Wawili wawili: Wachezaji wa Michigan State Marquise Gray (shoto) na Raymar Morgan walipewa tenda ya kula sahani moja na Hasheem Thabeet siku ya nusu fainali yao wikiendi ilopita ambapo timu ya UConn ilitolewa kwa mbinde.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. Taswira kali sana hiyo.
    Hivi ndivyo ndugu zangu wa Jangwani mlivyopaswa kuwalia dipu Flavio, Barakat na Aboutrika.

    ReplyDelete
  2. Kumbe mguu wake umejaa sumni.

    ReplyDelete
  3. Ebwana libeneke la taswiraz nimelikubali hapa, Duh.... Huyu jamaa aliyefotoa hii ni soo..
    Big up sana Hasheem Nilicheki Game replay jana ESPN, sio siri mkuu, unajitahidi sana.. Wakilisha kwa sana tu Kaka...
    mamilioni ya NBA yaleeee yananukia.

    ReplyDelete
  4. Hii kaka inaitwa "libit",ha ha ha ha ha ha,Duh!!

    ReplyDelete
  5. NICE PIC. MATAYARISHO YA NBA KUKUTANA NA 320 POUNDS ZA ALL MUSCLES SHAQUILE ONEAL, LOL.

    ReplyDelete
  6. Bwana Issa, kwanza nakupongeza kwa shughuli za kila siku kutuletea uhondo wa katika blogspot yako, pili napenda kukufahamisha kuwa mimi ni mfuatiliaji mzuri sana wa michezo hususani kikapu, Thabeet katika mechi hii ambayo nilikuwa naiangalia moja kwa moja alichemka vibaya sana Issa, hapo jamaa walikuwa wanafunga na hao walimzuia tu ili asichukue "rebound" jamaa apewe tu moyo lakini kwa kiwango chake hastahili kabisa sifa unazompandikiza, sina chuki binafsi ila napenda kuweka hili wazi. tunatakiwa kuwapa moyo wanamichezo ili waongeze jitihada na siyo kuwapa sifa ambazo hawana.

    Ni Hayo Tu.

    ReplyDelete
  7. ...wewe hater wa 11.36 seems ni wivu tuu au kutoelewa game,hivi wataalam wote wa kikapu waliompa Hasheem thabeet Big East player of the year na defensive player of the year bila kusahau ni all first American team (wako watano tuu marekani) yaani achievemnet zote hizo huzioni? au unataka kusema kapendelewa maana waswahili hamkawii kusema hivyo...kwa taarifa yako thabeet ataingia NBA na ni projected top five na haitaji support yako.wewe endelea na kutoa maneno yako ya uzushi tuu lakini watu wanasonga mbele,yaani roho mbaya tena kwa mbongo mwenzenu sijui zitawafikisha wapi?hasheem ni one of the best B/baller kwa sasa katika NCAA ndio maana pia alikuwa ni finalist wa NAISMITH award iliyochukuliwa na Blake Griffin juzi,subiri mwenzako by Nov atakuwa NBA na millions of contracts huku wewe na wivu na roho mbaya na uzushi wako sijui utakuwa wapi unaliwa na mbu au kupigwa baridi Alaska!

    ReplyDelete
  8. Mdau wa 11:36 naungana na wewe mkono kabisa, Mi pia niliangalia Game live, kweli Hasheem hakucheza kwenye kiwango cha kutosha na inaweza kuwa ni sababu ya wao kutolewa, kwasababu kocha alimpa nafasi sana, time out hakupewa nyingi may be alitegemea atabadili mchezo, lakini alipoanguka na kuumia kwa kutulia mgongo ndio ikawa kabisaa, baada ya watu wa physio kumkanda kanda ndio kidoogo tukamuona anainuka lakini hakucheza tena..
    pole Hasheem Lakini kazi bado kubwa, Ongeza bidii sana, Utatoka Sana Mtu wangu, Taifa linakuombea dua sana tu.
    Mdau UK.

    ReplyDelete
  9. Mimi siyo mtaalam wa huu mpira lakini mbona wamembana sana inaruhusiwa hii? Almost wanaonekana wamemshikwa kwa pamoja technically. Big up our boy...we looooove you ... keep up with your studies and good game...

