kuna wadau wamemtuhumu mkuu wa wilaya ya nanihii kwamba oooohh hapigi pamba na kwamba ze fulanzzz ndio ngama yake. haya semenio sasa, hicho nini. japo ni mtumba lakini si pamba jameni? hapo ni sauzi wakati mkuu huyo wa wilaya ya nanihii na mdau wa TBC walipotembela makao makuu ya muda ya bunge la afrika ambalo rais wake ni mh. mama getrude mongella

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. kaka umetoka mchicha sana yaani hapo sasa ndio unaonekana ni mkuu wa nanii ya nanii,isije ikawa ze fulanaz iko ndani ya suti maanake south najua kuna kibaridi flani.

    ReplyDelete
  2. Ze fulanazzz iko ndani..piga ua garagaza..ze fulanazz ndiyo inayoleta bahati na mvuto kwa bosi ili kukubalika kazini na kupandishwa cheo bila sababu! Duh Bro umependeza...sikujua kama ni wewe hadi niliposoma text hapo chini ya picha!! na hukujisahau kuweka mkonozzzzzz!!! Safi sana..wakati mwingine uwe unatuwekea picha kama hizi siyo kila siku fulanazzzzz hadi tumeichoka!!

    ReplyDelete
  3. Mh.... Mnyarugusu umependeza kama yako . Nahisi hiyo pamba ya TBC amekuazima kwa muda, na huyo uliye naye kama siyo yake mkirejea Tanzania inarudishwa studio kwa ajili ya kusomea taarifa ya habari.

    ReplyDelete
  4. kulikoni mikono mbele kama unasubiri mpira wa faulo?

    haaaaaaaaahaaaaaaaa!

    Big Up!

    ReplyDelete
  5. Si matani!! Kitu kimekubali lakini ze fulanaz ndio yenyewe!!

    ReplyDelete
  6. michuzzzii umetoka chiiichaaa

    ReplyDelete
  7. unaonakana kabisa kuwa wewe zi fulana tu, kwani mkao wako huo wa adabu zilizopitiliza, au anon alivyosema ,kama unasubiri direct kiki ya robato carlos, inatia shaka kuwa umezoea magwanda ya aina hiyo. hata hivyo, kajimwili ka kutundikia nguo za aina hiyo, unako. mkeo akiona hii, sahau kuvaaa ze fulana za zizu fashion.

    ReplyDelete
  8. eh!Kaka misupu umetoka chicha!
    kuna taarifa nimezipata kuwa wadau fulani wanataka kufika bei fulanazzzz!!!!!

    ReplyDelete
  9. acheni kufunga kifungo cha chini kwenye suti

    ReplyDelete
  10. duh kaka si mchezo ndani ya pambaz kama hiyo hata anfield unaingia bila wasiwasi wakidhani emile heskey karudi kuomba kusajiliwa tena.hahaha imekutoa kaka si mchezo hata ukiwa na muheshimiwa pinda mtu akiulizwa hapa gordon brown wa bongo ni yupi atasema ni wewe mkuu wa wilaya na nonihino ndio prime minister

    ReplyDelete
  11. Anony wa 1:03 Very funny...kweli michuzi mikonozzz mbele utafikiri anasubiri mpira wa faulo...hiyo mikono huwa inawekwa ili kulinda nanihiiiii!! nashangaa watu huwa hawazibi pua wala macho!! kulikoni...Suti imekubali michuzi (na-lobby ili asikose kuitundika hii comment)

    ReplyDelete
  12. Naomba kuuliza wa Afrika wenzangu.Hivi hiyo kanga,shuka ama kitenge sijui jina lake ambalo wa mama zetu wengi including VIP huwa wanabeba begani kazi yake nini?kama ni pambo je? huwainashonewa kwenye nguo ama inaegeshwa begani? Does it matter kama ina egeshwa left or right shoulder?By the way DC wa nanihii nice mtumba!!

    ReplyDelete
  13. Kafa ulaya ukizijulia zinaokoa sana. Umetoka mchicha mkuu.

    ReplyDelete
  14. Huyo jamaa mwingine hiyo suti ni kafiri, Duh, halafu kama hukujua ni hivi. Kifungo cha chini huwa hakifungwi. Hilo sio shati bali ni koti eboh

    ReplyDelete
  15. mkuu hiyo suti kama ungetinga nayo huku arabuni ukasema wewe ndo praimu minista wa nonihino lazima wangekubali, mtumba umetulia babaake!!

    ReplyDelete
  16. sijui ni kweli nionavyo ama nina makengeza!
    Maana naona kama mheshimiwa umesimama mguu mmoja mbele mmoja nyuma!
    na huyo jamaa mbona anakucheki kiroho mbaya? Ni nani huyo? Au ndoo kakuazima hiyo suti
    Kapicha kangerekebishwa kasoro hizo ndogo ndogo kangekuwa bomba saana!
    Kama huyo msela angetabasamu na wewe mheshimiwa ungesimama sawa sawa, sio kama hivi, shoto kulia kama mgambo
    Vinginevyo, picha hii ni kumbukmbu nzuri tu, HONGERA MHESHIMIWA, maana hata ulipokuja ukerewe mwezi aprili hukupendeza kama hivi.
    Mndengereko, Ukerewe

    ReplyDelete
  17. Lebo mbona haipo?

    ReplyDelete
  18. Kaka Michu umependeza!, na suti yako lakini next time usifunge kifungo cha chini.

    Sasa, ze fulanazz, si uipeleka
    e-bay? halafu some of the money utoe charity? si sisemi kama hutoi lakini najua utapata hela nyingi ukiwa wewe ni mkuu wa wilaya.

    ReplyDelete
  19. Sawa mmependeza, lakini mimi natoa kasoro kidogo. Si vizuri kuvaa suti halafu ukaweka kanga begani.
    Sasa amevaa kiafrika au kizungu ?

    ReplyDelete
  20. Anon 11:15 am.

    Lol!, lol!, smart of you, umeona mbali. True, why uvae suti na khanga begani?, very funny, lol!
    Amevaa kizu-Africa!, interesting!

    You made my day!

    ReplyDelete
  21. Kibabu, hii stailo ya kuegesha kanga/kitenge begani haina kazi maalum, ila ni mavazi ya kinamama zetu wa kitanzania tangu enzi za uhuru wakipenda sana kuvaa mavazi ya kitaifa magauni au vitenge kisha kilemba kirefi kwenda juu ambacho kinafanana na hiyo nguo inayotupiwa begani, na huwa haishonewi inaegeshwa tu, ndio maana mara nyingi utakuta wanapaniapania kila inapoonyesha dalili za kutaka kuponyoka hapo bagani, zaidi huvaliwa upande wa kushoto, ingawa si muhimu ili kukwepa au kuupumzisha shughuli nyingi zinazokabiliwa na mkono wa kulia,zaidi ya hapo mara nyingi huvaliva na kinamama si sana kwa wasichana, nakumbuka na kina baba walikuwa wanavaa mashati ya vitenge yasiyo na ukosi,na stailo hiyo ilikuwa inaitwa bunge, na baadhi wakishavaa hilo bunge wanashika na usinga mkononi, ila siku hizi ukidiriki kutembea umeshikilia usinga mkononi hapo hapo watajua wewe ni mganga wa kienyeji au unatambika.

    Nakubali kuwa hapo mh. kachanganya kidogo suti na utamaduni wetu wa kanga.

    ReplyDelete
  22. Shukrani sana anony wa March 23 10:31 nimekuelewa vizuri thanks again for taking your time kunifahamisha.God bless you

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...