MH. ANDREW CHENGE

MBUNGE WA BARIADI MASHARIKI NA WAZIRI WA ZAMANI MH. ANDREW CHENGE AMEJISALIMISHA POLISI (KITUO CHA OYSTERBAY) LEO KUFUATIA AJALI YA BARABARANI ILIYOTOKEA ALFAJIRI YA LEO MAENEO YA OYSTERBAY JIJINI DAR AMBAPO INASEMEKANA WATU WAWILI WAMEPOTEZA MAISHA YAO.

HABARI ZA AWALI ZINASEMA WATU WANAOSADIKIWA KUWA WAMEKUFA WALIKUWA KATIKA BAJAJI AMBALO LILIGONGWA NA GARI DOGO LINALOSADIKIWA KUENDESHWA NA MH. CHENGE.

HABARI KAMILI TUTALETA BAADAYE KIDOGO KWANI POLISI WANATARAJIWA KUTOA HABARI KAMILI KATIKA MKUTANO WA KILA SIKU PALE SENTRO MCHANA HUU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. Aisee pole sana mzee.....MBIJE,A-Kafanabo

    ReplyDelete
  2. wana mikutano gani wanayofanya hao Askari hapo Central,Wizi mtupu..last week nilikuwa kwenye dala dala ,kutokea Gongolamboto kwenda Ubungo,kufika eneo la shule pale Bakhresa ,gari ndogo salon likatuchomekea kwa mbele,drive ikabidi akwepe ili asije akalivaa lile gari,akaenda pembeni kidogo sasa kuna Mwenda kwa miguu mmoja alikuwa anavuka barabara,garli letu likamsukuma pembeni akaanguka,Dereva alitaka kusimama,Abiria baadhi kukamshauri akaripoti Polisi na hiii ni kutokana na usalama wa abiria na Dereva,maana eneeo la plae Kipawa si zuri haaswa kwa upande wa uporaji,ikabidi Dereva aendeshe gari mpaka kituo cha Polisi Tazara,tukafika tukapaki gari, Dereva akaitwa kwa ajili ya kuelezea tukio zima,na mimi nikiwa kama Shahidi sikubaki nyuma nikaenda,sasa wakawasiliana na wenzao waliokuwa eneo la Uwanja wa ndege kama kuna majeruhi ama maiti yoyote pale iliyotokana na ajali ya bus kubwa, Askari wa Uwanja wa ndege wakasema hawana taareifa ,tukasuburi mpaka kama nusu saaa, wakawasiliana tena wakadai hakuna lolote ,wala mtu aliyepeleka malalamiko pale...

    ok wakasema ngoja wamuite Trafiki atoke Buguruni Police ama pale mataa ya Tazara kwa ajili ya kwenda kwenye eneo la Kituo..kweli Trafik akaja( Jina tunalo ) NA KITUO CHAKE CHA KAZI NA NAMBA ZAKE ZA SIMU..SASA KILICHOFUATA BADALA YA KWENDA SEHEMU YA TUKI,WAKAMZUNGUSHA DRIVER PALE COUNTER ,THEN TRAFIKI AKAONGEAAA NAO NA AKAPEWA MSHIKO WA SH ELFU 50000 ,AKAENDA NAO POLICE KATI,CENTRAL KWAAJILI YA KUTOA MAELEZO,SIJUI KWANAINI MAELEZO HAYAKUCHUKULIWA TAZARA POLICE IKIWA NDIO KARIBU NA SEHEMU YA KITUO...SASA CHA AJABU KULE CENTRAL WAWKAENDELEA KUMSHIKILIA DRIVER WANABABAISHA HIKI NA KILE..NA MPAKA SASA KUNA KESI ETI ANATAKIWA APELEKE MASHAHIDI WAWILI WAKIWA NA BARUA...JAMANI HAKI IKO WAPI....ALIYEGONGWA HAKUATOKEA ,.,...DEREVA KAJISALIMISHA NI KOSA??? ANGEKIMBIA JE??? SASA LIPI JEMA HAPO???? NA WHY WACHUKUE HELA ???? ALIYEGONGWA WALA HAJULIKANI NA INAELEKEA HAKUUMIA NA ALINYANYUKA KUONDOKA ZAKE....KESI IPO CENTRAL HADI JUMATATU YA TAREH E 30 MAR .....ILA TUKO NAO SAMBAMBA AMA ZETU AMA ZAO...HATUTOKAA KIMYA .UONEVU UMEZIDI MIPAKA,...KULA HELA YA MTU THEN MUACHIE HURU ,KULA UNAKULA THEN UNAMSHIKILIA........WIZI MTUPU..

