JK akisalimiana na kocha marcio maximo ikulu dar wakati alipokula dina la mchana na wachezaji na viongozi wa timu hiyo kabla hawajaenda ivory coast kwenye michezo ya CHAN.
HABARI ZINASEMA MARCIO MAXIMO AMEKUBALI KUMWAGA WINO NA KUBAKI BONGO KWA MWAKA MMOJA ZAIDI BAADA YA KUONGEA NA 'WAHUSIKA' WAKUU WA UJIO WAKE HAPA BONGO USIKU WA KUAMKIA LEO.
RAIS WA TFF LEODEGAR CHILLA TENGA AKIONGEA NA WAANDISHI LEO, AMETHIBITISHA KWAMBA MAXIMO KESHAKUBALI KUONGEZA MKATABA WA MWAKA MMOJA, NA KILICHOBAKIA SASA NI YEYE KUANGUKA WINO TU.
GLOBU YA JAMII IMEONGEA NA MAXIMO KWA SIMU SASA HIVI KUTAKA KUJUA UKWELI, LAKINI KAITOLEA NJE NA HAKUKUBALI WALA KUKATAA JAMBO HILO, AKISISITIZA KWAMBA MAMBO BADO YAKIWA BIEN TUTAJULISHWA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. JAMANI SASA HUYU MWAKA MMOJA WA NINI TENA JAMANI? NA HUYU BADO UWEZO WAKE MDOGO JAMANI MBONA TAIFA LINAZIDI KUPOTEZA PESA NYINGI KUMLIPA MTU ANAYEFUNDISHA FASHION SHOW WEWE FIKIRIA HELA ANAZOLIPWA HUYU TUNGEKUWA TUNAVUTAVUTA BARABARA YA KWENDA KWETU SONGE INGEFIKIA WAPI MTU JAMANI HATA KOMBE LA MBUZI HANA KWENYE MKONO WATU BADO MNANGANGANIA WANINI HUYU AONDOKE BWANAAAAAAAAAAAAAAAAAAA SIO KIIVYO

    MDAU MWENYE UCHUNGU NA NNCHI YAKE NGATUNGA TMK.......

    ReplyDelete
  2. Bado huyu coach anahitajika kwa si chini ya miaka mitatu zaidi. Ndio kwanza safari inaanza. Pia vilabu vya ligi kuu vimsaidie sana, sitegemei vijana wakajifunze mambo mengi timu ya taifa. Pale wanakwenda watu walioiva kistadi za mchezo, nidhamu, malengo ya kufika mbali (sio Simba na Yanga kama vijana wengi wanavyodhani).

    Hongera sana Maximo aluta continua.......

    ReplyDelete
  3. Hureeeeeeeeeeeeee!sasa Maximo tuandalie timu ya CHAN 2011 na CAN 2012.Hongera Tenga na wadau wengine mliomshawishi kuongeza mkataba maana magazeti ya Angola yalishaanza kumpigia ndogondogo achukuliwe kwao.

    ReplyDelete
  4. Hureeeeeeeeeeeeee!sasa Maximo tuandalie timu ya CHAN 2011 na CAN 2012.Hongera Tenga na wadau wengine mliomshawishi kuongeza mkataba maana magazeti ya Angola yalishaanza kumpigia ndogondogo achukuliwe kwao.

    ReplyDelete
  5. Tumekufa sasa,
    Mkataba wa mwaka mmoja anaongezewa ili tushiriki mashindano gani yaliyopo mbele yetu jamani?
    Tanzania wil never win anything under Maximo leadership.

