HABARI TOKA BAGAMOYO ZINASEMA HOTELI YA PARADISE ILIYOPO BAGAMOYO INATEKETEA KWA MOTO.
KWA MUJIBU WA KAMANDA WA POLISI MKOA WA PWANI, AFANDE ABSALOM MWAKYOMA, JUHIDI ZINAFANYIKA KUUZIMA MOTO HUO KWA KUTUMIA WANANCHI KWA SASA. ILA AMESEMA MAGARI YA FAYA TOKA DAR YAKO NJIANI KWENDA HUKO.
HOTELI ZA JIRANI, AMESEMA KAMANDA MWAKYOMA, NAZO ZIKO HATARINI KUUNGUA MOTO KWANI UPEPO NI MKALI NA MOTO NI MKUBWA. HOTELI NYINGI ZA BAGAMOYO ZIMEEZEKWA MAKUTI.
HABARI ZAIDI KUFUATA BAADAYE...
--------------------------------------
HABARI ZINGINE ZINASEMA KWAMBA WAKATI HOTELI YA PARADISE INATEKETEA KWA MOTO HAPA DAR KATIKA JENGO LA BRITISH COUNCIL (PICHANI JUU) NAKO KULIKUWA NA MSHIKMSHIKE WA MOTO AMBAO UNASEMA ULILIPUKA KATIKA MOJAWAPO YA VYUMBA. HATA HIVYO WAFANYAKAZI WA BRITISH COUNCIL WAMEWEZA KUUZIMA CHAP CHA KWA KUTUMIA VIFAA VYA DHARURA WALIVYONAVYO KABLA FAYA HAWAJAFIKA.



It is so sad. It was a nice spot. I have been there twice - one back in 1998 and last January when I had a nice buffet and a swim. Oh, that was the day M-Bank staff were freaking out there too.
ReplyDeleteHAHAHAHAHAHA HUU NI WENDA WAZIMU
ReplyDeleteYAANI ZIMA MOTO TOKA DAR KWENDA ZIMA MOTO PWANI
HAHAHAHAHA
POLENI SANA WOTE WENYE MASILAI NA HIYO HOTELI.
HAHAHAHAHAHAHAHA
BONGO YETU TAMABARAAAAAAAAAAAAREEEEEEEEE
HAHAHAHAHAHAHAHAHA HAHAHAHAHAHAH AHAHAHAHAH AHAHAHAHAH AHAHAHAH A
Duh kweli bongo tambarare!
ReplyDeleteWagonjwa wabebwe kwenye difender/pick ups
Magari ya zima moto Bagamoyo mpaka yatoke Dar!
kuna umuhimu wa kuwa na magari ya zima moto kwani Bagamoyo ni miongoni mwa miji inayoingizia taifa fedha za kingeni.
ReplyDeleteserikali imeng'ang'ania ufisadi tu ona sasa moto umetokea mkoa wa pwani faya zinatoka dar!!!!! huo moto utakuwa unasubiri tu!!! hivi serikali haioni kwamba wakati umefika kila kitongoji cha mji kingekuwa na kituo cha faya??? Wizara ya Mambo ya Ndani tena ya Nchi ipo??? Na hili wanaliona?????
ReplyDeleteNimesikia kwamba pamoja na Paradise, kuna hoteli ya pili iliyoteketea huko Bagamoyo. Ninahisi kuwa ni Oceanic Resort, iliyo jirani.
ReplyDeleteWatanzania bila tukio kutokea kama hilo hawapati fundisho. Bora hilo litakuwa limewaamsha japo kujifunza. Hoteli kubwa zinajengwa nje ya mji lakini hazina vifaa vya kuzuia majanga kama karibu kama hayo ili tatizo likitokea liweze kutatuliwa japo kwa urahisi wanaishi kizembe zembe tu ilimradi hela inaingia mfukoni.
ReplyDeleteNasikia ni tatizo la Umeme na pia naomba mungu kweli liwe tatizo la Tanesco kwasababu hawa Tanesco sasa tumewachokaa. Kilio cha maskini hakisikiki (kilio cha samaki machozi huishia majini) labda huyo wa hotel atakuwa amewagusa Tanesco kidogo. Umeme tunakatiwa katiwa ovyo na kurudishwa mfano juzi tarehe 21 usiku umeme kila wakati unawaka na kuzima. Tanesco naona wamejisahau kuwa kuna watu wanatumia huo umeme na wanavyombo vya umeme ambavyo vinaweza kuleta maafa kwa kukata umeme na kuzima ovyo. Wao wanakata tu na kuzima utafikiri kuna mtoto anachezea hiyo mitambo sio mtu mzima.
Hakika inaonyesha jinsi gani hata sisi watanzania tunavyorudisha maendeleo yetu nyuma wenyewe. UJINGA, UPUMBAVU KABISA....
H....
Yaani magari ya faya yanatoka Dar kwenda Bagamoyo? Wakifika huko hotlei zote si zitakua zimeteketea? Jamani Tanzania jinsi watu tunavyoishi...Mungu anasaidia!! Yaani mpaka leo hakuna Fire station Bagamoyo? Hii hatari!!! Halafu tunataka watalii waende huko?
