JK katika picha ya pamoja na viongozi wenzie wa  SADC  kwenye jumba la kifalme la  Lozitha huko Swaziland, leo. Wengine toka shoto baada ya JK ni  Rais Robert Mugabe of Zimbabwe, Mfalme Mswati III  wa Swaziland,  Rais  Khaglema Montlante wa Afrika ya Kusini,  Rais Joseph Kabila wa Kongo  DRC), na Rais  Armando Guebuza wa Msumbiji. Wengine yuma toka shoto Waziri Mkuu  Phakalitha Mosisili  wa  Lesotho, Rais Bingu wa Mutharikawa  Malawi na Rais Rupia Banda wa  Zambia. Picha na Mdau Freddy Maro wa Ikulu
JK akiongea na Rais aliyeondolewa madarakani  wa Madagascar Marc Ravalomanana mjini Manzini, Swalizand, asubuhi ya leo muda mfupi kabla ya kuanza mkutano wa viongozi wa nchi za maendeleo ya kusini mwa afrika SADC.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Kichwabuta Mwendantwala, OSLOMarch 30, 2009

    Huyo FISADI MKUBWA Marc Ravalomanana anatafuta nini huko wakati wananchi wake wenyewe hawampendi ??? Unajua hii aina ya viongozi kama huyu wa AFRIKA wanapochukua madaraka wanajisahau na kuanza kujilimbikizia MALI mpaka wananchi wanachuki ndio wasiotakiwa. Kwani naye aliingia madarakanai kwa STYLE aliyoingia nayo KIONGOZI wa MAPINDUZI wa sasa. Sasa anaenda huko SWAZILAND anafikiri hao marais watamsaidia ikiwa wananchi wake wenyewe hawamtaki ?????? Huyo ni bora arudi nyumbani kwao au aende uhamishoni kwani alishaharibu na HAWEZI kurudi tena madarakani hata akienda kwa waganga wa kienyeji !!!!!

    RAI KWA VIONGOZI WENGINE WA AFRIKA
    Muingiapo madarakani jaribuni kutekeleza na kukamilisha matakwa ya wananchi kama ambavyo mnakuwa mmewaahidi na sio kwenda IKULU kwa tamaa na ULAFI mpaka uongozi unakuwa umekushinda.

    ReplyDelete
  2. TUPELEKE JESHI NA HUKOLIKAFANYE MAZOEZI KIDOGO KAMA ILIVYOKUWA KOMORO...MUDA SASA HATUJAPIGANA VITA JAMANI

    ReplyDelete
  3. Na nyie wa-TZ, mambo yenu wakati mwingine valuvalu! Ki-Anjoun! Halafu, Madag itajiunga na TZ!

    ReplyDelete
  4. ina maana hiyo mswati hana hata suti siku nyingine awe serious na mambo muhimu kama hayo,sasa hivyo vikanga si anawadisturb wenzie sana kwanza nahisi kikwapa kitakuwa kinatena,afadhali angevaa shati na suruali akafunga lubenga juu.

    ReplyDelete
  5. King amecheza heko kimavazi. Anaonyesha kutokuta mtumwa wa mawazo ya magharibi kwamba kuvaa suti na tai ndio unakuwa mheshimiwa.

    ReplyDelete
  6. King Mswati....Bravo! Ila punguza hiyo ya vidogo dogo! Inadhalilisha utu na heshima ya akina mama!

    ReplyDelete
  7. Jamani mwenzenu anaomba hifadhi huyo wala si kingine

    ReplyDelete
  8. KWANI KUANZIA LNI IMEKUWA KUVAA SUTI NDIO USTAARABU?
    HUO NI UKOLONI MAMBOLEO TU, KATIKA ULIMWENGU HUU WA LEO WAAFRIKA TUWE NA MAWAZO MAPANA NA FIKRA HURU, TUACHANE NA FIKRA ZA KUTAWALIWA.
    VAZI LA SUTI NI MATOKEO TU YA KUTAWALIWA, WALA SI CHENGINE.
    MDAU WA 5:48 NAONA MWENZETU UMEJAWA NA KASUMBA ZA WAKOLONI, NA KUONA KUWA SUTI NDO BAB KUBWA.
    KWA TAARIFA YAKO ULIMWENGUNI KUNA TAMADUNI KEDE KEDE, NA ISIKUPITIKIE KUWA KUVAA SUTI NDIO USTAARABU WA MWANZO.
    IMANCIPATE YOURSELVES FROM MENTAL SLAVERY, NON BT OURSELVES CAN FREE OUR MIND
    Mndengereko, Ukerewe

    ReplyDelete
  9. Kingi Mswati wa Tatu pokea zangu tano. Muda wa kuwa na serikali ya muungano wa mataifa ya afrika ukiwadia ninapendekeza APEWE URAIS wa kwanza.

    ReplyDelete
  10. Unajua ravo anamwabiaje kikwete
    Ravo: Kuna kaDJ kameleta rabsha sijui itakuwaje ndugu?
    Kikwete: Hawa maDJ balaa kabisaa kuna moja anaitwa Mbowe analeta za kuleta bongo...ila uzuri siyo muraa
    Ravo: Peleka vijana wako basi bwana
    Kikwete: Ahh! ongea na Qadafi ndio mkuu wetu sasa!

    ReplyDelete
  11. Dah nilidhani King ni mwanamke na hiyo nguo aliyovaa!

    ReplyDelete
  12. kama wewe basha hiyo kanga itakudisturb

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...