Mh. Chenge

Mbunge wa Bariadi Mashariki Mh. Andrew Chenge anashikiliwa na polisi kufuatia ajali iliyosababisha vifo vya wasichana wawili usiku wa kuamkia leo sehemu za oysterbay jijini dar, kamanda wa kanda maalum ya mkoa huu afande Suleiman Kova, amethibitisha.


Afande Kova amesema kwamba Mh. Chenge alikuwa akiendesha Toyota Pick-UP Hilux yenye usajili namba T 512 ACE ambayo iligongana na Bajaji yeney namba za usajili T 736 AXC na kusababisha vifo vya hao wasichana wawili ambao hadi sasa hawajaweza kutambulika.


Amesema marehemu walikuwa wamekodi Bajji na kwamba dereva wao alinusurika na hadi sasa hajulikani aliko na anatafutwa.
Afande Kova kasema Mh. Chenge ataendelea kushikiliwa wakati upelelezi unaendelea chini ya Naibu Mkurugenzi wa Makosa ya jinai Afabde Peter Kivuyo.


Afande Kova alimtaja mmiliki wa bajaji kuwa ni Bi. Zuwena Faith ambaye ameamriwa kuripoti polisi, ikiwa ni mojawapo ya hatua za kusaidia upelelezi wa kumsaka dereva wa bajaji aliyeingia mitini.
Miili ya marehemu, ambao wanakadiriwa kuwa na umri wa miaka 20 na 28 imehifadhiwa mochuari ya hospitali ya mwananyamala.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. pole kwa wafiwa,lakini jamani naomba tujadili hili. hizo bzjaji tangu zirihusiwe rasmi mwezi wa kwanza ,zishaua watu watano kwa ajari za aina hiyo.mie naona bajaji dar sio mahala pake.kwani hata india zilikoanzia ,wametengeneza mbadala ,na sasa zinaondoka barabarani,kwa nini bongo zisipigwe marufuku,au watu wazisusie. madereva wa vibajaji,wanaovertake vibaya ,wakifikiri hizo ni baiskeli tu au pikipiki. NAOMBA TUZIPIGE VITA,HAZILETI HATA SURA NZURI YA MJI.KWA WALIOSHAFIKA INDIA WANAFAHAMU,NAONGEA NINI.

    ReplyDelete
  2. Tutakomesha ajali za barabarani kama wanaosababisha vifo watahesabiwa kama wauaji wengine km wale wa wanaotumia Bunduki

    ReplyDelete
  3. jamani bajaji mpaka mjini utazani tuko india mnaona sasa nyie viongozi mnaposhindwa kubolesha nchi njaa zinawapelekea watu kuchacharika na bajaji kila kona
    na kama uchumi ukiwa mbaya na nyie mtaonja tu joto ya jiwe

    ReplyDelete
  4. inchi imekuwa kama ya wendawazimu,watu wanaingiza biashara bila mpangilio mara bajaji jijini wapina wapi mbona nyie hampandi bajaji? mmemuletea nani? nani kaizinisha biashara za bajaji jijini??
    mnajitia mikosi kwa uvivu wenu wa kufikili

    ReplyDelete
  5. mimi kwa kweli sio kwamba ninamtetea Chenge lakini sheria iko wapi? ukigonga mtu akifa hata makosa si yako unawekwa ndani. jamani lazima tuangalie ya msingi dereva wa bajaji kakimbia! moja kwa moja yeye ndie mwenye makosa, wanaita hit and run, sasa itakuwaje polisi wamshikirie dereva ambaye hakukimbia. na umeona uendeshaji wa bajaji DAR? si mchezo, vinapinduka kila siku, wanaendesha vibaya sana hata wengine hawana hata leseni. yaani wizi mtupuuu.

    ReplyDelete
  6. kwanini wabongo muishio nyumbani bongo wengi wao wanahasira na wabongo waishio ugaibuni??

    NATAKA KUSEMA HIVI SISI WOTE NI NDUGU WATOTO WA BABA MMOJA KAMA INNOCENT GALINOMA ALIVYOWAHI KUIMBA HAPO ZAMANI

    NA SIO WOTE WALIOKO UGAIBUNI NI WATOTO WA MAFISADI WENGINE TUMEJINYIMA NA KUCHANGA MPAKA TUKAPATA SAFARI LAKINI UTASHANGAA MTU ANAKASIRIKIA WATU BILA SABABU

    TENA UTAKUTA KINADADA WANAPENDA SANA KUJIREMBA ETI ANASHINDANA NA WATU WALIOKO UGAIBUNI
    JAMANI BONGO HAITALINGANA NA MAJUU HATA SIKU MOJA SISI HATUNASHIDA YA KUSHINDANA NA NDUGU ZETU MLIOKO NYUMBANI SANASANA TUNAWAONEA HURUMA NDUGU ZETU KULINGANA NA MAISHA KUPANDA NA SHIDA MNAZO KUMBANA NAZO.

