livingstone club: imenusurika
oceanic bay hotel: imeteketea yooooote

paradise resort:imeteketea yooote hata foronya haikuwahi kuokolewa
KATIKA KUFUATILIA KWA KARIBU BALAA LA MOTO HUKO BAGAMOYO, GLOBU YA JAMII INAPASHA KWAMBA HOTEL ZA PARADISE NA OCEANIC BAY (PICHANI) ZIMETEKETEA KABISA NA MOTO.
KWA BAHATI HAKUNA MTU ALIYEJERUHIWA ILA INADAIWA HASARA INAKADIRIWA KUWA YA MAMLILIONI YA SHILINGI.
SHUHUDA WA GLOBU YA JAMII ALIYEKO HUKO AMEHABARISHA SASA HIVIKWA VODA KWAMBA MAJENGO YOTE YA HOTELI YA PARADISE YAMETEKETEA NA KWAMBA HAWAKUWAHI KUOKOA HATA FORONYA AMA GODORO AMA UFAGIO.
HALI KAMA HIYO IMEREKODIWA PIA KATIKA HOTELI YA OCEANIC VIEW, AMBAYO NI JIRANI NA PARADISE, ILA YA LIVINGSTONE CLUB, AMBAYO PIA JI JIRANI KWA UPOANDE KWINGINE, IMENUSURIKA KABISA. INASEMEKANA HII NI KWA SABABU YA UPEPO WA BAHARI KUPEPERUSHA MAKUTI KUELEKEA OCEANIC HOTEL
AMESEMA KWAMBA MOTO HUO, ULIOANZA ASUBUHI, ULIDUMU KWA MUDA WA DAKIKA 15 TU NA HOTELI ZOTE MBILI ZIKAWA ZIMETEKETEA. YAANI FAYA AMBAO WALIKIMBIA TOKA DAR KWENDA BAGAMOYO KWA KASI ZOTE WAMEKUTA MAJIVU TU. PICHA KIBAO ZAJA MUDA SI MREFU UJAO..




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Now it`s time for the Goverment kuona umuhimu wa kuwa na Fire Station katika kila Mji na sio station tu,bali na maji kuwepo wakati wa tukio.Maana hii ni hatari kwa jamii.Jamani tunafanya vitu muhimu kama ni luxury wakati ni necessity.Can you imagine zima moto toka Dar hadi Bagamoyo??!!!??

    ReplyDelete
  2. Haya tena wadau sasa serikali yetu inaelekea wapi? are we really serious in emegency preparedness. I think we are not prepared for things like that. Fire itoke Dsm kwani Bagamoyo hawana Fire tender?Kwa barabara zetu zilivyonyembamba nafikiri watu wote wanaotumia bagamoyo road walikuwaharrased sana hiyo asubuhi.Haya tena mbilimbili mpaka pwani tutafika tu

    ReplyDelete
  3. Angalia sasa! hii ni kwa sababau ya kutokuwa na priorities, kitu kama kikosi cha zima moto kinatakiwa kiwepo kila mahali nchi nzima. at least kila wilaya iwe na kituo cha zima moto. lakini tatizo la nchi yetu ni viongozi wasio fikiri na kuwazia matumbo yao tu.
    Maisha bora yako wapi????
    Ngoja siku moto uwake Ikulu na naombea siku hiyo faya zote zisifanye kazi, then watajua umuhimu wake. Poleni bagamoyo.Mdau, Oslo

    ReplyDelete
  4. Ni vyema nayo maji yakapatikana watakapo amua kuweka Fire Brigade Bagamoyo maana hapa Dar tuu kwenyewe kuna wakati ilikua watu wakipiga simu kuomba msaada wa zima moto wanaambiwa maji hakuna au magari mabovu!!!

    ReplyDelete
  5. ZIMAMOTO INATOKA DAR KUJA KUZIMA MOTO WA BAGAMOYO? HIVI NI KWELI KUNA WASOMI SERIKALINI AMA NDIO BORA KIONGOZI NA SIO KIONGOZI BORA?
    NI MWAKA 2009 HATA MTOTO WA DARASA LA SABA UKIMPA OFISI ANAWEZA KUPANGA MIKAKATI BORA KULIKO VIONGOZI TULIOKUWA NAO.MJI AMBAO UMEJENGWA KWA AJAILI YA WATALII NA WANANCHI KUINGIZIA KIPATO TAIFA UNASHINDWA KUWEKEWA UDUMA MUHIMU?
    mdau "cha mtu mavi"

    ReplyDelete
  6. Ajali nyingine ya moto imetokea hapa Mtwara ambapo nyumba maarufu ya kufikia wageni iitwayo Chilindima imeteketea kabisa usiku wa Jumamosi tarehe 21/03/09. Gari la faya la Manispaa halikuwa na maji na lilitotoa msaada ni zimamoto ya bandari.

    ReplyDelete
  7. Duh! Maskini.. Hapo tena janga la ukosefu wa ajira...Tanzania ipo katika msukosuko wa fedha watu wanapunguzwa kazi huku majanga kama haya tena yanatokea kaka zetu, dada zetu, baba zetu na wadogo zetu wataishi vipi? Kwani hapo watanzania zaidi ya 20 watakuwa hawana ajira. Hapo hapo pato la Serikali limeanguka japo sio kwa asilimia kubwa ila linapungua kiasi fulani kwani Sehemu kama hizo zilikuwa zinachangia mapato kwa njia mbali mbali katika Nchi yetu. MUNGU INUSURU NCHI YETU...Watanzania tujifunze kupitia makosa jamani....MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRICA.

