MAMBO 25 YANAYOKUFANYA UWE MSWAHILI...
1.Unamwita mtu usiyemjua(wala kuonana nae kabla)anti au anko au sista ama braza.
2..Asilimia 90 ya CD pamoja na kanda za cassete za muziki ulizonazo nyumbani ni feki AU ni za kuazima.
3. Chumba chako kimejaa vitu (makorokoro) kwa kuwa hutupi kwa kuamini kuwa ipo siku utayahitaji kwa mfano karpet ukilitoa hulitupi n.k.
4.Una machupa ya maji matupu ya shampoo na perfume pamoja na vipodozi vingine umeweka tuu wala huna shughuli navyo.
5.. Watoto wako wote wana majina ya utani mfano babu ali, chidi,mamu, dida, Ngunyi, Songoroo n.k.
6.Hakuna mtu katika familia yako anayetoa taarifa kwako anapokuja kukutembelea mfano kaka,shangazi n.k..
7.Mifuko yako imejaa vitu kama vile vijiti vya kusafishia meno,tissue n.k ulivyochukua sehemu kama vile mgahawani.
8.Mama yako ana migogoro na ndugu na hawazungumzi kwa muda wa miezi 10 au zaidi.
9.Hupigi simu isipokuwa katika muda ambao gharama za kupiga ni nafuu(mfano usiku sana)na mara nyingi huwa una beep tu. Na uki beep unaangalia salio..
10.Ulipokua mdogo nguo unazonunuliwa pamoja na viatu ni vikubwa mara mbili ili uweze kuvivaa muda mrefu zaidi.

11.Wakati ukisafiri na ndege unabeba mzigo wa uzito mkubwa kuliko inavyoruhusiwa.

12.Unapomsaidia mtu na akafanikiwa basi utakuwa unasema kama sio mimi asingekuwa vile yule..

13. Unapenda kuhudhuria / kushiriki hafla na sherehe mbalimbali kama vile harusi, maulidi, Ubarikio n.k ambazo hujaalikwa na wala huhusiki.

14. Unapenda kuomba kununuliwa dola (credit), pombe, soda, sigara n.k

15. Unapoingia katika chombo cha usafiri unapenda kupigania/kukimbilia na hata kuingilia dirishani..

16. Unapohudhuria hafla au sherehe fulani unapenda kubeba bia, maji, soda na chakula kupeleka nyumbani wakati unarudi.

17. Unapenda kutembelea watu ovyo ovyo hata kama hujaitwa au huna jambo la msingi linalokufanya la kukupeleka kwao.

18. Unapenda kuongea saana kuhusu mambo ya watu wengine (Umbea), mara sijui fualni kafanya hivi, mara fulani hana lolote...

19. Unapenda sana kuongea unapokuwa na watu lakini maongezi yenyewe hayana msingi wowote, ili mradi tu uonakane nawe umo.

20. Unapenda sana kusoma magazeti ya udaku, kama vile Kiu, Ijumaa n.k. na pia habari zisizokuwa na elimu ndani yake. Kama vile Baba Ubaya, Toto tundu, Babu suni n.k.
21. Unakuwa mbishi sana kutoa michango ya harusi, ila kwenye mnuso wewe ndio wa kwanza kufika na wa mwisho kuondoka tena ukiwa ndiiiiiii....
22. Unaiga kila kitu toka kwa jirani yako badala ya kubuni mambo yako. Mfano akifungua grocery we nawe unafungua yako ubavuni, akifuga kuku, we nawe umo....
23. Unakuwa huendi out na mkeo na kama mkienda shughulini yeye hutangulia mbele kabisa na wewe unafuata nyuma kwa mbali kama watu baki, na huko mkifika hakuna kujuana. Ukionekana out na mtu basi ni nyumba ndogo
24. Unakuwa kila jambo la kila mtu kazini kwako unalijua, lakini la kwako hakuna anayelijua. ukiulizwa unakuwa mkali kama mbogo
25. Una tabia ya kuandaa pilau na kuku wakati wa sikukuu tu. Halafu mayai, matunda na maziwa unakula ama unaandaliwa ukiwa umelazwa hospitali

NOTE. Wapelekee na wengine ili wajue ni kitu gani kinawafanya kuitwa waswahili... ......kama mimi na wewe.

"TUBADILIKE" Cheers,
Shayo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 45 mpaka sasa

  1. Shayo - This is hilarious, nimecheka hadi nimelia, so many things are true!!! Yani ni ukweli mimi ni mara chache sana nilinunuliwa viatu vinavyonitosha, ili vilast muda mrefu…..by the time vimekutosha vimeshazeeka.

