Hasheem Thabeet akishangilia ushindi

Timu ya chuo kikuu cha Connecticut Uconn "Huskies" kwa mara nyingine tena imeibuka kifua mbele  katika mchuano mkali na wa kusisimua wa robo fainali Jumamosi kwa kuwatoa timu kali ya Missouri "Mizzou"kwa jumla ya pointi 82-75.

Katika uwanja wa Glendale Arizona uliojaa mashabiki 18,886 kama kawaida yake Hasheem Thabeet aliongoza ngome ya timu hiyo huku akiwa na rebound 13 na kupachika pointi 5 na kufanikiwa kuwafungisha virago timu hiyo ya Missouri na kuwa timu ya kwanza kupata nafasi ya kwenda Detroit Michigan kwenye nusu fainali hizo maarufu kama "Final Four" mwaka huu.

Timu hii ya Uconn inawania kupata taji hili kwa mara ya tatu ikiwa imeshawahi kulitwaa mara mbili katika miaka ya 1999 na 2004.

Habari kamili

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Hongera Hasheem lakini umeitoa timu yangu ya nyumbani.
    Aleyfex

    ReplyDelete
  2. Nimesoma mahali leo wanga washaanza kumchimba Hasheem kuhusu kwanini aliacha kutumia jina la baba yake blah blah walimwengu wabaya tumwombee Mungu aendelee halafu story yenye inaonekana kupikwa nimeiona kwenye yahoo news

    ReplyDelete
  3. Yeah, Thabeet fanya vitu vyako, nilicheki mechi yenu zidi ya Mizzou, boy, you are fighting Tanzanian, mama yako walikuwa wakimuonyesha mara kwa mara pale jukwaani na wale wapambe waliokuwa wakipeperusha bendera ya Tanzania. It was a beautiful thing to watch.
    Man, this boy got a bright future. I pray for ya.

    Mdau- the US.

    ReplyDelete
  4. Huyu bwana ana future nzuri sana kwake yeye na kwa Bongo kwa ujumla.
    Baada ya Olajuwan,Mutombo kuliwakilisha bara letu kwa kiwango cha juu sana NBA Mr Thabeet anaipeleka Africa in to the next level.

    ReplyDelete
  5. hao wajinga wanaolalamika ati amechange name ni watu hawajaenda shule jina ni lile lile ila for pronouciations it needed americanizataion yaani si rahisi kusoma Hashim Thabit ya kiswahili ikatamkwa kama ilivyo kwenye kiswahili jina hilo lina (Consonants)watu wa lugha wanajua hilo majina yote ya kiswahili au Kiarabu yana americanization yake kama Baraka Obama imekuwa Barack Obama, jina Obama limebaki hivyo kwa vile vowels zake ni hivyo hivyo kwenye Kiingereza! tuache ushamba na kasumba, hizi ni itikadi chafu wamatumbi!

    ReplyDelete
  6. Anony 6:38, si kwamba wanamchimba bali wanaeleza ukweli kuhusu maisha ya THABIT HASHIMU (Thabeet Hasheem)na suala lake la kulitupilia mbali jina la baba yake (la kibantu) akidai kwa mila za kwao ukimpoteza mzazi wako na ukawa ndo kichwa cha familia unaacha kutumia jina lake! Sina hakika kama ni kweli manake sijui kabila la Hashimu Thabit.

