Michuzi,
Naomba uniwakilishie hili kwa hawa TANESCO. Yahusu mabadiliko yasiyotambulika katika gharama za bei kwa wateja `TARRIFF INDEX 4', Wateja wengi katika mwezi huu tumeshangaa kubambikwa bei ya tarrif kubwa kuliko tulivyozoea.
Tunauliza ,Je bei za umeme (LUKU)i zimepanda(kutoka tsh.67.97 kWh hadi tsh.155.93/kWh. Manake mimi nilizoea kulipa 5,000/- kwa mwezi na kupata unit 60.8, lakini mwezi huu kwa bei hiyohiyo nimepata unit 26.5 tu, na huwa nanunua umeme huo mara moja kwa mwezi. Kwa unit walizo nipa itabidi sasa ninunue mara mbili au tatu kwa mwezi.
Naomba, mlirekebishe hili tatizo nyie watu wa Tanesco, kwani kufuatilia kwa sie tunaokaa nje ya jii, gharama za nauli zinazidi hata hiyo gharama ya UMEME, kwa kuambiwa njoo kesho, njoo kesho mhusika hayuko, nk. Na je ipi anuani yenu ya e-mail kwa wateja wenu kama tunataka kuwasiliana nanyi kwa e-mail?
Wenu mteja wa LUKU.
NB:Michuzi e-mail yangu iwe siri yako.
Wenu mteja wa LUKU.
NB:Michuzi e-mail yangu iwe siri yako.
(Poa-Michuzi)
TATIZO WATANZANIA HAMNA MUUNGANO WA KUWEZA KULALAMIKA AU KUANDAMANA KUPINGA JAMBO FLANI NDIO MAANA KILA KITU KINAENDESHWA KIOLELA.
ReplyDeleteBongo Tambarare
ReplyDeleteINAKERA SAAAAANA YANI ATA SIJUI NITUMIE LUGHA GANI KUELEZA HILI
ReplyDeleteSIKITIKO KUU LINALOWATESA WATANZANIA...
unajua EPA haitasiha nchini mana sasa kila mtu atakomoa kula kwa urefu wa kamba yake km ndo twachunana namna hii tena bila wala MAELEZO MAKINI
'"|\\+_0"|\@8**
Tutarudi tu kwenye "vibatali" na Kandili....
ReplyDeleteMichu!
ReplyDeleteHuyu jamaa analalamika kaibiwa na tanesco, halafu anasema eti anataka kuwasiliana na tanesco kwa e-mail maana 100 mia za nauli issue, sasa inakuwaje anabania e-mail yake? Haya ndo mwalimu JK aliita MANKANYANGE
kimsingi malalamiko yake yana walakini. Hivi jamani mtu gani analipa umeme 5,000 kwa mwezi? au huyu mkuu ameichezea hiyo luku?
LUKU ya 5,000/- Mwezi !!!
ReplyDeleteDuh, HONGERA Mzee.
Kuna walakini mahali. Nimelipa 10,000/= leo nikapewa unit 58 tu.email yao ni Customer.Service@tanesco.co.tz. Wakikujibu lakini ndugu yangu, niarifu ni dawa gani uliyotumia maana itakuwa ni muujiza fulani.
ReplyDeleteNna 100% aloleta hili lalamiko ni mwanamke...! Usiniuliuze nimejuaje!Anaibisha anyooshe mkono juu! We.. we.. we, nyie hamuisikii sauti???!
ReplyDeleteshilling 5000 tu umeme? mamaaaaaaa mimi bili yangu ya mwezi ikija chini ya $270 wakati wa winter nafurahi kweli na summer ni $190.... damn just $5.00 ???????? watalipwaje mishahara hao watu na kukeep mitambo yao? Kweli sometimes kama mtu umeme hauwezi tumia vibatari. Hamna kitu kinachokuja bila cost let's face it....Cheap shit ndio zinatufanya kila siku tuwe na poor quality things....Hapa nalipa so much kwa umeme lakini mgao hamna....na siku tu ukikatika napewa taarifa in avance na msamaha mkubwa sana napewa....kila siku watu wanapiga kelele umeme hamna, umeme wa mgao kumbe bill zenyewe ndio hizi...elfu tano.....itabidi tuamke waajiri wawalipe watu vizuri ili nao waweze kulipa bill zao na makampuni yaweze kutoa quality service.
ReplyDeleteNashangaa sana bongo magari, nguo, viatu na mambo ya mastarehe yote yanaprice tag za huku tuliko lakini hamna mtu anayelalamika sasa kwanini vitu muhimu vya maisha watu ni kulalamika. tukilipa vizuri tutapata quality nzuri
Kaka Micu kuna namna unaweza ukafikisha haya malalamiko EWURA kwa niaba ya wana blog ya jamii. Mimi naunga mkono kwamba kuna kamchezo wa kupandisha bei kametendeka. Na hii haitakuwa mara ya kwanza kwa TANESCO kupandisha bei kinyemela.Tafadhali tuwasilishie kilio hiki EWURA maana jadi ya TANESCO ni kutokujibu malalamiko ya wateja au majibu ya mkato na ubabe.