    But I’ll tell you this Shayo nimejifunza na mwanangu anavaa vitu vinavyomtosha………it’s a big step I know!!! Kwi kwi kwi!!! Mimi ni mswahili and I love it tho!!! Hahaha!!

    ReplyDelete
  2. hivi ni kwa nini neno mswahili huwa linatumika kwama ni kumdharau mtu au kumtusi. mfano mtu anamwambia mwenzake "wacha uswahili" au "jamaa ni mswahili ile mbaya" tena kuna wanaosema "waswahili bwana" na mengi mengineyo ni kwa nini jamani?

    ReplyDelete
  3. hukuwahi kusherehekea siku ya kuzaliwa kwako hadi umefika kuishi nje ya nchi sasa ni kila mwaka na kualika watu hata huwaoni mwaka mzima!!!!

    ReplyDelete
  4. Sasa wewe hapo juu inaelekea shule zero, hayo yote ukitoka nje ya nchi usa au uk ni magonjwa yanakuwa,mfano personality disorder,attention disorder,hayo ni magonjwa sio uswahili.watu wanalazwa. houston texas, kunawatu kila shughuli wamo na wakija watakuwa wnabeba chakula.

    ReplyDelete
  5. Pia ni sigh ya loneliness.ukiona mtu anatokatoka sana. Huyo yupo lonely hata kama ameoa. Na anafamilia.houston texas tumezidi du

    ReplyDelete
  6. Sasa wewe hapo juu inaelekea shule zero, hayo yote ukitoka nje ya nchi usa au uk ni magonjwa yanakuwa,mfano personality disorder,attention disorder,hayo ni magonjwa sio uswahili.watu wanalazwa. houston texas, kunawatu kila shughuli wamo na wakija watakuwa wnabeba chakula.

    ReplyDelete
  7. Duh! Ebwanae hiyo ni nomaa...Tukupigie makofi mara tatu... Hapo yani umegonga Ikulu...Sijui uko wapi yani ungekuwa karibu ningekupa zawadi ya busu langu kwani ladha yake hakuna aliyonayo duniani...

    Kuongezea kidunchu kama halipo hili labda sijasoma vizuri yani ni shauku niliyonayo kutoa maoni jamani: Kama ni mwanmke au mwanaume Anakuwa anapenda sana mambo ya vidole juu na nyimbo za mafumbo hata kama hana aliyegombana nae...

    ReplyDelete
  8. Aliyeandika hii post ni mswahili wa kupindukia!!

    ReplyDelete
  9. Namba 14: Unapenda kuomba kununuliwa dola (credit), pombe, soda, sigara n.k.

    Anaombwa nani sasa? Kama ni mswahili anaombwa basi feature yote haiko sahihi. A self-referential aspect...

    ReplyDelete
  10. Mbona havishekeshi me nimesikitika sana kuona shayo una poteza muda wako kuandika vitu visivyo na kichwa wala miguu.
    Hapa umetumia kama dakika 10-20kuandika huu upupu si bota 2 ungechukua ufagio usafishe pale sokoni tungekuona wa maana kabisa

    ReplyDelete
  11. We mchaga umeyajuaje hayo mbona huzungumzie mbege za bure.

    ReplyDelete
  12. naona toka ulipoanza kufanya hiyo research mpaka ukagundua yote hayo tayari we mwenyewe bonge la mswahili na inawezekana ndo mwenyekiti maana mtu asiye mswahili hawezi kujua yoote hayo uliyosema isipokuwa na we uwe mmojawapo unayefanya hayo mambo,ingekua njema ungeanzisha kadarasa cha kutoa tips namna ya kuacha uswahili hapahapa kwa michu najua atakupa nafasi maana waswahili wengi kweli wanakuja humu na zeutamu hujataja waswahili wanaenda sana mule kuharibiana,anyway hongera kwa matokeo ya uchunguzi uliofanya asilimia 90 ni kweli

    ReplyDelete
  13. Houston, Texas ni waswahili, nasikia ni dizain ile mbaya, wanawake na waume zao wote wambea kupiliza.

    Huku west cost haa, kila mtu na time yake na tunaheshimiana.

