timu ya taifa ya vijana ya enzi hizo ikiwa inaundwa na wacheji toka katika michezo ya mashule kama vile umiseta na umishumta ambao wengi kati ya hawa walikuja kuwa wachezaji nyota kwa muda mrefu kutokana na msingi waliopata kwa kucheza mashindano mashuleni na hatimaye kwenye timu za vijana za vilabu, jambo ambalo tulilisahau na kutegemea wachezaji watachipua tu kama mpunga makondeni.

siku hizi ni tofauti. yaani ni hadi hapo michezo hiyo ya mashule itapoanza ndipo tutaweza kuona cheche za wachezaji wa kibongo, kwani si rahisi kulea vipaji kwa mazoezi tu bila kiwepo kwa msingi wa kumjenga mchezaji kimashindano, hali ambayo ndiyo tunayo leo.
-michuzi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Michuzi,
    Na hiyo ndiyo argument kubwa ya Maximo. Kwamba tanzania haina mfumo madhubuti wa kuwachipua na kuwajenga wachezaji ili wadumu katika nidhamu ya kiwango cha juu cha mpira kwa muda mlefu. Wachezaji wetu wanatumia vipaji zaidi kuliko msingi wa mafundisho ya soka. Matokeo, Maximo analazimika kufundisha basics za mpira, ikiwa ni pamoja na kutoa pasi, kumiliki mpira, kufungua vyumba, na kumpa mchezaji pumzi badala ya kushughulika zaidi na formation na njia za ushindi. Analazimika kufanya yale ambayo wachezaji wanapoitwa kwenye timu ya taifa, wanatakiwa tayari wawe na hizo sifa kwenye timu walikokulia kimpira au waqnakochezea kwa sasa.
    Wengi wa wanaomlaumu Maximo hawataki kuuongelea udhaifu huu katika mfumo wetu wa soka. Wanataka ushindi na mafanikio ya haraka haraka bila uwezekezaji. Wanafikiri mpira ni miujiza.
    Nawasilisha.

    ReplyDelete
  2. Duuh umwanaspoti wangu wote ktk picha hii nimemjua Zamoyoni ambaye amesimama wa2 toka shoto na supa kiwelu aliechuchuma wakwanza toka kulia
    mdau
    kisiju pwani.

    ReplyDelete
  3. Ndio maana tunasema Maximo hajatujengea uwezo endelevu maana timu ya watoto ni kama haipo kwa hiyo akiondoka tunaanza upya na kocha mwingine na kwa kuwa tunataka ushindi wa haraka naye atachukua walio tayari kucheza sio kujenga timu ya watoto!!! Baada ya hapo muda wa JK utakwisha na tunarudi pale pale. TFF hamlioni hili?

    ReplyDelete
  4. Hivi hiyo 'Zamani' tuliwahi kunyakua kikombe gani? Naomba kuuliza wenye hizo khabari, maana huwa nasikia tu zamani, zamani!!

    ReplyDelete
  5. Faza achia basi hiyo Wichita madness...mbona unabana kaka? Mambo yenyewe jumamosi.
    Fanya kweli basi.

    ReplyDelete
  6. Du!! Hapo nimemfahamu mmoja tu hawa waliochuchumaa wa kwanza kutoka kushoto ni Sospeter Mwaluko mwanzoni alichezea timu ya Reli Morogoro na baadae akahamia kwa Wekundu wa Msimbazi, picha hiyo nadhani walikuwa kwenye tour moja ya michezo kule Brazil wakati akiwa Simba. - Ben

    ReplyDelete
  7. Wakwanza kushoto ni Sospeter Mwaliko alitokea Maji Dodoma akaenda Simba. Kwa sasa yuko Dar Halmashauri ya jiji (Sio mpira tena).

    ReplyDelete
  8. Michuzi swala uliloandika leo ni muhimu sana.Michezo sio mpira tu riadha.basket nk.mazoezi ya yanatakiwa yaanze mapema.Kuanzia shule za msingi,secondary huko ndio chimbuko la kupata wanamichezo na muhimu ni kuwaendeleza.Kuwe na data ya kuhusu kila mchezaji.Nikisema data ninamaana kuona maendeleo ya mazoezi yaanaendaje.Na hapo inakuwa rahisi kwa kocha kuona wapi kuna takiwa kuendelezwa.Wakianzisha mtindo wa kupata chipukizi basi miaka ijayo nchi yetu itakuwa na mafanikio mazuri sana.Serikali ingeipa kipaumbele swala hili.Kwani michezo pia inasaidia kupunguza kasi ya vijana kujikuta wameingia kwenye mkondo mbaya wa kimaisha.

    ReplyDelete
  9. huko zamani nasiki tanzani iliwahi kunyakuwa kombe la challenge cup. namjibu aliyeuliza huko zamani tanzania ilinyakuwa nini. kumbuka nimesema nasikia, mimi sikumbuki kwa hivyo ni lazima miaka mingi nyuma kabla sijakuwa na ufahamu wa football

    ReplyDelete
  10. Waliochuchumaa toka kushoto wa pili ni SAID GEORGE BEST (Taifa - Coastal Union Tanga).. dRU -- Upo wapi BEST!!???

