MAGARI YA FAYA BAADA YA KUWASILI BRITISH COUNCIL


HABARI TOKA BAGAMOYO ZINASEMA HOTELI YA PARADISE ILIYOPO BAGAMOYO INATEKETEA KWA MOTO.
KWA MUJIBU WA KAMANDA WA POLISI MKOA WA PWANI, AFANDE ABSALOM MWAKYOMA, JUHIDI ZINAFANYIKA KUUZIMA MOTO HUO KWA KUTUMIA WANANCHI KWA SASA. ILA AMESEMA MAGARI YA FAYA TOKA DAR YAKO NJIANI KWENDA HUKO.
HOTELI ZA JIRANI, AMESEMA KAMANDA MWAKYOMA, NAZO ZIKO HATARINI KUUNGUA MOTO KWANI UPEPO NI MKALI NA MOTO NI MKUBWA. HOTELI NYINGI ZA BAGAMOYO ZIMEEZEKWA MAKUTI.
HABARI ZAIDI KUFUATA BAADAYE...

--------------------------------------
HABARI ZINGINE ZINASEMA KWAMBA WAKATI HOTELI YA PARADISE INATEKETEA KWA MOTO HAPA DAR KATIKA JENGO LA BRITISH COUNCIL (PICHANI JUU) NAKO KULIKUWA NA MSHIKMSHIKE WA MOTO AMBAO UNASEMA ULILIPUKA KATIKA MOJAWAPO YA VYUMBA. HATA HIVYO WAFANYAKAZI WA BRITISH COUNCIL WAMEWEZA KUUZIMA CHAP CHA KWA KUTUMIA VIFAA VYA DHARURA WALIVYONAVYO KABLA FAYA HAWAJAFIKA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 26 mpaka sasa

  1. It is so sad. It was a nice spot. I have been there twice - one back in 1998 and last January when I had a nice buffet and a swim. Oh, that was the day M-Bank staff were freaking out there too.

    ReplyDelete
  2. HAHAHAHAHAHA HUU NI WENDA WAZIMU
    YAANI ZIMA MOTO TOKA DAR KWENDA ZIMA MOTO PWANI
    HAHAHAHAHA
    POLENI SANA WOTE WENYE MASILAI NA HIYO HOTELI.
    HAHAHAHAHAHAHAHA
    BONGO YETU TAMABARAAAAAAAAAAAAREEEEEEEEE
    HAHAHAHAHAHAHAHAHA HAHAHAHAHAHAH AHAHAHAHAH AHAHAHAHAH AHAHAHAH A

    ReplyDelete
  3. Duh kweli bongo tambarare!
    Wagonjwa wabebwe kwenye difender/pick ups
    Magari ya zima moto Bagamoyo mpaka yatoke Dar!

    ReplyDelete
  4. kuna umuhimu wa kuwa na magari ya zima moto kwani Bagamoyo ni miongoni mwa miji inayoingizia taifa fedha za kingeni.

    ReplyDelete
  5. serikali imeng'ang'ania ufisadi tu ona sasa moto umetokea mkoa wa pwani faya zinatoka dar!!!!! huo moto utakuwa unasubiri tu!!! hivi serikali haioni kwamba wakati umefika kila kitongoji cha mji kingekuwa na kituo cha faya??? Wizara ya Mambo ya Ndani tena ya Nchi ipo??? Na hili wanaliona?????

    ReplyDelete
  6. Nimesikia kwamba pamoja na Paradise, kuna hoteli ya pili iliyoteketea huko Bagamoyo. Ninahisi kuwa ni Oceanic Resort, iliyo jirani.

    ReplyDelete
  7. Watanzania bila tukio kutokea kama hilo hawapati fundisho. Bora hilo litakuwa limewaamsha japo kujifunza. Hoteli kubwa zinajengwa nje ya mji lakini hazina vifaa vya kuzuia majanga kama karibu kama hayo ili tatizo likitokea liweze kutatuliwa japo kwa urahisi wanaishi kizembe zembe tu ilimradi hela inaingia mfukoni.