    ReplyDelete
  14. Kwanza kabisa sikuifurahia hii hoja yako kwa kutumia neon `Mswahili’. Unaikashifu lugha na `utaifa wetu’ kwanini usitumie neno jingine kama `mshamba’ .Na pia ni vyema ukaliangalia boriti lililoko jichoni mwako kwanza…Lakini majibu yako ni kama ifuatavyo.
    1.Unamwita mtu usiyemjua(wala kuonana nae kabla)anti au anko au sista ama braza. (Swali je ulitaka aitweje(pendekeza)
    2..Asilimia 90 ya CD pamoja na kanda za cassete za muziki ulizonazo nyumbani ni feki AU ni za kuazima. (Hii inachangia na kipato chako)
    3. Chumba chako kimejaa vitu (makorokoro) kwa kuwa hutupi kwa kuamini kuwa ipo siku utayahitaji kwa mfano karpet ukilitoa hulitupi n.k. (Hata wenzetu wanapenda kutunza kumbukumbu(Wazungu)ili wajukuu waone nini ulichokuwa ukitumia.
    4.Una machupa ya maji matupu ya shampoo na perfume pamoja na vipodozi vingine umeweka tuu wala huna shughuli navyo. (kumbukumbu bwanaa)
    5.. Watoto wako wote wana majina ya utani mfano babu ali, chidi,mamu, dida, Ngunyi, Songoroo n.k. (Haya si majina ya Utani,ni majina kama StrongArm, Rootman etc)
    6.Hakuna mtu katika familia yako anayetoa taarifa kwako anapokuja kukutembelea mfano kaka,shangazi n.k..(kashifa
    7.Mifuko yako imejaa vitu kama vile vijiti vya kusafishia meno,tissue n.k ulivyochukua sehemu kama vile mgahawani. (Kashifa
    8.Mama yako ana migogoro na ndugu na hawazungumzi kwa muda wa miezi 10 au zaidi.(Kashifa
    9.Hupigi simu isipokuwa katika muda ambao gharama za kupiga ni nafuu(mfano usiku sana)na mara nyingi huwa una beep tu. Na uki beep unaangalia salio..(yes unabana matumizi, Wazungu wanabana sana matumizi, ushahidi hoja no 6
    10.Ulipokua mdogo nguo unazonunuliwa pamoja na viatu ni vikubwa mara mbili ili uweze kuvivaa muda mrefu zaidi. Unabana matumizi

    11.Wakati ukisafiri na ndege unabeba mzigo wa uzito mkubwa kuliko inavyoruhusiwa. (Unapelekea wenzako zawadi, sina ubinafsi mimi, sina uchoyo, kwahiyo nabeba zawadi nyingi)

    12.Unapomsaidia mtu na akafanikiwa basi utakuwa unasema kama sio mimi asingekuwa vile yule.. (Hata wazungu wanayo, lakini mmh, )

    13. Unapenda kuhudhuria / kushiriki hafla na sherehe mbalimbali kama vile harusi, maulidi, Ubarikio n.k ambazo hujaalikwa na wala huhusiki. (Sherehe zetu za Kiafrika ni za Kijamii, hazihitaji mwaliko)

    14. Unapenda kuomba kununuliwa dola (credit), pombe, soda, sigara n.k (Hii ni tabia, hata kama ni nani)

    15. Unapoingia katika chombo cha usafiri unapenda kupigania/kukimbilia na hata kuingilia dirishani..( Hii ni tabia tu hata majuu nimeona watu wanagombea ili kwenda na muda

    16. Unapohudhuria hafla au sherehe fulani unapenda kubeba bia, maji, soda na chakula kupeleka nyumbani wakati unarudi.(Sasa kwanini nisiwakumbuke wanangu,mke wangu angalau nayeye aonje nilichokula)

    17. Unapenda kutembelea watu ovyo ovyo hata kama hujaitwa au huna jambo la msingi linalokufanya la kukupeleka kwao.(Aisee, wewe sasa nimekujua ni nani,lakini huo ni upendo, udugu na kuthamini wenzako,sioni ubaya)

    18. Unapenda kuongea saana kuhusu mambo ya watu wengine (Umbea), mara sijui fualni kafanya hivi, mara fulani hana lolote... (Hii ni tabia,umbeya upo hata Ulaya,ndio maana kuna magezeti ya Udaku nk)

    19. Unapenda sana kuongea unapokuwa na watu lakini maongezi yenyewe hayana msingi wowote, ili mradi tu uonakane nawe umo. (Ipi bora,kukaa kimya au kuongea, manake wewe unaongea, sasa mimi nifanyeje…pendekeza)

