Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Wilbroad Slaa aikongea na waandishi. Shoto ni Mzee Edwin Mtei

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimewafukuza wanachama wake 15 na kutengua nafasi ya mjumbe wa Kamati Kuu kwa madai kuwa ni mamluki wanaoleta vurugu ndani ya chama hicho.

Uamuzi wa kuwafukuza wanachama hao ulifikiwa jana katika kikao cha Kamati Kuu kilichokaa kuanzia asubuhi hadi saa 6 usiku Dar es Salaam na ilifikia uamuzi huo, baada ya kuridhika na ripoti ya Kamati ya Bob Makani, iliyoundwa kuchunguza tuhuma zilizotolewa na wanachama hao dhidi ya Mwenyekiti wao, Freeman Mbowe.

Wanachama hao ni Abdul Mateleta, Nasir Chimko, Hamisi Msasa, Abdallah Kaoneka, Mkwanji Maulid, Bimkubwa Uwesu na Peter Katunka (huyu anadaiwa ni mtumishi wa Mbunge wa Ubungo, Charles Keenja). 

Wanachama wengine waliotimuliwa ni Zuberi Haji, Kimaro T, Bakari Shingo, Shaaban Salum, Adam Yasin, Said Mareja, Mwanahamisi Sadiki na Martin Mng’ongo, aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti wa Wilaya ya Kinondoni, ambaye inadaiwa alikuwa mpangaji na mshauri mkuu wa mpango wa uasi ndani ya chama na anavujisha  nyaraka zote.

Kamati Kuu ya Chadema pia ilitengua nafasi ya mjumbe wa Kamati Kuu ya Mecky Mzirai na kumpa onyo kutokana na kudaiwa kuvujisha siri za chama na kupanga mikakati ya kuleta vurugu ndani ya chama hicho. Hata hivyo rufaa yake ipo wazi kwa kusikilizwa endapo ataikata.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. 'CHADEMA chatema wanachama 15' siyo 'CHADEMA yatema wanachama 15'

    ReplyDelete
  2. hapo sasa tunapokosa uhaminifu

    ReplyDelete
  3. Sawa kabisa amuwezi kuwa na wanachama mamruki ndani ya chama mkawaacha tu. lazima kuwatimua wasijekivuruga chama, na wakajiunge uko walikokuwa wakitumwa.
    hawa watu wanaoongwaongwa hovyo ndio wanaovuruga ukuaji wa vyama na kudidimiza demokrasia. nashukuru pia kuwa ata mzee malecelea wa ccm kaliona hilo na ametaka pia chama chake kuwatimua watu wanaoendeleza majungu na malumbano yasioisha kwenye chama chake.
    Hongera chadema kwa kuanza.

    ReplyDelete
  4. MALUKI NI WENGI HAPO IKIFILA JULY 2010 KARIBU NA UCHAGUZI WATAJIFANYA WANARUDISHA CARD ZA CHADEMA NA KWENDA KUTUBU CCM HADHARANI ILI WAONDOKE NA KUNDI LA WAPIGA KURA WASIO NA UPEO WA FIKRA(VIBENDERA FUATA UPEPO).
    SAFARI HII OPPOSITIO PARTIES KUWENI MACHO NA LYATONGA MIMI NAAMINI JAMAA SI MWENZETU IMEKUWA NI KAWAIDA YAKE KUHARIBU MAMBO YA UPINZANI KARIBU NA UCHAGUZI,
    NIMESOMA ARTICLE YAKE MOJA IKISEMA:

    ``Huu ndio ufisadi ambao TLP inafanyiwa na Chadema, hizi ni hujuma, ndio maana Yusuf Makamba anatuambia sisi wapinzani ni kama mapaka waliofungwa kamba`` alisema.MREMA

    REF: 2009-03-21 11:26:17
    Na Mashaka Mgeta also available at
    http://ippmedia.com/ipp/nipashe/2009/03/21/133786.html

    ReplyDelete
  5. HIVI KUNA UBAYA GANI TUKIKABIDHI NCHI KWA CHADEMA?.....Japo for a test.........Manake hii menu ya maharage inachosha...ifike wakati tukubali kubadilisha diet.....Hata kama CHADEMA watakuwa hawafai kwani hao CCM wana uzuri gani?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...