Leo JK ameteua Wakuu wa Wilaya 15 new DCs, 7 wamestaafishwa na 54 wamehamishwa vituo, ili kuongeza chachu ya uwajibikaji katika kusimamia na kuratibu mipango mbalimbali ya maendeleo na uchumi ili kutimiza malengo ya serikali.
Kwa mujibu wa taarifa toka Ofisi ya Waziri Mkuu, Ma-DC wawili wamepangiwa kazi zingine na wawili wengine wamepangwa kufanya kazi katika jumuiya za chama tawala - CCM.
Walioteuliwa kwa mara ya kwanza ni Ms Mercy Sila (Arumeru - Arusha), Mr Norman Sigalla (Hai – Kilimanjaro), Col Issa Njiku (Misenyi - Kagera), Ms Angelina Mabula (Karagwe - Kagera), Dr Rehema Nchimbi (Newala - Mtwara), Francis Isaac (Mbulu - Manyara), Lt Col Benedict K Kitenga (Rorya - Mara) na Lt Col Cosmas Kayombo (Mbarali - Mbeya).
Wengine ni Christopher Ryoba Kangoye (Kwimba - Mwanza), Queen Mashinga Mulozi (Ukerewe - Mwanza), Fatuma Mwassa (Mvomero - Morogo), Fatma Ally (Nanyumbu - Mtwara), Juma Solomon Madaha (Tunduru - Ruvuma), Anatory Choya (Kishapu - Shinyanga) na Erasto Sima (Korogwe - Tanga).
Ma-DC waliostaafu ni Elias Marugu (Misenyi - Kagera), Deusdedit Mtambalike (Muleba - Kagera), David Holela (Babati - Manyara), Hawa Ngulume (Mbarali - Mbeya), Mashiba H Mashiba (Kyela - Mbeya), Col Peter Madaha (Nyamagana - Mwanza) na Gilbert Dololo (Kibaha - Pwani).
Ma-DC waliopangiwa kazi zingine ni Patrick Tsere aliyekuwa DC (Ilala – Dar es Salaam), na Doreen Kisamo (Uyui - Tabora). Mr Martin Shigela ambaye alikuwa DC (Lindi - Lindi) sasa ni Katibu Mkuu wa UVCCM ambapo Husna Mwilima (Hai - Kilimanjaro) sasa ni Katibu Mkuu wa UWT.
Waliobadilishwa vituo ni pamoja na Elias W. Lali kutoka Arusha – Arumeru kwenda Ngorongoro, Evans Balama toka Arusha – Arusha kwenda Ilala, Jowiko W Kasunga kutoka Arusha – Ngorongoro kwenda Monduli, Col Fabian I Massawe toka Dar es Salaam – Kinondoni kwenda Muleba, Abdallah A Kihato toka Dar es Salaam –Temeke kwenda Kyela.
Wengine ni Zainab Kwikwega toka Dodoma – Bahi kwenda Kasulu, Dr Ian J. Langiboli toka Dodoma – Chamwino kwenda Babati, Capt Seif A. Mpembenwe toka Dodoma – Kondoa kwenda Handeni, Halima Dendego toka Dodoma – Mpwapwa kwenda Kilosa, Lephy B Gembe toka Iringa – Makete hadi Chamwino na Elaston J. Mbwilo toka Iringa – Iringa kwenda Mtwara.
Wengine ni Darry I Rwegasira toka Iringa – Njombe kwenda Mpwapwa, Said M Mkumbo toka Kagera – Chato kwenda Temeke, Frank A Uhahula toka Kagera – Karagwe kwenda Tarime, Lt Col John Mzurikwao toka Kigoma – Kibondo kwenda Mpanda, Saidi Bwanamdogo toka Kigoma – Kasulu kwenda Kondoa, Raymond H Mushi toka Kilimanjaro – Rombo kwenda Arusha.
Wengine ni Jordan Rugimbana toka Kilimanjaro – Mwanga hadi Kinondoni, Rashid M Ndaile toka Lindi – Nachingwea kwenda Chunya, Anna Magowa toka Lindi – Liwale kwenda Hanang, Elias Goroi toka Manyara – Mbulu kwenda Nachingwea, Capt Geoffrey Ngatuni toka Manyara – Hanang kwenda Musoma.
Walohamishwa wengine ni Saveli Maketta toka Mara – Musoma hadi Namtumbo, Stanley Kolimba toka Mara – Tarime kwenda Uyui, Ms Miriam L Lugaila toka Mbeya – Rungwe hadi Misungwi, Halima Kihemba toka Mbeya – Mbozi kwenda Kibaha, Fatuma L Kimario toka Mbeya – Chunya kwenda Igunga.
Wengine ni Athuman H Mdoe toka Morogoro – Kilosa kwenda Mwanga, Hawa Ng’humbi toka Morogoro – Mvomero hadi Makete, Gishuli M Charles toka Mtwara – Mtwara kwenda Njombe, Jackson W Msome kutoka Mtwara – Newala kwenda Rungwe, Capt Assary Geofrey Msangi toka Mtwara – Nanyumbu kwenda Iringa.
