MUHISHIMIWA MICHUZI

KUNA MAHALI NIMESIKIA MJADALA WA UBAYA NA UZURI WA  WAWILI KUISHI PAMOJA KWA MUDA MREFU BILA NDOA,  SABABU  KUU ZILIZOTOLEWA  NI KWAMBA WENGI WANAHOFIA GHARAMA KUBWA  ZA HARUSI  NA WENGINE WANAHOFIA UKUBWA WA MAHARI. MIE NI MMOJA WA HAO AMBAO NAISHI NA MAMSAPU KWA MIAKA KAMA SITA HIVI BILA NDOA NA TUNA WATOTO WANNE. 

NAOMBA TUJADILI  JE, KUNA UBAYA GANI MWANAMKE NA MWANAUME KUISHI PAMOJA KWA MUDA MREFU BILA NDOA?

HAPO NAZINGATIA KWAMBA WAPENZI WANAWEZA KUISHI MILELE BILA NDOA NA WAKISEMA WAMEREMETE TU NDOA INAVUNJIKA. NA HIO NDIO HOFU YANGU MIMI, SIO GHARAMA ZA HARUSI WALA UKUBWA WA MAHALI WALA NINI. NAOMBA MSAADA WA MAWAZO WADAU...

MDAU WAKO
M.M.I.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 42 mpaka sasa

  1. Inabidi usaidiwe na Papa Benedict anyway kimila ukishakaa na mwanamke muda fulani hiyo ni ndoa tayari,hata Kanisa limatambua na watabariki tu lakini ni ndoa hiyo mzee,Kiislam ndio utapigwa mkeka.Lakini kwa kifupi we ndo ushaoa imetoka hiyo...

    ReplyDelete
  2. Kwa upande wangu mimi naona hamna maisha mazuri na matamu kama ya kumelemeta. hivi sasa ndoa yangu ikifika trh 25.06.2009 inatimiza miaka 17 na tayari nina watoto 5 toka tumelemete kwahali hiyo mimi nakushauri ndugu yangu melemeta uone miraha yake.sema ndio hivyo wanaume/wanawake wengine wanajuta na ndoa zao wanaona kama wameowana/wameolewa na jini kwa matatizo ndani ya ndoa zao.
    Mdau
    Kisiju pwani

    ReplyDelete
  3. huo ni uzinzi firauni mkubwa wewe..na usitumie blog ya jamii kupoteza watu hapa.
    unajua duniani ni wawili wawili na lazima ndoa iwepo tena halali, wewe unaleta habari zako za miaka 6 bila ndoa na unajisifia una watoto 6.
    hujui maadili wewe???
    ngoja kesho utakiona cha moto.

    ReplyDelete
  4. Naomba zitolewe maana(definition zifuatazo za ndoa
    (1) Mtizamo wa Kimila
    (2) Mtizamo wa Kikristo
    (3) Mtizamo wa Kiislamu
    (4) Mtizamo wa Serikali

    Anayeanzisha hoja nae aseme yuko katika mtizamo gani?

    Kuanzia hapo ndipo tuanze kujadili/ kuchangia.

    ReplyDelete
  5. ndugu yangu, lazima kuwe na tafauti kati ya binadamu na wanyama mungu alimpa mwana aadamu akili zaidi ya mnyama na akamtengezea utaratibu kwa kitu chake hata katika hili jambo la ndowa mungu alimpa mwanaadamu namna ya kumkutanasha na mwenzewe hadi kutengeneza kizazi chenue heshima na hadhi ya kuitwa mwanaadamu ndio maana huwezi kumuingilia mama yako , dada yako na mdogo wako sasa kwa kuzaa tu bila ya kuwapo taratibu zinazo kuwekeni nyinyi wazi na kizazi chenu katika hali kutambuana na mipaka yenu ni sawa na mnyama kuendelea hivi kuna uwezekano wa watoto wa mmoja kuingiliana aidha wa baba mmoja au mama mmoja tukawa kama wanyama ukweli kabisa tuachane na hiyo taratibu amabyo kwa mwaadamu mwenye akili timamu hawezi kuishabikia hata thamani ya kizazi chenyewe inapotea machoni mwa jamii hivi watoto wako hao sijui wanne au sita wana tafauti gani na watoto wa mbwa au paka ai kinyama chengine chochote maana ule utafauti kati yako na hawa viumbe wengine umeuondowa tuwache kuza za bila ya taratibu zinazotutafautisha na wanyama tunavitia aibu kubwa vizazi vyetu fikiria umezaa tu ukajitia ujabari ukasomesha kwa bidii zote huyo mtoto wako anamaliza phd ni msomi mzuri jamii unamuona kuwa ni mtu muhimu anayefaa kuwaongoza inapokuja hoja wa kumjuwa wasifu wake jamii inabaini kuwa alizaliwa tu bila ya wazazi wake kuowana hivi kweli tutakubali kuwa labda na rais ambae hana ukoo unajulikana wenye maadili nadhani itakuwa ngumu unaona namna gani gharama ya kuzaa tu bila ya kufata taratibu na iko mifano mingi watu wameshakosa dhamana mbali mbali katika jamii na hata akiwa mtu muhimu akitenda kosa japo dogo watu husema ah mtu mwenyewe ni mtoto wa uzinifu kubwa kama huyo mama yake umempenda kweli na unamuhitaji sana si kumuowa kuna tatizo gani