    Nasikia ni tatizo la Umeme na pia naomba mungu kweli liwe tatizo la Tanesco kwasababu hawa Tanesco sasa tumewachokaa. Kilio cha maskini hakisikiki (kilio cha samaki machozi huishia majini) labda huyo wa hotel atakuwa amewagusa Tanesco kidogo. Umeme tunakatiwa katiwa ovyo na kurudishwa mfano juzi tarehe 21 usiku umeme kila wakati unawaka na kuzima. Tanesco naona wamejisahau kuwa kuna watu wanatumia huo umeme na wanavyombo vya umeme ambavyo vinaweza kuleta maafa kwa kukata umeme na kuzima ovyo. Wao wanakata tu na kuzima utafikiri kuna mtoto anachezea hiyo mitambo sio mtu mzima.

    Hakika inaonyesha jinsi gani hata sisi watanzania tunavyorudisha maendeleo yetu nyuma wenyewe. UJINGA, UPUMBAVU KABISA....

    H....

    ReplyDelete
  8. Yaani magari ya faya yanatoka Dar kwenda Bagamoyo? Wakifika huko hotlei zote si zitakua zimeteketea? Jamani Tanzania jinsi watu tunavyoishi...Mungu anasaidia!! Yaani mpaka leo hakuna Fire station Bagamoyo? Hii hatari!!! Halafu tunataka watalii waende huko?

    ReplyDelete
  9. Huku magari ya zimamoto yakiwa mbioni, taarifa ni kwamba Hoteli tatu zimeshateketea hadi sasa:
    1. Paradise
    2. Oceanic
    3. Livingstone

    Kwa kudra ya Mwenyenzi Mungu, hadi sasa hakuna taarifa ya mtu yeyote kuwa ameumia.

    ReplyDelete
  10. Yani wabongo sijui tukoje,watu wanaanza kushangaa vitu hadi vitokee!!ina maana hamjui kuwa halmashauri nyingi tz hazina magari ya zimamoto.hatusikilizi bunge wala nini.Poleni wahanga

    ReplyDelete
  11. Duu kama magari yanatoka fire yatafika kweli yatakuwa yameshuungua na yenyewe(just joking)ila jaribuni kufikiria kama magari yanatoka kilomita kumi au kumi na moja huo mato uanawasubiri, nini maana ya kulipa kodi ina maana jiji lote linategemea magari manne na cha kushangaza ni vilevile british council kumetokea msukomsuko je wapi pa kupewa kipau mbele?

    ReplyDelete
  12. jaman jaman jaman bwana masupu hii kweli hatari..huwezi toka mkoa mwingine kwenda mkoa mwingine kuzima moto, si utakuta majivu tu ndo yalosalia?? hii kweli inatia uchungu sana wa maisha yetu watanzania.
    Tuna kila sababu ya kujivunia rasilimali zetu lakini viongozi hawatilii maanani majanga kama haya..
    haya sasa hoteli tatu kwa pamoja zote zimeteketea je utalii pwani utatuingizia kipato tena?? hayo marekebisho yake je serikali itaingilia?

    INAUMA SANA TENA SANA KUSIKIA ETI FIRE ZINATOKA DAR KWENDA BAGAMOYO KUZIMA MOTO..

    ReplyDelete
  13. Ngoja niangalie CHANU CHANU NETWORK KAMA(CNN) kama kuna habari zaidi naona michuzi na wewe kufika Bwagamoyo mbinde maana mpaka sasa hivi miyeyusho tu, niko kwenye computer kuanzia saa moja za kwa bibi (UK) na saa hizi ni saa sita kasorobo bado tu naona habari ndio hiyo hakuna la zaidi ya habari za kuvunjika mpya kuhusu Bwagamoyo au nini kinaendelea.

