MICHUZI NA WADAU WOTE,
LEO NAWAOMBA SANA MSAADA WENU WA    KUTAFSIRI MANENO YAFUATAYO KWA KISWAHILI.

LABDA TU NIWAFAHAMISHE KUWA MIMI NAFANYA KAZI NA WAZUNGU HAPA DAR  KUTOKA SPAIN.  MIONGONI MWAO HAWA JAMAA TULIBISHANA KWAMBA KISWAHILI HAKINA MANENO MENGI AU MSAMIATI WA KITAALAM KWA TEKNOHAMA.

MIMI KWA KWELI NIMETETEA ILE MBAYA KWAMBA TUKO FITI SANA KWA KILA NYANJA. SASA LEO SI NDIO KANITWANGA NA MANENO HAYO CHINI ILI NIMFAHAMISHE KWA KISWAHILI.  HAPO NDIO NILIPOPATA KIGUGUMIZI ILA NIMEMWAMBIA KWAMBA MPAKA KESHO NITAMPA JIBU, NISAIDIENI WADAU. MANENO YENYEWE NI KAMA IFUATAVYO....
 
“The directory already exists! Are you sure you want to install here and possibly overwrite existing file?
 
Warning: Using a folder that contains a previous version of gvSIG May cause the application to fail”
 
 
WAWEZA KUNIADIKIA MOJA KWA MOJA KWA EMAIL HII: 
haji.lukamba@isf.es
  
MZEE WA BUNJU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Wajuwa, Jogoo alimwambia Bundi--Wewe unanicheka kwa kuwa siwezi kuruka, jee wewe waweza kuweka
    Waambie jamaa hao watafsiri mambo hayo Kispania kwanza
    Wakatabahu

    ReplyDelete
  2. Hispania na kiswahili ndio palepale mwambie yeye kikwao je asirukie Kiengereza kubadilisha kiswahili.

    ReplyDelete
  3. "Tayari saraka ipo! Una uhakika unataka kuiingiza hapo na labda ukafuta faili(mpororo) (u)lililokuwepo?

    ReplyDelete
  4. Hao siyo wazungu basi waspanishi (they R not white)huku marekani kazi za chini na ngumu hao hawakatai

    ReplyDelete
  5. Kabrasha lenye hilo jina tayari lipo. Una uhakika unataka kulifuta na kutengeneza lingine?

    Onyo: Kutumia kabrasha ambalo lina 'gvSIG' ya zamani, kunaweza kusababisha matatizo.

    ReplyDelete
  6. wadau mliotafsiri.that's LOUD n CLEAR.
    kwa wale wadau mnaotaka awajibu kuwa watafsiri kwa Spanish kwanza huo utakuwa kuleta ubishani usio na msingi.
    sometimes watu wakiwa kazini kunakuwa na maneno/story ama maswali ya hapa na pale.haswa kama unafanyakazi na mtu toka taifa lingine ndo huwa noma zaidi.
    hivyo basi,sometimes swali juu ya swali haina umuhimu.jibu swali then kama unataka basi uliza swali kama hilo hilo kwa muhusika.

    mfano,"hey X,umekula?". wewe jibu kama ndio/hapana.kisha kama ungependa pia kujua basi muulize,"wewe je,umeshakula?".

    na sio, "hey X,umekula?". nawe "kwani wewe umekula?".
    hii kasumba ya swali juu ya swali tumeizoea sana hapa bongo but i'm sure tunaweza kubadilika slowly.

    Peace!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  7. WADAU SIO KWAMBA KISWAHILI KINA UPUNGUFU WA MISAMIATI ILA SISI WENYEWE HATUJUI KISWAHILI?BUT KISWAHILI KINAMANENO YOTE HAYO,LKN MCHANGIAJI WA MARCH26,6:13 AMECHANGIA VIZURI ILA KAKOSEA NENO OVERWRITE SIO KUFUTA BUT NI KUPANDIKIZIA AMA KUONGEZEA FAILI AMBALO LINAEXIST BILA KULIFUTA PIA MCHANGIAJI WA MARCH26 60:7 NAYE AMEJITAHIDI.