    ReplyDelete
  6. Kaka uzazi wa mpango !
    niaka 6 watoto 4 mnafanyaja nyie ?
    Kama sungura ? utaweza kuwapeleka wote shule hao ?
    Kaima

    ReplyDelete
  7. Mtoa mada ndoa ni kitu cha muhimu sana kwenye maisha huwezi kuniambia unaishi na mwanmke siku zote hizo bila ndoa eti unaogopa mtaachana huo ni ujinga.
    Kwanza mtawaleaje watoto wenu watoto wanatakiwa walelewe kwenye misingi ya ndoa.
    Hao watoto watakuwa wakubwa mabinti mama yao atawafundisha nini atawaaambia ukipata mtu anataka kusihi na wewe kubali tu mkakae au atawaaambia mjitunze hadi muolewe mfunge ndoa .
    Mimi kwa upande wangu ndoa siyo lazima lakini inapendeza mkiishi maisha ya ndoa na maisha matakatifu hayo mengine yote ni mambo ya dunia na ya kupita. mnataka watoto waige nini?
    Tena ufanye haraka ufunge ndoa wewe wa wapi?

    ReplyDelete
  8. Wewe hujui kuishi na mtu bila ya ndoa nisawa nakuzini na zinaa inakatazwa katika dini zote fanya ufunge nao ndoa ili muishi kwaroho ya amani.

    ReplyDelete
  9. Bwana we tayari iyo ni ndoa kabisa, sasa ole wako umeremete utatuambia miaka miwili ikiisha mpo pamoja utaniambia, ndoa zamani bwana sio sasa, uyo wa miaka 17 yeye asikudanganye miaka yao ilikuwa ya ndoa sio sasa.

    ReplyDelete
  10. Bila kufuata mtizamo wa kidini,kimila,au wa kiserikali ,wanawake wa siku hizi pia ni mchango mkubwa wa kufanya muishi tu bila ndoa kwa muda mrefu nahata mpaka mwisho japo mmezaa,mnapo anzana urafiki, unaona huyu ndie mwanamke atakae nifaa,ukikimbilia kuoa,baada ya kupata mtoto ndio ataanza kukuonyesha the other side of yeye,na hapo ndipo utakapo juta nakuona uchungu wa kukimbilia kumeremeta,ni vizuri kuishi pamoja for some time ndio mtajuana vizuri na kufikia uamuzi wa kumeremeta,wanawake wa sasa sio wale wa zamani,ndio maana ndoa hazidumu,kwamimi ninaona ni bora kuishi tu,haina tofauti na ndoa.Mdau nzega Tabora.

    ReplyDelete
  11. kwa sheria za dini yetu ya Kiislam,hapo kaka unazini tuu na mkeo na adhabu yake ni kali kesho kwa Allah (S.W.T)

    Kijamii hata kama umeishi nae miaka 20 na kuendelea lakini hamjaoana bado watu hawata kupeni heshima kama ambavyo mgekua mke na mume.

    ReplyDelete
  12. KUNA WENGI WANAPAYUKA ILA HAWAJUI WANACHOKIONGEA. MMOJA TU MWENYE AKILI TIMAMU ANIAMBIE WAPI BIBLIA INATAJA NDOA NA KUSHURUTISHA WATU KUFUNGA NDOA???? WENGI WAKO KTK NDOA NA NI MAFIRAUNI WAKUBWA INA MAANA GANI SASA??

    LA MSINGI NI KUWA NA MWENZA NA UKAMTAMBUA HIVYO NA MAKATENGENEZA FAMILIA, NDOA NI OPTIONAL NDO MANA YESU UMRI ULE HAKUWA AMEFUNGA NDOA. NDOA IS MAN MADE THING NA MSITAKE KUIKUZA HIVYO.

    KAKA LA MAANA NI HAPPY FAMILY NA KUHAKIKISHA KILA UPANDE (KWA MKE NA KWENU) MNATAMBULIKA KAMA WENZA NA UMELIPA MAHALI..KUMEREMETA NI MBIU TUU ZISIZO NA KICHWA WALA MIGUU.

