Ule mpambo wa watani wa jadi unasubiliwa kwa hamu na wakazi wa Washington Metro area na vitongoji vyake sasa kufanyika siku ya muungano, jumapili april 26, 2009  kwenye wanja letu la taifa la zamani (meadowbrook park) na msaidizi balozi mh Switebert Mkama anatarajiwa kuwa mgeni wa heshima.

Mara ya mwisho timu hizi ziliumana vikali june 15 mwaka jana na vijana hao wa msimbazi walisalimu amri ya bao 4-1 dhidi ya mahasimu wao Yanga ambao mwaka huu imezidi kuimarika baada ya kusajili vijana wapya,japo uongozi wa Yanga ulikataa kutaja majina ya usajili huo.

kwa upande wa Simba Mkakile(Bamchawi) yeye ametamba kwamba mwaka huu ni mwaka wao uteja kwa Yanga basi na habari tulizo zipokea hivi punde kutoka ndani ya uongozi wa Simba, kamati ya ufundi imepata mtaalamu kutoka Bwagamoyo ambae watamjaribu kwenye mpambano huo ambao unategemewa kuwa mkali na wenye vitambi ....oops vitimbi.... vingi.

Simba wamepata uzi mpya kutoka kwa mfadhili ambae hakutaka jina lake litajwe.  Jezi hizo zimeipa kiwewe Uongozi wa Yanga unaohangaika kushinda kwa wafadhili kujaribu nao wapate Jezi.

"Sisi hata kama tutakosa jezi, kuifunga Simba ni kama kumsukuma mlevi, sisi tutarudia kile kipigo june 15", mmoja wa viongozi wa Yanga ameiambia globu ya jamii kwa njia ya simu.

 Simba wao wana sema Yanga kuongea jadi yao na kwamba mwaka huu wakichungulia tu ni kipigo cha mbwa mwizi.

Mbali na mpambano huo, kutakuepo na nyama choma na kikombe kwa mshindi.

Wakati huo huo timu ya Bongo United fc,inayo jiandaa na mpambano na Houston Stars may 24,ipo kwenye mazoezi makali chini supa kochi Gharib Latto na mpaka sasa imeisha cheza mechi 4 za kujipima nguvu, Senegal,Malawi,Togo na Nigeria na imeshinda mechi 3 na kutoka droo na Nigeria. 

April 11 itaelekea Nc kwa mpambano wa kirafiki.

Ujumbe kwa Houston,Nyama ikishaingia Buchani Hairudi kua ng'ombe...
Ole wenu Houstoni Mkichungulia tu Hamtoki - kudadadadaaadeki!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. sikukuu ya wajinga michuzi

    ReplyDelete
  2. MKUU WA WILAYA SIKU YA WAJINGA WEKA BONGE LA PICHA YAKO NA MTU MAARUFU KUWA UMEFUNGA NDOA HAHAHA MAANA UONGO WA KUWA DC UMEFAA SANA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...