WADAU WAPENDWA,

KUNRADHI KWA KUINGIA HAPA SAA HIZI. HII NI KUTAKA KUTAMKA KWAMBA MDAU WA MILIONI 6 ANANUKIA MAPEMA KULIKO NILIVYOTARAJIA. YAANI ENDAPO MAMBO YATAKUWA MSWANO NA MOLA AKIJAALIA, TUTAMPATA MDAU WA MILIONI 6 HATA KABLA YA MWEZI WA SABA A.K.A JULAI. NA PIGA UA LAZIMA AONDOKE NA KITITA KINONO.

TAYARI NIKO MBIONI KUSAKA MFADHILI ATAYETOA DONGE NONO ZAIDI YA AWALI KWA MDAU ATAYEBAHATIKA KUWA WA MILIONI 6, KWANI ILE ZAWADI YA DOLA 500 NAONA KAMA HAITOSHI VILE. HIVYO WADAU KAENI MKAO WA KULA, NA TUOMBE MOLA MFADHILI APATIKANE HARAKA. LA, KAMA AKIKOSEKANA ITABIDI NIJIPIGEPIGE MIE MWENYEWE ILI ANGALAU SAFARI HII MDAU WA MILIONI 6 AONDOKE NA DOLA 1000. AU VIPI?

MDAU USIPATE SHIDA. KUTAKA KUJUA NAMNA LIBENEKE LINAVOKWENDA, ANGALIA CHINI YA GLOBU YA JAMII UPANDE WA KUSHOTO CHINI NA SOMA TARAKAMU ZINAKUELEZA NINI. 
NAOMBA KUWASILISHA

-MICHUZI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Najua Michuzi utashinda wewe au mwanao mnyamwezi buku?

    ReplyDelete
  2. Mjomba acha kubania breaking News za Stanford Brigde!

    ReplyDelete
  3. Mimi nimesahau wadau, inatakiwa iweje ili niweze kuwa mshindi wa hizo milions

    ReplyDelete
  4. Tukumbushane jinsi ya kula hizo million za michuzi sizizo na mwenyewe

    ReplyDelete
  5. Achakubana wewe Michuzi vipi? elekeza watu jinsi ya kushiriki,,sasa unaposema tuende chini mbona na kule hakuna hata maelekezo,,au hili shindano ni watu maalumu,,weka wazi haraka

    ReplyDelete
  6. Mkereketwa Yombo VitukaApril 15, 2009

    KAKA, BALOZI WA NANIHII, TAFADHALI SANA, NAOMBA GLOBU YA JAMII INIPIGIE KAMPENI ILI KUUTWAA UKUU WA WILAYA YOMBO VITUKA ILI NIPAMBANE NA MAFISADI KAMA US-GLOBBER NA FISADI ALUMNI MA MUZUMBE UNIVERSITY ECONIMCS PETER NALITOLELA

    ANGALIA WASOMI BANDIA WANAOJILETA KWENYE GLOBU YA JAMII NA KUJIITA WATAKATIFU; US BLOGGER NA PETER NALITOLELA AMBAO WANAKASHIFU SHULE ZENYE HADHI ZA OKSFODI NA MUZUMBE. WASIJE KUAMBUKIZA UGONJWA WAO KWA GLOBU YA JAMII.

    HII TUZO ITALIWA NA MAFISADI AMBAO KAZI ZAO NI KUTANGAZA CHUKI. SIYO KAMA DR. SHAYO NA MT. YOHAANA MASHAKA AMBAO WANATANGAZA UPENDO NA UZALENDO.

    KWA HIYO MIMI KAMA MZALENDO NATOA TAMKO KWAMBA HAWA WASALITI WALAANIWE

    MIMI KAMA MKEREKETWA NA MPINGA UFISADI NA USENENE NAMBA WANI, BADO NAWAPIGIA DEBE MWANAHRAKATI GENIUS, RAIS MTAJARIWA 2015 MT. YHANNA MASHAKA NA WAZIRI MUKUU DR. HILDEBAND SHAYO WA KULE RONDONI NA MACHO YA MUNENE JK JANUARY MAKAMBA

    LICHA YA KUSAKAMWA NA WAOSHA VINYWA KUTOKANA NA LUGHA YAO, NIMEPENDEZWA JINSI UNAVYOCHAMBUA MAMBO HASA KUHUSU MAENDELEO YA TAIFA LETU.

