MAREHEMU HAMIDU BISANGA (PICHANI) ALIYEFARIKI KWA AJALI YA GARI JUMAPILI USIKU HAPA DAR ANATARAJIWA KUZIKWA LEO SAA KUMI KATIKA MAKABURI YA KISUTU JIJINI, KWA MUJIBU WA TAARIFA YA KIFAMILIA. ALIKUWA NA UMRI WA MIAKA 56.

BISANGA, AMBAYE AMEACHA MJANE NA WATOTO 5, ATAKUMBUKWA KAMA MMOJA WA WAANDISHI WA HABARI HODARI WALIOFANYA KAZI DAILY NEWS KATIKA NAFASI YA MSANIFU MKUU WA HABARI.

MSIBA UKO NYUMBANI KWAKE OYSTERBAY MTAA WA CHISIZA NAMBA 1/11, JIRANI NA ILIPOKUWA LA DORCE VITA. UKITOKEA MJINI UNAKATA KUSHOTO KABLA YA KUANZA KUTELEMKA MWINUKO WA KUELEKEA HAPO ILIPOKUWA LA DORCE VITA.

HABARI KAMILI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. poleni Khadija Ahmed Hawa na wengine m/mungu akupeni moyo wa subira jamani ni msiba mkubwa huu.

    ReplyDelete
  2. Buriani Brother Hamidu mchango wako daima utakumbukwa na siye tuliokuwa wanafunzi chini yako.Daima tutakumbuka maneno yako ya busara na ucheshi kwenye kazi za uandishi.....Mola akulaze mahali pema peponi,Amina.

    Mike Mhagama.

    ReplyDelete
  3. MzeeKifimboChezaMarch 31, 2009

    We Michuzi.

    Kabla ya kuanza "Kutelemka MWINUKO" au "Kutelemka MTEREMKO?" We vipi wewe?

    Poleni sana Wafiwa

    ReplyDelete
  4. Poleni wafiwa.

    Kweli tuanatembea na vifo na hatujui siku wala saa lakini it is a shame jinsi bongo tuanavyopoteza watu kwa ajali za magari kila siku na sasa hivi tena na hivyo vibajaji.

    ReplyDelete
  5. Kifo cha Hamidu kimenishtua kweli. Nilimfahamu mara ya kwanza mwaka 1976 Iringa. Ilikuwa wakati wa sherehe za sabasaba kusherehekea miaka 22 ya TANU kuzaliwa ambazo zilifanyika kitaifa mjini Iringa. Tukiwa vijana wakati ule nakumbuka kwa sababu hoteli na guest zilizajaa wageni, marehemu mzee Kissoky alikuwa Mkuu wa Mkoa akaagiza mabaa yote yakae wazi usiku kucha ili watu wamalizie muda huko. Lo tukiwa na Bisanga na makomredi wengine tulikesha haswa. Since that time tulifahamiana. Jumapili iliyopita to be exact tarehe 22 Machi 2009, nilikutana naye pub ya BAKULUTU pale Kinondoni karibu na kwa John Fedha. Tuliongea mengi. Lakini safari hii tofauti na Iringa tukiwa watu wazima alinieleza jinsi alivyopata jackpot kutokana na mradi wa Luguruni na Kwembe ambapo walikuwa wanafidiwa viwanja na wizara ya ardhi. Kule kwembe na Luguruni alikuwa na shamba lenye ekari nyingi. Na fidia ilikuwa alipwe ni mapesa mengi vilevile. He had grand plans ambazo alinifahamisha. Lakini lo mipango ya Mungu ni mikubwa kumbe juma moja baadaye kaitwa mbele ya haki. Inna Lilahi wa inna illahi rajiuun. Mola ailaze mahali pema peponi. Amen.

    ReplyDelete
  6. Nawapa pole wafiwa.

    Nilifika katika tukio muda mfupi tu baada ya tukio!

    Njia nzima nilikua najiambia mmmh, eneo hili la Millenium ni baya sana kutumia "lane' ya ndani wakati wa weekend usiku. Ghafla mbele yangu kukaibuka msongamano!

    Kama kawa, wasamaria wema walikua wengi, wezi hawakukosekana. Isingekua askaria wa mabenki pale, wangeiba hadi soda kwenye kreti zilizokuwa katika pickup lililogongana na gari la marehemu!
    Naamini simu yake iliiibiwa na mwizi sidhani kama alipatikana!

    Tatizo la haraka lilikua kupata gari la kuukimbiza mwili, ambao ulikua umewekwa pembeni ya barabara na kupepewa. Nilihisi naona kichwa kinasogea kidogo lakini mwili ulikua umepoa. H
    Hakuna mtu aliyekua radhi kusimama na magari yalikua yanafosi kupita katika eneo la ajali.
    Nilikua na camera lakini nikasita kupiga picha, sikudhani ingekua poa!

    Natoa pole tena.

    Ila sehemu ile nimeshashuhudia zaidi ya ajali 5 HAPOHAPO! Yaani mpaka naona ni miujiza! Ni THE EXACT SAME SPOT!Tena huwa ni ajali mbaya sana.

    Kuna haja ya kuwa waangalifu sana barabarani, tusiendeshe wakati tumekunywa na TUPUNGUZE MWENDO tukiwa tunapita sehemu zote za vivuko vya watu na vituo vya mabasi.

    RIP

    ReplyDelete
  7. we patrick ujakuwa tu, habari za jackpot/fidia ya shamba mliongea wawili, sasa ya nini kuianika mtandaoni? babu mzima unapitiliza.

    ReplyDelete
  8. Poleni sana kwa familia.Hasa shemeji yangu na watoto. Nimesikitishwa sana na kifo cha rafiki yangu Hamidu. Lakini ndiyo mapenzi ya mola. Mungu awape nguvu za kuhimili hiki kipindi kigumu katika maisha yenu. Amina

    ReplyDelete
  9. nasikitika mno kupita kiasi kwa kumpoteza mpendwa shemeji yangu kwani mimi sikuwa tuu shemeji bali na urafiki pia anyway hatuna jinsi namwombea mwenyezi mungu akamlaze pema peponi na my dia sister wangu Tunu Mwenyezi mungu akupe faraji.

    ReplyDelete
  10. issa bisanga pole wangu!u knw we tugetha on this 1.. its K

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...