Mwanamziki wa dansi MR.Buti Jiwe aka Garinoma Jr. anayefanyia shughuli zake nchi Holland! ameibuka na Album ya moto wa kuotea mbali yenye jina na nembo yake "Buti Jiwe".

Mr.Buti Jiw,ni kizazi kipya cha "Mziki wa Dansi" wa bongo na tayari amejijengea umaarufu nchini Uholanzi na amepania kwenda kwa mwendo wa kasi wa kutimia BUTI JIWE lake kuhakikisha dansi lake linasambaa kila mahali duniani!

Nia yake hiyo nzuri inamfanya kupokelewa kwa mikono miwili ya washabiki pamoja na 
bendi mabali mbali za mziki wa dansi katika kila kona. Mr.Buti Jiwe anatoka katika familia ya wenye damu ya mziki, lakini mafanikio yake yanatokana na kujituma pamoja na nidhamu ya hali ya juu aliyo nayo,ambayo inawezekana kuwa mfano wa kuigwa na kizazi kipya cha "Mziki wa Dansi".

Mr.Buti Jiwe na CD yake  "Samahani" inaonekana kuanza kutawala vituo mbali mbali vya radio barani Ulaya. Mwendo huo wa kasi wa MR.Buti Jiwe, Garinoma Jr unaelekea kupiga teke kwa njia ya mziki katika kila kona duniani.

Mwanamziki huyo kijana mwenye majina ya kutisha Mr.Buti Jiwe aka Gari! Noma! anafananishwa na gari lenye mwendo wa kasi ya hatari kimziki! gari ambalo ukidandia ni hatari ya NOMA. wale wadau wanaotaka kuisambaza CD ya Mr:Buti Jiwe wasisite kuwasiliana na buti jiwe kupitia: 

butijiwe@yahoo.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Hongera bro, sasa ningetoa ushauri kama ikiwezekana weka hata sample ya miziki yako/wako ilituweze kutafuta soko. Nafikiri ni wachache wanaofahamu miziki yako.
    Mdau K.

    ReplyDelete
  2. Kaza Buti kaka,nakutakia kila la heri, kwa kufanikiwa kimuziki,sasa tungependa kusikia muziki wako, ili tuweze kuburudikana kiu chetu cha siku nyingi, mungu akubaliki.
    mdau M

    ReplyDelete
  3. Hivi ni Garinoma ama Galinoma?

    ReplyDelete
  4. hongera bwana Buti Jiwe!!!!kwanza kiasi nicheke jinsi hizi habari zenyewe zilivyopamba kibaraza cha jamii,yaani unawatishia maisha chipukizi wenzio hapa bongo?
    Buti Jiwe? teke lake sio la kawaida au?
    kamatia hapo hapo na songa mbele

    ReplyDelete
  5. unajua huyu mwandishi kafanya kusudi na haya maandishi ya kusanii!gari!noma lakini ni galinoma,nadhani anajua anachokifanya hili kuanzisha ligi hapa! haya tutafika tu kwa mbinu zenu hizi

    ReplyDelete
  6. wewe anony hapo juu vipi? unambiwa GARI!NOMA
    pia BUTI JIWE sasa kama unataka kuomba lift shauri lako,na kama utajipendekeza kukaa mbele ya hiko kiatu buti jiwe usije ukajutia maisha

    ReplyDelete
  7. sasa hili buti jiwe kamba yake au nyuzi za kufungia kiatu hiki zinakuaje?? huku si kuwatisha wanamziki vijana wenzio au?
    any way hongera sana ndivyo inavyotakiwa lazima utoe mfano hai
    katika mziki

    ReplyDelete
  8. te!te! mwe!mwe! bwana buti jiwe!
    hongera sana,haya akina wapi?mpo akina Banza Stone? Msafiri Diof?
    kijana mwenzenu huyo na Buti la Jiwe,anatisha

    ReplyDelete
  9. kaka Buti Jiwe kiatu cha hatari,
    kwanza hongera sana kufanikiwa kimziki,lakini kishindo cha buti jiwe lako mbona cha kutisha ?
    kulikoni?enelekea umejiamini kisawa sawa!kuna nguzo gani mgongoni kwako?story hapo juu inatisha

    ReplyDelete
  10. Huyu ni Henry galinoma ja alikuwa anakaa Mindu street,Upanga.

    He is very talent, kwani alishakuwa mwanariadha wa mbio fupi na alikuwa ni moto wa kuotea mbali jamaa wengi wa Upanga na maskani yetu Ghetto watamkumbuka na pia alikuwa anacheza mpira kwa sana tu.

    Mjusi

    ReplyDelete
  11. Haya Jongo hongera sana tena sana .Sasa nikitaka CD yako niipate wapi?
    MINDU HOYEEE!!!!

    ReplyDelete
  12. buti jiwe.i`m proud to see your picture in this blog.,and the story makes to get you many comments. i hear the songs,and they told me whats about.very strong....i`m looking forward to the next album. God bless you

    ReplyDelete
  13. Hongera sana bwana BUTI JIWE,Umeweza kutuwakilisha kijiwe chetu cha pale Upanga kwa mzee Pambe, Jombi Gheto, Castro team ya pale muhimbili, nakutakia kila la heri mzee Gari lenye noma, tuko pamoja na wewe.MINDU oyeeeeeeeeeee

    ReplyDelete
  14. Haya tena, tulichokua tunakisubiri kwa hamu tumekipata.
    mimi mwenye nilikua nashangaa mpaka hivi leo, nilikua sijakusikia katika fani ya muziki,na kipaji chako ulichokua nacho toka zamani pale Upanga, watu hawawezi kuamini kua wewe ndio ulie mfundisha Justine Kalikawe kupiga gita pale Upanga katika kitiwe chetu, na yeye akaibuka na kukuacha kua mwana reggae mzuri.ukufanya uchoyo.
    kaza uzi ndugu yangu ili uweze kufika mwisho wa safari yako.nakutakia kila la heri

    ReplyDelete
  15. BUTI JIWE, Gari lenye nomaaaaaaaa
    kaa mbele ufe

    ReplyDelete
  16. Kwanza nakupa hongera sana Bwana BUTI JIWE,kwa kufanikisha ndoto za wa penzi wa muziki wa dansi wa afrika Mashasiki.Ni muda mwingi tumekua tukisikilza nyimbo za kizazi kipya zenye,mrindimo wa Ulaya na USA,kiasi tumeweza kupoteza utambulisho wa muziki wa dansi wa nchi yetu.
    Sasa ,kwa muziki wako na mpangilio wake, umeweza kuturudisha katika ezi za akina Marijan Rajabu "jabali la muziki", Patrik Barisidya na Afro 70 na wengine wengi.
    Sasa tunakukubali kama mwanamuziki chipukizi wa muziki wa dansi la afrika mashariki,
    Na nakutakia kila la heri na uendeleze mwenendo huo huo wa BUTI JIWE, Gari - Noma, gari lenye mwendo wa kasi, shindana nalo upate ajali.
    Kaza buti mzee .


    Wako
    mdau
    kisiju pwani

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...