    SASA KWENYE MIKUTANO WANAONGEA NA HAYA MACHAFU WAYAFANYAYO??????
    YAANI SIKU HIZI USIPATE AJALI NI DILI ....TENA WANACHEKELEA AJALI BILA HURUMA...
    MICHUZI IWEKE HIYO PANAPOHUSIKA ANGALAU WAKIJISOMA WATAKUWA WAOGA .

    NI MIMI MDAU NA MKEREKETWA.

    ReplyDelete
  3. badala ya kusikitia waliopoteza maisha ,mnatoa pole kwa walioondoa maisha .

    ReplyDelete
  4. MICHUZI KAMA UNABISHA NAOMBA TUWEKEANE PESA KWA ATAKAYE SHINDA, MIMI SIKUWEPO ENEO LA AJARI NA NINASEMA KOSA LILIKUWA KWA MAREHEMU NA CHENGE ATASHINDA NA KUACHIWA HURU.

    ReplyDelete
  5. Pole sana Mzee na familia kwa jumla. Hili tatizo linaweza kumtokea mtu yoyote yule pole sana

    ReplyDelete
  6. KAKUSUDIA!!

    ReplyDelete
  7. Tunangojea sheria ichukue mkondo wake, je hapo polisi aliachiwa au aliwekwa ndani maana ktk ajali kama mtu kafa kwa kawaida dereva akipatikana haruhusiwi kuondoka ingawa sijui kama ni sheria, tunangoja tujifunze!!!!

    ReplyDelete
  8. Poleni sana wafiwa mungu azilaze roho za marehemu mahala pema peponi Amen.

    Vijisenti vitamaliza mchezo

    ReplyDelete
  9. NYINYI WABONGO MMEKULA VİCHWA NINI BAADA YA KUTOAPOLE KWA MAREHEMU NA DUGUZE MNATOA POLE KWA WATU WALIOPANA KTK AJALI KWELI TUPO KINYUME NA SHERİA ZA ULIMWENGU AU NDO KIDUMU CHAMA.NCHI KWELI IKIDODO NAWATU WATADODA

    ReplyDelete
  10. Mara nyingi waendesha bajaji wengi hawazingatii sheria ya barabarani, wanapenda sana kuchomekea na hasa Bagamoyo Rd, bajaji ni nyingi halafu unakuta hazina taa wala reflector hivyo kama usiku unaweza kuigonga. Pole kwa wafiwa, sheria ifuate mkondo. Hongera Chenge kwa kujisalimisha mwenyewe polisi.

    ReplyDelete
  11. Chenge to be responsible for the death it doesnt mean that is criminal lible,the accident is more of gross negligence manslaughter,which can happen to any driver,so the decision are on jury and which will more depend on the essence of the matter(conduct of defendant in all circumstances)....kwahiyo ndugu zangu tusikalie kila kitu ni ufisadi.law student(UK)

    ReplyDelete
  12. Wewe law student(UK), una bahati ya kuwa katika mazingira ya Kiingereza.

    Tumia muda wako kunoa hii lugha!

