JK akikaribishwa na waziri mkuu wa uingereza Bw. Gordon Brown Lancaster House leo
JK akiongea wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo baada ya mkutano wa  Pre G20 London Summit katika jumba la  Lancaster House jijini London leo. wengine toka shoto ni  rais wa African Development Bank Dr.Donald Kaberuka, Waziri Mkuu wa kenya, Mh. Raila Odinga, Rais wa Liberia Mh. Sirleaf Johnson, waziri Mkuu wa Ethiopia Mh. Meles Zenawi na Waziri wa Fedha wa Afrika Kusini,  Mh. Trvor Manuel. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. HII MIKUTANO KWA NCHI ZA AFRICA NI KASHFA NA ZAIDI TUNACHEKWA NA MATAIFA MAKUBWA.

    ReplyDelete
  2. JE, KABLA YA MPOROMOKO WA FEDHA DUNIANI SISI TULIKUWA KATIKA HALI NZURI? AU TUNABEBWA NDANI YA MELI AMBAYO HATUJUI IENDAKO? HUKU KWETU SI JUA WALA MVUA NI SHIDA TUPU TUKIACHA VIONGOZI WETU WANAOENDELEA KUNAWILI KILA KUKICHA.

    ReplyDelete
  3. Anony 1,hakuna nchi Zaidi ya Bustani Ya Eden iliyojengwa bila External Gears.Kwa namna gani?basi hapo ndio inategemea mipango endelevu,mikakati yakinifu na Sera mbadala kwa nyakati ambatano.
    Sasa wewe 1 hebu tupe mkakati mbadala utakaotuondolea AIBU ya kuchekwa na Mataifa Makubwa na sio kubweteka tu na kukaa kimya.Haya Shime yetu masikio tukusikie na macho tukusome.
    KAPILA M

    ReplyDelete
  4. Nashindwa kuelewa ni vipi mkutano huu uitwe Pre-G20 LONDON Summit!Wakati wote hao wanao onekana katika picha ni viongozi wa nchi ambazo sizo wanachama wa G20.Wameitwa tu na Gordon Brown kutaka kusikia kilio chao kuhusu Mparaganyiko wa Uchumi Duniani na kujua jinsi nchi za Afrika zilivyo athirika.Na muhimu zaidi kutaka kusikia nchi zenyewe za Afrika zimejitayarisha kiasi gani ili kukabiliana na misukosuko hiyo ya kiuchumi ambayo hakuna nchi yeyote Duniani itakayo bakia salama bila kuguswa kwa namna moja au nyingine.Sina uhakika iwapo kuna nchi yeyote ya kiafrika iliyojitayarisha kikamilifu kukabiliana na mparaganyiko huo wa kiuchumi duniani!Kujitayarisha maana yake ni kuwa na Mikakati, Mipango na Miradi Maalum itakayo ivusha nchi hizo katika mkanganyiko huu.Zungumzia mradi wowote,hautokosa nafasi na mahitaji ya Ufadhili toka kwa nchi Wahisani,kama miradi hiyo ipo na imetayarishwa ikisubiri utekelezaji.Kumbuka mpango huu lazima uwe tofauti na Mipango ile tulioizoea kila mwaka ikihitaji ufadhili toka nchi wahisani.Afrika bado imegawanyika katika masuala mbalimbali.Ushirikiano wa Kibiashara baina ya nchi za kiafrika bado ni wa kiwango cha chini sana!Bado tuko mbali sana na kuwepo kwa "African Monetary Fund",kuwepo kwa Sarafu Moja ya Afrika ambayo itakuwa na nguvu katika masoko ya fedha na hisa ya kimataifa!Sijasikia Viongozi wa nchi za Afrika wakikutana kujadili kwa pamoja athari za mparaganyiko huu wa uchumi duniani kwa Chumi za nchi za Afrika na jinsi ya kukabiliana na Changamoto hiyo!Mbali na mkutano huu wa karibuni ulioitishwa na IMF jijini Darisalama!Africa is still so divided on various issues related to inter trade and common market.Africa is still so dependent on industrialised west and does not seem to have any "exit plan"of its own out of the vicious circle of poverty and perpetual dependency!Kwa hiyo wanapokutana katika mialiko kama hiyo ya pre-G20,nchi za kiafrika hazina nguvu kabisa ya majadiliano isipokuwa kusubiri "HISANI ZA NCHI TAJIRI!".Hawalazimiki kutusaidia.Kutusaidia au kutotusaidia "NI HIARI YAO TU".Tutaendelea na mwelekeo huu hadi lini?Afrika imeshakamilisha miaka 50 toka baadhi ya nchi zake zilipo anza kupata Uhuru wa Kisiasa!Kwa nyingine hata miaka 60!Lakini kla kukicha Bora Ya Jana!--tonnie--

    ReplyDelete
  5. When you see such faces of African Heads of State gathered together in an important dialogue with the Leaders of the Industrialised Countries like it is about to happen this week,what immediately crops up your spine is the chilling realisation of "What Has Africa Got To Offer" to the rest of the World in this scenario of Unequal Exchange in International Trade? Africa can only engage in a competitive dialogue with the Industrialised Countries if "Africa has anything to offer"to the World!If they will remain mere Recipients of Aid but nothing to offer in return,the mutual exchange will no longer remain mutual,the competitiveness of the trade exchanges will no longer remain competitive,the equal partnership concept between the Industrialised and Africa will forever remain a "pipe dream".Have these African Heads of State gone to London "to offer something" to the World? Or have they gone there simply as "Recipients of Aid?".Until such time when Africa ceases to remain a "Dummy Variable" in the Equation of UnEqual Exchange and Trade,we will have assured ourselves of a permanent seat at the back of the Dock of the Civilised World!Where are you Africa?-----tonnie-----

    ReplyDelete
  6. We Anony March 17, 2009 9:52 AM

    You sound to be someone related to Kikwete or CCM or Government generally.

    No one is there to develop Tanzania, which external gear you mean here ....????

    Dont you know Africa was underdeveloped by same people we are embrancing nowadays.

    No body is there for Tanzania interest ... every body is there for the benefit of his/her own country and his/her voters ...

    And those big nations wants to maintain the supremancy at any cost ....

    They will say this or that but the closing line is their own stomaches and not yours

    You just go there and wait to get exploited under the umbrela of Globalization

    ReplyDelete
  7. WATANZANIA TUKUMBUKE ENZI ZA MWALIMU NCHI ZA NORDIK ZILMWAGA MISAADA MINGI SANA TANZANIA KIASI CHAKUMFANYA MWALIMU ASIISIKLIZE BENKI YA DUNIA, LAKINI CHA AJABU MISAADA YOTE ILILIWA NA KITU PEKEE KILICHOBAKI NI MRADI WA SHULE YA SEKONDARI YA KIBAHA! SISI HATUBEBEKI KWANI HATA TUKIJUA VIONGOZI WETU WANAKULA VIPI MISAADA HATUTAKI KUBANANA MITAANI KAMA WANAMADAGASKA, HIVYO TUTAENDELEA KUWA MASIKINI DAIMA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...