Marcia Maximo
Siku moja baada ya serikali kumwongezea mkataba wa kukinoa kikosi cha timu ya taifa kwa mwaka mmoja zaidi , kocha Marcio Maximo amejibu vikali tuhuma zinazoelekezwa kwake na makocha wazawa ikiwa ni pamoja na kumtuhumu kutotoa ushirikiano kwao.
Pamoja na kukanusha madai mbalimbali ya makocha hao , Kocha huyo Mbrazil alisema ameshangazwa na baadhi ya makocha kumrushia tuhuma na kudai pengine wanatafuta kuandikwa na vyombo vya habari.
Maximo alisema hayo jana jijini Dar es Salaam katika mahojiano maalumu na mtandao wa www.dailynews.co.tz na kuongeza kuwa hata kama hakuja nchini kutoa mafunzo kwa makocha wazawa amekuwa na ushirikiano mzuri na wenyeji wake na kusikiliza maoni yao ndani na nje ya uwanja wa soka.

“Katika mkutano wa mwisho wa makocha uliofanyika hapa nchini niliwaeleza wazi makocha kwamba ofisi yangu iko wazi na wao wako huru kuja kwa ajili ya kubadilishana mawazo ya utaalamu wa soka pamoja na uzoefu”.
Alisema lakini kwa mshangao mwitikio wao umekuwa mdogo kwani ni wachache ndiyo wameweza kufika jambo ambalo alilitafsiri kuwa linawezekana kuwa ni makocha hao wanaona aibu kuzungumza naye na hajui sababu yake ni nini.
Hata hivyo kocha huyo aliongeza anaamini kila kocha ana uzoefu wa aina yake katika kufundisha soka na kama kocha mtaalamu hakuja nchini kufundisha pekee bali kujifunza ujuzi mpya pia.
“Nimekuwa nikimsisitizia Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Sunday Kayuni kuandaa mjadala maalumu wa pamoja na makocha wazawa kwa ajili ya kubadilishana ujuzi na mbinu za ufundishaji soka,”alisema.
Maximo ambaye anatarajiwa kuondoka nchini leo mchana kwenda kwao Brazil kwa ajili ya mapumziko ya wiki mbili, alisema hakuongeza mkataba wake kwa ajili ya kitita cha fedha anachopewa bali kwa sababu amejikita kuhakikisha soka la Tanzania linainuka kufikia ngazi ya kimataifa.
“Hivi karibuni tulipokuwa Ivory Coast wakati wa michuano ya Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wanaocheza Ligi za Ndani (CHAN), nilipata ofa za kufundisha timu za mataifa mawili yanayoheshimika kwenye soka, awali Afrika Kusini walinifuata ili nijiunge nao lakini niliwaeleza fedha kwangu si lolote,” alifafanua Maximo.

Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Mh. George Mkuchika akipiga stori na Maximo huku Rais wa TFF Sir Leodegar Chilla Tenga (kulia) na mwandishi wa Michezo wa Star TV wakisikiliza

Maximo anatarajiwa kurejea nchini katikati ya mwezi ujao wakati kikosi cha Taifa Stars kitakapoingia kambini kwa ajili ya kujiandaa na michuano mingine ya kimataifa.
Wakati huohuo wadau kadhaa wametoa maoni yao kuhusiana na kuongezwa kwa mkataba wa kocha Maximo na kupongeza uamuzi huo uliofanywa na serikali na TFF.
Mmoja wa wadau hao kocha maarufu nchini ambaye pia ni kocha wa kikosi cha taifa cha wanawake ‘Twiga Stars’ , Charles Boniface Mkwasa , alipongeza uamuzi huo na kusema muda alioongezwa utampa nafasi ya kukamilisha programu zake alizoanzisha kwenye timu ya taifa.
Hata hivyo Mkwasa ameitaka TFF kusaka kocha mzawa kwa ajili ya kumsaidia majukumu Maximo ambaye kwa maoni yake atajifunza masuala kadhaa kutoka kwa mtaalamu huyo na kuisaidia nchi pale mkataba wa Maximo utakapokwisha.
“Maximo ni kocha ambaye anatoa ushirikiano mkubwa kwetu na amekuwa akikubali ushauri na mawazo yetu lakini amekuwa na nafasi ndogo ya kuyaongeza kwenye mafundisho yake lakini sasa tuna matumaini atayafanyia kazi baada ya kuongezewa muda huo wa mwaka mmoja,” alisema Mkwasa.
Katika hatua nyingine Maximo amewaomba wadau wa soka nchini na umma wa Watanzania kuwasaidia wachezaji kudumisha nidhamu katika harakati za kufanya waweze kuishi kama wachezaji wa kulipwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana kwenye ofisi za TFF Karume Ilala Maximo alisema: “Kuna haja ya jamii yote kusaidia kuwaeleza wachezaji kucheza soka ya kitaaluma, si ile ya wachezaji kutokuwa na nidhamu au mchezaji anafikia kujisingizia kuwa ni majeruhi.
Hili kocha peke yake hataweza”. Alisema kuwa wanachotakiwa wachezaji ni kuhakikisha wanajitunza na hata pale watakaporudi kwenye klabu zao kwa kufuatilia kula mlo kamili na hata kwenda gym mara mbili kwa wiki.
“Kikosi changu kinaonekana sasa kimebadilika, tulipowafunga Ivory Coast, nilitegemea ningekuta wachezaji labda wanashangilia, lakini ilikuwa ni tofauti, pamoja na kuwa na furaha ya ushindi lakini walikuwa wametulia.
Maana suala la ushindi halikuwa geni kwao, labda hali kama hiyo ingetokea miaka ya nyuma.”
Akizungumzia hatua yake ya kusaini mkataba mpya, Maximo alisema kuwa pamoja na kuwa alikuwa akihitajika na timu mbili, lakini alijiona anaguswa na ombi la Tanzania la kutaka kuendelea kuifundisha.
Aidha, Maximo aliwashukuru viongozi wa TFF, serikali kwa ujumla akiwamo Rais Jakaya Kikwete, Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo George Mkuchika na Naibu wake Joel Bendera kwa kushirikiana naye.