ReplyDeleteHuku magari ya zimamoto yakiwa mbioni, taarifa ni kwamba Hoteli tatu zimeshateketea hadi sasa:
ReplyDelete1. Paradise
2. Oceanic
3. Livingstone
Kwa kudra ya Mwenyenzi Mungu, hadi sasa hakuna taarifa ya mtu yeyote kuwa ameumia.
Yani wabongo sijui tukoje,watu wanaanza kushangaa vitu hadi vitokee!!ina maana hamjui kuwa halmashauri nyingi tz hazina magari ya zimamoto.hatusikilizi bunge wala nini.Poleni wahanga
ReplyDeleteDuu kama magari yanatoka fire yatafika kweli yatakuwa yameshuungua na yenyewe(just joking)ila jaribuni kufikiria kama magari yanatoka kilomita kumi au kumi na moja huo mato uanawasubiri, nini maana ya kulipa kodi ina maana jiji lote linategemea magari manne na cha kushangaza ni vilevile british council kumetokea msukomsuko je wapi pa kupewa kipau mbele?
ReplyDeletejaman jaman jaman bwana masupu hii kweli hatari..huwezi toka mkoa mwingine kwenda mkoa mwingine kuzima moto, si utakuta majivu tu ndo yalosalia?? hii kweli inatia uchungu sana wa maisha yetu watanzania.
ReplyDeleteTuna kila sababu ya kujivunia rasilimali zetu lakini viongozi hawatilii maanani majanga kama haya..
haya sasa hoteli tatu kwa pamoja zote zimeteketea je utalii pwani utatuingizia kipato tena?? hayo marekebisho yake je serikali itaingilia?
INAUMA SANA TENA SANA KUSIKIA ETI FIRE ZINATOKA DAR KWENDA BAGAMOYO KUZIMA MOTO..
Ngoja niangalie CHANU CHANU NETWORK KAMA(CNN) kama kuna habari zaidi naona michuzi na wewe kufika Bwagamoyo mbinde maana mpaka sasa hivi miyeyusho tu, niko kwenye computer kuanzia saa moja za kwa bibi (UK) na saa hizi ni saa sita kasorobo bado tu naona habari ndio hiyo hakuna la zaidi ya habari za kuvunjika mpya kuhusu Bwagamoyo au nini kinaendelea.
ReplyDeleteila wanasemaga kuwa kwa muoga hakuendi kilio,,tembo akinyolewa tia maji
ReplyDeletetusilaumu sana kwani hatuna budi na sisi kuwa makini kwani hitilafu hizo hizo na hapa hapa karibu zinatokea na mpaka hayo magari ya fire yaje yafike tayari vitu vishateketea. nini bagamoyo
hapo magomeni tu utokee moto tu utayasikia magari ya fire yanavyokimbizana na foleni then yakifika pale yanakuwa hayana maji
Mungu utunusuru
Jamani isijeikawa watu wwnye wivu na nche yetu maana',tanzania inakuwa so fast huku marekani kutwa nzima minigeria, inajiona imetokea tanzania. Nchi zao hawazitaki tena.halafu raisi wetu anaaminika na kipendwa sana mikutano anaalikwa someyimes”kutoka africa mwenyewe.tanzania oyeeeeeeeeeeee
ReplyDeleteWewe hapo juu inaepmba tatizo liwe la tanesco unamatatizo .hizo ni hoteli tatu sehemu tofauti ,something is fishing. Halafu inaelekea. Wewe ni wale mafisadi wanaotaka tanesco ife mtegeme fisadi dr mwakyembe na kina tenende wati wa mbeya. greed
ReplyDeleteHaya ya kuungua moto yalishawahi kutokea Mombasa....hoteli za makuti zikateketea. Ikatokea kuwa makuti yakakatazwa lakini sijui ni kwanini waliendelea kuwa na makuti. Serikali inasema mambo hayafuatiliwi...sasa kilichotokea si kigeni na nilijua litatokea. Sasa watu wakae mkao wa kufanya biashara kwa uhakika si mambo ya kuweka nakshi hatatiri. Pole kwa waashirika.
ReplyDeleteTATIZO SI FIRE DEPARTMENT TOKA DAR KWENDA PWANI( 1972 POLITICAL BORDERS ).
ReplyDeleteSUALA NI UMBALI TOKA ENEO LA TUKIO TOKA KITUO CHA ZIMA MOTO.
KAMA KITUO CHA ZIMA MOTO KINGEKUWA 5 MILES UPENDA WA DAR WANGEWAHI .
BOTTOM LINE, ZIMAMOTO TOKA AIRPORT DAR , HAIWEZI KUWAHI MOTO UNAOTOKEA GOBA .
UMASIKINI NI KIKWAZO KTK HUDUMA KAMA HIZI. LAKINI JAMANI WAHUSIKA TUJITAHIDI KUSOGEZA HUDUMA MUHIMU KWA WANANCHI. HOSPITALI KWANZA THOU .