    NADHANI MIMI NITAIPELEKA HII MAKALA KWA WABUNGE WETU KULE DODOMA
    MHESHIMWA RAIS MTARAJIWA, TUNAKUUNGA MKONO, NA TUTAZIDI KUKUOMBEA DUA, ILI MUNGU AKULINDE DHIDI YA MAADUI AMBAO PIA UMEONYESHA UNA UPENDO NAO KAMA VILE US- BLOGGER

    MZEE WA PAMBA, JAKAYA MRISHO KIKWETE TUNAMPA KURA TENA, 2010 KWA MASHARTI KWAMBA LAZIMA ATUPE MIBARAKA YAKE KWA AJILI YA 2015.

    MZEE MZIMA, MZEE WA BAGAMOYO, MZEE MTANASHATI, MZEE WA PAMBA, TUNAOMBA UWABARIKI WANAO.

    MBARIKI MT. YOHANNA MASHAKA AMABYE PETER NALITOLELA NA US-BLOGGER WA OKSFODI ANAMUWANGIA, MBARIKI, SHAYO, MBARIKI JANUARY PAMOJA NA RIDHWANI

    Mh. MT. Mashaka, January, Dr. Shayo na Ridhwani. Kwa hiyo naomba msinisahau ifikapo 2015 HAMNA MSHABIKI MWINGINE NCHINI TANZANIA ZAIDI YANGU .

    ZIDUMU FIKRA ZA MZEE WA PAMBA JK
    ZIDUMU

    KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
    KIDUMU

    KIDUMU FIRKA ZA LAIS MTARAJIWA 2015
    ZIDUMU

    ZIDUMU FIKRA ZA MAKAMU 2015
    ZIDUMU

    USGLOBBER NA PETER NALITOLELA WALAANIWE
    WALAANIWE

    MKEREKETWA, YOMBO VITUKA !!!!
    -----------------------------------
    Dakika 30 za Internet Café Zimekwisha

    ReplyDelete
  7. Naomba kama unaweza ufafanue zaidi jinsi libeneke linavyokwenda.
    Nikiwa naangalia kompyuta chini upande wa kushoto kwangu sioni namba za watumaji habari zinavyoongezeka. Naona Michuzi, siku,tarehe...na mwisho kabisa kulia namba za maoni zinavyoongezeka. Au unamaanisha mtoa maoni wa milioni sita? Na kama ni hivyo mtoa maoni kwenye habari ipi, hii au zingine, maana kuna zaidi ya moja.

    ReplyDelete
  8. Bro Michuzi wewe miyeyusho. Kifuta jasho changu cha mshindi wa tatu mpaka leo hujanitumia wakati mwenyewe ulitangaza nikutumie ushahidi. Safari hii mwe! sikeshi tena kusubiri hiyo zawadi.

    Mdau
    Cardiff

    ReplyDelete
  9. Kuhusu hizo namba, ni idadi ya watu wanaofungua mtandao wako. au let us say those who browse your website. for now is 5595330

    ReplyDelete
  10. Daah... mi nahisi kuchanganyikiwa sasa, mwenye blog yake anasema tarakimu ziko upande wa "kushoto", mi kwangu hapa inanionyesha ziko upande wa "kulia" ndo nahangaika hapa kuzitafuta manake nahisi za upande wa kushoto zimekuwa transparent.

    ReplyDelete
  11. Pole Bro Mithupu, halafu nilitaka kukurekebisha namba ipo kulia na sio kushoto ya blog yako kama ulivyosema

    ReplyDelete
  12. ITAKUWA INAFURAHISHA KAMA
    MDAU WA MILLION 6 APEWE MILLIONI 6
    MDAU WA MILLION 7 APEWE MILLIONI 7
    TUENDELEE HIVYO HIVYO MPAKA COUNTER ISIMAME.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...