    ReplyDelete
  6. sijui nicheke au nilie kwa taarifa hii

    ReplyDelete
  7. Maximo ameleta mapinduzi ya soka Tanzania lkn sidhani kama alikuwa anahitaji kuongezewa mkataba. Tunahitaji mtu mwenye mawazo mapya zaidi ya Maximo aendeleze na kuboresha alichoanzisha Maximo. Mazuri yote aliyotufanyia kama kuifikisha taifa star hapo ilipo, kuleta amasa kwa wananchi kuipenda timu yao, kushawishi wadhamini nk...Maximo mpaka leo hana kikosi cha kudumu taifa star, mnategema nini toka kwa Maximo?? Maximo ametengenza makundi ndani ya timu, ameleta umungu mtu, ana masiha ya visasi, mpaka leo ameshindwa kumsamehe Kaseja, leo tumesikia kawatimua kina chuji na boban...sidhani kama huo mwaka utaleta mabadiliko ya kweli zaidi ya kutukazazi sie wadau tuliokata tamaa na soka la kibongo.
    Mungu ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  8. Sasa Michuzi inakuwaje?? kama Maximo hajakubali wala kukataa unawezaje kupost habari hii na kusema Breekkkkiiiing nyuuuuuzi? Wahusika unaosema wameongea naye ni kina nani?? kwanini unaficha ficha mambo? Tupe habari kamili.....Kuna waalimu nimewakuta wanakunywa beer saa za kazi mchana huu mitaa ya wilaya yako!! utaratibu wa kuwachapa viboko ukoje au ni hadi wafelishe wanafunzi tu?

    ReplyDelete
  9. Jamaa katikisa hadi kapata alichotaka. Natanguliza pole kwa wadanganyika!!

    ReplyDelete
  10. Hii ni habari mbaya kwa soka la Tanzania.
    Ni dhahiri Maximo kafanya mazuri kwa soka letu lakini pia huu ulikuwa wakati muafaka wa yeye kumpisha mwingine. Sijui kwa nini akina Tenga hawalioni hili. Au kwa kuwa mshahara ukichelewa hana kelele?
    Kwa kuwa itabidi tuubebe huu mzigo wa Maximo nashauri (sijui nani atampa ujumbe huu) awape wafungwa wake nafasi ya pili. Nina maana akina Kaseja.

    ReplyDelete
  11. Bwana Michuzi naona na wewe unaendeleza utamaduni wakipumbavu kama waandishi wenzako wabongo wakuandika vichwa vya habari ambavyo habari yeyewe inakuwa tofauti kabisa. hivi ujinga huu mtaacha lini? Wewe unasema Kocha amekubali mkataba alafu ukisoma maelezo unasema mwenyewe amesema mambo bado hayajawa tayari yakiwa tayari atakufahamisha. Sasa kwanini kichwa cha habari kiwe kocha akubali mkataba? Hivyo ndivyo mekuwa mkiuposha umma miaka yote hivi mnajua wajibu wenu kama waandishi wa habari kwenye jamii? Kwanini huwa hamfanyii uchunguzi habari zenu kabla yakuziripoti? Na kama basi habari zinakuwa ni tetesi bado semeni hivyo basi na punde mnapokuwa na uhakika wa habari zenyewe warudieni wananchi na kuwaeleza mwendeleo wa habari iliyokuwa tetesi.Msiishe tu kuripoti walichosema watu au mlichosikia alafu habari inakuwa imekwisha.Baada yakuripoti habari uliikia au kuifuatilia ichambue habari yenyewe elezea wananchi upungufu uliokuwepo kwa alietoa maelezo. Kwa mfano habari ilioripotiwa kwenye nipashe kuwa wazii mkuu ametaka kampuni inayomiliki mapato ya ubongo ichunguzwe lakini wakati huo huo waziri anasema yeye hafamu miliki wahio kampuni. KWELI HII INAWEZEKANA? Na mwandishi ameshia tu kusema hapo badala ya kuendelea kuwaonyesha wananchi kuwa hadithi hii ya waziri mkuu inautata mkubwa sana. huo ni mfano mmoja wapo tu kati ha habari zote mnatoyuandikia. Wakati mwingine tunajiuliza kwenye nyinyi ni waandishi wa habari? Mzee kama wewe wa Dairly News unaboronga kiasi hiki inakuwaje?

