
Mbunge wa jimbo la Bariadi Magharibi Andrew Chenge (mwenye suti na tai) amepandishwa kizimbani leo katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, Dar, na kusomewa mashtaka matatu baada ya gari aliyokuwa akiendesha kugonga Pikipiki aina ya Bajaji na kusababisha vifo vya watu wawili.
Mwendesha mashtaka wa Polisi David Mwafimbo alitaja makosa yanayomkabili Chenge kuwa mawili ni ya kusababisha vifo vya watu wawili, na kosa la tatu ni kuendesha gari kwa uzembe barabarani ambapo mtuhumiwa alikana mashitaka yote.
Kesi hiyo inaunguruma mbele ya Hakimu Emerius Mchauru na imeahirishwa hadi April 30 mwaka huu. Aliachiwa kwa dhamana ya shilingi Milioni moja na mdhamini mmoja.
----------------------------
kunradhi wadau,
awali hapa palikuwa na picha na habari ya msiba wa Hamidu Bisanga. Maoni yaliyokuwapo hapa hayahusiani na picha na habari hii ya sasa. samahani kwa usumbufu wowote utaojitokeza.
-Michuzi
This comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDeleteThis comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDeleteThis comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDeleteThis comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDeleteThis comment has been removed by a blog administrator.
ReplyDeleteTegemea sanaa nyingi zaidi juu ya hili
ReplyDeletekibati kimemgeukia? ndo maana watu wanakimbia tu wakigonga dar. huwezi jua upepo utageukia wapi. niliona kwenye ile picha alivyokua anaelezea jinsi ajali ilivyotokea yule afande alikua na kiboko nikazania ilikua achapwe mtu pale.....hahahahha wanataka kumpunguzia vijisenti vyake baba wa watu.....na dereva aliyekimbia itakuaje yeye? Huyo dereva hata kama alikua hana kosa lakini once ukisha kimbia basi unajitakia mengine Hit and run ni kosa..
ReplyDeleteKwa nini asishitakiwe pia kwa kosa la kuendesha gari ikiwa na expired insurance? Maana hilo ni kosa na haswa kwa mwanasheria kama yeye! Au maafande watasema hawajaiona hiyo bima?
ReplyDeleteKwetu sisi tunaotumia barabara haya ni mambo ya bahati mbaya pole sana mzee! na pia pole kwa waliopatwa na msiba mwenyezi Mungu azirehemu roho zao mahala pema kwa aliyejiandaa kiroho.
ReplyDeleteSuala kama la ajali tusiingize siasa jamani mambo mengine tuyaache kama yalivyokuwa, kwa hili linaweza kumpata yeyote!
Sikitiko langu ni kama mdau aliyepita amesema ukweli, bima iliyokuwa ktk kioo cha gari ilikwisha,japo!!!!! mambo ya fweza ile inaweza kukatwa ndani ya dakika kumi na ukaambiwa ilikuwa haijabandikwa kwa bahati mbaya. Mambo ya pesa nduguni zangu, matabaka lazima tukubali usindikizwaji wenyewe kwenda mahakamani kama unakwenda arusini eskoti kuubwa! ukitaka mambo hayo labda upige watu makofi.
TUNAFANANISHA MAUAJI YAKE NA DEUS MALYA TUNANGOJA MATOKEO HAPO NDIO MTAJUA...... DEUS MALYA WETU MMMH NGOJA TU
ReplyDeletekosa la reckless driving or causing death for reckless driving adhabu yake ni faini ya sh.20,000 kwa mtu mmojax2=sh40,000.
ReplyDeletemahakama alopelekwa haiwezi kumfunga mtu kwa kosa kama hilo.
pili chenge anadai hajajonga wakati bajaj imelmbwa kote nyuma? maanake sie viziwi hatuoni!
tatu dereva wa bajaj atapoteaje? basi kauawa na kutupwa baharini kuondoa ushahidi.
kama chenge hakuwa na bima, nani atalipa gari yake?sembuse wafiwa!
imeripotiwa bima ya gari yake ilipita muda hadi alipokamatwa hakuwa na bima. mbona shtaka hilo halipo?
kama alidai bima ipo,lazima zichunguzwe serial numbers. ya zamani itajulikana na feki lazima itakuwa na no mpya kwa hiyo kama ikiwekwa hadharani, waliokata bima zenye serial numbers zinazokaribiana na chenge watajitokeza na kusema walikata bima zao lini...waandishi mikono mirefu nyie. TAKUKURU inapsawa kuwapitia mnaharibu jamii kwa njaa mbaya.
na hii nayo usitoe...who cares
kosa la 4 la kuendesha gari bila bima ya gari naona au wamesahau ama mzee vijesent ameshafisadi kamanda kova na mwendasha mashitaka? kweli hakuna usawa tanzania, jaribu wewe kuendesha gari bila bima utaona cha moto!!!
ReplyDelete