JK anapokea zawadi ya kapu kubwa la asili kutoka kwa bi Leseko  Lekaukau,afisa muuguzi mwandamizi wa hospitali ya kumbukumbu ya Letsholathebe II iliyoko katika mji wa Maun nchini botswana katika siku ya pili ya ziara ya rais kikwete nchini humo 
"NIMEPENDEZA"? JK  anamuliza bi Leseko Likaukau,afisa muuguzi wa hospitali mara baada ya kumkabidhi rais zawadi ya kofia wakati wa sherehe ya uzinduzi wa hospitali hiyo huko Maun nchini Botswana
JK na mwenyeji wake Luteni  Jenerali  Seretse khama Ian khama wa botswana wakishangilia mara tu baada ya rais kufungua rasmi hospitali ya kumbukumbu ya  Letsholathebe  II yenye vitanda zaidi ya 200 iliyojengwa mjini maun huko botswana
 
 JK na wenyeji wake wakila nyama ya kuponda ya asili iitwayo Setswa. Nyama hiyo hupikwa na kuliwa na wanaume pekee. Kulia kwa JK ni Kgosi au chifu Tawana Noremi na aliyekaa shoto kwa Luteni Jenerali Khama ni naibu waziri wa botswana mh. G. Matlahabaphiri.
 

JK na wenyeji wake wakiwa chini ya mti ambao hutumika na wazee wa jadi wa Botswana kwa ajili ya kupanga na kutoa maamuzi mballimbali katika jamii yao ijulikanayo kama Kgotla (bunge). JK amesharejea nchini jana jioni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. mmh mbona kazi wanaume bado wana mambo hayo ya uroho uroho kama zamani baba wa nyumba ndo mlaji paja la kuku na firigisi ole wako zitoweke

    ReplyDelete
  2. mtume JK wetu hayo ni makende ndio maana wanakula wanaume watupu mwee,sio steki

    ReplyDelete
  3. Rais wa Botswana ni kichwa mtu niliwahi kumsikiliza ana malengo na mikakati kabambe. halafu ni msela kwa hiyo ombeni namba

    ReplyDelete
  4. mh.jk umeulizia hiyo nyama kama ni halal?usijilie tu wewe ni muumin

    ReplyDelete
  5. Jamani mie nimeishi Botswana kwa miaka kadhaa. Ni kweli Setswa ni chakula ambacho huandaliwa na wanaume. Lakini hiyo ilkiwa zamani. Nimehudhuria funerals kibao za Watswana, Setswa inaliwa na kila mtu sasa hivi, hata ukienda supermarket, ipo inauzwa. Kwa hiyo habari ya kwamba inaliwa na wanaume tu, hasa katika karne hii ni misleading!

    ReplyDelete
  6. Mhe Michuzi...Seswaa (siyo setswa) ni nyama inayoliwa kwenye sherehe..iwe msiba, harusi n.k.. Kwa uzoefu wangu sijawahi kufika kwenye sherehe yeyote nikakuta kwamba eti seswaa inaliwa na wanaume tu. Hiyo siyo kweli kabisa. Hata watoto wanakula. It is really delicious. Hasa ukitilia maanani kwamba nyama Botswana ina taste tofauti sana na ile ya TZ. Karibuni Botswana!

    ReplyDelete
  7. majiko yanayoonekana picha ya chini kabisa yanaitwa BUSH BABY ni maarufu sana nchi za kusini hasa Botwana na Namibia

    ReplyDelete
  8. Rais amerudi... tumbo vipi Mh. rais halisumbui?

    ReplyDelete
  9. Angalia jinsi Jk na mwenzake walivyokula "Boots" babkubwa!

    ReplyDelete
  10. ndio mdau kumbe na wewe umezisoma hizo boots eh babkubwa

    ReplyDelete
  11. JK mshkaji sana,poa sana!!

    sasa na apo chini ya mti na "suti za western vipi"

    safi sana kaenda zindua hospitali botswana jina linabaki pale.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...