    ReplyDelete
  10. Watu wenye roho za kichawi ni hatari sana (kama anony April 06, 2009 11:36 PM), jihadharini nao na hata makwenu msiwakaribishe! Hasheem (7'3" center) amechaguliwa kwenye All American 2nd Team, NBA draft top 10 ndani. Sisi watanzania wapenzi wa basketboli tunapata faraja kubwa sana! Kila la kheri Hasheem, mola akulinde na mahasidi wenye kuhusudu!

    Mdau Boston

    ReplyDelete
  11. Jamani huu ni uwanja wa maoni.Kila mtu ana uhuru na haki ya kusema kile anachofikiri kuwa ni sahihi.Hakuna haja ya kurushiana matusi na kejeli.Kama huna vigezo vya kupinga hoja kwa nini usinyamaze tu?Point inafika ki-urahisi bila jazba wala kashfa.
    Mdau kachangia hoja yake,watu wanakuja huko na jazba zao-ooh hater,mchawi!!!
    Thabeet anacheza vizuri lakini sifa ni kubwa kuliko kiwango chake.Ukweli ni kwamba anatumia vizuri umbo lake jambo ambalo mtu yeyote mwenye akili na umbo kama hilo anaweza kufanya.Na ndio maana katika hiyo picha wanamminya chini kwa sababu wanajua vingenevyo hawawezi kumdhibiti.
    Tusiwe wafuata upepo wa vyombo vya habari.Angalia mwenyewe na utoe mawazo yako.
    Nadhani dhumuni la maoni ni kujenga.I hope anapata nafasi ya kusoma maoni haya ili apate mitazamo tofauti ya watu na achambue kati ya mchele na pumba.
    Sasa unapomsema mchangiaji mchawi,hito inamsaidiaje Thebeet?
    I said it before,sidhani kama yuko tayari kwenda NBA.Anahitaji kuwa "mobile" kwenye court na siyo kutegeshea rebounds na ku-dunk tu,na hiyo inahitaji pumzi na stamina.
    Wote tunamtakia mema tu.Kushinda au kushindwa kwake hakubadilishi maisha yangu au yako!!
    Sam.

    ReplyDelete
  12. this is too much now, i got the feeling him and his friends are the one keeping posting these stories. Enough is enough, we know who he is, we know he is good player what we don't want is stupid post about him every week.

    ReplyDelete
  13. wewe mteteaji wa april 07, 2009 2:12 ukiwa wewe mwenyewe umesema all first American team (wako watano tuu marekani) huoni kama kigezo kilichotumika ni finyu sana? kama wako watano tu sio number kubwa ya wachezaji ya kuweza kujigamba kuwa the best. kweli anajuwa kucheza basketball lakini there are too much binzari in the curry if you ask us!!!!!

    ReplyDelete
  14. Mchangiaje wa boston april 07, 2009 7:25 am, hebu tueleze ni faraja gani uipatayo? unless kama kuna maana nyengine imeibuka ya neno faraja ningelipenda kufahamu na kujuwa mafanikio ya hasheem yanakupaje wewe faraja.

    ReplyDelete
  15. faraja ni kubwa kwa maana kwamba Watu kibao ukiwaambia umetoka Tanzania wanakuuliza ndio wapi? hata ukiwaambia East Africa kesho yake wamesahau. Haseem anatangaza jina la nchi kama kina Mutombo. Anacheza kwa manufaa yake binafsi na brand ya nchi inanufaika. Nadhani unaelewa nikisema brand ya nchi. Brand inayojitangaza ndio inayofahamika. Mfano wanariadha wa Kenya wanashiriki sana kwenye Marathon. Mara nyingi Kenya au Ethiopia ndio wanashinda. Hivyo inafanya urahisi kuuza kahawa ya Kenya au Ethiopia in international markets kuliko ya Tanzania hata kama ya Tanzania ni nzuri zaidi inakuwa kwenye competitive disadvantage. Mtu akisema anafarijika na jitihada za Hasheem jaribu kuumiza kichwa utaelewa kuliko kumshambulia mtu. Nakuunga mkono mtu wa Boston. Hata kama tuna Tanzanite Serengeti na Mlima Kilimanjaro hivyo havitoshi kujitangaza.

