Mbunge wa jimbo la Bariadi Magharibi Andrew Chenge (mwenye suti na tai) amepandishwa kizimbani leo katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, Dar, na kusomewa mashtaka matatu baada ya gari aliyokuwa akiendesha kugonga Pikipiki aina ya Bajaji na kusababisha vifo vya watu wawili.

Mwendesha mashtaka wa Polisi David Mwafimbo alitaja makosa yanayomkabili Chenge kuwa mawili ni ya kusababisha vifo  vya watu wawili,  na kosa la tatu ni kuendesha gari kwa uzembe barabarani ambapo mtuhumiwa alikana mashitaka yote.

Kesi hiyo inaunguruma mbele ya Hakimu Emerius Mchauru na imeahirishwa hadi April 30 mwaka huu. Aliachiwa kwa  dhamana ya shilingi Milioni moja na  mdhamini mmoja.
----------------------------
kunradhi wadau, 
awali hapa palikuwa na picha na habari ya msiba wa Hamidu Bisanga. Maoni yaliyokuwapo hapa hayahusiani na picha na habari hii ya sasa. samahani kwa usumbufu wowote utaojitokeza.
-Michuzi


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  2. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  3. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  4. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  5. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  6. Tegemea sanaa nyingi zaidi juu ya hili

    ReplyDelete
  7. kibati kimemgeukia? ndo maana watu wanakimbia tu wakigonga dar. huwezi jua upepo utageukia wapi. niliona kwenye ile picha alivyokua anaelezea jinsi ajali ilivyotokea yule afande alikua na kiboko nikazania ilikua achapwe mtu pale.....hahahahha wanataka kumpunguzia vijisenti vyake baba wa watu.....na dereva aliyekimbia itakuaje yeye? Huyo dereva hata kama alikua hana kosa lakini once ukisha kimbia basi unajitakia mengine Hit and run ni kosa..

    ReplyDelete
  8. Kwa nini asishitakiwe pia kwa kosa la kuendesha gari ikiwa na expired insurance? Maana hilo ni kosa na haswa kwa mwanasheria kama yeye! Au maafande watasema hawajaiona hiyo bima?

    ReplyDelete
  9. Kwetu sisi tunaotumia barabara haya ni mambo ya bahati mbaya pole sana mzee! na pia pole kwa waliopatwa na msiba mwenyezi Mungu azirehemu roho zao mahala pema kwa aliyejiandaa kiroho.

    Suala kama la ajali tusiingize siasa jamani mambo mengine tuyaache kama yalivyokuwa, kwa hili linaweza kumpata yeyote!

    Sikitiko langu ni kama mdau aliyepita amesema ukweli, bima iliyokuwa ktk kioo cha gari ilikwisha,japo!!!!! mambo ya fweza ile inaweza kukatwa ndani ya dakika kumi na ukaambiwa ilikuwa haijabandikwa kwa bahati mbaya. Mambo ya pesa nduguni zangu, matabaka lazima tukubali usindikizwaji wenyewe kwenda mahakamani kama unakwenda arusini eskoti kuubwa! ukitaka mambo hayo labda upige watu makofi.

    ReplyDelete
  10. TUNAFANANISHA MAUAJI YAKE NA DEUS MALYA TUNANGOJA MATOKEO HAPO NDIO MTAJUA...... DEUS MALYA WETU MMMH NGOJA TU

    ReplyDelete
  11. kosa la reckless driving or causing death for reckless driving adhabu yake ni faini ya sh.20,000 kwa mtu mmojax2=sh40,000.
    mahakama alopelekwa haiwezi kumfunga mtu kwa kosa kama hilo.
    pili chenge anadai hajajonga wakati bajaj imelmbwa kote nyuma? maanake sie viziwi hatuoni!
    tatu dereva wa bajaj atapoteaje? basi kauawa na kutupwa baharini kuondoa ushahidi.
    kama chenge hakuwa na bima, nani atalipa gari yake?sembuse wafiwa!
    imeripotiwa bima ya gari yake ilipita muda hadi alipokamatwa hakuwa na bima. mbona shtaka hilo halipo?
    kama alidai bima ipo,lazima zichunguzwe serial numbers. ya zamani itajulikana na feki lazima itakuwa na no mpya kwa hiyo kama ikiwekwa hadharani, waliokata bima zenye serial numbers zinazokaribiana na chenge watajitokeza na kusema walikata bima zao lini...waandishi mikono mirefu nyie. TAKUKURU inapsawa kuwapitia mnaharibu jamii kwa njaa mbaya.

    na hii nayo usitoe...who cares

    ReplyDelete
  12. kosa la 4 la kuendesha gari bila bima ya gari naona au wamesahau ama mzee vijesent ameshafisadi kamanda kova na mwendasha mashitaka? kweli hakuna usawa tanzania, jaribu wewe kuendesha gari bila bima utaona cha moto!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...