    ReplyDelete
  14. ila wanasemaga kuwa kwa muoga hakuendi kilio,,tembo akinyolewa tia maji
    tusilaumu sana kwani hatuna budi na sisi kuwa makini kwani hitilafu hizo hizo na hapa hapa karibu zinatokea na mpaka hayo magari ya fire yaje yafike tayari vitu vishateketea. nini bagamoyo

    hapo magomeni tu utokee moto tu utayasikia magari ya fire yanavyokimbizana na foleni then yakifika pale yanakuwa hayana maji

    Mungu utunusuru

    ReplyDelete
  15. Jamani isijeikawa watu wwnye wivu na nche yetu maana',tanzania inakuwa so fast huku marekani kutwa nzima minigeria, inajiona imetokea tanzania. Nchi zao hawazitaki tena.halafu raisi wetu anaaminika na kipendwa sana mikutano anaalikwa someyimes”kutoka africa mwenyewe.tanzania oyeeeeeeeeeeee

    ReplyDelete
  16. Wewe hapo juu inaepmba tatizo liwe la tanesco unamatatizo .hizo ni hoteli tatu sehemu tofauti ,something is fishing. Halafu inaelekea. Wewe ni wale mafisadi wanaotaka tanesco ife mtegeme fisadi dr mwakyembe na kina tenende wati wa mbeya. greed

    ReplyDelete
  17. Haya ya kuungua moto yalishawahi kutokea Mombasa....hoteli za makuti zikateketea. Ikatokea kuwa makuti yakakatazwa lakini sijui ni kwanini waliendelea kuwa na makuti. Serikali inasema mambo hayafuatiliwi...sasa kilichotokea si kigeni na nilijua litatokea. Sasa watu wakae mkao wa kufanya biashara kwa uhakika si mambo ya kuweka nakshi hatatiri. Pole kwa waashirika.

    ReplyDelete
  18. TATIZO SI FIRE DEPARTMENT TOKA DAR KWENDA PWANI( 1972 POLITICAL BORDERS ).
    SUALA NI UMBALI TOKA ENEO LA TUKIO TOKA KITUO CHA ZIMA MOTO.
    KAMA KITUO CHA ZIMA MOTO KINGEKUWA 5 MILES UPENDA WA DAR WANGEWAHI .

    BOTTOM LINE, ZIMAMOTO TOKA AIRPORT DAR , HAIWEZI KUWAHI MOTO UNAOTOKEA GOBA .

    UMASIKINI NI KIKWAZO KTK HUDUMA KAMA HIZI. LAKINI JAMANI WAHUSIKA TUJITAHIDI KUSOGEZA HUDUMA MUHIMU KWA WANANCHI. HOSPITALI KWANZA THOU .

    ReplyDelete
  19. We Anon wa 03:10PM....hizo Hotli haziko sehemu tofauti, zote zipo kwenye msururu mmoja, yaani zinafuatana na moto unaenda ukiambukiza Hoteli zingine kwasababu zipo karibu mno.

    ReplyDelete
  20. Huu upumbavu mtupu hoteli kama ziko karibu na bahari kwa nini hawakuwa wabunifu kuweka pampu za kuwawezesha watumie maji ya bahari???
    Maji ya kuzima moto si lazima yaletwe na gari la zima moto.Kama unafanya uwekezaji wa mamilioni lazima ufikirie namna ya kukabiliana na majanga kwa kutumia nyenzo zinazokuzunguka.Majengo yenyewe ya makuti walitegemea nini.Hata hivyo nawapa pole sana kwa maafa.

    ReplyDelete
  21. Tukusanye uwezo tuwe na magari ya zimamoto kwenye miji ya Bagamoyo,Kibaha,Mkuranga(Kisarawe),Ikwiriri na Mafia.

    ReplyDelete
  22. Huo usumbufu wa kupata kibali cha kuvuta maji ya baharini ni karaha!!