    20. Unapenda sana kusoma magazeti ya udaku, kama vile Kiu, Ijumaa n.k. na pia habari zisizokuwa na elimu ndani yake. Kama vile Baba Ubaya, Toto tundu, Babu suni n.k. (Hii ni hobby, ni kama wewe unavyopenda kusoma magazeti ya xxx, kwa vile yameandikwa na wadhungu. Lakini hawa waliochapa magazeti ya udaku watapatia wapi pesa. Wewe tatizo lako una kasumba
    21. Unakuwa mbishi sana kutoa michango ya harusi, ila kwenye mnuso wewe ndio wa kwanza kufika na wa mwisho kuondoka tena ukiwa ndiiiiiii...(Kashifa hii, wewe tatizo unapenda kujikweza, unapenda uonekane, sasa mimi kipato changu ni kima cha chini nifanyeje. Mafisadi mumetuibia,na sehemu ya kuturejeshea angalau kidogo ni sehemu kama hizo, mmmh kwanza sinywi pombe…)
    22. Unaiga kila kitu toka kwa jirani yako badala ya kubuni mambo yako. Mfano akifungua grocery we nawe unafungua yako ubavuni, akifuga kuku, we nawe umo....(Natafuta maendeleo, huo ni upinzani wa maendeleo, lakini mbona na wewe unapenda kusema watu…)
    23. Unakuwa huendi out na mkeo na kama mkienda shughulini yeye hutangulia mbele kabisa na wewe unafuata nyuma kwa mbali kama watu baki, na huko mkifika hakuna kujuana. Ukionekana out na mtu basi ni nyumba ndogo(MMMh, hapa unamsema rafiki yako,hapo sipo)
    24. Unakuwa kila jambo la kila mtu kazini kwako unalijua, lakini la kwako hakuna anayelijua. ukiulizwa unakuwa mkali kama mbogo(Kashifa
    25. Una tabia ya kuandaa pilau na kuku wakati wa sikukuu tu. Halafu mayai, matunda na maziwa unakula ama unaandaliwa ukiwa umelazwa hospitali(Kashifa)

    NOTE. Wapelekee na wengine ili wajue ni kitu gani kinawafanya kuitwa waswahili... ......kama mimi na wewe.

    Mswahili origional

    ReplyDelete
  15. Hayo yanakuhusu wewe mwenyewe Shayo, eti mtu akae na machupa na ma-carpet yasiyo na kazi, huu si ni uchafu jamani, na wewe shayo umayajuaje haya kama siyo kwamba wewe ndo uko hivyo.

    ReplyDelete
  16. Kinachofurahisha hapa kwa wale wanaojua maana ya 'uswahili' (hii haina uhusiano na lugha)ni kwamba ukisoma kutoka 1 hadi 25 basi mwandishi (Shayo) anawakilisha barabara mtu huyo anayeitwa 'mswahili'.

    ReplyDelete
  17. 15. Unasoma huu uswahili wa shayo hapa Blog ya Jamii

    ReplyDelete
  18. Kumbe tumesikitika wengi sasa aliyeandika hii yeye mkoloni sio? kama umezaliwa Tanzania penda usipende lazima tujivunie sie ni WASWAHILI, USA ni American na ENGLAND ndio English Kenya Kenyataz Sio ni Waswahili natunajivunia kuwa wa Swahili anayebisha na abishe usitake kuvuruga ya mwenzako uliyeandika kama Nchi imekushinda haya kivyako. Pazi.

    ReplyDelete
  19. BORA USWAHILI KULIKO USHAMBA. MICHUZI AKINIAHIDI ATATOA MADA ZANGUNITATOA HAPA KWANI WENGI WASHAMBA SANA, KWA MAANA YA KUIGA MAMBO YASIYO NA MANUFAA NA KWENDA KINYUME NA UTAMADUNI.ANANIMINYIA SANA.

    ReplyDelete
  20. MCHAGGA na u comedy wapi na wapi ? post yako ziro, vitu vingi ulivyo andika hata havi exist ktk culture ya kiswahili.

    Na kuwa mswahili,ni nadharia ;
    kama vile kuwa machinga, hata wachina wanaouza vitu tunaweza kuwaita machinga(ingawa hawajatoka kusini).

    mswahili hawezi kumwita mswahili mwenzie we mswahili,mfano kina yakhe kule pemba.
    Hilo ni jambo lililo letwa na wakuja, kutokana na kushindwa ku deal na mazingira.

    Kama upo marekani au Uk. Utagundua yale mambo amabyo home ungeyaiita ya kiswahili, wazungu na niggaz wanayo saana tu.

    ReplyDelete
  21. maada imekaa vizuri ila naomba kumtetea shayo..siyo mswahili hata ukiangalia jina shayo ni wa bush tu. issue no. 10 bwana hiyo ni kweli hata wazazi wangu walikuwa wananinunulia viatu vikubwa.

