baba wa taifa akiteta na rais wa zanzibar na makamu wa kwanza wa rais mzee aboud jumbe (shoto) na makamu wa pili wa rais mzee rashidi mfaume kawawa huku kiongozi a frelimo samora machel akiwa kabana pemebeni. hapa ni katika uwanja wa ndege wa dar ambapo mwalimu alikuwa anasafiri na wengine walikuja kumsindikiza. jaribu kuwaza walikuwa wanaongelea nini..

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Yeah...na kule nyuma namuona Hayati Sokoine...!!Labda walikuwa wanabishana kuwa nani atakuwa mkubwa Nyerere akisafiri...kila mmoja anasema nipe mimi..Nyerere anasema Wewe Jumbe sikuamini..hupendi muungano..na wewe Kawawa Mfupi mno watu hawatakuheshimu..!!

    ReplyDelete
  2. kwa kweli huku ni kupoteza muda na rasilimali za taifa.

    unakuta makamu, waziri mkuu, spika, na mawaziri karibu wote, wanakwenda kumuaga au kumpokea raisi.

    hawa hawatilii maanani muda wao wa kazi. ni utamaduni mbaya ambao tunapaswa kuachana nao.

    ReplyDelete
  3. Jumbe: 'Ndugu Rais kabla hujaondoka malizana kabisa na huyu Mmakonde(Samora) vinginevyo akae na vijana wake kule Nachingwea mpaka urudi'.
    Nyerere: 'Hayo hayakuhusu, maagizo yote nimemwaachia Moringe'.

    ReplyDelete
  4. Kibalaghshia hicho kinaonyesha kuwa JKN alikuwa habagui dini. Watanzania wengi bado hawajaelewa mafunzo ya JKN kuhusu udini na ukabila. Mungu atujaaliye tuelekee usawa, tushirikiane kujenga nchu bila kuandalia paji la uso, kidevu, kichwa wala kifua.

    ReplyDelete
  5. Walikuwa wanaongelea kuhusu ukombozi kusini mwa Afrika.

    Balozi si unakumbuka mwalimu alikuwa mwenyekiti wa nchi tano zilizo mstari wa mbele ( Tanzania, Zambia, Angola, Msumbiji na Botswana)

    ReplyDelete
  6. Jumbe:Mwalimu kawawa anapiga mno overtime kiasi kuwa cheki zake ni kubwa mara mbili za ya kwangu mimi.
    Mwalimu:Nimemwambia Rashidi kuwa kuanzia wiki ijayo apumzike ili operesheni vijiji usimamie mwenyewe kidogo cheki yako iende juu ili msizidiane sana, halafu nikirudi nataka taarifa ya ASP kama wameafiki kuungana na TANU.

    Mdau Msolopogazi USA.

    ReplyDelete
  7. Hapo hata viongozi wenyewe unawaona kwanza wote ni wakweli,pili waaminifu na tatu wanaupendo kwa watu wao ,enzo hizo hapo NENO FISADI LILIKUWA HALIJULIKANI,wala msamiati huo ulikuwa haupo,hapo Baba wa taifa alikuwa anawakabidhi majukumu yake kila mmoja,siyo leo mara jaji mkuu anabishana na spika,mara waziri na katibu mkuu wanabishana kupitia vyombo vya habari ,hakuna kabisa maadili ya uongozi VURUGU TUPU!MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE WOTE

    ReplyDelete
  8. yaelekea Samora alikuwa mtiifu na mnyeyekevu sana R.I.P Comrade ALUTA CONTINUA!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...