Habari yako mr.michuzi.mimi nikiwa mfatiliaji wa mtandao wako uhu.napenda kutoa malalamiko yangu.

Nijuavyo mimi ukipenda yanga uwezi kuacha kafatilia habari za samba na kuzitoa kwa wananchi wazisoma na kuelewa na kujua mbivu na mbichi.
Na ukipenda samba uwezi kuacha kutoa habari za yanga.rakini sio kwako wewe michuzi mpenzi yako kwa msondo ngoma yakufanya utaki kujua wala kutoa habari zinazo husu sikinde ngoma ya ukae wadau wako wazielewa na kufatilia.na ukitia mambo yanausu sikinde basi kidu na kwa bahati mbaya sana.laki habari za msondo ngoma kwakua wewe ni shibiki wao zikauki katika mtandao wako.
ok mimi sikuzui kupenda nicho kuomba uwe unakwenda sikinde na kutoa habari zao kama unavyotoa habari za bendi yako uipendayo ya msondo ngoma.izi bendi ndio bendi kubwa nchi kwe pamoja na mapenzi yako kwa msondo na sikinde nao watendee haki mtandao wako ni muimu napend uwe fea usibaguwe.
nyinyi wandishi na wana habari kwa ujumla wenu mnajukumu kubwa kuzitangaza na kuzilinda izi bendi zetu za kitanzania.
kiushindani na kimaadili zenyewe ndio zimebakia ushikiano wenu ni muimu san asana.samahani kama nimekuuzi lakini ukweli ndio uwo.
Wako mdau

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. malalamiko yenye hata hayaeleweki na kusomeka vizuri kwababu ya uandishi mbaya, jifunze kwanza kuandika bila kukosea herufi, kamilisha neno na sentensi zieleweke ndo ulete malalmiko yako hapa ujibiwe..

    ReplyDelete
  2. Bwana mdau next time uwe unarudia kusoma ulichoandika kabla ya kukituma hewani, unatupa kigugumizi cha ulimi bwana katika kusoma, hata lugha ya kiswahili inakupa shida, wee vipi bwana.


    mkereketwa wa kiswahili.

    ReplyDelete
  3. anons wa kwanza na wapili chondeni jamani abiria wa mkuu wa nanihino si wa aina moja tupo tabaka za kila aina hapa inabidi tusabiliane tu ili tupate ridhiana la sivyo tutawanyima wageni wengi nafasi kwenye jamvi hili, maana wahenga walisema akili ni nyele kila mtu ana zake, na kulenga si kufuma, kumradhi jamani

    ReplyDelete
  4. Chamuhimu nikujua nini anacho-ulizia au hoja yake nini, tukianza kuchambua makosa ya herufu, sarufi na lugha utakuta hata wewe mkosoaji umeteleza mahala fulani. Lakini pia kuna lahaja za makabila, wengine wanavyotamka ndivyo wanavyoandika, kwaheri wanasema kwaheli, nk.
    Nafikiri ujumbe umefika kwa Michuzi, kuwa aache `umsondo saana, au Usisiemu sana, ujue sisi sote ni abiria wake.
    M3

    ReplyDelete
  5. Hata. Huyu shida yake ni kwamba mbona taarifa za Bwawa la Maini (au sijui Bwawa la firigisi?) ndiyo nyingi zaidi na siyo za timu nyingine?

    P.S Lakini kama 'Liverpool' ni 'Bwawa la Maini', basi 'Kijitonyama' ni 'Little River Meat'!!

    ReplyDelete
  6. Hapa Ndo tunajiuliza kweli kutumia computer kweli unahitaji kwenda shule?Mana duuuuuuuh yaani hata barua inaandikwaje,yani hapa inaonesha mdau hata la saba umekimbia vidumu vya maji,by the way ujumbe wako umefika!

