Ofisa toka ofisi ya Mhariri Mtendaji wa magazeti ya serikali ya Tanzania Standard Newspapers (TSN) Media group Mkami Chacha (kulia) na Mwandishi mwandamizi wa HabariLeo Ikunda Erick, wakimjulia hali mpiganaji Athuman Hamisi Msengi, walipokwenda kumtembelea kwenye Hospitali ya Milpark jijini Johannesburg, Afrika Kusini leo asubuhi. Mpiganaji Hamisi amelazwa hapo kufuatia ajali ya gari huko Kibiti, Mkoa wa Pwani, takriban miezi mitatu ilopita na kupata majeraha kwenye shingo na uti wa mgongo. Kwa mujibu wa Da'Mkami na Ikunda, hali yake inaendelea vyema

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Kwa kweli nafurahi kuona kaka Athumani anaendela vizuri. Tunaendelea kumwombea. Mungu ambariki.

    ReplyDelete
  2. Mwenyeezi Mungu na ashukuriwe! sura yake na huo mkao inaonyesha wazi kuwa anaendelea vizuri sana na siko alikotoka.
    Alhamdulillah na Inshaallah Mwenyeezi Mungu atakuafu zaidi na utarudi mzima kufanya kazi zako na kuungana na familia yako na wapenzi/marafiki zako. Amin.

    ReplyDelete
  3. Kaka Athumani. Nazidi kukuombea mungu akupe afya njema. Wana AKUDO tuna kumiss sana kwenye matamasha yetu. Wewe ulikuwaga mdau wetu mkuu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...