Mahojiano baina ya Mwandishi maalum Barnabas Lugwisha na Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania, Ephraim Mafuru, kuhusu mikakati ya Vodacom kwa mwaka huu.
Swali: mwaka 2009 mmeuanza vipi ?
Jibu :Swali lako ni pana sana, lakini sisi kama Vodacom Tanzania, tumejipanga vizuri sana ili kuhakikisha kwamba mwaka huu Vodacom inaendelea kutoa huduma bora kwa wateja wake,huduma ambazo zinakata kiu yao ya mawasiliano.
Aidha nachukua nafasi hii kuwashukuru kwa dhati wateja wetu, ambao kwa kweli wametufanya tuongoze miongoni mwa mitandao, kama shukrani yetu kwao , tumejitahidi kuwapatia wateja wetu huduma bora, pamoja na kuwarejeshea sehemu ya kile tunachokipata kupitia programu mbalimbali kama vile Tuzo Pointi na Tuzo Droo.
Katika TUZO DROO, wateja wa Vodacom wamekuwa wakijishindia Sh. milioni 40 kila mwezi tangu kuanza kwa programu hii karibu miezi kumi na mbili sasa, katika programu hiyo kubwa kuliko zote iliyowahi kuzinduliwa na Vodacom. Vile vile kila wiki wateja saba wa Vodacom wamekuwa wakijinyakulia nyakulia Sh. milioni moja kila mmoja wao wakati wateja wengine 100 kwa kila wiki wamekuwa wakijishindia muda wa maongezi wa thamani ya Tsh 50,000.
Kupitia programu hizo , Vodacom Tanzania imeweza kuyabadili maisha ya Watanzania kwa kuwezesha miongoni mwao kuwa mamilionea.
Swali :Kwa muda mrefu sasa mmekuwa mkidhamini michezo ama sanaa mbali mbali hapa nchini, kwa mwaka huu vipi ?
Jibu : Kwa kweli hakuna mabadiliko, bado tunaendelea kuwekeza katika michezo kwa mapana zaidi, natumia neno kuwekeza kwasababu, sisi tunachokifanya ni zaidi ya udhamini kama ambavyo imezoweleka.
Mathalani, tunapodhamini mashindano ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 12 katika mchezo wa tenesi, maana yake ni kwamba tunawekeza kwa vijana hao ili baadaye waje kupeperusha bendera yetu vema katika jukwaa la kimataifa.
Kumbe basi utaona kuna maeneo ambayo Vodacom tunawekeza kwa vijana, ili kuvumbua vipaji na hatimaye kushiriki kuviendeleza.
Nitakupa mfano mwingine, tumekuwa na programu mbalimbali za kuibua vipaji vya soka kwa vijana wadogo hapa nchini kama vile VGSS, sasa kupitia programu hizo, vijana wenye vipaji wanaibuliwa, baadhi yao wameshasajiliwa na timu za Ligi Kuu ya Vodacom, sasa vijana hao watacheza kwenye Ligi Kuu ya Vodacom ambako huko nako wanatukuta (Vodacom inadhamini Ligi hiyo) hivyo basi utaona jinsi neno kuwekeza linavyokuwa na maana ninayoizungumzia.
Swali : Kwa niaba ya wasomaji wangu, hebu nieleze maendeleo ya huduma yenu ya Vodafone M-PESA mliyoizindua mwaka jana.
Jibu: Labda kabla ya kujibu swali lako, napenda nichukue fursa hii kwa faida ya Watanzania wenzangu kukupa maelezo fasaha ya huduma hii.
M-PESA ni njia iliyobuniwa ya kutuma fedha ambayo inamuwezesha mteja wa Vodacom Tanzania kutuma fedha kwa kutumia simu yake ya mkononi kwa njia ya ujumbe mfupi na mtumiwaji anaweza kuwa mteja wa mtandao wowote ule.Huduma hii tunaitoa kwa ushirikiano na mtandao wa kundi la Vodafone.
Sisi ni wa kwanza hapa Tanzania ni wa kwanza kuanzisha huduma ya aina hii, inapokuja kwenye ubunifu Vodacom Tanzania kwa kweli inaoongoza.
Swali: sawa, kwani njia hii ina tofauti gani na njia nyingine za utumaji wa fedha?
Jibu: Kwa kweli njia hii ni tofauti sana na njia nyingine za kawaida za utumaji pesa,M-PESA ni njia ya haraka, rahisi na salama ya kutuma pesa, kizuri zaidi unapotuma huna haja ya kwenda kaunta ya benki ama ofisi kutuma Pesa, kupitia M-PESA mambo yote yanaishia katika kiganja chako, kwa maana hiyo unatakiwa kuwa na simu ya mkononi na kuwa mteja wa Vodacom, baada ya hapo yote yanawezekana.