    ReplyDelete
  16. Anony April 7, 12:28
    Inawezekana kwamba yeye Hasheem mwenyewe ndio anayepost kwenye hii blog, au maybe ni marafiki zake, So what? still doesn't mean that haters shud start spittin' fire for no reason. he just wants to share with all of us, who usually claim to be "supporting him".. sasa hapa unashindwaje kuendelea kum-support? au ulitaka wewe ndio uwe umeleta hii post maybe then ungemkubali mtoto wa watu na juhudi zake. Kumkosoa haikataliwi na wala sio vibaya, lakini lazima ujue unakosoa nini? Je wewe unaijua b.ball vizuri? unajua sheria za mchezo huo? if Yes, then give him constructive criticism, na usivunje sifa wanazompa wengine. he deserves both constructive criticism and praise!!!
    I give him 2 THUMBS way way way up for his improved game. His stats are looking up good, and that's how it shud be.


    ukipendabogapendanaualake.blogspot.com

    ReplyDelete
  17. mbwegelembwegelApril 07, 2009

    Dogo huyu anaenda NBA , ingawa bado haiva ipasavyo kama wapambe wake wanavyo mpamba.
    Dogo ongeza juhudi , usivimbe kichwa mapema.

    ReplyDelete
  18. MIMI NAMUUNGA MKONO MDAU WA 11;36. HUSKIES WANA NYOTA AITWAYE A.J. PRICE PIGA UA KOCHA JIM CALHOUN HAWEZI KUMWACHA NDIYO ROHO YAKE.
    WANAMTUMIA HASHIMU (HASHEEEM) INAPOBIDI. JAMAA TUMPE MOYO NA JITIHADA ZAKE ZISIPAKWE SANA MAFUTA KWANI ATAJISAHAU NA KUJIONA KWELI AMESHAKUWA MUTOMBO NAMBA MBILI!!
    MHH! MICHUZI FATILIENI KIDOGO HABARI ZA MCHEZO HUU NA MUWE MUNA BALANCE NA SIYO KUTUJAZIA TU.
    KWA KWELI TIMU YAO KIBOKO NA INAHESHIMIKA KWENYE HIZO COLLEGE COMP. NA ZOTE HIZO NI JITIHADA ZA HIGHEST PAID COACH WALIYENAYE, CALHOUN.
    NDIYO MAANA WALIPOFANIKIWA KUINGIA NUSU FAINALI KILA, ZONGO KIABO ZILIANZA PAMOJA SHUTUMA KADHAA ILI KUWACHANGANYA WANA HUSKIES.
    TUKIACHA HAYO, HASHIMU ATAENDELEA VIZURI KAMA ATAFANYA JITIHADA NA KUCHUKUA MAONI YA BOTH SIDES; MAZURI NA MABAYA AMBAYO YATAMTIA CHACHU NA KUFIKIA KIWANGO CHA JUU.
    HATA PRE MATCH PRESS CONFERENCE CALHOUN HUWA ANAWATUMIA WACHEZAJI WAKE NYOTA, A.J. PRICE, JEFF ADRIEN LAKINI SIJAWAHI KUMWONA NDUGU YETU HASHIMU. HIYO INAAMANISHA BADO ANAJIFUNZA NA YUPO KWENYE KUNDI LA JUNIORS NA SIYO SENIORS. KIJANA BADO MDOGO HUYO INGAWA NI MKUBWA KWA MACHEDA...KIWANGO BABA

    ReplyDelete
  19. mdau wa 2:12AM April 7, nadhani unatakiwa kwanza kusoma na kuelewa badala ya kukurupuka na kujibu, siko kwa ajili ya kujibizana hapa, napenda tu ufahamu kuwa yale yalikuwa maoni yangu na ni mtazamo wangu kuhusu Hasheem Thabeet Manka na game. Mimi nilisema nilichokiona katika mechi hii na siyo kupitia picha ya issa au delayed match uliyoiona wewe, mimi niliona game live na nilichosema ndicho nilichokiona, Thabeet anajitahidi kuwa katika game ila sifa anazopewa ni kubwa mno kulinganisha na kiwango chake. kwa mwendo huu tunaoenda nao tutashindwa kumsaidia mwenzetu badala yake tutamuangamiza kwani ataona tayari keshafikia kiwango kumbe bado sana, anahitaji mazoezi sana na pia asisahau ana shule. Ninamtakia kila la kheri Hasheem acheze NBA ila siyo mwaka kesho kama mnavyosema kwa kweli. bado sana.

    Ni hayo tu.

    ReplyDelete
  20. Hi ,hata kama kiwango ,bado msimvunje moyo ,jamani hata hivyo atakuwa kapata elimu ya bure aijarishi kama ana kiwango. sio sawasawa na nyie wabeba mabox ,na kwa taarifa yenu wame draft ,NBA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...