kituo cha daladala cha mtaa wa pramukhswami street, dar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. Dugu zangu iko na furaha kuba kutoa jina ya hindu kwa mitaa yetu.

    ReplyDelete
  2. Ina maana wamekosa majina ya kibantu? Hivi wabongo tuna bongo au chawa wamejaa ubongoni.Ndiyo nchi yetu ina hawa wahamiaji lakini sio kila kitu kichukuliwe na wao.Pambaf Jiji.

    ReplyDelete
  3. Utajuaje kuwa ufisadi ni halali? Unamiliki beach, unabadili jina la mtaa na kuweka lako!

    ReplyDelete
  4. Hii tabutupu sisi watu wabara sijui tutasomaje hayo majina

    ReplyDelete
  5. aah michuzi unanikumbusha mbali mitaa hiyo ya Haidari Plaza-posta suremender kwa wanjanja enzi hizo sio mchezo.
    mdau Manchester

    ReplyDelete
  6. Eh bwana ndio,

    hichi ni kituo cha muda ama?
    Na kituo chetu cha posta mpya bado kihai au ndio hichi mbadala wake?
    Tupe data kaka.

    -- Mtanzania daima.

    ReplyDelete
  7. Haki kabisa, nasikia tamu, siku mingi nataka ona nyumbani yangu kuna ile taa moja ndefu na jina la baba mke yangu, napata ushungu kabisa ona siku mingi sirikali haijui kama sisi iko tajiri kuliko Juma.

    ReplyDelete
  8. Ndugu Michuzi au mdau ye yote, unaweza kujua kwa hakika ni nani kati ya serikali ya jiji/mitaa na serikali kuu huwa anafanya uamuzi wa mwisho kuhusu ubatizaji wa mitaa? Au ni utaratibu gani rasmi tunaoufuata katika kubatiza majina!
    ninatanguliza shukrani

    mlalahoi

    ReplyDelete
  9. haya basi bandikeni majina za wa christo au warabu...kama iki leta furaha!!!

    ReplyDelete
  10. aah michuzi unanikumbusha mbali mitaa hiyo ya Haidari Plaza-posta suremender kwa wanjanja enzi hizo sio mchezo.
    mdau Manchester

    ReplyDelete
  11. Jamani hatutukani wala hatukalifishi jina hilo lakini jina hilo linatoka wapi? mbona tuna watu wengi nchini kwetu na wengine wapo nje ya nchi ambao wamechangia nchini kwetu na wengine wametoka hapa hapa dar na majina yao hatuyaoni? au mpaka wafe? sio vizuri hivyo jamani!

    ReplyDelete
  12. Sasa Mdau umemebeba maboxi hadi kiswahili umesahau au ndiyo kuzuga huko. Au unaongea kichaga? haya bwana Bongo pazuri sana,

    ReplyDelete
  13. HUYU PRAMUKWASHAMI NI MWANACCM NA NI MFADHILI MKUBWA WA CHAMA HIVYO HATUNA BUDI TUMUENZI. MITAA YOTE DAR KUWA NA MAJINA YA WANACCM TU WAKE, WAUME NA WATOTO WAO.

    ReplyDelete
  14. Kwa kifupi kama kutamka hilo jina ni kazi, basi sema Purukushani Street.
    Kwa mana nyengine mkienda miji ya watu mkakuta mtaa unaitwa kwa jina la kitanzania itakuwa ni ufisadi?
    Watanzania tena tusisabihishe kila kitu na ufisadi tutakuwa hatuna upeo tena wa kufikiria ila tutagota na ufisadi tuuuuu!!!

    ReplyDelete
  15. Acheni kubagua. Wahindi ni sehemu ya jamii ya Tanzania kama jinsi wengine tulivyo. Naogopa kukiri kuwa wahindi wachache wame impact hii nchi kuliko siye wabantu Million 40. Ukweli unauma lakini inabidi uumie kwanza kabla haujaelewa - na ukishaelewa unakuwa huru. The truth sets you free.

    Kwanza hii ni mitaa ya uhindini. Ni sawa na ile pilipili iliyo shambani inayomuwasha asiyehusika nayo.

    Mitaa iko mingi tu uswahilini wala haina majina. Tunaishia kusema naishi kwenye ule mtaa wenye duka la mangi. Au, eti, naishi opposite na dispensari ya Dr. Mvungi.

    ReplyDelete
  16. Hivi nyie mnaobagua wenzenu, mnafikiri Sewa Haji alikuwa ni Msukuma? Kwa taarifa yako alikuwa mfanyabiashara baniani aliyetetea sana waswahili wapate hospitali.

    Na je Karimjee Jivanje alikuwa ni Mdengereko?

    Selander alikuwa Mpogoro? Mbona madaraja yamejengwa mengi lakini tumeshindwa kuyapa majini - inabaki, daraja la Kajima!

    Ile shule ya wahindi Shaaban Roberts, wameiita kwa jini la Mungu wao wa kihindu? Mzizima je? Unaelewa kuwa Mzizima siyo Mhindi bali ni kijiji cha Wazaramo kilichokuwepo kwenye saiti ilimojengwa Dar?

    Au mpaka iitwe Nyerere Road? Zitakuwa ngapi sasa? Au labda Chenge Street ndiyo utafurahi siyo?

    ReplyDelete
  17. Panjuan S. KumarApril 17, 2009

    Kidu gani wabongo mnaleta chuki ya jina yetu ya hindu.Hii ni jina ya guru wetu sababu sisi hindu tume dominate all uchumi ya hapa na ndio natoa fadhili kuba kuba tyumeona tuite mtaa wetu jina ya guru wetu.

