mtoto lazaro akiuguzwa na mama yake jovina zacharia nyumbani kwao buguruni
sehemu ya mguu wa mtoto lazaro ambayo inazidi kuoza kwa kukosa matibabu

Jina : Lazaro William. 

Umri : Miaka 13. 

Anapoishi : Buguruni. 

Shule anayosoma : Hekima Shule ya msingi, Darasa la sita. 

Hospitali alizokwishatibiwa : MOI(Idara ya mifupa katika hospitali ya Taifa Muhimbili), Bugando Mwanza, Nkinga Tabora, Burere Hospital Kibaha for Bone and Joint Surgery. 

Nambari ya Akaunti: William, Jovina Zacharia, NMB(House Branch) Bank Ltd, A/c No.2231603793. 

Mawasiliano : Unaweza kuwasiliana na Mama wa mtoto na pia kuongea na mtoto 0752 191296.

                        Barua pepe : tmajaliwa@yahoo.com. 

Maelezo ya ziada:

  Mtoto huyu alianza kuumwa kuanzia mwaka 2000 mwezi Julai.

MOI walisema kuwa akifika umri wa miaka 18 tatizo litakwisha,lakini hadi sasa hali ni mbaya sana.

  Burere Hospital Kibaha Dr. alisema kama akishindwa yeye kumtibu hadi kupona basi itabidi apelekwe India kwa matibabu zaidi, mwaka jana Dr alishindwa akashauri mtoto apelekwe India.

  Dr. Arab wa Hospitali ya Appollo tawi la Dar es salaam ameshauri mgonjwa apelekwe India kwa matibabu zaidi. Ugonjwa unaomsumbua ni OSTEOMYELITIES.

  UKWELI ANATESEKA SANA. Gharama zote zilizomuwezesha kutibiwa katika hospitali mbalimbali zilikuwa ni michango kutoka kwa wasamalia wema.

Mama yake mtoto huyu alitelekezwa na baba yake muda mrefu sana wakiwa Mwanza. 

MUNGU AWABARIKI SANA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. TATIIZO LAKE HILO LINAITWA CHRONIC OSTEOMYELITIS, UAMBIKIZO WA BAKTERIA KATIKA MFUPA NA MISULI INAYOUZUNGUKA MFUPA. AELEZE X RAYS ZINASEMAJE KUHUSU NI KIASI GANI MFUPA HUO TIBIA AU FIBULA UMEADHIRIKA , NA KAMA ANATAKA KUBADILI AU KUPANDIKIZA MFUPA MWINGINE. MAELEZO ZAIDI YATASAIDIA KUHARAKISHA MICHANGO.

    ReplyDelete
  2. msikae kufadhili umisi tuu na timu za mpira, fadhilini maisha, nyie kina bakhresa, n.k.

    ReplyDelete
  3. mtu akitaka kwenda nje kushiriki michezo serkali inalipa gharama, akita kupata matibabu serikali inajitoa. pigia kura ccm 2010.

    ReplyDelete
  4. shayo na john mashaka wanajifanya wazalendo changia hapa.sio maneno matupu kila siku kwa balozi Mithupu.

    ReplyDelete
  5. ndugu zanguni haya ndo mambo ya kufanya sisi watanzania sasa hii ni baraka kwa yule yoyote atakayejitoa kwa uwezo wake kumsaidia huyu mtoto kwa pesa, sala na ushauri wa kitaalam mungu akubariki sana utapona vizuri kabisa tunaomba details za kutuma hiyo fetha wadau nawaombeni sana tuwasaidie watu kama hawa ni baraka kwetu sote. nafikiria ningekuwa mimi! ningehitaji msaada pia

    ReplyDelete
  6. Kwako anony wa 7:22PM,
    Sahihi kabisa jinsi unavyoelezea. Nfupa mwingine ulishatoka na mwingine unaendelea kuota.
    Kwa kuwa mama yake si mtu aliyesoma,basi ni vigumu kujua kama anataka kubadili au kupandikiza mfupa mwingine, ISIPOKUWA YEYE ANAOMBA MATIBABU KWA AJILI YA MTOTO WAKE.
    Mimi sijawahi kuona X-Rays zake, lakini MOI walikataa kutoa file lake ili liweze kutusaidia kufuatilia matibabu maeneo mengine.
    Kama unaweza kuniandikia,basi nitafuatilia hizo X-Rays halafu niziweke ili watu wote wafahamu na kurahisisha matibabu yake.
    Ahsanteni sana,
    tmajaliwa@yahoo.com

    ReplyDelete
  7. MICHUZI NAOMBA UWEKE THAMANI YA FEDHA... NI KIASI GANI KINATAKIWA?

    MCHUMI WA TEXAS

    ReplyDelete
  8. Mchumi wa Texas,
    Michuzi ameshaniandikia kuwa nifanye estimates za gharama halafu nimpe ili aweke katika blog. Nafanyia kazi halafu nitampatia ili mjue gharama zinazoitajika.
    Pia nilitaka kufahamu kama ni wewe ambaye ulimpigia Mama mtoto na pia uliongea na Mtoto mwenyewe?

    Anony wa 5:00AM.
    Unaweza kutuma mchango wako katika account ambayo imeelezwa katika Blo, hiyo Akaunti ni maalum ambayo Mama amefungua kwa ajili hiyo.
    Wote MUNGU AWABARIKI SANA KWA KUGUSWA. KUTOA NI MOYO NA SI UTAJIRI.
    tmajaliwa@yahoo.com.