    ReplyDelete
  12. Hoyaaa!!!!!!Maximo endeleza lebeneke la soka Tanzania, kwani unaitajika sana tu, Hao wengine ni longolongo tu, Huko nyuma bongo ilikua bwelele hata mpira hauonekani,Hongera mkuu, na ingia hatua nyingine mpya ya soka kwa Tanzainia yetu, kila kona waitambue soka ya bongo.

    ReplyDelete
  13. Jamani tuwe waangalifu katika kukosoa.Na tuwe makini zaidi katika kuchambua habari!Alichokisema hapa Michuzi ni kwamba,sasa kwa uhakika Serikali imethibitisha kukubali kumpa Kocha Maximo mkataba mwingine wa mwaka mmoja zaidi.Kinachosubiriwa kwa hivi sasa ni yeye mwenyewe kutia saini makubaliano ya mkataba huo.Na kwamba,katika hali yeyote ile hakuna sababu zitakazo mfanya Maximo asikubali nyongeza hiyo ya mkataba wa mwaka mmoja,kwasababu hapo awali alishasikika Maximo kwa kauli yake mwenyewe akitamka kwamba yeye hana hiana yeyote ya kuendelea kufundisha Soka nchini Tanzania,iwapo serikali itaridhia kumpa mkataba mwingine wa kubakia nchini kufundisha soka.Na alipoulizwa na Michuzi kwa simu,Maximo alimjibu kwamba,asiwe na mchecheto,afanye subira,akishamwaga wino mambo yote yatakuwa hadharani.Sijui kama nimepotoka,Michuzi mwenyewe atanisahihisha hapa.Lakini cha muhimu nilichotaka kuzungumzia hapa ni kuipongeza serikali kwa uamuzi wake huo.Ni uamuzi wa busara sana.Na nina amini kwamba huu bila shaka utakuwa ni mkataba wake wa mwisho Maximo kufundisha Taifa Stars labda miujiza itokee afanikiwe kuifikisha Taifa Stars kwenye kilele cha mafanikio ambacho hakikutarajiwa na wengi na yeye mwenyewe akakubali bado kuendelea na mkataba mwingine mpya hapa nchini.Mwaka mmoja kwa ukocha wa soka sio muda mrefu,ni mfupi sana!Taifa limeshawekeza sana kwa Maximo katika kipindi hichi kifupi alichokuwepo hapa nchini.Ingekuwa hasara kubwa zaidi kwa Taifa kumwachia aondoke hivi sasa angalau Taifa Stars ikiwa imeonyesha mabadiliko makubwa sana katika ubora wa kusakata kabumbu!Katika muda huu wa mwaka mmoja,ni busara pengine iwapo Maximo atapangiwa kutoa mafunzo ya muda mfupi ya Ukocha wa Soka kwa Makocha wetu wanaochipukia hapa nchini pamoja na mambo mengine atakayo pangiwa kuyafanya.Katika mashindano yaliyopita huko Ivory Coast Taifa Stars ingeweza kabisa kufika Robo Fainali na pengine hata Nusu Fainali kama isingekuwa Uzembe wa Wachezaji wenyewe kuota mapembe hata kabla ya kipenga cha mwisho.Kwa hiyo tumpe ushirikiano Maximo katika muda huu mfupi uliobakia badala ya kupoteza muda kuendelea kumsakama kwa maneno ya kuvunja moyo.

    ReplyDelete
  14. Inaelekea kuna wadau nia yao ni kuwa na kikosi cha kudumu tu Taifa Stars. Hapo ndipo Maximo ataonekana anafaa. Kwa mtazamo wangu kinachohitajika ni nidhamu na kujituma kuichezea timu ya Taifa. Miaka ya nyuma, ilikuwa ni rahisi sana kutaja timu ya Taifa kwa sababu ya majina. Maximo amejitahidi kuondoa hiyo kasumba, ambayo ni sumu.

