Rais Ahmed Abdallah Mohamed Sambi wa Muungano wa Visiwa vya komoro akimtukuku JK medali ya ushujaa na heshima ya Taifa la Komoro kwa kutambua mchango wake katika kukikomboa kisiwa cha Anjouan.Rais Kikwete yupo nchini Komoro kwa mwaliko wa Rais Sambi kuadhimisha mwaka mmoja tangu majeshi ya umoja wa Afrika yakiongozwa na Tanzania yalipokikomboa kisiwa cha Anjouan
JK na Mwenyeji wake Rais Ahmed Abdallah Sambi mara baada ya kumtunuku heshima ya juu ya taifa hilo kwa kuvika medali kwa kutambua mchango wake katika kukikomboa kisiwa cha Anjouan.Shrehe hizi zilifanyika Missiri Stadium kisiwani Anjouan

Mkuu wa majeshi ya Ulinzi na Usalama ya Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange akivikwa medali ya kishujaa katika kutambua mchango wa majeshi ya Tanzania katika kukikomboa kisiwa cha Anjouan



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. jamani hivi mwamunyange ana watoto wa kike,kwani jicho hilo mwana, ni noma eti.

    ReplyDelete
  2. Jicho jicho hilo la kinyakyusa. Akiwa na binti basi itakuwa ni balaa tupu utaibiwa mzima mzima watu watasema amekuloga.

    ReplyDelete
  3. Jicho hilo Mwanangu shuti linaita, Bwana wewe hilo jicho mwanangu, walipate,Binti zako mwanangu weee!!! manake watakua warembo wa jicho si mchezo.

    ReplyDelete
  4. wee, usituzingue hapa, kila ukienda ukirudi jicho jicho jicho!
    huna ulichokiona ila hilo? ovyoo!

    ReplyDelete
  5. jenerali mzima wa jeshi la tz unavaa asumini aghhhhhhhhh!

    ReplyDelete
  6. CHONDE CHONDE WASIFANYE MCHEZO WA KOMORO MADAGASCAR KWANI TUTAACHIWA WAJANE NA YATIMA WENGI KWANI KULE NI MAJI MAREFU...

    ReplyDelete
  7. jamani mie hayo macho hoi bin taabani. Yaani huyu mkuu angekuwa mwanamke ingekuwa balaa kubwa jijini. macho yanaita tu yenyewe. Anyway pongezi sana kwa kutunukiwa hizo medal.

    ReplyDelete
  8. Anon. mar 29 1:59 Pole kwa kukereketwa na hizo asumini, naomba ukumbuke kila nchi ina tamaduni zake na vitu vya thamani wanavyovithamini na kuvipa hadhi kubwa hasa katika kuonyesha upendo na furaha, kumkirimu na kumkaribishia mgeni. m.f nchi nyingi hutumia roses ambapo linaonekana ni ua la thamani kubwa kimtazamo na kharufu yake ni nzuri sana, sasa hizo asumini ingawa ni ndogo sana hata ikiwa moja tu imejifichakharufu yake inahanikiza, na hapo hilo shada akae nalo hata kwa robo saa tu kisha alivue basi koti kama halijafuliwa litanukia hadi anarudi Tanzania harufu haijafifia, hiyo ndo siri ya maua hayo, zaidi ni kuwa hivyo viji-ua kwa tamaduni za watu wa pwani ni ua la thamani sana na linapendwa sana hasa maharusini au kinamama kutunga na kuweka kwenye nyele kama kibanio,au kuweka makabati ya nguo na kadhalika na kadhalika, kwani ni marashi asilia, wale wangazija, tanga, unguja, pemba na wazaramo wanajua zaidi khabari zake kwa kusisimua miada ya pua.

    ReplyDelete
  9. We Mbwige nini hapo juu ulitaka avae nini? Kila nchi inautamaduni wake..Hao huoni wanautamaduni wa kipwani?

    ReplyDelete
  10. watu weweeeeee...ful jicho...WANYAKYUSA OOOOYEEE!!!KIDUMU!!

    ReplyDelete
  11. wewe uliyeguswa na asumini ni kwa nini hukumpigia kelele mheshimiwa rais ilahli nae pia kavishwa? kumbuka kila nchi zina tamaduni tafauti.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...