    ReplyDelete
  9. hizi habari za kupeleka wagonjwa nje kutibiwa zinazidisha gharama.
    wenye moyo wangejitolea au kushawishi wawekezaji kuanzisha hii plastic surgery bongo.vifaa vyake ni ghali lkn watu wakijitolea ikianzishwa hiyo branch hapa itasaidia wagonjwa wengi kwani gharama zitapungua baadae.

    note bongo hatuna plastic surgery or brain surgery,hata madokta wenye ndoto ya kuspecialise ktk hizo branch wanashindwa kutokana na ukosefu wake.

    aidha wasamaria wema mungu awabariki kwa kila mchango mtaoutoa

    ReplyDelete
  10. chronic osteomyelitis ni ugonjwa ambao kutibu ni very difficult. mtu anaweza kufanyiwa surgery hadi 15 asiweze kupona. Daktari atakayekwambia kuwa a single surgery itatibu huu ugonjwa ni muongo. So hata huko india idadi ya surgery ni nyingi. ukiangalia hiyo picha mguu hauna discharging sinus kinachoonekana ni defect ya skin inayosababisha mfupa kuonekana kwani distal third ya leg mbele hakuna msuli ni subcuteneous tissue kidogo na bone(UGOKO)kama akionyesha x-ray na tukiona new bone formation ya kutosha na hamna sign ya infection inawezekana kuweka flap ya muscle na graft, hahiitaji India, kama wanakwenda MOI basi ni DR Gani wanamuona .Kumbukeni India au sehemu nyingine duniani hakuna miracle ,kama mtu akiwahi mapema kila kitu kinakwenda vizuri.
    Kibaha Dk yule ni bingwa hawezi kusema hivyo, Moi hawakai na x-ray za mgonjwa labda kuwe na special study.Sasa mimi naona kabla ya kwenda India arudi MOI amuone afisa uhusiano atasaidiwa.Wadau wengine ingieni kwenye mtandao na msome X,nic osteomyelitis mtaona huu ugonjwa ukoje zipo article zenye maelezo ambayo kila mmoja ataelewa

    ReplyDelete
  11. Anony unayetumia mail ya majariwa, mfupa unaoota kwenye chronic osteomyelitis nni involucrum ie new bone formation .HUWEZI KUPANDIKIZA MFUPA ( bone grafting) kwenye infection itafail tu ,so ni vizuri mtuelewe natural history ya disease then tuanze kucomment. NAsisitiza tena mtomto aende MOI haitaji kwenda india kwa ajili ya chronic osteomyelitis. Brain surgery, plastic surgery, heart surgery n.k zinafanywa very successful hapahapa bongo

    ReplyDelete
  12. Madaktari bingwa pia wapo Bongo nakumbuka nilifanya kazi na Dr Kinasha wodi ya mifupa. Kwakweli ni neurosurgeon mkali sana ila sijui where abouts zake ila kwa kazi yake nampa heko. So wataalam bongo wapo labda sema rushwa ndio inatutawala watanzania.Pia kama mtu unataka kusaidia ni bora tu umsaidie mtoto sio kuomba X-ray kwanza it is not ethical. That is considered part of the patients medical record. A patient has a right to privacy. Kesha waonyesha picha ya mguu inatosha.

    ReplyDelete
  13. Yaa ila kuonyesha mguu na sura basi confidentiality ya patient imeshatoka tena huyum mgonjwa ni underage. So waende na mtoto na wachukue x-ray mpya (watapigwa bure na status ya mfupa itaonekana na matibabu yatatolewa. Unajua wagonjwa rushwa wanataka kutoa wenyewe, tena wagonjwa wanaotoa rushwa ni wale wasio na matatizo makubwa. Ila kutoa rushwa ni mbaya sana kwa unaonyesha kwamba ujari watu waliokutangulia wapate hiyo servise ni mbaya sana. Utaona mtu kaumia anafika Hospitali basi ndugu wanaanza kuzunguka ,oooh tunatafuta mtu / Daktari ili awe wake.Wakati mtu akifika tu lazima anatibiwa na jinsi alivyotibiwa lazima Daktari husika aeleze kwenye vikao vya asubuhi vya madaktari wote 'kitimoto' Lakini utashangaa ooh tunatafuta Daktari, basi wanakutana na wajanja wanachukua hela na wanasema tunampelekea Daktari. Daktari kutibu mgonjwa ni lazima hivyo atatibu tu hata asipopewa hela ila ndugu watajua kuwa mgonjwa katibiwa sababu ya hela.
    So mgonjwa huyu aende Moi atatibiwa kwa taratibu za serikali na kama hana msaada basi apate barua toka serikali za mtaa , atapewa matibabu yote na MOI na kama MOI wakishindwa , watatoa report na kuandika barua na ataaenda nje na MOI ndo watapendekeza aende nchi gani ,hata Germany or UK na siyo lazima nje.
    Mpelekeni mtoto MOI msimnyime haki yake ya msingi

    ReplyDelete
  14. michuzi tunaomba gharama nzima matibabu sisi wabeba box tuanze kuchangamka kumsaidia mtoto

    ReplyDelete
  15. BADO TUNAKUSANYA TUNALETA CHOCHOTE,TUTAKACHOJALIWA.
    MZALENDO,TX.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...