    NAWAKILISHA MIE

    ReplyDelete
  13. Mdau, umepotoka, ni kinyume na mapenzi ya Mungu, ni kinyume cha serikali na jamii.

    Kwanza unamwitaje "mansapu" wakati umwamini? Amejitoa kwako kabisa mpaka amezaa watoto wanne bado humwamini?

    Pili; Unapoishi na mwanamke bila kufunga ndoa rasmi yenye baraka za Mungu, Mungu mwenyewe alie asili ya ndoa anakuona wewe ni muasi tu(mzinzi). Hivyo unaishi ndani ya laana ndugu yangu. Kwa hiyo tubu kwanza na umeremete na my wife wako RASMI mbele za Mungu na jamii yote.

    Kisheria hamtambuliki ninyi kama wanandoa, watoto wenu wanakuwa kwenye hati hati.

    Mwananke anapoona una wasiwasi nae hajitoi kwako 100% kwani anafikiria kuwa kuna siku ataachika. Hana guaranteen kwenye hiyo familia.

    NOTE: Naomba tubadilike kimtizamo unapoanza safari ukiwa umepanda gari kuwa itatokea ajali, kuna uwezekano ajali itokee kweli. Kwa nini usiwe na mawazo chanya kuwa utafika salama na kule uendako utafanya hili na lile? Gari likiyumba kidogo, basi ni raisi sana kuruka na ukaumia au kupoteza maisha. Ndoa ni KUAMINIANA NA KUVUMILIANA. Usipomwamini mwenzako hutajitoa kwake 100% bali nusu nusu. Matokeo yake ni kutokuwa na mafanikio kwa kushindwa kuwa na maono ya kesho.
    Kwa leo haya yanatosha
    NAWASILISHA

    ReplyDelete
  14. kakangu ni kweli usemayo lakini inategemea sana sijui inakukuwaje mkifunga ndoa mambo hubadilika yametokea kwa wengi sana. Mfano Ally Choki kaamua tu kuoa maskini hata ndoa haikudum na ziko nyingi tu sio Ally tu. Mammbo mengine ni kumwachia mungu

    ReplyDelete
  15. Jamani Ndoa ni baina ya wale wawili wakiamua kumeremeta sawa wakiamua kutokumeremeta sawa.
    Ili mradi watu wanapendana na wana imani kwa Mungu kumeremeta hakuna maana yoyote zaidi ya kufurahisha jamii ingawa ndani inawezekana ikawa ni uozo mtupu nyumba kidogo lukuki, na mabuzi bwerere.

    Mimi nitawaheshimu watu wawili walioamua kuishi pamoja, kuwa na familia hata kama watakuwa hawajameremeta ili mradi tu wao wenyewe kwa imani yao wameungana.
    Kama mkristo naamini neno hili:
    Matayo 19:4-6 Neno hili halisemi kuwa mtaenda kwa padri au Pope kuwaunganisha bali wewe na mwenzio hata kama wazazi hawataki ni nyie na Mungu wenu
    Sijui katika imani nyingine ikoje lakini Kikristo naamini hiyo iko wazi.
    Haya masheria ya kudanganya unakwenda jumuiya ili Padri akufungie ni unafiki.
    Ukimsoma vizuri MT Paulo kwa Wagalatia itakusaidia kukuweka huru kuzingatia imani yako kwa Mungu na sio imani yako kisheria .
    Kama kumeremeta ni muhimu ni wangapi kati yetu tunapanda St Peter, Joseph na kuapa mbele ya Mungu, Kanisa na kongamano kuwa .......kwa raha na shida......... na mwezi hauishi??? au huku ukijua kabisa kuwa unadanganya???
    Mbarikiwe!!
    Mzawa

    .Unaweza pia kugoogle story moja ya Ann Loving alafu ujiulize kama Mungu hakuibariki.