Wengine ni Samwel Kamote toka Mwanza – Ilemela hadi Bukoba, Danhi Makanga toka Mwanza – Kwimba kwenda Kibondo, Magalula S Magalula toka Mwanza – Misungwi hadi Lindi, Paul Chiwile toka Mwanza – Ukerewe kwenda Liwale, Mathew K Nasei toka Mwanza – Magu kwenda Muheza, Lt Col Serenge M. Mrengo kutoka Pwani – Bagamoyo hadi Ilemela, Ali N Rufunga toka Pwani – Rufiji kwenda Manyoni.
Wengine ni Major Bahati Matala toka Rukwa – Sumbawanga kwenda Kahama, Thobias Mazanzala toka Rukwa – Mpanda kwenda Sumbawanga, Gabriel Kimolo toka Ruvuma – Namtumbo kwenda Mbozi, Peter Toima Kiroya toka Ruvuma – Tunduru kwenda Rombo, Amina Masenza toka Ruvuma – Mbinga kwenda Shinyanga.
Waliohamishwa vituo wengine ni Khadija R R Nyembo toka Shinyanga – Kishapu kwenda Chato, Col (rtd) Edmund Mjengwa toka Shinyanga – Shinyanga kwenda Mbinga, Magesa Mulongo toka Shinyanga – Bukombe kwenda Bagamoyo, Florence A Horombe toka Singida – Singida kwenda Bukombe, Pascal Mabiti toka Singida – Manyoni kwenda Singida, Cleophas Rugarabamu toka Tabora – Igunga kwenda Nyamagana.
Wengine ni Kassim Majaliwa Majaliwa toka Tabora – Urambo kwenda Rufiji, Lt Winfrid F Ligubi toka Tanga – Handeni kwenda Urambo, Elizabeth Mkwasa toka Tanga – Korogwe kwenda Bahi na Zainab Kondo toka Tanga – Muheza kwenda Magu.
Mwanamtandao Norman Sigalla naona wamekupa kitengo. Kila la heri
ReplyDeleteNDUGU ZETU JAMANI NATANGAZA UPENDO UTAWALE KATI YA MLIOKO BONGO NA UGAIBUNI HASA KWA AKINA DADA,
ReplyDeleteSISI TULIOKO UGAIBUNI TUNAWAPENDA SANA NATUNAWAOMBEA MEMA KILA SIKU ILI SIKU MOJA BONGO IWE KAMA UGAIBUNI
MSIKAZANIE KUSEMA BONGO TAMBARARE BADO HAPAJAWA TAMBARARE ILA TUNAOMBA SIKU MOJA IWE TAMBARARE KWANI NI KWETU.
Naona kuna mada ndani ya mada!,Nirudi kwenye mada, heko JK!, endelea kutembeza fagio!, fukuza wote wasiowajibika!
ReplyDeleteJAMANI NYUMBANI VIPI MBONA KILA SIKU MABADILIKO LAKINI MAENDELEO HAKUNA! WATU WALE WALE NATHANI CHA MUHIMU NI SERA TU! MBARIKIWE NDUGU ZETU BONGO
ReplyDeleteNIMESOMA WAKUU WOTE WALIVYOPIGWA MAPANGA HUMU NA JK. AJABU MKUU WA WILAYA YA NANIHII (TEGETA), AMENUSURIKA! MHH HII WILAYA INA WALAKINI...TUTAONA YETU MACHO
ReplyDeleteHongera Bro. Lt Col Cosmas Kayombo. Mtu safi sana na huo ni mwanzo najua utafika mbali sana. Kaza uzi!!
ReplyDeleteMkuu wa wilaya ya nanihii mbona sioni jina lake hapa? Au anaendelea na kazi katika wilaya yake ya nanihii. JK hongera ila watanzania nadhani wana kiu ya maendeleo na si mabadiliko ya mara kwa mara yasiyoleta tija.
ReplyDeleteJamani yule jamaa yangu Ibrahim Marwa bado anapeta na ukuu wa wilaya?? Yuko wilaya gani siku hizi maana simuoni katika list hii au yeye mabadiliko hayakumgusa??
ReplyDeleteNi mchapa kazi na mtafutaji mzuri kwa njia halali, namfagilia wa wa waaaa.
Mkuu wa wilaya ya nanihii balozi nanihii hajaguswa na mabadiliko haya...Duh ze fulanazzzzzz ina fanya vitu vyake!! au labda ni utendaji mzuri tu ...tusimsingizie!! Hajawahi hata kutishia kuchapa mtu viboko atahamishwa vipi? Najuuuuuuuta kukufaham!!!
ReplyDeleteDr Rehema Nchimbi(MPYA) HIRI JINA SIJARIELEWA VIZURI. MHESHIMIWA TUNASHUKURU KWA KUTUTANGAZIA MA DC, SASA MHESISHIMIWA TUTANGAZIE BASI NA MAJINA MATATU YA WANAOAJIRIWA NA TRA NA BOT PAMOJA NA QUALIFICATION ZAO
ReplyDeleteNI MAONI TU, INAWEZEKANA KULIKUWA NA ULAZIMA WA KUTEUA WAKUU WAPYA KWA SABABU YA WACHACHE WANAOSTAAFU.