    ReplyDelete
  7. wote hapo chini mko wrong...na wale wote waliocomment kwenye yahoo vile vile wako wrong wala hawakumsikia yule mtangazaji wa CBS alimention last name ya Thabeet ambayo ni Manka..Hasheem Thabeet Manka kwahiyo jamaa alidrop Manka akabakia na Middle ambayo ni Thabeet...lakini commentator aliitamka kama MENKA ndio kwenye yahoo hawakumention MANKA thats why wale wamarekani wenye vichwa vibovu wakawa wanabishana wenyewe kwa wenyewe

    ReplyDelete
  8. Nyie kimewauma sana jamaa kudrop jina lake la mwisho na kubadilisha spelling za jina eenh?
    Na hata kama kabadilisha wewe kinakuuma kwani ndugu yako huyo?
    Mbona mamake mwenyewe hajalalama wala kusema lolote?
    Na bado akionyeshwa kwenye TV waliandika anatumia jina la Manka as well as his borther and sister too..!
    Kwa hiyo nyie acheni porojo zenu za uswahilini kubishana mambo ambayo hayana faida maishani mwenu..!!
    Kama alikuwa anataka asiujulishe huo u-Tanzania wake na kujifanya wa kishua asingesema kasoma Makongo..!!
    Kwa hiyo hiyo ni juu yake yeye na kwa manufaa yake yeye..!!
    Na huyo jamaa aliyesema jina lake ni Hashimu Thabiti umekosea mzee ni Hashim Thabit, kwa tuliosoma nae Vituka na Makongo ndio tunayajua hayo.

    ReplyDelete
  9. Mi nashindwa kuelewa jamaa na stori zake.Mara alipata chuo kwa internet mara kuna mtu alimfanyia mpango...jamaa anaboa !

    ReplyDelete
  10. Nimemuona alivyokuwa nahojiwa kweny big 10 channel.Walikua wawili tu waliohojiwa na yeye ndio mmoja wao. ukweli ni kuwa kijana anajitahidi na english yake kama ana miaka si zaidi ya minne usa basi anajitahidi saaaana tu.kuhojiwa kwenye public namna hiyo na bado accent haikutokeza sana kama kina matombo amejitahi

    i wish him all the best jumamosi wakipambana na michigan

    ReplyDelete
  11. wabongo acheni umbeya. kijana anauza sana nyie wivu umeshawaanza. naona majasho ya puani yanawaanza kutoka. amebadili jina s what. kwani ndio mpira hatauweza tena? kaeni mkao wa kula mwenzenu anapaaa soon mtamsikia nba

    ReplyDelete
  12. Jamaa analiletea sifa taifa, habari ndiyo hiyo. Kama akiitwa au kujiita Hashim, Hashimu, Hasheem au Kikapu ni uamuzi wake binafsi kama mtu mzima ambao tunapaswa kuuheshimu. Sheria za nchi yetu zinaruhusu mtu kujibadili jina kwa hiyo haendi kinyume na uTz.
    Tumpe pongezi anavyopambana kijasiri katika michuano ya NCAA. Hayo mashindano ni mazito, wachezaji walio wengi NBA walijijengea sifa katika ngazi ya NCAA. Sio kwamba nazidharau timu zetu za nyumbani lakini timu zinazopambana sasa hivi katika michuano ya NCAA zikicheza na mabingwa wetu Tz hata tukiwa na Maximo wa mpira wa kikapu kwa mwezi mmoja itakuwa vigumu sana kupona.
    Wadau tunakutakia mafanikio na uendelee kuliletea taifa letu sifa.

    ReplyDelete
  13. OBAMA KAMUALIKA WHITE HOUSE JUST FOR DINNER ONLY NA KUKUKMBUSHANA KISWAHILI...UKIANDIKA HIVI COMM ZAKO ZITAPITA.
    WHERE IS FREEDOM OF SPEECH. KAMA UNATAKA WATU WACHANGIE WAPE UHURU AS LONGER HAWATUSI MTU.

    ReplyDelete
  14. mdau unaonaje tukichapisha fulanaz yenye picha yako kama michael jordan vile halafu uwe tm yako ht. ulaji huo baba ake vikapu 5 tokana rebound 13, big up mjomba tuchapishe ngwamba za wavu wavu jezi no yako tumeiona.usibadili tu. kudadeki blog kama enzi ya utawala wa nyerere.ukimkosoa mtu umepotezwa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...