    ReplyDelete
  18. mimi jamani sioni shida kuona majina ya utamaduni mwingine nchini kwangu kwani dunia ipo wazi sasa hivi na hata nchi nyingine wana majina ya kiswahili,ila hawa ndugu zetu wa kihindi wa kizazi hiki wanakera wakitaka umaarufu ndo wanajifanya watanzania na kiswahili wanajua lakini wakiwa wanataka kwenda uk na canada wanatukana kabisa eti wanakimbia shida na watanzania wanawatesa ndo maana wamejaa canada!inanikera sana ndo maana miss tanzania yule watu hawamkubali hadi sasa hivi ni wanafiki!

    ReplyDelete
  19. MAJINA YA MITAA HAYATOLEWI KAMA PIP HUTOLEWA KAMA KUMBUKUMBU KWA MTU ALIYEFANYA JAMBO AMBALO WANANCHI WAMELIKUBALI NA KULITHAMINI CHA AJABU MADIWANI WACCM DAR WANAONDOA MAJINA MUHIMU YA ZAMANI NA KUJIPA WAO NA WAFADHILI WAO KIASI DAR LEO TUNA MAKAMBA, DITOPILE, MWANAMWEMA NA MINGINE MINGI TU YA WANACCM AMBAO HAKUNA LA MUHIMU WALILOIFANYIA JAMII LICHA YA AJIRA ZAO AMBACHO SI KIGEZO, TUYAKATAE MAJINA HAYA. HAO WANAOHUSISHA MASUALA YA UBAGUZI LABDA WATUELEZE KAMA LIVINGSTONE ALIKUWA MMANYEMA. KUNA WATU WALIOIBADILISHA KINONDONI KAMA BRYSON LAKINI HAWANA MITAA. MADIWANI WA CCM DAR ACHENI UBINAFSI WA KUTAKA KUJULIKANA.

    ReplyDelete
  20. Mpiga picha umenikumbusa mbali!!ngongolamboto /posta kulivyo na shida ya mabasi,acheni tuu wapaki kila mahala jamani....nakumbuka unatembea toka posta mpaka mnazi mmoja unasubiri basi litoke uwanjandege unarudi nalo posta na kuanza safari tena....duu mwacheni mungu aitwe mungu!!huku niliko sina shida ya mabasi...mshukuruni mungu kwa kila jambo.Amen

    ReplyDelete
  21. hahahhhahhaaaa tih tih tih,,dah "CHENGE STREET" hii imetulia sana annon apo,,,hahahahaa
    ila ulimbukeni kabisa kwanini jina gumu ivi???afu wala hatumjui kabisa km ni mtu au miungu ya nini sijui KATIKA JINA LA YESU SHINDWAA
    sii bora iitwe "MENGI STREET",NGASSA STREET,SUMAYE STREET,KINGUNGE STREET,PENDO STREE nk nk
    nyamafu zao '"\||&**@
    au unalipia nini ni km kibiashara ivi labda nasi tujue tuje wapi tujiandikishe tulipie tubandikwe mitaa

    ReplyDelete
  22. Hiyo ndio Bongo bwana ukiwa na vijisenti lolote linafanyika,Nyie Hamjui kama kuna mtu kafadhili kuweka vibao vya mitaa maeneo ya makumbusho na mitaa mingine akaweka jina la show room yake?
    Madiwani wa Bongo hawana neno ni kiasi cha kujifanya mfadili tu ukabandika mitaa jina la babu,bibi,mama mkwe wako ,mkeo ilimradi udakishe tu.
    ndugu yangu hapo juu nakuunga mkono hilo basi hapo linanikumbusha siku moja nilitembea umbali mrefu kutafuta usafiri ,lakini nchii nilipo basi linakwenda na muda wake tu hata kama hamna abiria jamani tufanye kazi kwa bidii siku 1 tutafika.

    ReplyDelete
  23. Hivi si kuna watu walishanyofoa vibao hivyo na kurudishia jina tunalolitambua la Kisutu? Kuna mitaa haina majina kama watu wanataka kuipa mitaa majina, sio kutuchanganyia habari.
    Hilo jina ni la kiongozi wa dini fulani. Ni kama jina la mtaa kuwa mtaa wa Aga Khan au Mtaa wa Papa Benedicto wa Pili. Kwa kweli kwa kiongozi wa dini kama mnataka kulienzi jina lake jengeni shule au hospitali, msinyang'anye majina ya mitaa.

    ReplyDelete
  24. KWA HERUFI KUBWA ACHENI UBAGUZI JAMANI NCHI ZA WENZENU PIA KUNA MITAA HAIJAPEWA MAJINA YA KWAO.KAMA MTAA UMEJAA WAHINDI KWANINI WASIITE JINA HILO KUTAMKA SI ISSUE HATA WAHINDI NI WATANZANIA MBONA WANATAMKA MAJINA YENU YA KINYAMWEZI HUKO.HAPA UHOLANZI UNA MITAA YENYE MAJINA KAMA, MANDELA BRIDGE,MANDELA STRAAT, AFRIKALAAN OR AMERIKALAAN ACHENI UBAGUZI WA KIJINGA JINA TU MNAPIGA MAKELELE.PINGENI RESOURCES ZENU KUCHUKULIWA SIO JINA KUITWA KIHINDU.

    MDAU

    NETHERLANDS

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...