Deus Mallya akipelekwa kuanza kutumikia kifungo leo huko Dodoma
Kijana Deus Mallya (27) aliyekuwamo kwenye gari lililopata ajali na kusababisha kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe, amehukumiwa kwenda jela miaka mitatu baada ya kupatikana na hatia ya kuendesha gari kwa mwendo kasi.
Hukumu hiyo iliyotolewa leo, ilimfanya wakili aliyekuwa akimtetea, Godfrey Wasonga, kulia mahakamani hapo na kusababisha shughuli za mahakama kusimama kwa sekunde kadhaa.
Wakili huyo alilia baada ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mkoa wa Dodoma, Thomas Simba, kusoma vifungu vya kumtia hatiani mteja wake ambaye licha ya kuendesha kwa mwendo kasi, alihukumiwa kwa kuendesha gari bila leseni.
Hata baada ya hakimu kumaliza kusoma vifungu na kumtaka wakili atoe utetezi kabla ya hukumu, Wasonga alifanya hivyo huku akilia. Katika hukumu yake, Hakimu Simba alisema ameridhika na ushahidi wa upande wa mashitaka ambao ulitolewa mahakamani hapo.
Hakimu alisema makosa aliyobainika kuyafanya Mallya, yana adhabu kali, lakini alimpunguzia kutokana na ombi la mshitakiwa. Katika kosa la kuendesha gari kwa mwendo kasi na kusababisha kifo, alisema kwa mujibu wa sheria namba 63 kifungu cha pili (A) adhabu yake ni kifungo cha miaka mitatu jela.
Alimhukumu pia kwenda jela mwaka mmoja kwa kosa la kuendesha gari bila leseni na kusema kwamba adhabu zote zinakwenda pamoja. Kwa mujibu wa hakimu, kifo cha Wangwe kilisababishwa na kubanwa mlango wa gari wakati wa ajali na kwa mujibu wa ushahidi uliotolewa na shahidi upande wa mashitaka namba nne, tano na sita, inaonyesha dhahiri mshitakiwa huyo aliendesha gari licha ya yeye kukana mashitaka hayo.
Hata hivyo, kabla ya hukumu kutolewa, Wakili Wasonga aliiomba mahakama itoe adhabu ya faini kwa mteja wake ombi ambalo lilitupiliwa mbali na mahakama. Awali, akijitetea kabla ya hukumu, Mallya aliiomba mahakama kumpunguzia adhabu kwa kile alichodai kuwa ana wazazi wanaomtegemea.
Vilevile alidai kwamba anasomesha yatima na kwamba wapo vijana anaowasaidia kutokana na biashara zake na anamsomesha mdogo wake pia. Akizungumza baada ya hukumu nje ya mahakama, Wakili Wasonga alisema hajawa na uamuzi wa kukata rufaa hadi hapo atakapokaa na mteja wake (Mallya).
Ajali hiyo iliyosababisha kifo cha Wangwe na hatimaye kusababisha kijana huyo afungwe, ilitokea Julai 28 mwaka jana saa 2.30 usiku katika eneo la Pandambili, wilayani Kongwa takribani umbali wa kilometa 120 kutoka Dodoma.
Wangwe alikuwa akitoka Dodoma kwenda Dar es Salaam ambako pamoja na masuala mengine, alikuwa akienda kuhudhuria mazishi ya mwanasiasa mkongwe, Bhoke Munanka.
Ajali hiyo ilizusha utata mkubwa baada ya familia ya Wangwe kudai kwamba ndugu yao aliuawa na hivyo kulazimu waite madaktari kufanya uchunguzi kabla ya kuzikwa nyumbani kwake, Kemakorere, Tarime mkoani Mara.
Mbunge aliyechukua nafasi yake ni Charles Mwera.
hii ndio uonevu wa kupindukia. why give him jail term? huyu kijana alitakiwa kuachiwa kwa muda aliokaa rumande. hii ilikua ajali na kama kila mtu anaekutwa na ajali atafungwa basi jela zetu zitajaa. hivi sheria ya tanzania inaongozwa na siasa au uswahili? mbona watu wengi wanapelekwa jela wakati jela zetu hazina nafas? watu wengi tanzania ambao wako jela wasingetakiwa kuwa huko. serikali ijue these people wakishakwenda jela tabia zao zinabadilika kuwa mbaya na hii ni hasara kwa taifa letu.
ReplyDeleteWajina, huyu jamaa kala mvua ya miaka 4 jumla ingawa bado haiwezi kuziba pengo la Mh Wangwe halafu naona kama wamempendeleea sana au kwasababu Wakili wake alilia Mahakamani. Siku kweli sana kila sehemu wazianza Bungeni sasa hivi Mahakamani
ReplyDeleteAlifanya makosa kwenda kumwendesha mbunge. Angebanana kwa kina sijui Sumry sijui nani yasingemkuta
ReplyDeleteSAMAHANI NAOMBA NIULIZE KIDOGO JAMANI MAREHEMU SI ALIKUWA BOSI?JE NI DEREVA GANI ANAWEZA KUMUENDESHA BOSI WAKE MWENDO KASI NAE AKAKAA KIMYA?AU MAREHEMU ALIKUWA NA HARAKA ALIMHALAKISHA BOSI?
ReplyDeletePILI HUYU DEREVA MNAVYOMFUNGA MKEWE MTAMPA HELA ZA MATUMIZI NA HII NJAA KALI ILIYOPO??
MWISHO KABISA HUYU DEREVA KTK KESI YAKE ALIKUWA NA WAKILI AU ALISIMAMA MWENYEWE TU?
Sasa ndo mpate picha kwamba wanasiasa wengi ni wababaishaji tu, maana najiuliza INAWEZEKANA MBUNGE AKAENDESHWA NA MTU AMBAYE HANA LESENI? ALIKUWA HAJUI AMA ALIPUUZA? Huyu jamaa alistahili apigwe Fine tu na sio kumpeleka jela, maana huku uraiani kuna wahalifu ambao ndo wanastahili kwenda jela, hili suala limepelekwa kisiasa zaidi.
ReplyDeleteKibajaj
mie nashangaa watu mmekasirika hakimu kumfunga mallya kwa mwendo wa kazi badala ya kuulizia mahakama walizopelekwa kina mudhihiri!
ReplyDeleteInawezekanaje mtu akaajiri dereva bila kumuonesha leseni au alifoji maana Tanzania tumezidi
ReplyDeleteduh...kesi nyingine iliyoenda spidi. Wa za EPA na kadhalika je?
ReplyDeletemtoto
Mbona sijasikia hukumu za madereva wanaoendesha mabasi na ma lori na magari mengine ambao wanateketeneza mamia ya watu kila kukicha kwa kusababisha ajali za kizembe? Hizi hukumu zingekuwa zinatolewa kwa kila ajali inayotokea, maana ukisiliza kwenye taarifa ya habari utasikia dereva kakimbia, wakipatikana hawasemi kinaendelea nini. wakina Mallya wapo wengi sana wanaua watu na hawachukuliwi hatua yoyote.
ReplyDeleteNaungana na anony hapo juu Mudhihir alipelekwa mahakama gani? huo wote ni ubabaishaji
ReplyDelete