RAIS Jakaya Kikwete amebadilisha vituo vya kazi kwa Wakuu wa mikoa 11 ambapo mkuu wa mkoa wa Dodoma William Lukuvi atakuwa Mkuu mpya wa Mkoa wa Dar es Salaam na Abbas Kandoro anakwenda Mwanza.
Taarifa iliyotolewa leo na Ofisi ya Waziri Mkuu ikiwa imesainiwa na Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Aggrey Mwanri, lengo la mabadiliko hayo ni kutoa msukumo zaidi wa shughuli za serikali.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dk. James Msekela anahamia Dodoma.Wakuu wa mikoa wengine waliobadilishwa ni Enos Mfuru kutoka Kagera kwenda Mara, Issa Machibya kutoka Mara kwenda Morogoro, Said Kalembo kutoka Morogoro kwenda Tanga, Mohamed Abdulaziz kutoka Tanga kwenda Iringa na Amina Mrisho kutoka Iringa kwenda Pwani.
Wengine ni Dk. Christine Ishengoma kutoka Pwani kwenda Ruvuma, Monica Mbega kutoka Ruvuma kwenda Kilimanjaro na Mohamed Babu kutoka Kilimanjaro kwenda Kagera.
Mabadiliko hayo ya wakuu wa mikoa yamefanyika wiki tatu tangu Rais Kikwete afanye uteuzi wa wakuu wa wilaya kwa kuteua wapya 15
Let the Musical Chairs begin...
ReplyDeleteLANGU MOJA MABADILIKO HAYA KWA SABABU YA UTENDAJI MZURI KTK MIKOA YAO AU MBAYA? KWA MTAZAMO WANGU NAONA SERIKALI YETU INA KAZI YA KUBANDIKA NA KUBANDUA NIA HAYO TU.
ReplyDeleteJE WANAJUA NI NINI KAZI ZAO HUKO WAENDAKO? mdau.
mwanza mbona tunaonewa hivi anayetoka na anayeingia wote sawa. Mwanza anatakiwa arudishwe yule ambaye yuko Rukwa. OLE NJOOLAY
ReplyDeleteANGEWAHAMISHA WAKUU WA MAHAKAMA,LABDA TUNGEONA HUKUMU YA UFISADI.
ReplyDeleteIkiwa 1+2=4 ninauakika ata 2+1 Jibu litakua 4 tu.Siasa za mwaka47,tunaendelea nazo.
ReplyDeleteMbeya?????!!!!!
ReplyDeleteWIZI MTUPU.
ReplyDeleteHivi hakuna RC anayeiweza Iringa? Nadhani huyu anayekuja ni wa tano tangu 2006 - maRC watano katika miaka mitatu!
ReplyDeleteTui nalio, veyaa!
Yaani katika mabadiliko yote haya mbeya hajaibadilisha? kweli kuna mpango wa kuuharibu mkoa wa mbeya. najua michu huwezi kuiweka hii ila habari ndio hiyo.
ReplyDelete