    HAO WAISPANIOLA WASIWAZINGUE WAMBIENI WAYATAFSILI WAO MUONE KAMA WATAWEZA NA NDIO MAANA KUA MKARIMANI NI KITU KIGUMU MNO.

    WATAISHIA KUTUMIA SOFTWIRE KUTRANSILATE(KUTAFSIRI) HAYO MANENO KIKWAO

    ReplyDelete
  8. Mdau usijiukajaribu kuwaambia kutafsiri Kispain, kwani tafsiri yake ni hii...


    El directorio ya existe! ¿Estás seguro de que desea instalar aquí y posiblemente sobrescribir los archivos?

    Advertencia: El uso de una carpeta que contiene una versión anterior de gvSIG Puede causar la aplicación a fracasar "

    ReplyDelete
  9. Jamani katika misamiati ya kiteknolojia kiswahili bado kipo nyuma hapo ni ubishi tu, lakini kwa kweli tupo nyuma. Ingekuwa kweli ni lugha yetu kweli mtu mother tongue mpaka aulize kwa michuzi? je angeuliza kitu kama "may i have some water" ungekuja huku kuuliza?

    Mdau hapo juu hivi wale hispanics wa marekani kwani ni watu wa kutoka spain?au wanaongea tu kispanish? waspain hutoka europe na kusema kweli sio latinos kama wa mexico.

    ReplyDelete
  10. Onyo: Soo la kutumia jalada lenye gvSIG ya zamani usiombe

    ReplyDelete
  11. wadau walioleta ubishi wa kipuuzi hawatakaa wakaendlea.

    NI kweli kiswahili kina upungufu sana wa misamiati na wala usijaribu kufananisha spanish na kiswahili, kwani hata kiingereza chenyewe kimeopoa maneno kibao kutoka spanish.
    na wale walioko USA ni latinos na sio spanish pamoja na kujwa wanazungumza spanish.
    Kama Kina shayo na mashaka wangejadilia mambo yao kiswahili labda ingesaidia kukuza kiswahili

    ReplyDelete
  12. Unajuwa ndugu yetu...mimi ninawasiwasi kwamba wewe kazi yako ni kutafsiri kingereza kwa kiswahili...na naona hapo umekwama na unahitaji msaada...lakini uje utuambie methali ya kswahili bla blabla...kila lugha ina methali ya kswahili...na kuna ugha zingine juwezi kutafsiri kwa lugha nyingine

    ReplyDelete
  13. Ndugu uliyeuliza swali jaribu jibu hili:Directory inatokana na neno direct ambalo maana yange ni kuonyesha hinyo chukulia directory ya TTCL,ni mwongozo wa namba za simu za wateja.Hivyo basi
    `` Mwongozo upo! una uhakika unataka kuweka hapa kwani unaweza kufuta kabrasha lililopo?

    ONYO:Kwa kutumia kabrasha lenye gvSIG ya awali inaweza kusababisha kutofanya kazi.

    Kuwa makini unapouliza maswali kama ni ya ITsema ili washughukike nayo wenyewe sisi tunasaidia tu lugha.nina uhakika wote hatujakutosheleza sasa ungunga upate jibu upokee na mshahara kabisa mwezi umeisha.

    ReplyDelete
  14. we ongeaongea tu kiswahili na uwaambie hiyo ndo maana yake wataelewa kama unawapwaga?

    ReplyDelete
  15. Mwongozo tayari upo! Je una uhakika unataka kuhifadhi faili hapa na kufuta ambalo tayari limeshahifadhiwa?
    Tahadhari: Kutumia kabrasha lenye gvSIG ya zamani,kunaweza kusababisha matatizo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...