Mtandao wa JamiiForums wakati ukiendelea kukupasha kinachoendelea nyumbani huku ukikupa fursa ya kutoa maoni yako unakupa fursa ya kipekee kuweza kuburudika mtandaoni.
JamiiForums (zamani JamboForums) kwa sasa ina miziki ya rika mbalimbali na za kila aina. Dhamira ya JF si kujitangaza kupitia Michuzi Blog bali kukufahamisha kuwa kuna zaidi ya kile kilichokuwepo mwanzo.
Kuburudika chagua aina ya muziki uupendao:
au
Na endapo utakumbana na tatizo usisite kuwasiliana na wahusika kwa kubonyeza CONTACT us.
Wenu
Invicible


sijui kaka utaiweka hii au kuitupia kapuni lakini lazima niseme tu....Watu wengine wanahitaji communication skills......hiii sentensi ina maana gani?????? Dhamira ya JF si kujitangaza kupitia Michuzi Blog bali kukufahamisha kuwa kuna zaidi ya kile kilichokuwepo mwanzo. sasa kama sio kutangaza ni nini?
ReplyDeleteSiku hizi watu wakija na matangazo yao waambie possibility ya wewe kuedit tangazo ipo. Ni hayo tu
Nakuunga mkono Mdau wa kwanza.Watanzania wengi tunaongea kiswahili kisichofasaha(Grammatically) tunaandika/kuengea staili ya "bora liende" ili mradi ujumbe ufike.Cha ajabu mtu akikosea kuandika/kuongea Ung'eng'e tunamcheka.Cha kwanza tujali na kupenda kuongea kiswahili fasaha sio kuburuza buruza.
ReplyDelete