    ReplyDelete
  11. Mwenye Afro safu ya pili toka kulia (wa pili) Ahmed Amasha .. dRU .. yu wapi huyu naye?

    ReplyDelete
  12. Mkuu Michuzi, TFF au yeyote anayejua, hebu tujibuni Tanzania imewahi kunyakua vikombe vingapi vya Kimataifa?, sio Zamani Zamani! Hebu leta data hapa!! Kuna Mdau anasikia kuna challenji cup, ni kweli? Lini? na ni hao akina Mogella au Tenga ndio waliolileta? Walipitia training gani?

    ReplyDelete
  13. hivi umiseta bado ipo au nkapa nayo aliiua

    ReplyDelete
  14. Mafanikio makubwa tunayojivunia yaliyopatikana zamani ni kucheza kwenye African Cup of Nations mwaka 1980. Ni mafanikio kwa sababu wakati huo ni timu nane tu zilizokuwa zinashiriki. Timu iliyoshiriki iliundwa na vijana walioandaliwa wakiwa chipukizi na timu za watoto za enzi hizo. Naukumbuka mchango wa vijana wa Dr Stancilescu.

    ReplyDelete
  15. ...Hakuna Said George hapo! Hii Timu ilikuwa Timu ya Vijana ya Taifa iliyokwenda Norway kwenye mechi za kirafiki mwaka 1981 Wakati Tayari Said George aliishakuwa mchezaji mkubwa tu. Waliporudi ndio miezi michache baadaye kocha Ruud Guntendorf akawapandisha daraja akina Mogella, Amasha na wengineo ambao wakafanya mambo makubwa tu kwenye michuano ya Challenge Cup ambayo mwaka huo ilifajika Dizim na Taifa Stars ikafika fainali na kutolewa na Kenya bao 1-0 ambapo Kenya ikamchukua Mwali mbele ya maelfu ya waTZ! Michuano hiyo ndiyo iliyompandisha chati zana Zamoyoni Mogella.

    ReplyDelete
  16. Kucheza kwenye 8 bora cup of African Nations mara moja tu (1980)ndio yaliyokuwa mafanikio ya kuwa na timu ya Vijana? Na ndio Zamani Zamani Zamani tunayoisikia? Hakuna mdau mwenye data zozote kuhusu kunyakua kombe?

    ReplyDelete
  17. nimeweza kumtambuwa linford christie wa kwanza kulia waliochuchumaa baadae alikwenda england kwa ajili ya riadha.

    ReplyDelete
  18. Ninakumbuka miaka ya katikati ya 70 nilipokuwa Shule ya Msingi Kigoma, kulikuwa na mashindano ya riadha kila mwaka kwa shule za msingi zikifanyika pale Shule ya Sekondari Kigoma.
    Nakumbuka siku hiyo ilikuwa ndiyo kama Olimpiki yetu. Siku kadhaa kabla ya michezo hiyo kila shule ilikuwa ikijitayarisha kikwelikweli hasa. Na siku ya mashindano ilikuwa ni siku muhimu kabisa kwa washiriki kuzitetea shule zao.
    Nakumbuka katika mashindano yale waliwahi kupatiikana wachezaji wa riadhaa wa Taifa kama vile Noela Noel, binti alikuwa anakimbia sana.

    Vilevile nakumbuka kulikuwa na kama ka-world cup ketu kwa shule zote, wakati huo akina Thabit Mgunda - Kiezya, Mengi Amani, Yusuf Abed - Aga Khan, Moshi Dayan, Isaac na Joseph Mwakatika - Muungano. kule Ujiji ndiyo usiseme akina Ali katolila na wengine wengi.
    Hakika kilikuwa ni kipindi kizuri sana kwenye michezo katika shule za msingi.
    Sasa hivi sijui mambo ni aje?

    ReplyDelete
  19. Mdau anayesisitiza anataka kujua makombe tuliyochukua tulipokuwa na timu za vijana namwomba asiangalie soka tu, kuna michezo mingine ambayo badala ya makombe inatoa medali. Majina kama Filbert Bayi yameng'ara kimataifa na yalitokana na kuwepo kwa mfumo wa kueleweka wa michezo kwa vijana, pamoja na matatizo ya umaskini uliokuwa nayo. Hata hayo mafanikio ya kisoka ya kufika fainali za Afrika 1980 bila kuchukua kombe ni tofauti na hali ilivyokuwa bila kuwa na vijana ambapo tulikuwa sio washindani tena bali ni washiriki. Kuchukua kombe si lelemama ndio maana Urusi na China hazijawahi kuchukua kombe la dunia lakini zimekuwa zikishindana. Uwezo wa kushindana ni hatua ya kwanza kuelekea kuchukua makombe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...