
Wataalamu wa Iran katika kituo cha utafiti wa kisayansi cha Royan mjini Esfahan, wiki hii wamefanikiwa kuzalisha mbuzi wa kwanza kwa njia ya Cloning katika kituo hicho.
Kuzaliwa kwa mbuzi huyo kwa njia ya cloning kunafuatia silsila ya utafiti wenye mafanikio wa wanasayansi wa Kiirani wa kituo cha Royan, na ni baada ya huko nyuma, kuzaliwa kondoo kwa njia hiyo hiyo ya cloning ambaye alipewa jina la Royana.
Mkuu wa kituo hicho, Dr. Mohammed Hossein Nasr Esfahani, amesema kuwa mbuzi huyo wa kike alizaliwa mapema siku ya Jumatano na amepewa jina la Hana.
Lengo la utafiti huo wa ku-clon wanyama limetajwa kuwa ni kuiwezesha Iran kupiga hatua katika utafiti wa kitiba, likiwepo suala la kuwatumia wanyama waliozaliwa kwa njia hiyo katika kutengeneza antibodies dhidi ya magonjwa mbalimbali.
Mkuu wa kitengo hicho aidha amesema lengo kubwa lililowapelekea kufanya cloning ya mbuzi huyo ni kumtumia katika kutibu wagonjwa wa mshituko wa moyo au stroke.
Hadi sasa ni nchi chache tu duniani ambazo zimefanikiwa kuzalisha mbuzi kwa njia wa cloning . Nchi hizo ni Marekani, Uingereza, Canada, China pamoja na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Kwa maelezo zaidi ponyeza …
http://www.google.com/
Shukran,
Mdau Tehran.


Mbona ana makengeza mbuzi mwenyewe! LOL
ReplyDeleteDa! Ebwana ndioooooo, Mbuzi anapozi la kufa mtu.
ReplyDeleteMdau Davey
wametoa mbuzi gay
ReplyDeleteNA DUBAI PIA AMEZALIWA CLONED NGAMIA ANAITWA INJAZ, TUWEKEE NA HIYO PIA BASI.
ReplyDeletehilo ni jini la kiiran sio mbuzi
ReplyDeleteMhhh, huyu mbuzi niaje? Mbona jicho lake linaita kinamna!!!
ReplyDeleteCLONING NDO NINI JAMANI??
ReplyDeleteTUELIMISHANE UMU