    Ila inabidi tuangalie main source siyo uswahili ni uchimi mbovu. kwa sababu mzazi akinunua kiatu kikubwa anajua kwa miaka fulani hatanunua tena kiatu

    point moja umesahau Shayo ...mtu anapotoa ahadi halafu haitimizi ,,..huyo ni mwahili tena mkubwa

    mdau netherlands

    ReplyDelete
  22. sidhani kama mdau amekashfu lugha .........ila anamaanisha uswahi wa pwani babake na siyo lugha .mimi mwenyewe napenda lugha yangu


    mdau netherlands

    ReplyDelete
  23. ikiwa umetumia lugha ya kiswahili basi wewe pia ni mswahili pure na hivyo vyote umevijuaje maana mimi mwenyewe ndo leo navisikia.

    ReplyDelete
  24. Nimesoma na sidhani hii inaendana na kuwa mswahili. Uswahili ni tabia ya kuwa muongo au kutotimiza maneno yako, unrealistic.

    Mfano wa hoja zako, majina kama braza, aunt au uncle yanatumika na kila mtu sio waswahili tu . Mtoto mdogo kila mtu akikutana naye ni aunt au uncle.

    Nina asilimia kubwa tu ya cd ambazo sio original its cheap to download from your pc na hiyo sio uswahili

    Hata wazungu au mabibi na mababu zetu wanavikorokoro wamehifadhi lakini sio waswahili

    Nick names kwa watoto ni jambo la kawaida na sio uswahili.

    Viatu kwa watoto kununuliwa vikubwa ni la kawaida.

    Kila kitu ulichoandika hapa has nothing to do with mswahili. Nashangaa watu wanaku support for nonsense. Tafuta terminology nyingine

    ReplyDelete
  25. Vitu vingine umeandika vya ukweli lakini nimekuja gundua wazungu /nigga ni Noma hatuna tofauti, wao wamezidi tabia zao mbaya, wavivu,wachafu na kubana matumizi ndo usiseme,wanakula viporo, loh!
    Pia na 17 kutembeleana muhimu, kujuliana hali pia kisaikolojia ni afya. kuliko kukaa kwenye screen ya Tv/Pc peke yako ni bora kuonana na watu'live''kucheka kuwa na touch sio kila siku wewe na familia yako tuuuu. get more exposed.
    Koku

    ReplyDelete
  26. naona wengi wenu mnamkashifu Shayo mkidhani kwamba ni mwandishi wa hii hoja, Hiyo ni message ya kuforwardiana kwenye email, nadhani yy tu kaweka jina lake hapo chini. Niliforwardiwa msg hii nadhani miaka mi4 iliyopita, na mwandishi hakuwa shayo. So umsimlaumu shayo na yy ameforwardiwa akaamua kutuletea hapa kwenye globu yetu.

    ReplyDelete
  27. USISHANGAE WATU WANAMSUPPORT MWENYE POST HII, SABABU WATU WENGI HUMU NI WAGENI.

    NANUKUU;
    The Swahili are a people and culture found on the coast of East Africa, mainly the coastal regions and the islands of Kenya and Tanzania, and north Mozambique. According to JoshuaProject, the Swahili number in at around 1,328,000.[1] The number of Swahili speakers, on the other hand, numbers at around 90 million people. The name Swahili is derived from the Arabic word Sawahil, meaning "coastal dwellers", and they speak the Swahili language.

    uswahili ni nadharia, haimaanishi watu wa Dar,Tanga,zanzibar,wala mombasa.

    kwa mfano, hata huyu mchagga, ni mswahili.unapataje muda wa uzusha uongo wa aina hii, we chizi nini?
    Viatu vikubwa hata,wamisri yawezekana wananunulia watoto wao.

    BUT, WASWAHILI WANAISHI MAENEO HAYO YA MWAMBAO.

    Kama kutotimiza ahadi na uongo ni uswahili, then wahaya wana qualify kuitwa waswahili.

    ipo tofauti ya mwizi na tapeli ,kweli si kweli ?

    ReplyDelete
  28. KWA NYONGEZA TU;
    Official Dini ya swahili people ni Islam bcoz most of swahili people are Muslims.
    but theres christian na wapagani kama mimi ambao ni waswahili.

    NANUKUU;
    This point is often obscured by the Swahili linguistic tradition in which those who speak the language are often called Swahili (Waswahili) regardless of their actual ethnic origins. In other words, the term 'Swahili' can mean 'those who speak Swahili' or it can mean 'ethnic Swahili people'.