    Sasa ukiwa na kikosi cha kudumu(milele), hao wengine watapata lini nafasi ya kuonyesha vipaji vyao, na wapo wachezaji wengi tu.

    Uanachana wa Simba, Yanga, CCM, CUF, CHADEMA, unaweza kuwa wa kudumu. Timu ya Taifa ni nidhamu na kujituma. Mwenye kuamua ni kocha, ushauri anaopewa unaweza kuwa ni mzuri, lakini halazimiki kuukubali.

    ReplyDelete
  15. NASIKIA KICHEFUCHEFU HATA KUISIKZA HIYO TAIFA STAZ,MAXIMO NA APEWE HUO MKATABA NADHANI NDO KWANZA ITANICHOCHEA KUPENDA CLUB NA TIMU ZA NJE!MAANA HAIWEZAKANI MTU KAMA MAXIMO ATUKOSESHE RAHA WATU NA HASIRA ZAKE ZA KIKE....,WENYEWE WADAU MMEONA KAMBANIA KASEJA GHARAMA ZAKE TUMEZIONA,LEO HII AMEMBANIA CHUJI NA BOBANI BS TUTAENDELEA KUONJA LADHA YA HIYO GHARAMA,HIYO MIHELA ANYOPEWA MAXIMO ALET SAY WANGEPEWA MAKOCHA WA NDANI SI TUNGEKUWA MBALI?NAKUMBUKA USEMI WA WENGI NA NAENDA KKUAMINI SASA KUWA MAKOCH AWA NJE HAWAWEZI KULETA USHINDI AU UBINGWA KWA NCHI NYAING ZA KIAFRICA MIFANO IPO WENYEWE MNAJUA,MISRI ILE PALE,CONGO DRC KAMA KAWA,ANGOLA NDO KABISA,ZAMBIA JE?NAWAKILISHA WADAU

    ReplyDelete
  16. Samahani wadau, Hivi kuna anajua malipo kamili ya huyu Maximo?
    Nasikia analipwa mkwanja wa nguvu ila sijawahi kupata figure kamili, please help.

    Wakola

    ReplyDelete
  17. CONGRATULATIONS MR.MAXIMO.WEWE NDIO KOCHA UNAYEFAA.NA SASA NIDHAMU ITAKUWA 100% WATANZANIA WENGI WANAELEWA KAZI KUBWA ULIYOFANYA KUTUFIKISHA HAPA.KEEP IT UP.

    ReplyDelete
  18. Hongera sana Maximo kwa kazi nzuri uliyofanya ya kukuza soka letu kutoka huko ulikotukuta wakati tukichechemea.una kila haki ya kupewa mkataba mpya na pia bonus.
    Congratulations Maximo.Kuwa mkali hivyo hivyo ili nidhamu iwepo.

    ReplyDelete
  19. Maximo oyeeee, wenye wivu wajinyonge.

    ReplyDelete
  20. Mimi nashindwa elewa hapa hasahasa mnaosema hatuwezi shinda chocgote under Maximo leadership.
    Kabla ya kuwa naye tulishinda nini?.
    Mpira Tanzania hautaendelea kama tunashindwa kuelewa kuwa mpira ni nafasi ya Kocha, nakama Baba ndani ya nyumba Wachezaji ni Lazima wamuheshimu Kocha bila heshima hata sehemu ya Kazi inakuwa chungu.
    Habari ya kuwakumbatia wachezaji hata kama wana nidhamu mbaya muda wake umepitwa na wakati.
    Hao kina CHuji walidhani anaondoka wakaleta za kuleta sasa wanajuta na bado ukiisha anaongezewa mwingine wa miaka mitanokwa ajili ya kuiandaa timu na World Cup 2014-Brazil

    ReplyDelete
  21. Maximo akitumia wachezaji wa Yanga wanawafunga waarabu wa sudan huko Khartoum. Wachezaji hao hao wakienda kwa Kondic wanapoteza mwelekeo wanachukua thelatha kwa waarabu wa Misri. Wanaodai Maximo hana lolote waangalie hilo. Wengine kelele nyiiingi kumlaani wakati hawaiungi mkono timu ya taifa japo kwa kulipa viingilio kuangalia mechi. Noma sana.