    ReplyDelete
  16. Mmh! Hakika mwanamke na mwanaume kuishi bila ndoa ni ubaya..
    1. Kwanza Dini zote hazikubaliani na mapendekezo zimekataza uzinifu hivyo hao wawili wanapokaa pamoja ni kuwa wanazini haijalishi kuwa wako wamezaa au wanapendana saaana hakuna mtu anayetembea pembeni hiyo ni UZINIFU tu, hawajakubalika kisheria ya kidini wala kiserikali.
    Maisha mazuri yenye Baraka na mema ni yale ambayo mwanamke na mwanamme wanakuwa wamefunga ndoa. Tuepuke mambo ya dunia ya kuridhisha roho tu tukasahau pia yupo Muumba na maamrisho yake.

    a) Hii tukiicheki kikawaida pia pasipo mambo ya dini inakuwa haijatulia. Inamkandamiza mwanamke na mwanaume kuwa ndiye mwenye power zaidi. Nasema hivi kwa sababu, mwanaume anakuwa anahaki ya kufanya chochote wakati wowote ule anapokuwa amepata kimada, au hata anapokuwa amejisikia kumuingiza mwingine japokuwa alikuwa na mwanamke ambaye ameishi nae muda mrefu.
    b) Mwanamke huyu ni rahisi kunyanyasika kwasababu anakuwa hana rights za kutosha zitakazo mtetea saana, na tatizo hili litajawakuta watoto pale ambapo mwanamke huyu atakuwa meshazaa na huyo mwanaume. Kwani anaweza kuachwa kama mwanamke aliyekutwa barabarani akabebwa kwa short time na watoto wale wasithaminiwe na mwanaume na hata kutothaminiwa ktk baadhi ya makabila mfano kimila upande wa mwanaume iwapo mwanaume ataamua kumuacha mwanamke huyo.

    Najua wako watakao nipinga kuhusiana na hili lakini hili ndilo linalopelekea sana wanawake wengi kuwa na watoto ambao wanaambiwa hawana baba na watoto wamitaani japo babazao wapo ila tu ni kuwa watoto hao walizaliwa nje ya ndoa.

    Hakika mwanamke Anathaminika akiolewa kuliko kuzaa bila kuolewa.. Manamke aliye olewa anauwezo wa kucheza na sheria za ndoa. Wanawake wengi wanakuwa hawatambuliki upande wa mwanaume hasa pale inapotokea mwanaume yule amefariki.

    Wapo wanaume wachache wenye kujua thamani ya mwanamke hao ndio wanaothamini mwanamke wakimzalisha bila kufunga ndoa hapa Tanzania.

    2. Mahari kwa upande wangu sioni kuwa ni sababu/kigezo cha mwanaume kuona kuwa ni mzigo mzito kwa yeye kuacha kuoa na kuishi na mwanamke hata kumzalisha bila ndoa.
    Yapo baadhi makabila yanayo waozesha mabinti zao kwa mahari kubwa lakini tukumbuke pia kuwa hizi tamaduni ndizo zinasababishia wanawake wengi kunyanyasika kwa mwanamme na kuwa ngumu kurudi nyumbani kwa wazazi kwa kuhofia mahari iliyolipwa ni kubwa. Hii inakuwa kama umemuuza mwanamke sio kwa mwenyewe kupendana na mwenzie imesababishia wakaoana.

    Naamini kuwa jamii imeendelea, wengi wamesoma/wanaupeo wa kufikiria. Tufikirie kuwa mahari hiyo kubwa tunayomtoza mwanaume je huyu mwanaume na mwanamke ndio wanaoenda kuishi pamoja pengine kuanza maisha je wanauwezo wa kutosha kimapato na hitawaathiri? Na je wanaoenda kuishi na watakao taabika kiuchumi ni nani ikiwa mwanaume huyu atakandamizwa na mahari kubwa na yeye hana uwezo wa kulipa mahari hii?

    Mimi sitawezea kuisemea dini nyingine kwasababu sizifahamu vizuri nasemea Uislamu mahari ni ridhaa ya mwanamke atakayo kubali inategemea yeye anamuona vipi huyo mume wake wa baadae.
    Mahari kwa kiislamu hata Dua/Aya ya quraan inatosha kuwa mahari kama mwanamke ameridhika, hata kupewa kitabu Fulani labda cha dini na msala inatosha katika mahari. Mahari ni kitu chochote kile ilimradi mwanamke awe ameridhika. Na vingine vitakavyo fuatia labda ni vile vidogo vidogo vya wazazi labda mkaja nk.

    Kuhusu gharama za harusi kwa upande wangu sioni pia ni kigezo kwa sababu harusi sio lazima iwe kubwa. Harusi sio ushindani kwanza ukiangalia ndoa nyingi zile ambazo zilizokuwa kubwa sana hazidumu. Ndoa ni Baraka tu upate kutoka kwa wazazi wa pande mbili na kiongozi wa dini basi inatosha. Ndoa kubwa ni mambo tu yadunia binadamu wameyakuza.

    Hayo ndio maoni yangu mimi Mdau. H.

    ReplyDelete
  17. TAADHARI
    NAOMBA WACHANGIAJI TUELEWE KUWA MTOA HOJA HANA SHIDA NA MAHARI WALA GHARAMA ZA KUMEREMETA.