    ReplyDelete
  29. Hamna uswahili kumuita mtu usiyemjua aunt,inaonyesha respect maana hamjuani.kuweka vitu vya zamani wazungu wanatunza saaaaaaaaaana msijidanganye.Aliyeandika hii mada either ni mshamba hajui wazungu wanaishije anachukulia mambo ya kwenye filamu au limbukeni tu wa maisha amesahau YA KALE NI DHAHABU.mengineyo yooote siafiki nayo naona hata ujinga kuyasoma yote.WATANZANIA ACHENI UJINGA,FIKIRIENI MAMBO YA MAANA.SIJAONA LA MSINGI HAPA KWENYE MADA,PUMBA TUPU

    krs
    netherlands

    ReplyDelete
  30. sifa kubwa ya kuwa mswahili ni kutokutimiza ahadi na TIME almost wakati wote,na kuwa na visingizio vingi kila kukicha,swala la uhamifu kwa mswahili halipo, mswahili anapenda kufuatilia mambo yasiyo mhusu, mswahili ni mtu asiye na dira wala msimamo.Bora kuwa mmakonde kuliko mswahili.

    ReplyDelete
  31. machapisho ya mtu aliyefrustrate yanajionyesha kabisa,lakini kwa sababu wasomaji wengi walio na access na internet,hasa walio nje ya nchi kwa sababu ndo waliofrustrate zaidi,basi wanatumia blog ya jamii kupitisha ujinga wao.kwa mwenye akili hii ipo wazi kabisa kuwa huyu bloger,kakosa kazi,anafikiria kurudi kwao,lakini anaona atachekwa,sasa anaikasirikia jamii yake.kwa sababu kinyume na hayo aliyoandika ,anataka kusema ,wazungu,huko anakofanyia utumwa ndao wapo sahihi. hayo mengine kwtu sie ni utamaduni,hayatabadirika leo.
    pole ndugu,maisha magumu ndo yanakufanya uandike hayo.

    ReplyDelete
  32. Kuna watu ambao wakienda kwa watu lazima wale hao kuwitaje?

    ReplyDelete
  33. Bwana Shayo unahitaji ukombozi wa kifikra. Bado umeathiriwa na fikra za kikoloni. Jivunie "uswahili" wako kwani ni wazi unaonesha au unaakisi hali ya kipato cha huyo "mswahili" mfukoni ndio maana kutokana na uchache wa rasilimali una(ana)pigana vilivyo kuitumia rasilimali kidogo uliyo(aliyo)nayo ili uweze kuishi. Huu si ushwahili ni tabia ya binadamu ambayo ni ya asili kulingana na mazingira yake aliyomo.
    Achana na desturi ya kila kibaya basi ni cha mswahili,badala yake jenga dhana kwamba masikini ana uhaba wa rasilimali,hivyo ana budi kutafuta njia mbadala ya namna ya kuishi na kujiridhisha

    ReplyDelete
  34. Mimi haki ya Nani tena nafurahi kuwa mswahili, najivunia sana kuwa mswahili. Kwa hayo yote uliyosema mi naona faida ya kufanya hayo mambo uliyoorodhesha na sioni kama ni vitu vya aibu bali ni vya kujivunia. Waswahili Oyeeeeeeeeeee.

    ReplyDelete
  35. mimi sio dr wa watoto na wala si dr na wala sina akili lakini kitu ambacho ninajua ni kuwa mtoto anakua haraka kwa hiyo usipokua mwangalifu utakuta ngua na viatu vinambana vyote