    ReplyDelete
  22. Haya mnaomtetea maksimo

    Si alijifanya kuwa kapata timu kuwait?aende basi atuachie soka letu.Sijui kwa nini watu hawaelewi.Maksimo kapata bahati ya kufundisha soka ktk mazingira mazuri ndo maana anaonekana anafaa.Hana uzuri wowote.kibaya zaidi ni mgumu kufanya naye kazi si mnaona hata wabrazil wenzake wamemkimbia ?
    haya tuendeleze tu uozo hata katika sekta ya michezo.anajidai kuanza kuunda timu nyingine ya nne wakati mpaka leo ana timu tatu tayari.wenye kumbukumbu mnakumbuka alihaidi nini alipofika ?mbabaishaji huyu .nina wasiwasi kama wanaomshabikia washawahi hata kuchezea timu ya darasa utotoni

    ReplyDelete
  23. BAADHI YA WATU WANA CHUKI ZISIZO ZA MSINGI NA MAXIMO.HAWASEMI SABABU GANI HAFAI.HAKUNA GROUND ZOZOTE ZINAZOWEZA KUONYESHA WEAKNESS ZA MAXIMO ZAIDI TUMEONA MAFANIKIO AMBAYO HAYAWEZI KUPUUZWA.NINACHOONA SABABU KWANINI BAADHI YETU WANAMCHUKIA NI KUWA NI KOCHA ANAYEFUATA NIDHAMU HAJALI WEWE NI NANI ILI MRADI UTIMIZE WAJIBU WAKO.KAMA WANASEMA HAFAI MBONA KATUTOA MBALI KWA KIPINDI KIFUPI CHA MIAKA MIWILI NA NUSU.JAMANI TUWE WAKWELI TUWEKE PEMBENI TOFAUTI ZA UYANGA NA USIMBA NA TUTAMBUE MAFANIKIO ALIYOYALETA KOCHA WETU.TUMPE USHIRIKIANO.KUMBUKENI NIDHAMU KWENYE TIMU NI LAZIMA HAKUNA MCHEZAJI ALIYE JUU YA NIDHAMU.HUNA NIDHAMU HUFAI HAKUNA KUBEMBELEZWA TUMESHINDWA KUONA WACHEZAJI WA AFRICA WANAOCHEZA MPIRA WA KULIPWA WALIVYO NA NIDHAMU KWA NINI WACHEZAJI WETU WASIIGE KWA AJILI YA MAFANIKIO YAO.TUJIFUNZE

    ReplyDelete
  24. maximo hana timu inawweza kumchukua zaidi yetu.amesema ana program ya miaka mitatu.atakuwa anaongezewa mwaka hadi mwaka.binafsi sitokwenda kuitiza stars kwa kipindi cha maximo akiwa kocha.alianza KUBEEP TOKA ALIPOTOKA IVORY COAST KUWA ANA PROGRAM YA MIAKA MITATU.KOCHA MAKINI HUWA ANA WAKILI NA WASHAURI WAKE SIO KWA MAXIMO.
    SITARAJII CHOCHOTE KWA STARS UNDER MAXIMO.HILI KOMBE LA CHAN LIMEANZA MWAKA HUU KUSEMA KUWA KWA MIAKA 29 NDIO MAXIMO KATUINGIZA FAINALI SIO KWELI.PIA FIFA HAWALITAMBUI KOMBE LA CHAN.FUATILIENI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...