    ReplyDelete
  7. Mungu aziweke roho za Marehemu Mahali pema na Pole sana Mr Chenge kwa yale yote yanayokusibu....siasa ni mchezo mchafu sana! Mungu ainusuru roho yako.

    ReplyDelete
  8. mungu aziweke roho za marehemu mahali pema peponi

    ReplyDelete
  9. MARA NYINGI NIMESEMA SHERIA ZA NCHI YETU ZINA SIASA NA USWAHILI. KILA SIKU WATU WAKIPATA AJALI WANAWEKWA NDANI. SASA NI SABABU GANI CHENGE AWEKWE NDANI WAKATI YULE DEREVA WA BAJAJI AMEINGIA MITINI. KAMA MAMBO NDIO HIVI TANZANIA SIJUI TUTAISHIA WAPI. HUKO POLISI KUNA MTU ANATAKA APANDISHWE CHEO. MAHAKIMU WETU PIA WANAPENDA SANA KUWAPA WATU VIFUNGO VISIVYO LINGANA NA MAKOSA. TAFADHALI RAISI WETU KIKWETE PITIA UPYA SHERIA ZA TANZANIA.

    ReplyDelete
  10. MH! MIMI SIJUI MAGARI LAKINI HII HABARI YA CHENGE TULIYOANDIKIWA ALIKUWA ANAENDESHA TOYOTA HILUX PICK-UP WAKATI GARI LENYEWE LILIPATA AJALI NI TOYOTA LANDCRUISER, INATUCHANGANYA.
    HII INAONEYSHA JINSI GANI WAANDISHI WETU WASIVYOKUWA MAKINI NA KUTOJUA AMA KUFAHAMUA KILE WAKIANDIKACHO.
    MWINYI ALIPOSHAMBULIWA (ASSAULT) NA KIJANA MMOJA, TUKAANDIKIWA TENA KWA HERUFI KUBWA-MWINYI APIGA KOFI-! EEE, WA JEMENI KAMA HABARI ZA MASANJA NA KUBONYEZA KIZENJI! HATARII

    ReplyDelete
  11. POMBE SI CHAI

    ReplyDelete
  12. yeah hata mimi hapa nitasema leo...chenge simfagilii sana lakini hapa kulikoni aekwe ndani na yeye hakukimbia alivyopata ajali? bongo na sheria zao mbona kazi? ukigongwa waekwa ndani? ndio maana kila mtu anakimbia akipata ajali manake hujui ni nani kakugonga...hata kama huna kosa unaweza ukaishia jela kama huna fweza. manake huyo ni chenge kawekwa labda siku mja ..mimi na walala hoi wenzangu ingekuaje

    ReplyDelete
  13. Ni kweli kabisa wewe mtoa maoni wa March 28, 2009 3:14 AM hujui vizuri (kuangalia)magari. Hebu jaribu kuangalia tena kwenye hiyo picha hapo juu, utapata uhakika kuwa unachosema sio sahihi. Acha kuwaponda waandishi kila mara ingawa mara nyingi nao huwa wanachemsha,wanashindwa hata kufanya spelling check.

    ReplyDelete
  14. Wewe anony uliyesema habari ya 'Hit and run' unaniachia maswali.... Je iweje hiyo bajaji igonge kwa nyuma gari ya mh imeumia kwa mbele? hapo nani kagonga! kagongwa au wamegongana ki vipi??? Lakini pia.... ninawaza tu... huyo dereva kakimbia au kakimbizwa??? vijicent vyaweza mengi!!!

    ReplyDelete
  15. Ni kweli waandishi wa bongo wengi wao hudhani wanaweza kuandika kila habari.... hii si kweli .... yapo maeneo yanahitaji kuwa na utaalam wa kina ili uweze kueleza jambo kwa jamii mchanganyiko...na endapo huna kitu unamtafuta mtaalam husika kuzungumzia jambo hilo....usione soni!! Bongo tambarare hata ukiona waandishi wakihoji juu ya jambo .... utawahisi kuwa weupeeee!!! wapiga picha (video)wao ndio bure kabisa wanakalia kumwonyesha mwenzao kuliko tukio husika...hovyoooo.. mnalohilo!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...