We Anon wa 03:10PM....hizo Hotli haziko sehemu tofauti, zote zipo kwenye msururu mmoja, yaani zinafuatana na moto unaenda ukiambukiza Hoteli zingine kwasababu zipo karibu mno.
ReplyDeleteHuu upumbavu mtupu hoteli kama ziko karibu na bahari kwa nini hawakuwa wabunifu kuweka pampu za kuwawezesha watumie maji ya bahari???
ReplyDeleteMaji ya kuzima moto si lazima yaletwe na gari la zima moto.Kama unafanya uwekezaji wa mamilioni lazima ufikirie namna ya kukabiliana na majanga kwa kutumia nyenzo zinazokuzunguka.Majengo yenyewe ya makuti walitegemea nini.Hata hivyo nawapa pole sana kwa maafa.
Tukusanye uwezo tuwe na magari ya zimamoto kwenye miji ya Bagamoyo,Kibaha,Mkuranga(Kisarawe),Ikwiriri na Mafia.
ReplyDeleteHuo usumbufu wa kupata kibali cha kuvuta maji ya baharini ni karaha!!
ReplyDeleteKweli kabisa Anon wa mar 23 3:24 Hapo wataweka lawama kwa Serekali Kuweka angalizo ni muhimu sana mara nyingi tunaweka vitegauchumi vyetu bila maangalizo muhimu ya majanga yanapojitokeza,Maskini waliokuwemo humo napiga picha labda ingetokea usiku si ni shida kubwa na watoto.Nina m.f mdogo wa tukio lililotokea tulipokuwa huko hoteli mojawapo Bagamoyo hukohuko kuna hoteli yenye maua ya majani mengi sana mpaka inakuwa kama uko kwenye pori fulani ila yamewekwa katika hali ya matunzo ila yamezidi sana mpaka yanageuka nyumba za kujifichia nyoka ikafika usiku wakati wa chakula cha jioni tukamtuma mtoto akawaite wenzake chumbani ili kupata chakula, wakati wanarudi wakatusimulia wamekutana na nyoka mkubwa anaambambaa kwenda kwenye vyumba vya kulala , ilitushitua na kabla hatujachukua hatua yoyote, kale katoto ketu kadogo, kalienda mojakwamoja hadi kwa waiter na kumshitakia hilo aliloliona, bila ajizi yule waiter alimchukua mtoto akamuomba akamuonyeshe huyo nyoka alikomuona, bahati mbaya walimkosa, sijui sasa kama huyo mdudu alipatikana pindi nyengine au alijeruhi mtu . Mimi ilinisumbua kidogo nikawaza sana endapo labda mtoto mmoja angemkanyaga yule mdudu si angemuuma, na angemuuma usiku ule sijui tungeanzia wapi yaani mpaka leo namkumbuka huyo nyoka ingawa hakutudhuru sisi wengine je? Hayo maua ni mazuri na yanapendeza ila yakizidi hadi kwenye koridoo yanalete mushkel yanatunza wadudu
ReplyDeleteUnajua tatizo ambalo ninaliona mimi, nikuwa tunajifunza kitu tatizo likitokea,kama mambo shwari,watu hawajali. Mfano, magari ya daladala yanavyojaza utafikiri watu wamejazwa kwenye magunia, tuombe Mungu ajali isitokee.
ReplyDeleteHalafu cha kuchekesha, kwenye daladala viti vimebananishwa kiasi kwamba wenye miguu mirefu inabidi wakae upandeupande, fikiria ajali ikitokea hapo itakuwaje, kama umepona utavunjika miguu. Tetenasi zimajaa kila kona.
Sasa hapo viongozi wahusika hawajali wanasubiri litokee lakutokea ndipo wataanza kubuni mbinu mpya, unajua kwanini ili bosi wao ajue kuwa wanafanya kazi.
M3
Hiyo gari ya zimamoto kutoka Dar kwenda Bagamoyo ina mafuta ya kutosha kweli? Na je, wanabeba maji kutoka Dar au watakuwa na hydrants za kutumia Bagamoyo?
ReplyDeleteUnajua watz tuna akili fupi muno.. Ebu ona huyu annon wa Tarehe March 23, 2009 2:53 PM anasema eti rais wetu anapendwa na kualikwa mikutano ya nje. Na huyu anon anaonekana kuwa proud sana na kitendo cha rais wake kupendwa. Hivi ndivyo mindsets zetu watz zilivyo. We cannot take effort to think, even a little bit.
ReplyDeleteKwahiyo upendo anaopewa rais wako kuitwa miktanoni ulaya huku hapa nyumbani miundombinu ikiwa hai-exist wewe kunakuongezea kitu gani zaidi ya umaskini? Wake up Tanzanians. Kodi mnazolipa zinapaswa kufanyiwa kazi kuwapunguzia bugudha wananchi, na sio kutumika ku-finance political campaigns. Wake up people!!!