ReplyDeleteILA WANAOHAMISHWA DU, MBONA WENGI HIVYO..SASA HIVI RAIS WETU AMEDECLARE KUWA HALI YA KUYUMBA KWA UCHUMI IMEINGIA TZ NA ITATUAFFECT SANA. NINAVYOELEWA SERIKALI, UHAMISHAJI MAMILION YA SH. YATATUMIKA...MAANA WENGINE KUNA KUHAMISHA MIFUGO, NA WENGINE WATASINGIZIA MIFUGO WASIYOKUWA NAYO ILI MRADI TU WAJIPATIE VISENTI N.K.
HIVI UHAMISHAJI WA AINA HII INA MAANA UTENDAJI KAZI UMEKUWAJE?
ILA NAONA MKUU WA WILAYA WA NANIHII YEYE HAJAGUSWA
Naona mjomba Tsere kawekwa kando, sijui atakuwa Balozi nchi gani!!
ReplyDeleteWewe mdau hapo juu uliyeongea kuhusu gharama za uhamisho kwenye kipindi hiki cha mtikisiko wa uchumi duniani umeongea pointi nzuri sana,umeharibu ulipoweka utani huko mwishoni.
ReplyDeleteSerikali yetu bwana,juzi bwana Lipumba amewambia wapunguze matumizi yasiyo ya lazima lakini wapi
Masoud Masoud DC Marwa bado yuko Same. Yeye kama maDC wengine hawakuhamishwa. Marwa ni hard working na muadilifu.
ReplyDeletehapo hakuna kitu maana watu ni wale wale hapo ni kama alivyosema jamaa ni kupoteza pesa maana watasingizia mpaka mababu zao ili pochi litune MUNGU IBARIKI TANGANYIKA SORY TANZANIA
ReplyDeleteTusubiri siku mbili tatu hadi Aprili mosi kwa habari zinazomhusu mkuu wa wilaya ya nanihii.
ReplyDeleteHongera sana Dr Rehema Nchimbi. Mdau uliyeuliza kuhusu Dr Rehema Nchimbi si mpya. Ni mjumbe wa NEC na ni mjumbe wa UWT. Pia ni mkufunzi UDSM idara ya Historia.
ReplyDeleteDAVID VILLA
ReplyDeleteNAWITHDRAW SENTESI YANGU YA MWISHO KUHUSU MKUU WA WILAYA WA NANI HII ILI MAONI YABAKIE NA NGUVU....
UKWELI INASIKITISHA KAMA KULIKUWA NA ULAZIMA WA KUHAMISHANA NAMNA HII WAKATI WANATAKIWA KUBANA MATUMIZI.
CHEKI MAKINI NA HIZO HAMISHO, WENGINE UTAONA WANATOLEWA KASKAZINI KUPELEKWA KUSINI....
NDO MAANA NAULIZA? KUHAMISHANA NAMNA HII KUNAHUSIANA NA NINI NI KWAMBA UTENDAJI WA KAZI UMEKUWAJE, JE KUNA ULAZIMA HIVYO KIPINDI HIKI? SI AJABU UTASIKIA WAKUU WA MIKOA NAO UHAMISHO KARIBUNI.
WATAKAOKUWA NA DATA KUTOKA SIJUI HAZINA WAJE WATUAMBIE ZOEZI LIKIKAMILIKA TSH NGAPI ZIMETUMIKA KUHAMISHANA.
NI HATARI LAKINI...VINGINE TUNAJITAKIA...
HII NCHI HAIHITAJI MKUU WA WILAYA HATA MMOJA. KINACHOTAKIWA NI KUWAFUTA KAZI WOTE NA SAVINGS ZITAKAZOPATIKANA ZIELEKEZWE KWENYE SHUGHULI ZA KIMAENDELEO KAMA KUJENGA BANDARI NA RELI MPYA YA KATI. ACTUALLY HATA WAKUU WA MIKOA HATUWAHITAJI TUNACHOHITAJI NI TUME ZA KITAALAMU KAMA YA "KEENJA" KUFANYA KAZI ZA KIMAENDELEO MIKOANI. HAWA WAKUU WA WILAYA NA WA MIKOA NI WANASIASA NA KIMSINGI SIASA IMESHINDWA KUTULETEA MAENDELEO NCHI HII.
ReplyDeleteWANAOSEMA JK MDINI MBONA ANACHAGUA WAKRISTU KILA SIKU.LAKINI BADO ANAAMBIWA MDINI.
ReplyDeleteHongera kaka Norman you deserve it.Kila la kheri ila tu usijisahau kama wengine,i believe theres is more to come this is jus the beginning .Mungu akutangulie.
ReplyDeleteMdogo wako. Loleza.(97-99).
Kaka Michuzi tunashukuru kwa habari ila tunaomba utufanyie utafiti hili zoezi limeigharimu au litaigharimu serikali kiasi gani cha pesa.
ReplyDeleteJK ange balance kwani kwenye 15 wapya waislam ni watatu tu waliobaki wakristu.angempa balozi Michuzi ili wawe wanne.
ReplyDelete