    ReplyDelete
  23. Kweli kabisa Anon wa mar 23 3:24 Hapo wataweka lawama kwa Serekali Kuweka angalizo ni muhimu sana mara nyingi tunaweka vitegauchumi vyetu bila maangalizo muhimu ya majanga yanapojitokeza,Maskini waliokuwemo humo napiga picha labda ingetokea usiku si ni shida kubwa na watoto.Nina m.f mdogo wa tukio lililotokea tulipokuwa huko hoteli mojawapo Bagamoyo hukohuko kuna hoteli yenye maua ya majani mengi sana mpaka inakuwa kama uko kwenye pori fulani ila yamewekwa katika hali ya matunzo ila yamezidi sana mpaka yanageuka nyumba za kujifichia nyoka ikafika usiku wakati wa chakula cha jioni tukamtuma mtoto akawaite wenzake chumbani ili kupata chakula, wakati wanarudi wakatusimulia wamekutana na nyoka mkubwa anaambambaa kwenda kwenye vyumba vya kulala , ilitushitua na kabla hatujachukua hatua yoyote, kale katoto ketu kadogo, kalienda mojakwamoja hadi kwa waiter na kumshitakia hilo aliloliona, bila ajizi yule waiter alimchukua mtoto akamuomba akamuonyeshe huyo nyoka alikomuona, bahati mbaya walimkosa, sijui sasa kama huyo mdudu alipatikana pindi nyengine au alijeruhi mtu . Mimi ilinisumbua kidogo nikawaza sana endapo labda mtoto mmoja angemkanyaga yule mdudu si angemuuma, na angemuuma usiku ule sijui tungeanzia wapi yaani mpaka leo namkumbuka huyo nyoka ingawa hakutudhuru sisi wengine je? Hayo maua ni mazuri na yanapendeza ila yakizidi hadi kwenye koridoo yanalete mushkel yanatunza wadudu

    ReplyDelete
  24. Unajua tatizo ambalo ninaliona mimi, nikuwa tunajifunza kitu tatizo likitokea,kama mambo shwari,watu hawajali. Mfano, magari ya daladala yanavyojaza utafikiri watu wamejazwa kwenye magunia, tuombe Mungu ajali isitokee.
    Halafu cha kuchekesha, kwenye daladala viti vimebananishwa kiasi kwamba wenye miguu mirefu inabidi wakae upandeupande, fikiria ajali ikitokea hapo itakuwaje, kama umepona utavunjika miguu. Tetenasi zimajaa kila kona.
    Sasa hapo viongozi wahusika hawajali wanasubiri litokee lakutokea ndipo wataanza kubuni mbinu mpya, unajua kwanini ili bosi wao ajue kuwa wanafanya kazi.
    M3

    ReplyDelete
  25. Hiyo gari ya zimamoto kutoka Dar kwenda Bagamoyo ina mafuta ya kutosha kweli? Na je, wanabeba maji kutoka Dar au watakuwa na hydrants za kutumia Bagamoyo?

    ReplyDelete
  26. Unajua watz tuna akili fupi muno.. Ebu ona huyu annon wa Tarehe March 23, 2009 2:53 PM anasema eti rais wetu anapendwa na kualikwa mikutano ya nje. Na huyu anon anaonekana kuwa proud sana na kitendo cha rais wake kupendwa. Hivi ndivyo mindsets zetu watz zilivyo. We cannot take effort to think, even a little bit.

    Kwahiyo upendo anaopewa rais wako kuitwa miktanoni ulaya huku hapa nyumbani miundombinu ikiwa hai-exist wewe kunakuongezea kitu gani zaidi ya umaskini? Wake up Tanzanians. Kodi mnazolipa zinapaswa kufanyiwa kazi kuwapunguzia bugudha wananchi, na sio kutumika ku-finance political campaigns. Wake up people!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...