Waziri wa  Elimu na Mafunzo Prof. Jumanne Maghembe (katikati) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo wakati akitangaza matokeo ya uchaguzi wa wanafunzi wa kuingia kidato cha tano na katika vyuo vya ufundi kwa mwaka wa masomo 2009. Kushoto ni Kaimu Kamishina wa Elimu Leonard Musaroche na kulia ni Msaidizi wa Waziri Alfred Kilasi. 
-----------------------------------------------
Idadi ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano mwaka huu katika shule za sekondari za serikali na vyuo vya ufundi kwa awamu ya kwanza, imeongezeka kwa asilimia 22.37 ikilinganisha na mwaka jana. 

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe, akitangaza matokeo ya uchaguzi wa wanafunzi hao jana, alisema jumla ya wanafunzi 30,246 waliomaliza kidato cha nne mwaka jana wamechaguliwa kuendelea na kidato cha tano na vyuo vya ufundi, na kwamba kuna ongezeko la wanafunzi 5,389 sawa na asilimia 22.37, ikilinganishwa na mwaka jana ambapo wanafunzi 24,935 walichaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi. 

Akitoa ufafanuzi, Prof. Maghembe alisema mwaka huu kwa awamu ya kwanza wanafunzi 29,478 kati yao wakiwemo wasichana 12,349 na wavulana 17,129, wamepangwa kuingia kidato cha tano katika shule 144 za serikali na wanafunzi wengine 768 kati yao wasichana 11 na wavulana 757, wamepangwa katika vyuo vinne vya ufundi. 

habari kamili

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Hii safi sana matokeo yalipotoka walituambia kufaulu kumeshuka kwa asilimia kadhaa ambazo sizikumbuki. Leo wanatuambia wanaoenda kidato cha tano wameongezeka kwa asilimia kadhaa.

    This means na yeyote mwenye akili timamu atakubaliana nami kuwa ni wizara ndio iliyoongeza aidha kwa kuongeza idadi ya shule au kuongeza idadi wa wanafunzi kwa shule zilizopo. So kwangu mimi heading nzuri na ambayo iko fair ingekuwa "WANAOKWENDA KIDATO CHA TANO WONGEZWA" Vinginevyo tunajidanganya wenyewe na si vinginevyo!

    ReplyDelete
  2. Kuongezeka kwa wanafunzi watakaosoma kidato cha tano ni habari nzuri kwa taifa lakini msiishie kuchekelea tu kuongeza idadi na kusahau kuwa na waalimu wenye vitendea kazi ili wapate elimu bora. Kingine msisahau kwamba hawa vijana wakitoka hapo wanatazamiwa kuingia chuo kikuu cha yunivasiti. Msije kusema eti hamna uwezo wa kuwasomesha kwa sababu ya uchaguzi.

    ReplyDelete
  3. Unajua huu ujinga wa kufikiri kuwa walioingia kidato cha tano ni wale waliofaulu na kuchaguliwa na serikali utaisha lini? Sasa wewe Professor mzima hata hujui kuwa tuko kwenye soko uria na hivyo lazima ku-involve sectors zote including zile za binafsi..mnafanya kuwa elimu ni ile inayotolewa na serikali peke yake? Tunaomba mtupe data za nchi nzima ukizingatia pia wanaoenda shule binafsi hata kama wana division 4 si wanaenda High School? Shida yenu ni nini?

    ReplyDelete
  4. Kwa bahati mbaya kipimo cha wanasiasa ni wanafunzi wangapi wamechaguliwa, shule ngapi zimejengwa, wangapi wameanza darasa la kwanza n.k ndio maana suala hili linaongelewa sana ila UBORA (waalimu, vitabu n.k)hauongelewi na ndio maana watoto wao wanasomeshwa nje!!! Tukiongeza wanafunzi tu bila ubora wa elimu kwa ujumla tunajidanganya, tufahamu kwamba hata shule zenye maendeleo duni huwa kuna mwanafunzi wa kwanza.

    ReplyDelete
  5. Ni muhimu sana mwandishi wa habari hii angefahamisha sababu ya ongezeko hilo.. Lakini hajaelezea... jamani taaluma ya uandishi wa habari imeingiliwa...... Habari inakuwa imepigwa tikitaka

    ReplyDelete
  6. michuzi upo bussy sana leo nini maana kuna ajali ya treni dodoma imeua 15

    ReplyDelete
  7. Ni nje ya mkitadha wa picha...lakini yafaa isomwe:

    By SUKDEV CHHATBAR, Associated Press Writer Sukdev Chhatbar, Associated Press Writer – Sun Mar 29, 11:13 am ET

    ARUSHA, Tanzania – A goods train hit a stationary passenger train in central Tanzania Sunday, killing at least 15 people, a government official said.

    William Lukuvi, the regional commissioner of Dodoma town where the crash occurred, said the accident happened around midday Sunday.

    ReplyDelete
  8. Mzee wa kijiji habari za saa hizi? nilikuwa nauliza kuhusu ajali ya train Dodoma vipi? mbona hutoi taarifa zozote maana sisi wadau wa kwa bibi mkubwa tunaziona kwenye teletext kwenye mlinga(TV), naomba tupe habari kamili maana wasiwasi umetushika reli ya kati wabara tupo wengi tunaotumia reli hiyo na ndugu zetu pia kwenda bush.

    ReplyDelete
  9. MICHUZI KUNA AJALI YA TRAIN IMETOKEA DODOMA! MBONA HUJATUPA HABARI ZAKE????

    ReplyDelete
  10. HIVI NI KWELI IDADI NDIYO INAYOONESHA MAFANIKIO YA KUPASI AU MAKSI NDIZO ZINAZOONESHA KUPASI? JE, NI KWELI DARASA LENYE WANAFUNZI WENGI WALIOCHAGULIWA NDILO LINALOONESHA KUFAURU KWA MAKSI ZA JUU KULIKO LENYE WANAFUNZI WACHACE? NDIYO SABABU HATA TAKWIMU ZETU TANZANIA NI UTATA MTUPU. HAPA WAZIRI ANATAKA TUAMINI KUWA WIZARA YAKE IMEFANYA KAZI KUBWA SANA.

    ReplyDelete
  11. BALA BALA BALA WANGAPI WANAANZA PRIMARY SCHOOL?
    NA WANGAPI WANAFIKA A LEVEL?
    BLABALABLAAAAAAAAAA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...