MH. HADIJA MSONGO, HAKIMU ANAYESIKILIZA KESI YA KINA LIYUMBA NA WENZIE, LEO AMEEKLEZA NIA YAKE YA KUTAKA KUJITOA KUISIKILIZA KWA KILE ALICHOTAJA KUWA MWENENDO TATA WA KESI HIYO.

PAMOJA NA MAMBO MENGINE MH. HADIJA MSONGO AMESEMA MWENENDO WA KESI HIYO UMEKUWA TATA HASA BAADA YA YEYE KUTOA DHAMANA KWA MSHTAKIWA LIYUMBA HATA BAADA YA KUPEWA PASI ILIYOISHA MUDA WAKE, NA BAADA YA KUTOA AMRI YA KUFUTA DHAMANA YA LIYUMBA BAADA YA KUBAINIKA KWAMBA PASIPOTI ALIYOTOA HAIKUWA ILIYOTAKIWA KUTOLEWA.

AMESEMA MALALAMIKO YA WANANCHI PAMOJA NA JAMHURI (SERIKALI) KUPITIA VYOMBO VYA HABARI VIMEIFANYA KESI HIYO KUONEKANA INA UTATA NA KUONEKANA KAMA VILE HAKI HAITENDEKI.

HIVYO KAAMUA KUCHOMA NA TAYARI KESHAMWANDIKIA BOSI WAKE HAKIMU MKUU MKAZI MFADWIDHI MAHAKAMA YA KISUTU, MH. ADDY LYAMUYA, KUMOWMBA AMPANGIE HAKIMU MWINGINE KUSIKILIZA KESI HIYO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Sasa kweli siku zote hizo alikuwa hajaliona hilo? Hapa kuna kitu tumefichwa! Du sasa naona huo u EPA umeingia mahakamani. Any way ngoja tuone nini kitafuata. Kaka Michu uko juu kwa kutupa newz

    ReplyDelete
  2. Siasa na Magazeti yanapoingilia kazi za kitaaluma hayo ndo matokeo.

    Kwa mitazamo wangu kama hapa Bongo kungekuwa na alternative ajira, wakweli na waaminifu wangekuwa wanajiuzulu hizi kazi zenye mashinikizo yasio na maana. lakini kwakuwa hakuna inabidi ukubuliane ilimradi watoto waende shule.

    ReplyDelete
  3. OK LET US SEE

    TARATIBU MAMBO YATAJULIKANA TU,KESI HII VIZITO WAPO NA INAWAHUSU,MNAKAUMBUKA WADAU,NILIULIZA IVI HII GUTS YA JAMAA VIGARI VYEKUNDU YATOKA WAPI?MARA PCB KAITWA KAPOTEA SIKU KADHAA,MARA PASI MBOVU IKAKUBALIWA,

    MAGAIDI SIO LAZIMA WAJILIPUE AU WALIPUE NY TWIN TOWERZ AU LONDON

    kitaeleweka tuuuu

    ReplyDelete
  4. BIG UP KAKA MICHUZI KWA KUTUPA HAYA MAMBO YANAYOTOKEA KWA FASTA SANAAAAAAAAAAAAAAAAA ILA KAMA ALIVYOSEMA MWENZANGU HUYO JANE SAID KWAMBA HAPA KUNA KITU, HATA MIMI NAAMINI NI KWELI HAYA TUTAONA KITACHOFUATA.....

    MDAU ABDALLAH E NGATUNGA TEMEKE MIKOROSHINI......

    ReplyDelete
  5. WAPI WAMUACHIE TU LIYUMBA WA WA2! HATA KAMA ALIIBA KWANI MJENGO HAWAUONI ULIVYOTULIA?LAZIMA TUWE WASTAARABU BWANA!NANI AMBAE ASINGEKULA? WAMSAMEHE TU!

    ReplyDelete
  6. Hakimu amefanya la maana kujitoa kabla watu hawajaanza kumwaga ushahidi.

    ReplyDelete
  7. naskia harufu ya mlungulaaaaa!

    ReplyDelete
  8. michuzi nilisema mimi mtu myenye akili timamu hawezi kukata tawi alilolikalia.na bado visingizio vya kumwaga hiko njiani vyaja



    Mbega

    ReplyDelete
  9. UKITAKA KUMUUWA NYANI USIMTAZAME USONI HAKUNA KUMSAMEHE WALA NINI INABIDI ANYEE DEBE HUYO WANAZOLOTESHA MAENDELEO YA NCHI NYINYI NA VIGALI VYEKUNDU VYENU MNATAKA ASAMEHEWE HAMUONI HATAHURUMA KWA WANA NCHI HOSPITAL HAZINA DAWA,SHULE HAZINA MADAWATI,VIJIJINI WANAKUNYWA MAJI MACHAFU ACHENI HIZO TENA WAMTAIFISHE VITU VYAKE VYOTE MALAYA WA KIUME

    ReplyDelete
  10. Huyu hakimu ndiye aliyempa Liyumba dhamana wakati hakukamilisha taratibu na pia kuwasilisha documents za uongo ikiwa ni pamoja na passport iliyotumika ingawa upande wa mashtaka ulipinga asipewe dhamana baada ya kuona hayo mapungufu.Hivyo sitashangaa kuona anajitoa huyo hakimu kwa kuwa ana-feel guilty na anaona kabisa amefanya blunders.Mahakama zetu zimejaa rushwa ukiwa na fedha hutafungwa lakini ukiwa maskini utafungwa hadi ukome hata kama hujafanya kosa.Tutaendelea kuona vigogo wakifikishwa mahakamani lakini tutaona wangapi watafungwa.

    ReplyDelete
  11. Hivi Wadau kosa la Liyumba ni nini??? Alivunja sheria gani??
    Nilisoma maelezo ya wakili wake kwa kiasi fulani nikaona mmmmmmmmh kuna jambo hapa. Maana ameiomba mahakama ifute madai namba mbili ambayo hayaonyeshi kosa bali yanadai tu kwamba aliiletea taifa hasara kiasi fulani!!
    Kama ni kweli hilo si kosa tu la kinidhamu au kiutendaji na sio kosa la jinai??
    Hizi kesi tusipozichungulia vizuri inawezekana kabisa zikawa ni viini macho maana madai yanachongwa kiasi kwamba kisheria wanajua kabisa yatafeli.
    Kuanzia sasa ninawaomba wale wenye macho wajaribu kuzichungulia vizuri hizo charge sheets.
    Mfano Mramba anadaiwa kutofuata ushauri wa TRA na kulisababishia taifa hasara. Sasa hapo kosa la jinai liko wapi??!! Kwanza yeye kama waziri si lazima afuate ushauri wa TRA katika kufanya maamuzi.
    Jamani tufungue macho viini macho vingi hapa .........yale yale ya kina Kiula.

    Mzawa

    ReplyDelete
  12. wengi wanaropoka bila ya kujua hasa kosa alilotenda ni lipi. ni rahisi watu kupiga kelele bila ya kuuliza ni sheria gani amevunja. jamani tuiachie mahakama itende kazi yake. unaona wengine wa epa wameruhusiwa kwenda nje ya nchi kusalimia watoto wao. nadhani wanasheria wameona kesi zao hazina ukali. nafikiri chuki na kelele ni kwasababu ya umasikini na elimu zetu za chini.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...