    HOJA NI: KUNA UBAYA GANI WA MWANAMUME NA MWANAMKE KUISHI PAMOJA KWA MUDA MREFU BILA KUFUNGA NDOA?

    KEY WORDS: UBAYA, KUISHI PAMOJA & KUFUNGA NDOA/NDOA

    NOTE: Wanaofeli mtihani si kwamba hawajui, ila wa hawajibu kile waalichoulizwa.

    ReplyDelete
  18. TAADHARI
    NAOMBA WACHANGIAJI TUELEWE KUWA MTOA HOJA HANA SHIDA NA MAHARI WALA GHARAMA ZA KUMEREMETA.

    HOJA NI: KUNA UBAYA GANI WA MWANAMUME NA MWANAMKE KUISHI PAMOJA KWA MUDA MREFU BILA KUFUNGA NDOA?

    KEY WORDS: UBAYA, KUISHI PAMOJA & KUFUNGA NDOA/NDOA

    NOTE: Wanaofeli mtihani si kwamba hawajui, ila wa hawajibu kile waalichoulizwa.

    ReplyDelete
  19. Mhhh!!!! Haka kajamaa kanajua kupepeta ngono zembe, yaani miaka 6 watoto 4 tayari?
    Kwa taratibu ya baadhi ya dini wewe na huyo unayemwita mamsapu wako nyote ni wazinifu wakubwa na kama unaamini dini yoyote basi adhabu yake siku hiyo parapanda itakapolia ni kubwa mno. Tubu kwa mola wako na ufunge ndoa halali ili ukubalike katika jamii, daini na mola wako.

    ReplyDelete
  20. Ndoa ni kama mduara hivi, walio NJE ya huo mduara wanahamu sana ya kuingia ndani kuona kukoje!, na walio NDANI, wanahamu sana ya kutoka nje baada ya kukaa humo ndani, ajabu wanaotaka kutoka Nje ni wengi sana kuliko wanaotaka kuingia, japo katika suala la uzoefu ni Vizuri ukaingia ndani kuona kukoje kisha uamue.....kama unaweza kupata maziwa Tesco kuna haja gani ya kufuga Ng'ombe???
    Mzee wa K.

    ReplyDelete
  21. ndugu yangu, unauliza swali hili hapa ukijua watu wana mitazamo tofauti nadhani maana yako ni kuleta tu mjadala hapa, hakuna mwenye shida na jibu bali tu kupata mitazamo hapa hewani.
    Hongera sana ni topic irresistable hata kwangu.
    1. una maana gani ndoa?
    Mimi ndoa kwangu ni KIAPO CHANGU kwa mpenzi wangu, mbele ya Mungu na kasisi wake na ndugu na wazazi wangu ninaowaheshimu sana hapa duniani, kwamba nimekubali kumchukua huyu mtu kuishi naye, nikiwa nimeamua kwa akili yangu,
    kwa hiari,
    kwa elimu na ujuzi wangu,
    katika hali zote za kiutu uzima,
    hadi kifo.

    Ninajua huu ni binadamu kama mimi, ana udhaifu kama wangu,
    ila uamuzi wangu si wa kutumia mapenzi ya hisia, bali ni UAMUZI WA KUMFANYIA MATENDO YA UPENDO HA HESHIMA, wakati nataka au yeye anataka.
    si kimbilio langu la raha, si ukombozi wangu wa pesa, chakula, watoto, hayo ni matokeo tu.
    Wakristu huapa mara chache sana, mojawapo ni hapa, tukijua raha na shida zake.
    Wewe ndugu yagu, kama haya mambo huna haja nayo, wewe kaa tu, hakuna neno KAMAMMEKUBALIANA KWA HIARI WOTE WAWILI, ila kama ni uamuzi unaoufsi kwa mwenzio unajua mahali pa kujiweka na kumuweka mwenzio,
    dicteta, na mtumwa,
    mwenye kutoa sauti na msikilizaji,
    si wapenzi wawili.
    Wanawake wengi tunapenda kuwa na roho tulivu, kujua tunapendwa, ni pamoja na kusikia ukisema mbele ya watu unaowaheshimu sana (wazazi na Mungu!!) kwamba unaapa kuwa na mimi.
    si kumeremeta wala nini.

    ReplyDelete
  22. Michuzi,

    Sioni ubaya ili mradi chochote mnachokifanya wewe na mamsapu wako kinadocuments. Hii ni sababu lolote laweza kutokea. Ikitokea unafariki, mamsapu wako anaweza kufukuzwa kama kuku na watoto akanyang'anywa incase ni makabila yanayodhamini mali kuliko utu.

