Picha ya pamoja ya viongozi wa muda baada ya ufunguzi wa
Tanzania Association Reading uliofanyika tarehe 15/03/2009.
Mkutano huo ulihudhuriwa na wawakilishi kutoka International
Organisation for Migration ( IOM UK) akiongea na wajumbe chini, pamoja na Mwakilishi kutoka
University of Edinburgh (Nyerere Scholarship).
Katika Mkutano huo, Viongozi wa muda walichaguliwa ili kuweza kufanya
maandalizi ya Mkutano Mkuu.
Viongozi hao ni kama wafuatao;

Mwenyekiti - Hussein Chang'a
Makamu Mwenyekiti - Bernard Chisumo
Katibu - Salome Buraganya
Katibu Msaidizi - Peter Respigy
Mweka Hazina - Flora Mkonyi
Mweka Hazina Msaidizi - Mbaruku Bendera
Wajumbe wengine wanne ambao ni;
Lulu
Joas
Mohammed Upete
Richard Kibaja

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. HAWA WATU WA READING WANA MATATIZO MAKUBWA.BALOZI KAFUNGUA UMOJA WA TANZANIA NAO WANAFUNGUA UMOJA WAO.KWANINI TUSISHIRIKIANE?
    KUNA CHAMA CHA KINA MAMA TAWA CHINI YA MAMA KILUMANGA.WAO NAO WAMEFUNGUA CHAO PEKEE YAO KINAITWA DIASPORA WOMEN ILI KUSHINDANA NA MAMA KILUMANGA.KWANINI TUSIWE WAMOJA?
    UBINAFSI MBAYA.

    ReplyDelete
  2. TUONESHENI BASI PICHA ZA WAJUMBE WENGINE PIA AU MAJINA AU IDADI YA WANAJUMUIA HAO WA TANZANIA ILI TUWAFAHAMU NASI WADAU AMBAO TUKO UGAIBUNI.

    ReplyDelete
  3. Ndugu zangu,mie nimeishi hapa London tangu enzi ya Malecela,Balozi wote (ukiacha huyu mama Majaar)wamekuwa wanachoka kuvutana na watanzania sababu ya ..ulalamishi,kutokuhamasika,ulaghai(mmoja Mchaga,alichonga barua kuwa anasomeshwa na serikali na kasma yake imechelewa na chuo kinamfukuza masoma,hivyo balozi amkopeshe pesa atarudisha ndani ya majuma 2.Kumbe alikua mjakazi kwenye mashua na aliachwa gati ya hapa London.Akatumbua rupia).Watanzania wengi hatukubaliani hata kwa mema.Rais anasema KASI MPYA,NGUVU MPYA NA ARI MPYA.Reading ongezeni kasi na bidii.Mlikaa kimya muda mrefu hakuna aliye waletea..sasa mnavuta kasi eti mnalaumiwa...Hii ulaya Vituo vikuu viko vijijini...Wa Chaga wanapangana hapa London..Zubaa Uchekwe..
    MBASI Lyamba LA Mfipa KISERU

    ReplyDelete
  4. wizi mtupu

    ReplyDelete
  5. mchango wa tatu hauleweki.Malecela na mwanafunzi analiyeomba asomeshwe ni irrevant.

    swali la msingi kwanini watu wa Reading hampendi kuwa wamoja?watu hao hao utakuta CCM reading ,mara wamefungua jumuiya fulani. yaani kila wakisikia JK yuko UK basi itaundwa jumuiya ya ujanja ujanja.

    Mmewaalika IOM wao kazi yako kuwaondoa overstayers sioni relevance ya kuwaalika hapo.

    Jumuiya hii haina uhai mrefu kwani haina baraka za balozi na sisi watanzania tuliotangaguliza umoja kama silaha yetu.

    wanaotaka scholarships ya Mwalimu Nyerere pitieni www.ed.ac.uk habari zote ziko humo.

    Reading kasi ya credit crunch imekuwa kubwa imeangukia kwenye jumuiya. ila siku hizi serikali ya UK haitoi ovyo GRANTS kwenye jumuiya.

    Tizameni TA na Zenjydar salama wanavyowajibika kwa watanzania bila kujali katoka bara au kisiwani.
    misiba ya juzi hakuwaona wanadai kuwa makada wa chama.

    ReplyDelete
  6. Jamani hapa sasa tutarudi nyumbani hata mzee wa IMO yupo?Buku tatu mfukoni na moto,yayayayas Kambi Nimekupata kaka muulizie huyo mzungu basi

    ReplyDelete
  7. RICHARD KIBAJA (MZEE WA BOZA KWA MNENE)AU NIMEKOSEA !!!

    ReplyDelete
  8. Safi sana Anna..... you go gal we need people like you. Keep up the spirit! Musa

    ReplyDelete
  9. Hallo watu wa Reading:

    Ninasoma University of Reading by distance learning na nitakuja huko baadae mwaka huu;

    Mnapatikanaje? Je ninaweza kujiunga na nyie kwa kuwa ninasoma huko huko? Japo by distance learning?

    Ninajua baadae ningependa kuwashirikisha kwenye mahafari na mambo mengine.

    ReplyDelete
  10. RICHARD KIBAJA NDO UNAKULA KUCHA AU? DUHH HUJAACHA TU...E BANA EE SASA LINI TUNAENDA KUANZA KAMPENI BONGO YA URAISI?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...