Swali: sawa, mbali na huduma ya utumaji wa Pesa, M-PESA ina huduma nyingine zaidi?
Jibu : Ni swali zuri sana hilo, mbali na huduma ya utumaji wa fedha, M-PESA inatoa fursa kwa mteja wa mtandao wa Vodacom kupata mambo mengi mazuri zaidi, kama vile uwekaji wa fedha (DEPOSIT),utoaji wa fedha, kununua muda wa maongezi mbali na hayo mteja anaweza pia kupata taarifa mbalimbali za akaunti yake ya M-PESA , kama vile kujua salio, kubadili na namba ya siri.
Swali: Mteja anajiunga vipi na huduma ya M-PESA?
Jibu: Kujiunga ni rahisi sana, anachotakiwa kufanya mteja ni kwenda kwa wakala wa M-PESA aliyekaribu naye na baada ya usajili rahisi mteja anakuwa amejiunga na huduma hiyo ya M-PESA na sasa anaweza akatuma fedha mahali popote pale Tanzania .
Kwakweli njia hii ni rahisi sana inawawezesha wateja wetu wa Vodacom kutuma fedha kwa wapendwa wao waliko katika kona mbalimbali za Tanzania , ambao hupokea ujumbe wa kujulishwa kwamba wametumiwa Pesa ndani ya sekunde chache mno.
Baada ya kupokea ujumbe huo mtumiwaji huenda kwa wakala aliyekaribu naye na na kupewa fedha zake kwa haraka sana .
Lakini pia huduma hii imeondoa hatari waliyokuwa wakiipata baadhi ya wateja wetu ambao wamekuwa wakikwangua kadi za muda wa maongezi (recharging Vouchers), kwani wakati mwingine anayetuma aliweza kukosea namba ya anayemtumiwa na
Hivyo Pesa kwenda kwa mtu mwingine, kwa kweli hii njia ya M-PESA ni salama zaidi na ya uhakika.
Swali: Sasa hebu rejea kwenye swali langu la msingi
Jibu: M-PESA kwa kweli imekubalika, Watanzania wengi wameipokea na kuikubali kwa kweli, tunashukuru kwamba malengo yetu ya kuanzisha huduma hii yanafanikiwa lakini kubwa zaidi ni kuwafikia Watanzania wengi walioko maeneo mbalimbali hapa nchini.
Hivyo basi ni suala la kujivunia kwamba mtandao wetu umetapakaa sehemu mbalimbali hapa nchini kiasi kwamba hata Watanzania walioko mikoa ya pembezoni mwa nchi yetu wanapata huduma hii.
Kwa niaba ya Vodacom ninawashukuru sana na nina wahakikishia kwamba Vodacom Tanzania itaendelea kuwajali, labda tu kabla sijamaliza napenda niwakumbushe, kuhusu gharama zake, ni rahisi sana , mteja analipia kiasi kidogo ambacho hawezi kuhisi chochote, ni kidogo sana , na yote hii tumefanya ili kuwawezesha wateja wetu kupata huduma hiyo bila kuongezewa mzigo wowote.
Huduma hii iko nchi nzima, kwa kweli ni huduma muhimu sana kwa maendeleo ya nchi yetu, hivyo nina toa wito kwa wateja wetu wa Vodacom waendelee kujiunga na huduma ya M-PESA


yaani meba box akiwa wakala wa m-pesa nadhani fedha atakayokuwa anapata atajutia muda aliopoteza kupiga box.yaani ukiwa na pound 5000 unaenda mafinga pale unakodi kajiofisi stand pale unalipa laki 6 kwa mwaka then unaregista kama agent watu wanatransact mpaka 100m kwa siku mafinga tu wewe unakuwa unacommissio ya 4m kila siku ,sasa kwanini ubebe box au ndio akili nzitooo?
ReplyDeleteBarnabas Lugwisha mbona hujauliza gharama zao za simu, voda kwenda voda ni aghali kuliko tigo/zantel kwenda voda, mi nilihama voda nilishindwa, huduma za jamii hakuna kabisa, zilizopo za kuzuga tu, hiyo vodazone duuuh ndio kichekesho zaidi, anyway ni biashara ila ningekuwa mimi mafuru ningeionea huruma jamii inayonipa mshahara!
ReplyDelete