SOURCE:


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Hakuna umuhimu wa "MALUMBANO" kati ya "MAXIMO NA WAALIMU WENGINE" wala kufikiria kama kuna nchi zingine zinahitaji uwezo wake wa kuwahudumia,hayatotufikisha mbali katika kuleta heshima ya mpira wa kimataifa katika nchi yetu.

    MAXIMO anahitajika kupewa uhuru wa kutimiza aliyoyahahidi kuyaleta katika TAIFA STARS,anahitajika pia kuheshimu na kusikiliza maoni mbali mbali ya waalimu wengine nchini kuna wengi wana kiwango cha utaalamu kutufikisha hapo "MAXIMO NA EL BASHIR" wametufikisha.

    Waalimu wengine wakiacha ubinafsi na kupewa uwezo wote toka serikalini,uwezo ambao haukuwepo wakati uliyopita,uliwasimamisha kiutaalam kutufikisha tulipofikia.

    Tunashukuru wakubwa wanaohusika wametukubalia na kuwapa nafasi"MAXIMO na EL BASHIR ya kuendelea.

    Mhs waziri Mkuchika na Naibu Mhs Bendera wahakikishe pia
    viongozi wa TFF wanahusishwa katika maswala magumu ya kutoa uamuzi wa kila siku,maoni na kiuwezo katika gharama za matumizi,bila ya hivyo kuna hatari ya kutofikia katika lengo letu la kiwango cha mpira wa kimataifa,malumbano yataendelea.

    mickey@mail-online.dk
    DENMARK

    ReplyDelete
  2. Maximo sio kocha.mtu wa majungu sana mara wachezaji mara makocha.hakuna timu iliyompa ofa zaidi ya kutudanganya ili tuingie kichwa kichwa kumpa mkataba mnene.
    tenda ya kumuongezea kocha mkataba.ilitakiwa itangazwe ili makocha wengine wagombee.
    maximo anatuona Watanzania wajinga sana.kwani heshima na hadhi tuliyompa haipati kokote duniani.CV YAKE IMEKAA UJANJA UJANJA.
    SIKU AKLIONDOKA NITACHINJA KUKU.

    ReplyDelete
  3. MAXIMO!!! MAXIMO!!!! BADO ANAHITAJIKA ZAIIDI YA MWAKA MMOJA HIVI, KAMA MIAKA (3)KATIKA KUINOA TAIFA STARS,NAJUA WAZI WAKINA MKWASA NAO WANANG`ATA NA KUPULIZIA INAONEKANA AWAMPENDI MWENZAO,HATA HIVYO MUNGU ANAMUONGOZA KUWAFUNDISHA UPENDO ILI MPUNGUZE KUMCHUKIA!!! MAXIMO ANAIPENDA TANZANIA NA TAIFA STARS, MUNGU AWENAYE SIKU ZOTE MPAKA TUTAKAPOFIKIA PALE TUNAPO PAHITAJI SIO KWA HARAKA HIVYO POLEPOLE!!!

    MDAU` HOLLAND!!!!

    ReplyDelete
  4. wape wape eeeeeehh vidonge vyao, wakimeza wakitema shauri yao..

    ReplyDelete
  5. Nakubaliana na mawazo ya mdau wa Denmark na kama alivyosema Maximo kama makocha wanahitaji ushauri au kubadilishana mawazo na ufundi milango ipo wazi.Makocha wetu wa Kitanzania tuache kulalamika muanzishe "initiative" wenyewe mnaweza ku-interact na Maximo wala msiwe na "inferiority complex" mwenzenu Maximo alishawaambia milango ipo wazi kwa nini hamuendi?mnabakia kulalamika pembeni bila,acheni utamaduni wa kulalamika.Muache chuki yeye Maximo alivyoletwa kufundisha soka huko TZ,alipewa job description yake ya kufundisha soccer na kunyanyua kiwango cha soka na hiyo ni kazi anayofanya sasa yeye amejitolea kukutana na ninyi basi tumieni hiyo nafasi.

    ReplyDelete
  6. Maximo haipendi nchi yetu anapenda pochi letu tu.
    anataka kukaa zaidi ya miaka mitano maana kasema anakwenda kwao kuchukua program ya miaka mitatu.ili mwakani mkataba ukikaribia kuisha aanze kulia kuwa anataka kumalizia program yake.
    anakula pesa nyingi sana kinyume na elimu au ujuzi wake mdogo.

    ReplyDelete
  7. KUMBE NI MKWASA NA MZIRAIIIII!!!!!!
    POA TUU!

    ReplyDelete
  8. alafu nyie majungulization!!!! acheni chuki binafsi haifai italeta tafalani. Maximos is the beast!!!!
    kada boy!
    sinza!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...