    ReplyDelete
  7. Msimlaumu mdau kwa matatizo ya lugha katika ujumbe wake. Hayo ni matatizo ya mfumo wetu wa elimu. Tena basi anastahili pongezi maana kuna uhakika wa zaidi ya asilimia 75 kwamba hakufundishwa kutumia kompyuta katika shule aliyosoma. Ujumbe wake wa msingi uko wazi kwamba anaona kuna upendeleo katika utoaji habari zinazohusu chombo kimoja dhidi ya kingine mfano Simba vs Yanga au Msondo vs Sikinde. Kuna wadau walishawahi kulisema hili juu ya habari za bwawa la maini kupewa upendeleo.
    Nadhani hii hoja ya mdau ni ya msingi lakini kwa upande mwingine tukumbuke kwamba tofauti na tunaponunua gazeti na kutoa pesa, hatumlipi mkuu wa nanihii chochote kutuhabarisha. Kadhalika hii ni globu ya jamii, mdau yeyote mwenye chochote anakaribishwa. Nadhani ingekuwa vema mdau awe anazileta hizo habari za kina Sikinde na Msondo.

    ReplyDelete
  8. Habari za Samba si ziko tele kule Blog ya Brazil? Duka la viatu unataka liuze mpaka heleni?

    ReplyDelete
  9. Samahani natoka nje ya mada kidogo.Nimesoma kwenye gazeti la mwananchi kuwa mshahara wa wabunge wa Tanzania ni Shs MILLIONI 7 kwa mwezi acha marupurupu.Je kuna ukweli? Na kama ni kweli wanalipwaje na nchi maskini sana duniani kiasi hicho cha mshahara? Je kuna kazi gani kubwa wanazozifanya hao wabunge wakati madaktari wetu wanalipwa laki 4 kwa mwezi.Swali langu kwa Watanzania,JE NI HAKI KULIPA HIZO FEDHA KIASI HICHO KWA HAO WAWAKILISHI WETU AMBAO WENGI WAO WANASINZIA TU BUNGENI?

    ReplyDelete
  10. Hivi michuzi amekua TMZ? Nani anamsponsor? hizo sehemu atakua anaenda hata kama haenjoy jamani....Kama analipwa poa lakini blog yake ni ya bure aende sehemu asizoenjoy kwa hela yake just to make you happy? Wewe kama unakwenda huko mtumie habari atakuwekea. Ingekua hao unaowasema wanacheza kwenye hall moja kwa usiku mmoja halafu haweki habari za wengine hapo ningekusikiliza lakini watu hao najua watakua wanapiga miziki yao majumba tofauti ataweza vipi???????

    Mara matasema mnataka habari za Tabora na wengine watataka habari za msumbiji...tushukuru kwa hiki tunachokiona angalau tumeona mahoteli yakiungua ...who knew...bagamoyo inategemea fire engine za Dar mjili...LOL....bongo tambarare kweli

    ReplyDelete
  11. Naomba nijipendekeze kwa mkuu wa wilaya ya nanihiii. nijibu malamiko haya.

    Sio kweli kwamba mkuu wa wilaya anapendelea. kama ujuavyo bendi ya Sikinde ilikuwa inamilikiwa na shirika la DDC hivyo walikuwa na mikataba yao. ikiwa ni pamoja na kwamba hawaruhusiwi kufanya chochote pasipo mwajiri kujua.

    ikiwa ni pamoja na utoaji habari.
    Msondo wako huru leo wanapiga hapa kesho kule hivyo ni rahisi sana kupata picha zao na habari kwa ujumla wakati bendi ya DDC hupinga katika kumbi zinazomilikiwa na shirika

    kwa mara ya kwanza baada ya kuvunjika mkataba na DDc wamefanya onesho pale leaders club kwa kutumia mgongo wa msondo, na watu tukawa tunaona kama bendi ya wapi sijui na mzee ngurumo akawa anawashauri kutumia maeneo kama haya ili wajulikane hasa na wadau wa kizazi hiki.

    na kama mkuu wa wilaya angekuwa na upendeleo hata maoni yako asingetoa hewani.

    hii ni blog ya jamii na sisi wote tunajisikia furaha kuchangia na kuipitia kila siku.

    wadau hasa mnaoishi nje ya TZ sio vizuri kutuandia kwa lugha za kigeni na hata tukitoa maoni mnatukosoa sana mara herufi.
    kama hii tunaita blogu ya jamii basi tutengemee wachangiaji toka makundi yote yanayounda jamii.katika jamii kuna maamuma,mbumbumbu,wasomi kama ninyi na watoto wa mafisadi ambao wako kusoma nje n.k

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...