    wacha kuwatolea watu asira zako ndani ya hii blog

    ReplyDelete
  36. JAMAA MBONA SASA TUNAENDELEZA MATUSI YALE YALE YALIYOPITWA NA WAKATI?
    Ni miongo mingi imepita tangu tusi hili lilipovumbuliwa, na kwa mastaajabu mpaka leo bado tu nyie mnaliendeleza?
    Tena wengine, hasa huyu anonymous wa 6:09 amevuka mipaka kabisa kwa kututukana kuwa ni waongo, tusiotimiza ahadi na ni unrealistic, jamaa mpaka lini tutaacha kutukanana hivi?
    Vitabu vingi vya reference vinawazungumza waswahili kuwa ni jamii ya wenyeji wa pwani ya Afrika Mashariki ambao lugha yao ya mawasiliano ya kila siku ni Kiswahili.
    Nilipokuwa chuoni nikisomea lugha, tulifundishwa kuhusu historia ya kuenea lugha hii katika Afrika Mashariki kwamba ulihusishwa na dini ya Kiislamu, na huko Uganda kulikuwa na mbinde kidogo kiswahili kisienezwe kwa sababu za nature ya nchi yenyewe. Sikuelewa sana juu ya hilo wakati huo mpaka hapo 1990 nilipokwenda Burundi kwa study tour, nikakuta pale Bujumbura ukijitangaza wewe mswahili watu wengi watakuhusisha na uislamu, na hata lugha ya mawasiliano ya misikitini na katika mikutano ya Waislamu ilikuwa ni Kiswahili. Buyenzi, Nyakabiga na Bwiza, maeneo ya Waswahili ndio pale Uzumbura yalikuwa na idadi kubwa ya Waislamu.
    Hapa sikusudii kuleta udini, lakini ninachokusudia kusema kuwa SISI WASWAHILI, JAMII YA WATU WA PWANI, HATUPENDI TUNASIBISHWE NA TABIA CHAFUCHAFU. Wala hakuna ushahidi wowote wa maana kuuhusisha uswahili na uongo, fitna au kutotimiza miadi.
    Waingereza walikuwa na msemo wao wa "MPE MBWA JINA BAYA KISHA UMUUE" Naona na hii ni mbinu iliyotumika kumdhalilisha na hatimaye kumdharau mtu wa pwani. Ikishakuwa wewe ni mswahili, basi maana yake iwe wewe ni mshenzi, mwongo, huna maana, huna ustaarabu, ili jamii ikuchukie. na kweli ikawa hivyo. Hata wakati mwingine ukenda kupeleka posa, wakikugundua tu wewe ni mswahili inakuwa vigumu kukubaliwa. Wewe mswahili bwana!
    Tafadhalini jamaa, uswahili si dhambi wala uovu. Wala kwa kweli si haki kuendelea kututukana bila sababu za msingi. Uswahili ni sababu ya uumbaji wa Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye alyetuteulia kuzaliwa pwani. Na sisi ni binadamu kamili, wenye uwezo na maadili sawa na wengine, kwa ushahidi mwingi tu.
    Otherwise kama kuna mwenye hoja ya kuunasibisha na uovu kwa ushahidi halali wa marejeo na aulete kadamnasi.
    Vinginevyo jamaa chonde, tusi hili likome.
    Mndengereko, Ukerewe

    ReplyDelete
  37. Nadhani mtoa mada ana lake jambo na WASWAHILI au kuna jambo lililomkuta kwa hiyo anafikiri wenye tabia hiyo ni WASWAHILI.
    SHAYO inaonekana dhahiri hajawahi kusafiri ama kutoka nje ya hapo alipo kwa hiyo anafikiri hayo yote hufanywa na WASWAHILI. Laiti kama angejua maana neon MSWAHILI, asingekenua meno na kutukana WA PWANI.
    Kuna watu kibao maarufu kama akina David Beckham, Michael Jacksons na wengine wengi tu maarufu ambao si WEUSI, wana tabia kama hizo na wemewahi kugombana na hata wazazi wao; hao pia ni WASWAHILI.
    Mtindo wa watu kuweka vitu upo. Isipokuwa sisi WABONGO tusiojua thamani ya vitu vyetu, ndiyo tunaodhani kila afanyae hivyo ni MSWAHILI!
    Watu waishio DUNIANI(siyo BONGO ) kuna kitu kinaitwa OLD IS GOLD au ANTIQUES.
    Mababu zetu hasa waliopigana vita vya DUNIA wana vitu ambavyo kama wangejua wangejipatia MAMILIONI ya fedha za KIGENI laiti kama wangejua wapi wanaweza kuviuza hasa UINGEREZA.
    Hata hivyo hakuna kinachoshindikana. Siku hizi kuna EBAY na kama kuna mtu ana vitu vya VICTORIAN ANTIQUES toka kwa babu au bibi yake, anaweza kujiingizia mamilioni kwani ni mali na vina soko kubwa. Hao wanaonunua nao ni WASWAHILI!
    Ugomvi, kutembeleana bila taarifa hivyo vitu vipo ila kwa sababu ya ROHO MBAYA hasa WACHAGA, wanaona kama vile MGENI amekuja kumaliza CHAKULA au ataharibu bajeti yao! Hiyo ni HULKA na ipo siyo kwa WASWAHILI. Laiti kama isingekukuta, usingeijua. AISIFIYE MVUA IMEMNYEA.
    Nadhani SHAYO umeona MSWAHILI na ukapata bahati ya kutoka nje kidogo kuona dunia. Kwa hiyo familia ya mkeo ambaye pengine ameishi PWANI muda, unahisi kama ni ya WASWAHILI. Hiyo ipo hata kwa WAZUNGU.
    Leo tunavyozungumza, ROONEY anaishi na mdogo wake kwenye jumba lake la kifahari. Angekuwa MWEUSI watu wangedai shauri ya USWAHILI. Lakini na WAZUNGU pia wanafanya, je ni WASWAHILI?
    Ukitaka nikupe mifano hai ya kila mada uliyotoa, nitajaza BLOG ya MWEZI wote wa nne. Hayo machache yanachosha kukutoa MATONGOTONGO na ukae kitako utafute maana ya NENO HALISI LA MSWAHILI. Nyie ndiyo mnaokuja na LUGHA za AJABU na KUCHAFUA KISWAHILI. NI MTWANA WEWE…
    NENDA CHUO KIKUU CHA Dar ukawaone maprofesee wakupe maana halisi ya MSWAHILI na siyo KUKURUPUKA kama nyoka alieyona NGUCHIRO.
    ALAMSIKI...WA BARA