    ReplyDelete
  13. Law student (UK) ungeandika kiswahili ungetufikishia ujumbe wengi zaidi. Kuuliza si ujinga. Jury ndo nini na ina nafasi gani katika kesi hii? Kama ni accident inakuwaje tena gross negligence manslaughter?

    ReplyDelete
  14. Where is the bajaji driver? nasikia amekimbia na mpaka sasa hajaonekana. Kwanini?

    ReplyDelete
  15. Hivi we law student(uk)hiyo ndo law unayosoma huko uk!!? manake nakushauri ungeenda English course for 1 year kabla course haujaenda nayo mbali. ulichoandika hapo sio English bali umeunganisha tu maneno ya English..law inataka queen's English si cockney! pole kwa wafiwa na chenge!

    ReplyDelete
  16. kweli wewe ni law student. how can you call a fatal manslaughter? hivi wewe unadhani watanzania hawajui principle ya innocence? nyie ndo malawyer mtakao kuwa mafisadi kama yeye.

    ReplyDelete
  17. Mimi% Haya ndio mambo ambayo watanzania tunatakiwa kushikamana kuondoa uonevu. Watanzania tunaoneana sana. Hawa polisi utafikiri hawajui kazi yao, wamehitimu vyuo vipi jmn! KHA!

    ReplyDelete
  18. jamani manslaughter ni kuua bila kuwa na intention. huyu law student (uk) nadhani alikuwa anamaanisha kuwa vijisenti hakuwa na intention ya kuwaua hao watu. Kwa hiyo hawezi kuwa charged na murder bali manslaughter.

    Jury ni watu wanaosikiliza kesi na mwisho kutoa maoni yao juu ya evidence iliyotolewa...i.e: kama ameua makusudi au kaua bahati mbaya. Hakimu ndo anatoa hukumu.


    mtoto

    ReplyDelete
  19. MICHUZI I KNOW U HAVE THE RIGHT TO YOUR BLOG,BUT LAKINI KUONA COMMENT ZA WADAU NA KUAMUA KUWEKA KAPUNI SIO UUNGWANA, REGION CLUB VIONGOZI KUNYWA MPAKA ASUBUHI MATOKEO YAKE YANAJULIKANA WAMEKUFA WAKITOKEA HAPO WEKA MAONI YA WADAU ACHA UOGA WEWE NI MWANDISHI WA HABARI ULIYEBOBEA.

    ReplyDelete
  20. jamani tanzania iache kutumia jungle law. hivi kweli inakuaje mtu apate ajali ashikiilwe na polisi. kwa kawaida mtu kama huyo alitakiwa kuandikisha hiyo ajali na kama kuna lolote anapelekwa mahakamani. hizi sheria za tanzania hazieleweki kabisa. mbona mara nyingi tunasikia jela za tanzania zimejaa sana na huku mahakimu wetu wanapenda kufunga watu hovyo. hivi majaji huchunguza adhabu zinazotolewa na mahakimu. wakati mmoja nilishangaa kusikia padri fulani anafungwa miaka saba eti kwasababu alijipatia ticket ya ndenge kwa njia ya udanganyifu. huyo padri alitakiwa alipe iyo ticket pamoja na faini. kesi nyingine ni ile ya mallya kwenda jela miaka mitatu kwasababu ya ajali. sijui hii ilikua siasa ama vipi

    ReplyDelete
  21. wewe law student umejichafua.... hiyo lugha imekumwaga bora ubadili fani.... mwe! Uje ufundishe hapa kijijini kwetu tumeanzisha kashule ka english course kwa watoto wetuz... tehetehe
    Namwomba dereva wa kibajaji ajitokeze atuambie ukweli.... ama basi abip tumpigie atuambie kunako simu....kama ni yeye alikosea aombe radhi.... vijicent bwana ....mbio .... kimyaaa... au basi mwenye kibajaji atupeleke nyumbani kwa dereva ...mbona hii rahisi!!!au naye kakimbizwa??? nyie!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...