second.

    niliona kwa jay leno siku moja, yule mwanamke aliyekua ana act kwenye jerry sinfield[sp]show. walikua wanamhoji akasema alikua summer vacation tz.walivyomuuliza how was it, jibu halikua zuri. alisema ukiona tembo kwa mara ya kwanza unafurahi, then another elephant, then another one. mwishowe hutaki kuwaona tena....ushauri kuwe na vivutio vingine [be creative people}vikiambatana na hiyo kutazama wanyama.hawa watu wepesi kuwa bored sana and they always speak their minds.

    ReplyDelete
  13. Naungana na kilio cha wadau wengi kuhusu tunavyopigwa bao la kisigino na watani zetu.
    Ila ushauri wangu kwanza ni kwa serikali kuurekebisha uwanja wa ndege na kuliendeleza shirika la ndege la bongo,au la wawekeze Precission Air.
    Uwanja wa Jomo Kenyata unachoice nyingi za flight kitu ambacho kinashusha sana gharama za ticket.Ndege za Ulaya zinazohudumia JK Nyerere ni chache mno,tatu kama sikosei,KIA kwenyewe ndio KLM tu.
    Sasa baada ya hapo ndio tuendelee na kujinadi!!!

    ReplyDelete
  14. Watanzania wengi hasa wanaopewa kuwajibika na kutangaza hawafanyi kazi ipasavyo.Sasa kama jirani ameona window of oppurtunity na wewe umelala fofofo kwa nini asiitumie??Mimi ni mtanzania na naishi London kwa kufupi ni kwamba hatufanyi juhudi za makusudi katika kutangaza nchi yetu,inamaana hatuna mawazo bunifu ya kufanya utafiti wa namna ya kujinadi kwa manufaa na kisasa kwa gharama nafuu.Mi sijasomea marketing wala advertsing ila kwa akili ndogo niliyonayo nashauri wizara zote na ubalozi wawe na blog zitakazoruhusu watu wa kawaida kutoa maaoni yao ili mazuri wayafanyie kazi waachane na siasa za Mao na KGB usiri katika kila jambo.Wenzenu wachina hamuwaoni wajanja wamebadirika wamebadiri mtazamo na policy zao wanafanya biashara nzuri sasa.Mwisho,siyo dhambi kukodi mtaalam kutangaza utalii kutoka nchi zenye kuvuitia watalii wengi duniani kama Uswisi na kusaidiwa kujitangaza.Ni ushauri wa bure to kutoka kwa mwananchi mkereketwa

    ReplyDelete
  15. POOR TANZANIANS muda wote ni kulalamikia jirani anayefanya vizuri.Tufanye utafiti kwani ni wapi wanapotuzidi ujanja ili tuwapiku.Ni rahisi na haihitaji Masters degree wala fedha kutoka kwa wafadhiri....!

    ReplyDelete
  16. Ama kweli Wazungu waliaribu akili za watu weusi, yaani watu mnalumbana, kujisifia na kugombania Wazungu mashuhuri wamekuja Tanzania na kupanda Mlima Kilimanjaro. Wengine mmediliki kusema kabisa kwamba kuna wachache ambao walikuja na kuona tembo, walipoona tembo mara ya pili na tatu, wakakinai.. So what the F%&*?
    You can't please evrybody. And just because somebody didn't like everything he/she saw in Tanzania, shouldn't make you small. Kama Wazungu wanakuja Tanzania kupitia Kenya, ni kosa la nani? Letu au Wakenya? It's shame. F*&%^

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...