ReplyDeleteLUKU inasaidia sana wenye kipato cha chini, kwani unajikuna pale unapopafikia, kwahiyo huyo jamaa kutumia 5,000/- kwa mwezi ndio uwezo wake. Chukulia mfano kama anatumia taa peke yake inaweza kuzidi ikawa hata pungufu ya hiyo hela.
ReplyDeleteSwali hapa ni kwa Tanesco kumjibu muhusika, tusiangalie mambo mengine
Inawezekana kabisa kwa mtu kutumia tsh 5000 kwa mwezi inategemea na matumizi yake hivyo tusianze kumlaumu ama kumfikilia vibaya kuwa ni mmoja wa wanaochokonoa luku zao. inawezakana ana kiosk tu cha kuuzia askilim na machungwa.
ReplyDeletelakini ukweli ni lazima tuseme kuwa Tanesco wanaongeza bei ya umeme kinyemela maana hilo tatizo alilosema mdau sasa limekuwa sugu, kila unaponunua umeme gharama za ununuzi zinazidi kupanda.mimi nilikuwa natumia shs 25.000 kwa mwezi. lakini ajabu nyumba ni ileile hakuna mabadiliko niliyoyafanya, sasa natumia 30.000 mpaka 35.000 kwa mwezi.
Naomba balozi wetu, misupu utupelekee tatizo hili ewura ili watujibu kupitia katika blog yetu hii ya jamii.
ACHENI UNAFIKI WENU NYIE.MNAFIKIRI NI KWANINI WALIAMUA KUITA LUKU? KILA MTU ANATUMIA NA KULIPIA UMEME KULINGANA NA UWEZO WAKE. KAMA WEWE UNA UWEZO WA KUTUMIA JIKO LA UMEME, PASI N.K, MIMI NIACHE NIWASHE BALBU ZANGU NA KAREDIO KANGU TU. NDIO MATUMIZI YANGU MUHIMU, NA HUO NDIO UWEZO WANGU. SIO LAZIMA NITUMIE KAMA WEWE UNAVYOTUMIA
ReplyDeletewakati naondoka tz 2001 niliacha kwa mwezi home wanalipa sh 4,000/= bill ya maji, umeme 12,000/= nilirudi 2008 nikakuta maji 28,000 kwa mwezi na umeme 36,000/= ktk familia ya watu 3! nikajaribu kufuatilia chanzo kisomi nikagundua umeme ulipopanda kwa 5% kutoka sh 12,000/= ulifikia sh 20,000/= i.e 60% kihalali na maji kutoka sh 5000/= iliongezeka kwa 20% mpk 12,000 hii nisawa na 300%.
ReplyDeletemafuta tunaambiwa yamepanda kwa 5% kutoka sh 1200 mpk 1600/= kwa kweli huku nikugeuzana maboya kimahesabu ya kitoto kama hatujui vile. NAOMBA UTARATIBUMZIMA UNAOTUMIKA KUCHAGUA VIONGOZI WA EWURA
USHAURI WANGU WADAU MAMLAKA YA EWURA WAPEWE UONGOZI WA WANAFUNZI WA UDSM
shilling 5000 tu umeme?
ReplyDeleteHuyu ni mwehu ayeishi bongo anajifanya yupo nje hajui lolote khs huku eti analipa $120, 190 nchi gani hiyo na ambayo umeme unakatika katika mpk wanakupigia simu hata maelezo yake yanaonesha mswahili leo kaingia net,jiheshimu lkn Nisiseme sana huwenda anamaanisha $ ya zimbabwe au nchi zngine za africa. hapa nilipo umeme ulikatika 2004 saa1 mpk saa 12 jioni tena walikuw wanafunga transformer mpya na matangazo yalianza kutoka wiki tatu kabla ya kuomba radhi kwa usumbufu
Swali zuri but to the wrong people!!!!!!! Afu wewe anon 1:56 dont be funny! Huwezi linganisha bongo na US in any way! Dammy, get a life!
ReplyDeleteSwali zuri but to the wrong people!!!!!!!
ReplyDeleteNi kweli mwanawane, kwani wengine wakijaribu kudai haki na kuziweka hadharani ili kila mtu aona,achangie na majibu yotolewe,ili kila mwenye tatizo kama hilo afaidike, wengine wanakandia!
Hawa Tanesco walitakiwa wachukue nafasi hiyo kuelezea tatizo lipo wapi, tujue, kuliko kusubiri kila mmoja awatembelee ofisini kwenu.
Mimi nilienda nikaonana na muhasibu wao kule maeneo ya Posta, akasema kuna hitilafu katika computa zao, hata wao staff wamebebeshwa bei ya kawaida, alisema eti ikirekebishwa unit zitakuwa kama kawaida.
Cha ajabu mpaka leo sijaona mabadiliko. Je wateja tuliodhulumiwa tufanyeje. Na nyie mnaomshambulia mtoa hoja, angalieni nini hoja sio hali ya kipato chake. Wewe kama unauwezo wa kutumia 30,000, kwa mwezi ujue kuna wengine hata hiyo 3,000/- inampiga chenga.