    Inawezekana mama akafariki ukapatishwa shida na ndugu wa mama ukalipishwa mahari ya maiti. Hili ni common sana.

    Wewe unashindwa nini kwenda kuandikisha ndoa kwa serikalini na kufunga ndoa saa nne asubuhi pamoja na mashahidi wawili tu? Mi nimeshasimamia ndoa kama hiyo na baadaye watu wanarudi kazini kimya. Hii ni kwa kuprotect mkeo na watoto.

    Kama huna shahidi niombe nitakusimamia tu.

    ReplyDelete
  23. Miaka sita watoto wanne
    Miaka 6 = Miezi 72
    Miezi 72 gawanya kwa watoto 4 = 18

    Ina maana kila mtoto alipokuwa anafikisha miezi 18 mwingine alikuwa anazaliwa, meaning wakati mtoto anapokuwa na miezi tisa mama anashika miamba nyingine.

    Unaweza ona kila baada ya miezi tisa mama alikuwa mjamzito na kama ni hivyo ni lazima atakuwa amechoka mbaya mbaya. je una twins? kwani mahesabu hapo yatakaa vizuri zaidi and make a lot of sense. Wazazi wake walitakiwa wakujie juu so far kwa kuweka tu ndani na kuzalisha.

    Since mama atakuwa amechoka na shurba zote hizo mimi napendekeza upate vasectomy watoto wanne ni tosha kabisa. Halafu pia ufunge ndoa

    ReplyDelete
  24. Mdau uliyeleta hoja wewe fanya kile roho inapenda bwana.

    Kama nyote wawili mko poa na maisha yenu mnafurahi nani wa kuwapangia bwana... "eti furaha ya kweli ni mpaka ukifanya harusi?"

    Nani kasema bwana!?? Hiyo ni furaha yako, sio ya kila mtu.

    Mambo ya dini ni kati yako na Mungu, sisi sio kazi yetu kukuhukumu kwa misingi ya dini. Sisi binadamu tutakuhukumu kwa misingi ya sheria zilizotungwa na Bunge ... ambapo hujavunja sheria yoyote.

    ReplyDelete
  25. Nina miaka 25 nimeishi na mwanamke miaka 3 nina mtoto mmoja matarajia kufunga ndoa mapema 10.04.2009 raha sana yani karibumi hakuna mchango wala sherehe

    ReplyDelete
  26. Someone once said: There is nothing like being happily married - as you are either "happy" or "married" - not both. Yes, mutually exclusive events - for those who remember high school probability...

    ReplyDelete
  27. Is that what they call "kuoa mkeo" or "kuolewa na mumeo" then? That would be nice, wouldn't it? Rather than just marrying someone you met in a queue for LUKU...

    ReplyDelete
  28. Mnaoshangaa watoto wanne miaka 6, kwanini hamjiulizi kwamba inawezekana wamezaa mapacha mara mbili? Na pia wengi mnaonekana kutafsiri ndoa kwa mtazamo wa kimagharibi na tafsiri za ndoa kwa mujibu wa dini za kigeni au dini za 'kwenye vitabu' kama ukristo na uisilamu! Kama hao watu wameamua kuishi pamoja na wazazi wa pande zote mbili wameridhia tatizo li wapi? Ndoa ni mioyo yao kama wanaaminiana hawatoki nje ya uhusiano wao kuliko wale wanaooa na kuendeleza ukicheche nje ya ndoa zao. Pia nadhani tuite harusi maana ndoa watu wanazifunga sana hata kabla hawajaenda kanisani na misikitini. Hapo kwa huyu mdau hakuna uzinzi kama watu mnavyomshutumu,ili mradi tu hawatoki nje ya huo uhusiano wao.

    ReplyDelete
  29. UMEINGIA KATIKA LILE WIMBI LA WALIOPOTOSHWA NA WAJINGA WACHACHE, ALIYEKUAMBIA KUWA NDOA NI HONEYMOON SIKU ZOTE NI NANI, NDOA NI CHALENGE KILA SIKU, NA NDIO MAANA WACHACHE SANA WANADUMU KATIKA NDOA NA KAMA HAUPO READY KUZIKABILI CHALENGE HIZO BASI USIOE KABISA UENDELEE KUWA BACHELA NA SI KUZAA ZAA OVYO HALAFU UNATANGAZA KWA WATU. SIJUI UPANDE WA WENZETU WAISLAMU, LAKINI KWA WAKRISTO UFANYAVYO WEWE NI ZINAA NA IMEKATAZWA KWENYE BIBLIA, JITAHIDI UENDE UKABARIKI NDOA YAKO UISHI KATIKA MAISHA YANAYOMPENDEZA MUNGU, UTAOGOPA MPAKA LINI, NDOA NI UVUMILIVU NA KAZI NZITO SI LELEMAMA KAMA WATU WANAVYOFIKIRI.