    ReplyDelete
  8. Mji kama bagamoyo ni uzembe wa viongozi wenyewe, pakishakuwa na vitu vikubwa kama mahoteli hayo ingebidi waweke zima moto karibu.
    Kuwa nazo nchi nzima inaweza kuwa tabu mwanzo kwani kuna baadhi ya sehemu kwa kweli hazihitaji hiyo huduma.

    ReplyDelete
  9. Waache kujenga na makuti jamani! Hayo makuti ni fire hazard ile mbaya. Sawa yanapendeza na kuvutia watalii lakini pia yanaungua kirahisi. Tusisahau moto pale Bagamoyo College of Arts na Bahari Beach Hotel.

    ReplyDelete
  10. Habari Kaka Michuzi na ahsante kwa kutupatia breaking news. Mimi ni mwenyeji wa Bagamoyo na nakumbuka miaka kadhaa iliyopita balaa hili ilikikumba Chuo Cha Sanaa huko huko kwetu Bagamoyo ambacho kilijengwa kwa style ya kuvutia ya makuti mpaka chini . Kinachonishangaza viongozi wa serikali walikuwa wapi kuepusha majanga kama haya baada ya Experience ile mbaya, vilevile baada ya kuona Chuo cha sanaa kimeteketea nadhani uongozi wa hoteli husika walitakiwa waweke mikakati madhubuti ya kuepuka balaa kama hili. Hili ni somo basi kwa wamiliki wengine wa mahoteli zilizopo Bagamoyo na hasa hasa kule kwa watani zangu Zanzibar, maana mahoteli kibao ya makuti yapo maenei ya Nungwi na Jambiani. Tujifunze utamaduni wa kujitahadhari kabla ya janga halijatokea......Ushauri wangu kwako mdau anzisha kampeni kabambe ya kuhamasisha wenye mahoteli Zanzibar wachukue tahadhari, hata ikiwa ku raise funds kwa ajili ya kununulia magari ya zimamoto, gharama za ununuzi wa magari haya huwezi kulinganisha na hasara ya Mabilioni inayoweza kutokea. THANKS

    ReplyDelete
  11. Wanangoja wafadhili kutoka nje kuweka hayo ya faya brigedi!

    ReplyDelete
  12. Hoteli Kwishnehi!
    Bima che?

    ReplyDelete
  13. Hatuwezi. Tunahitaji wawekezaji na wafadhili.

    ReplyDelete
  14. Lini tutaachana na take away life? Mheshimiwa rais na wahusika wako ni lini tutaachana na maisha haya? hapa ni kwetu ni Tanzania yetu kwanini tunaishi kama vile tuna kwetu?
    Waziri wa utalii kipindi kile mama Zakia Meghi alishawahikuzungumzia hotel za namna hii kwamba watu wapunguze kutengeneza take away hizi,sasa leo yanajitokeza je ilikua hamna umuhimu wa kuyafanyia kazi maneno yake?au habari yake ilivyouza magazeti tu ndio basi?
    Haina haja ya kumaliza keyboard yangu kwa kuandika saana ila ni kwamba tujipange tukamfufue aliyetuloga na kutufanya tuwe na serikali yenye viongozi wasiojua wajibu wao wala kutaka kufanya kazi walizoteuliwa kwa ajili,na kuishia kuishi kwa dili tu. Kila mtu anawaza dili tu,dili tu,dil....
    Mkuu wa wilaya anakili ameshalipia gari ya zimamoto lakini kwa sababu za urasimu gari hiyo imechelewa kufika ukiuliza kwa nini unaambiwa dili tu,dili tu....

    ReplyDelete
  15. kwa ujumla, huduma za jamii Tanzania ni sifuri.Kuanzia huduma za hospitali,taa za barabarani hadi hiyo zimamoto.Hili sio suala la Raisi wa nchi kusimamia, ni viongozi wa ngazi za chini,kuhakikisha wanapata bajeti ya kutosha kwa ajili ya huduma za jamii. kwanza sitashangaa kusikia hakukuwa na ambulance pamoja na emergency team kwa ajili ya yoyote aliyeumia kwenye janga hilo. halafu tunasema tanzania imeendelea, hata zima moto bagamoyo hamna!!!!????

    ReplyDelete
  16. Kuhusu ufukwe wa "coco beach" pamoja na fukwe nyingine dar,hili wala sio swala la mjadala, magari yasiruhusiwe kuegeshwa kwenye mchanga au kandoni mwa ufukwe. ufukwe ni kwa watu kupunga upepo na sio magari kuharibu ufukwe. wananchi pia waelimishwe,kwasababu watanzania wengi wanadhani kuegesha gari zao ufukweni ndio matanuzi!!!Kuhusu serikali ya jiji,kwa ujumla wamelala, au hamna fungu la kujenga egesheo la magari,au inabidi basi designer toka nchi zilizoendelea aje kuwafundisha ni jinsi gani waweze kuiboresha fukwe hiyo na ipendeze.mimi nakaa nje ya nchi,mwaka wa kumi na 5 sasa,nikija likizo na kupita hapo coco beach, ni uchafu mtupu na naona aibu sana. hakuna life guards,hakuna chochote.kwa ujumla,hakuna ustaarabu.hata mtu akizama, anakufa bila msaada wowote.
    solutions:
    1).Kama hela ipo, bado hao city planners wapelekwe nje na kujionea jinsi gani fukwe zinavyotunzwa(au wapelekwe hotel za watu binafsi zanzibar na kujionea wenyewe).
    2)Wapewe watu binafsi waindeleze kwa mkataba.
    3)Wananchi waelimishwe kuhusu kutunza fukwe,kupitia vyombo vya habari.
    4)Magari yasiruhusiwe kabisa,kwa kuweza kuzuia hiyo,basi vijengwe vizuizi vikubwa vya kuzuia magari yasiingie.

    asante

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...