JK (aliyevaa kanzu ya Rangi ya udongo) akishiriki katika kuuswalia mwili wa Marehemu Mbaraka Selemani Kikwete wakati wa ibada ya Mazishi iliyofanyika kijijini Msoga,wilaya ya Bagamoyo leo jioni. Marehemu Mbaraka Kikiwete ni mtoto wa Kaka yake JK, Mzee Selemani Kikwete

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Nafikiri kiswahili safi ni kanzu ya rangi HUZURUNGI
    Tafadhali kumbuka kuna watu wengi wasoma blog kujifunza lugha
    Naomba samahani,mie si makujua
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  2. Nadhani kiswahili safi sio HUZURUNGI ni HUDHURUNGI

    ReplyDelete
  3. Anonymous wa kwanza na wewe umekosea sio HUZURUNGI ni HUDHURUNGI.

    Wafiwa tuko nanyi katika sala na maombi katika kipindi hiki kigumu cha majonzi, poleni sana.

    ReplyDelete
  4. Inna lillaah wa inna illaah rajiun.

    ReplyDelete
  5. Sasa anony wa kwanza hicho ni kiswahili safi? manake unakosoa mwenzio wakati ww mwenyewe uko wrong!! Toa kwanza kibanzi ndani ya jicho lako..

    ReplyDelete
  6. HUYO JAMAA ALIESHIKA SIJUI,KAMERA AU KITABU SIJUI NINI,INAONEKANA HAYUPO KABISA KIMAWAZO KATKA SUALA HILO YEYEYUPO KIMWILI,HEBU MCHEKI ANAKOANGALIA AU NDIYO MAMBO YA TAHADHARI BOSI AZIZABULIWE KIBAO

    ReplyDelete
  7. Mdau wa 3.08 naomba samahani. Kiswahili nilichosema kama mdau wa kwanza ni safi na halisi.Mdau wa pili kasema kwamba nimepotea kidogo kwani hiyo rangi ni hudhurungi siyo huzurungi.Nakukumbusha katika lugha ya kiswahili--zu na dhu- are interchangeable kama vile huzuni na hudhuni,uzaifu na udhaifu.Bila shaka wewe nami twatumia kamusi tofauti na tuna tofauti ya kijografia tulipo zaliwa
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  8. Ohooo... hapa masibani patakua hapatoshi sasa hivi, maana waswahili na waswahilina wameanza hapa hapa, mara rangi ya uzurungi, udhurungi, udhuru. mara rangi ya kahawia. Mara rangi ya samawati, mara rangi bahar mara rangi ya magharib. Haya bwana kupotea njia ndo kujua njia, na kujifunza kwaja hivihivi ila usiwe mbishi bila sababu toshelevu tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...