    ReplyDelete
  38. hata wamakonde ni sehemu ya swahili culture.

    uswahili kwa maana ya nadharia, woote mnao hangaika kuuzungumzia ni waswahili, kwa nini usitumie muda wako kujifunza vema utamaduni wako na kusaidia nduguzo uliowaacha maporini kwenu ?

    ReplyDelete
  39. In general mtanzania yoyote atakuwa ni mswahili kwasababu ya lugha yetu ya kiswahili. Mfano mzuri Mkenya atatuita watanzania wote ni waswahili. Sidhani kama kuna kabila wala group yoyote inayoweza kujivunia kwamba wao ndio waswahili. Nadhani kuna mgawanyiko kidogo wa watu wa bara na pwani lakini sio waswahili vs wakurya au makabila mengine. Kuna makabila ya mikoa ya pwani na dar kama wazaramo wakwere, na waendereko, Tanga na pia mikoa ya kusini na zanzibar nk.
    Mswahili ni usemo unaotumika hata bara vijijini unapokuwa maneno maneno na no vitendo. Mtu atakuambia acha uswahili, hilo ni la kawaida. Watanzania wote ni waswahili, pwani wana accent yao, wasukuma, wahaya, wachaga na makabila mengine yana zao.

    Wafaransa wanatokea ufaransa, kiingereza uingereza, kirusi warusi, kijapani wajapani, kichina wachina, waswahili tanzania na kenya (especially Mombasa)

    ReplyDelete
  40. MNDENGE WA UKEREWE sadakta.. we mswahili swaaafi tena nadhifu kabisa, umenitanabahishia hapa kuwa wewe ni mswahili asilia kwa kiswahili chako cha ndani kabisa hapa jamvini, naamini kuna baadhi ambao wameingia kwenye dictionary kutafuta tafsiri ya baadhi ya misamiati uliyoyatumia hapa au kuna wale wenzetu wanojiita wa bara waima wazungu baadhi yao wametoka kapa hapa,

    Iweje uzungumze kiswahili halafu unajitoa kwenye waswahili hebu tujiulize hilo. Napenda asili na nasaba yangu, kabila na utaifa wangu sifedheheki na wala sifadhaiki ninapoitwa mswahili

    Mswahil Asilia.

    ReplyDelete
  41. Hilo suala la kumnunulia mtoto viatu au nguo kubwa ni kawaida kabisa tena popote lipo hata ulaya sasa ww umnunulie mtoto nguo inayomtosha mfano mtoto ana miezi 4 umnunulie nguo ya miezi 4 si anavaa wiki mbili tu haimtoshi...lazima ununue kubwa kama ya kuanzia miezi 6 coz mtoto anakua haraka... kwahio kwa mkataba huo wa kununua exact size utakuwa unakwenda dukani kila kukicha na unajaza manguo tu ambayo ni useless.....Sometimes we have to be practical sio suala la uswahili bwana umechemsha hapo....

    ReplyDelete
  42. WEWE UMEISHI ULAYA unajifanya kila kitu cha uswahili ni kibaya mimi najivunia uswahili wabongo wengi wakifika ulaya hata mikutano ya waswahili wanajifanya kutumia kiingeleza jiulize ni mkutano gani wazungu wakiwa tanzania wakatumia kiswahili huu ni ulimbukeni jamani badilikeni sio kila kitu cha mzungu ni kizuli iam so proud to be tanzanian

    ReplyDelete
  43. wakati mwingine kujibu hizi hoja ni kama ujinga vileee!

    lakini acha nimshangae huyu aliyetaja wamakonde.

    Uswahili si kabila, wala kuwa swahili people si kabila, tupo wa Dar, wapo wa mombasa, wapo wa visiwani , n.k.

    Kinachofanya uwachokoze wamakonde nini, kama si umaskini ?

    ReplyDelete
  44. sasa uswahili sifa mbaya?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...