    ReplyDelete
  30. ndoa ni mkataba wa kuishi na umpendaye na huwa inasaidia sana kusolve matatizo yoyote mbeleni kwani sisi wote ni binadamu tunakosea.sasa usijidanganye kwamba ukitia sign mkataba wa kuishi na huyo umpendae kutakuwa na matatizo hakuna.nenda katia kasign mkataba wala usimualike mtu wala nini ukipewa cheti cha ndoa kakitupe kwenye kabati endelea kuishi kama unavyoishi nae sasa hivi.

    ReplyDelete
  31. Huyo ni kimada kwa mila na desturi.

    ReplyDelete
  32. Asante kaka Michu na ndugu mtoa mada! Katika hili naona kuna watu wanachanganya mambo iwe kwa kujua au kwa umbumbumbu na kuchukulia mambo kama mazoea tu.
    Nisaidieni ni lini wawili huchukuliwa kama wana ndoa? Je, ni pale:
    1. Mahali ikitolewa na wazazi kuruhusu waishi pamoja?
    2. Wakikamilisha taratibu za kidini juu ya kuishi kama mume na mke?
    3.Waishio pamoja baada ya kutoa mahari lakini bila kufuata taratibu za kidini(kwenda kwa Sheikh, Padri au Mchungaji)huhesabiwa kama Wazinifu?

    Kama watu wataendelea kuamini kuwa msingi na uhalali wa hiyo iitwayo ndoa ni kuapa na kusaini karatasi mbele ya wanadamu tuwaitao wawakilishi wa Mungu, huku wakiendelea kupuuza umuhimu wa mapenzi kama msingi wa wawili kuishi pamoja ndivyo kusambaratika kwa jamii kutakavyoongezeka.

    Ni nani kati ya wachangiaji awezaye kuthibitisha kuwa watoto waliozaliwa na mke na mume waishio pamoja kwamba wanakuwa wamezaliwa nje ya ndoa na hivyo kukosa haki?

    Je, ni kweli kwamba ukishakuwa na certificate ya ndoa inakupa kinga ya kufungishwa virago kama mapenzi yametoweka?? Wanawake wengi huamini hili kuwa wakishavishwa pete za ndoa basi wamefika hata wakifanya madudu, mkataba hautenguliwi, hujisahau kuwa mume na mke hawaunganishi na viongozi wa dini bali mapenzi ya dhati chini ya msingi wa haki, heshima na usawa!

    Binafsi nawaheshimu sana wale walioamua kuishi pamoja kwa mapenzi ya dhati baada ya kupata baraka za wazazi hata kama hawajaenda mbele ya hao wawakilishi wa Mungu na kutomeremeta!

    Mbarikiwe
    Mdau, Oslo ya Norway

    ReplyDelete
  33. Ndoa za nini kama bado mnafuata watoto wa watu? Ukiishi bila ndoa kwanza mnaheshimiana maana unajua mtu ukileta za kuleta anaanza....!!! Nashauri ambao hamjaoa acheni kabisa mambo ya kufungana Pingu...hizi ndoa zimekuwa tu Ndoano hazina hili wala lile..hao waliofunga ndoa ndo mafuska wakubwa kumchezea tu Mnyazi Mungu..!! Paulo katika Bible anasema kama hamuwezi acheni kabisa sio mnaoa halafu mnawaka tamaa..!!

    ReplyDelete
  34. huo ni uzinzi

    ReplyDelete
  35. wanaume wengi wanakimbia kuwajibika ndio maana wanakaa muda mrefu na wanawake bila ya kuwaoa, miaka 6 yote hiyo kama unamuona hafai au unaogopa mtaachana mkioana kwa nini mpaka leo mpo pamoja, unamvunjia heshima yake tuu huyo dada nina uhakika anataka kuolewa ila kwa kuwa ushapewa ngombe wa bure huna haja nya kununua maziwa, nachukia sana wanaume wanaokaa na wanawake kwa muda mrefu bila kuoa, uhuni tuu unasubiri bibi mwengine mzuri akitoa uachane na huyo wa miaka 6 uchukue mwengine, kwani unaona ndoa ni kujifunga, wanaume wengi waliokuwa hawajatulia hizi ndio dalili zao hawaoi ng'o.shame on you.wewe huna lolote unakimbia responsibilities na humpedi sana huyo binti maana ungekuwa unampenda ungemuoa zamani.

    ReplyDelete
  36. Ninachojua mimi,mwanamke akiolewa tu heshima,raha,mapenzi,amani ndani ya nyumba etc vyote vinaisha inaanza utumwa kwa mwanaume.
    The best way ni kumuweka kinyumba weeeeeeeeeeeeee mkazaa mkamaliza ujana ndio ukamuoa.Kama hutaki kuamini-jifunge kamba uone kama utapona!
    KT

    ReplyDelete
  37. Wewe mtoa hoja wa Oslo ya Norway, watu kama nyinyi ndio ninaowatafuta sikuzote niwanyofoe mapumbu yenu, huna haya kabisa! Watoto wote wanaozaliwa nje ya ndoa wanajulikana kama BUSTARDS, si kosa lao bali kosa la wajinga kama wewe na huyo mtoa mada pia. Wanaume wenye tabia ya kukimbia responsibilities kama za kujicommit kwenye ndoa hawatakiwi kabisa, unamuweka binti wa watu bila ndoa eti kwa kuogopa ndoa kuvunjika, upuuzi mtupu, halafu huna haya unatotoa nae watoto wanne, ni sawa tu na kuzaa nje na wanawake wengine hakuna tofauti. Ngoja mmoja wenu aondoke(God forbid), hapo ndipo mtakapoona umuhimu wa ndoa. Usiwasilize hao vitombi wanaokuambia eti ukifunga ndoa cha moto utakiona, kama mmeishi miaka yote hiyo hicho cheti cha ndoa ndio kitaleta hayo mapepo? Yaani umeniboa kuliko!

    ReplyDelete
  38. Weeee!! Anyn. wa March 20. 11:10 pm

    Wewe umepofushwa na imani zenu za mapokeo hivyo unadhani taratibu nyingine hazifai!! Tena waonyesha U mbaguzi na mnyanyasaji wa watoto, kisa wazazi hawajaenda kwa wawakilishi wa Mungu!! Aibu!! Responsibility na commitment gani unataka kama nimelipa mahari kwa wazazi na twaishi kwa amani na kutimiziana wajibu na haki pamoja na za watoto bila matatizo?? Hadi niende kwa mchungaji au sheikh ndio iitwe ndoa?? Siafikiani nawe, hata shheria ya ndoa inatambua ufungaji ndoa wa aina tatu: 1. Kimila, 2.Kidini na 3. Kiserikali. Sasa mnaopinga ndoa za kimila mmetokea Tanzania ipi??

    Someni sheria ya ndoa muelewe haki na wajibu wenu mbele ya jamii juu ya hadhi ya ndoa. Ukitumia imani yako kuhukumu MITAZAMO YA wengine utakuwa umechemsha sana.

    Sikubaliani na wale waamuao kuishi tu bila kupata ridhaa za wazazi au kufuata taratibu zinazowatambulisha kama mume na mke, pia siafiki kama watu wasipoenda kwa sheikh, mchungaji au serikalini kwamba wanaishi nje ya ndoa.

    Suala la vurugu na dhuluma kwa mama au watoto baada ya mmoja kufariki ni muendelezo tu wa Watz kutoheshimu haki za binadamu pamoja na kuendekeza utegemezi kwa ndgu (hawa ndio wanaokimbia responsibility kwa kuishi maisha ya kuvizia vya wenzao).


    Mdau toka Oslo ya Norway

    ReplyDelete
  39. Kwa hiyo wewe kuwa na watoto wanaharamu huoni shida? Watoto watakosa raha wakiitwa bastards but huo ndio ukweli, they are bastards na ni sababu baba na mama hawafanyi tendo la ndoa, wanazini kwa miaka 6 sasa.

    ReplyDelete
  40. Hakuna ubaya wowote iwapo wote wawili mmeridhia na imani yenu pia ya kidini au ya kimila usiende kinyume na hayo.

    ReplyDelete
  41. Nyie wote mlio kwenye ndo, huwa mnajushua sana. Kwanza hamna watu wazinzi kama wanandoa. Kwa hiyo acheni unafiki. mimi nimekaa na partner wangu zaidi ya miaka kumi. Watu wana funga ndoa wanaachana, tunawakuta engo na na vibustani/vidumu, tunawastahi tu.

    What matters is you love and respect each other, marriage certificate is just a formality, kama kugongewa visa tu ya kwenda ulaya.

    WANANDOA KUWENI WAAMINIFU MNATIA AIBU KWA UZINZI WENU MNAOFANYA HADHARANI. KHAA HADI KINYAA!!!!!

    ReplyDelete
  42. Halafu wewe Anon March 22, 2009 11:56 AM:

    Shika adabu yako, mtoto ni zawadi kutoka kwa mwenyezi mungu. hakuna mtoto haramu. tena ukome.

    Wewe ndio mwanaharamu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...